arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 31.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» HILI NDILO TAMKO LA OBA ...
» Mtoto ateseka miaka 15
» POPOBAWA AMENITESA MIA ...
» MAMA WEEE! MBAVU ZANGUU ...
» Just hang me! (Ninyon ...
» ‘Surprise’ katika mapen ...
» Kagera Sugar wafunga ki ...

 

WAKAZI WA MANYARA NA ARUSHA WALIVYOICHANGAMKIA PAJERO.

photos  
Wiki iliyopita, timu ya Promosheni ya Bahati Nasibu ya jishindie Pajero, inayoendeshwa na kampuni ya Global Publishers, ilikuwa Mkoani Arusha na Manyara kuhamasisha wasomaji wake. Picha zifuatazo, zinaonesha jinsi wasomaji wa magazeti ya Global Publishers katika mikoa hiyo walivyochangamkia Promosheni hiyo ambayo droo yake ya mwisho inatarajiwa kuchezwa Alhamis ijayo, April 9 jijini Dar es salaam.

WAKAZI WA MANYARA NA ARUSHA WALIVYOICHANGAMKIA PAJERO.
Wakazi wa Arusha maeneo ya Mbauda Sokoni, wakiwania kuponi za Jishindie Pajero, Jumamosi wiki iliyopita.

WAKAZI WA MANYARA NA ARUSHA WALIVYOICHANGAMKIA PAJERO.
Mmoja wa wasomaji wa magazeti ya Global Publishers, maeneo ya Ngaramtoni, Arusha, (aliyeinua gazeti na kitabu katikati) akiwahamasisha wasomaji wengine wa eneo hilo kushiriki katika Bahati Nasibu ya Jishindie Pajero, kwa kununua magazeti ya kampuni hiyo.


WAKAZI WA MANYARA NA ARUSHA WALIVYOICHANGAMKIA PAJERO.
Wananchi wa Arusha mjini eneo la Soko Kuu, wakiwania kushiriki katika Bahati Nasibu ya Jishindie Pajero, kwa kununua magazeti na vitabu mbalimbali vya kampuni ya Global Publishers.

WAKAZI WA MANYARA NA ARUSHA WALIVYOICHANGAMKIA PAJERO.
Wasomaji wa magazeti ya Global Publishers wa Monduli, mkoani Arusha, wakiwa wamejipanga kupata magazeti na machapisho mbalimbali ya Global Publishers.

WAKAZI WA MANYARA NA ARUSHA WALIVYOICHANGAMKIA PAJERO.
Mkoani Manyara pia wasomaji wa magazeti maarufu ya Global Publishers, walishiriki kwa hamu kubwa katika kununua magazeti ya kampuni hiyo, ili kushiriki katika Bahati Nasibu ya Jishindie Pajero.
Picha: Musa Mateja /GPL.
    (31 March 2009)
Views: 287 | Maoni (1) |

 

KAMERA YETU ILIVYOFIKA KIJIJINI KWA MH. LOWASSA

photos  
KAMERA YETU ILIVYOFIKA KIJIJINI KWA MH. LOWASSA
Kamera yetu pia iliweza kunasa shughuli mbalimbali za wakazi wa Monduli, ikiwa ni pamoja na kinamama waliokuwa wakitumia usafiri wa ‘punda’ katika kubebea bidhaa zao kuelekea katika masoko mbalimbali.

KAMERA YETU ILIVYOFIKA KIJIJINI KWA MH. LOWASSA
Wakazi wa Monduli, wakiwa sokoni katika harakati za kila siku za kuuza na kununua bidhaa mbalimbali kama walivyonaswa na kamera yetu.
Picha: Musa Mateja /GPL.
    (31 March 2009)
Views: 346 | Maoni (0) |

 

‘Ushindi ya Kabula’ kuwekwa videoni

uwazi  
‘Ushindi ya Kabula’ kuwekwa videoni
Na Abraham Makinda

Msanii wa muziki wa Injili nchini, Kabula J. George, anatarajiwa kuirekodi albamu yake ya ‘Ushindi’ ambayo nyimbo zake zimeanza kuwashika watu wengi wanaozisikiliza kupitia vituo vya radio nchini, kwenye video...

    (31 March 2009)
Views: 565 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

BI. LUCY NA UGONJWA WA AJABU

uwazi  
BI. LUCY NA UGONJWA WA AJABU
Na Elias Ally, Iringa
DUNIANI kuna magonjwa mbalimbali ambapo kuna mengine hayajawahi hata kuonekana na mengine kutokea kwake kwaweza kukawa ni mara ya kwanza....
    (31 March 2009)
Views: 1041 | Maoni (5) | Soma Zaidi

 

AJALI YA CHENGE MAPYA YAIBUKA

uwazi  
AJALI YA CHENGE MAPYA YAIBUKA
Na Waandishi Wetu

WAFANYAKAZI wenzake na marehemu katika Hoteli ya Mwanza, ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, wameibua mambo mapya kwa kutoboa siri za Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi na Mwanasheria Mkuu wa zamani wa serikali, kwa kueleza uhusiano wake na mmoja wa Marehemu Vicky ulivyokuwa kabla ya ajali...
    (31 March 2009)
Views: 4401 | Maoni (19) | Soma Zaidi

 

VIONGOZI WETU WANATUTOA KAFARA

uwazi  
VIONGOZI WETU WANATUTOA KAFARA
Waandishi Wetu, Dodoma na Dar

KUFUATIA ajali nyingine ya treni iliyotokea Jumapili mwishoni mwa Wiki iliyopita katikati ya Stesheni ya Gulwe na Msagali wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo watu 7 walikufa papo hapo na wengine 7 kujeruhiwa, wahanga waliohojiwa na Uwazi wameilaumu Serikali kwa ajali za mara kwa mara zinazolikabili taifa na kusababisha maisha ya maelfu ya raia wema kupotea...
    (31 March 2009)
Views: 619 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

ADUI WA CCM YUPO NDANI!(2)

Pasua Jipu  
Wiki iliyopita nilianza kuongea juu ya Adui wa CCM yupo ndani ya CCM yenyewe na kama adui huyo hayuko ndani basi CCM haina sababu yoyote ya kuhofia maadui wa nje, maana hawatakizulu Chama hicho kikongwe nchini. Niliongea mengi na mwisho nikashauri kama Mtanzania, kwamba ni wakati mzuri wa Chama Cha Mapinduzi kuingiza damu changa ndani ya chama chao, kuwekeza katika siku za usoni badala ya kuendelea kubakiza madaraka mikononi mwa wazazi wetu ambao wamenza kuchoka, huu ni wakati wa wao kupumzika. Leo naendelea…
    (31 March 2009)
Views: 210 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

NILIMUUA MUME WANGU NIOLEWE NA TAJIRI – 16

Mikasa ya kusisimua  
Mke wa mtu anapanga mashambulizi ya kimya kimya ili kumuua mumewe aweze kuolewa na mwanaume tajiri mwenye asili ya kiarabu na kwenda kuishi Uarabuni, wametumwa wanaume watatu waliopanda ndani ya teksi maeneo ya Mlandizi na kumuwekea bastola kichwani tayari kumuua. Jambo moja analotamka mumewe anamuomba Shakila amwambie sababu au kosa gani linalostahili kifo? Mkewe anamjibu kuwa hajamkosea jambo lolote isipokuwa ameamua kufanya hivyo ili akaolewe na mwanaume tajiri mwenye asili ya kiarabu, mumewe anamruhusu akaolewe na kumtaka asimuue kwani watoto wake watabaki yatima na hakuna wa kuwalea.Je, nini kitaendelea? Fuatilia mkasa huu wa kuhuzunisha utajifunza jambo...
    (31 March 2009)
Views: 1641 | Maoni (12) | Soma Zaidi

 

THE BLOOD DEAL - 39

hadithi za Shigongo  
Msichana mrembo Priscilla ameingia mikononi mwa wanyonya damu, wanaomlazimisha kufanya kazi haramu ya damu. Halikuwa jambo rahisi kwa Priscilla kukubaliana na watu hao katili. Maishani mwake hakutaka kuua kiumbe cha Mungu, anapinga na kuomba arudishwe nyumbani Tanzania lakini Jimmy anamwambia lazima wamnyonye damu kwa kuwa ameshindwa kufanya kazi akisisitiza kila anayeingia ndani ya jumba hilo lazima akubaliane na matakwa yao vinginevyo mauti humfika.

Moyo ulimuuma na kuanza kulia, anaingizwa chumba maalumu kwa ajili ya kunyonywa damu kisha anaambiwa hapo ndipo uhai wake utakapotoweka. Katika chumba hicho chenye chupa nyingi za damu za makundi tofauti, Priscilla alishuhudia mwanaume mweusi akinyonywa damu mshtuko mkubwa ulimpata na kupoteza fahamu.

Katika hali ya kutisha, Priscilla anaanza kunyonywa damu taratibu, sindano ya kwanza ilipoingia mwilini alihisi kizunguzungu, baadaye akahamishwa chumba kingine ambako alivuliwa nguo zote na kulazwa juu ya kitanda, Wairimo mwanamke mweusi akakabidhiwa afanye kazi yake, baadaye Jimmy anaingia na dumu la lita tano Priscilla akahisi kifo kilikuwa mbele yake.

Huruma ilimuingia sana Wairimo na kuanza kumtetea Priscilla, baadaye anamuomba Jimmy atoke ili waweze kuongea naye, walibaki wawili katika chumba chenye chupa nyingi, Wairimo anapomweleza siri na mafanikio ya kazi ya damu, Priscilla anajikuta akiridhia na kuingiwa na uchu wa kuwa bilionea.

Muda mfupi anaanza kuzoea maisha magumu ya unyonyaji damu aliporidhia kazi ya damu, wanaondoka Humberg nchini Ujerumani na kuingia jijini Dar es Salaam, kazi kubwa mbele yao ikiwa kunyonya watu damu na kuisafirisha hadi nchini Ujerumani nyumbani kwa Jimmy.

Ndani ya jiji la Dar es Salaam, wanyonya damu hao wanashukia Hoteli ya Sweet Dream iliyopo Masaki, wanafanya mazungumzo kwa siri juu ya kuanza kazi yao, jinsi gani wangeweza kufanikisha zoezi hilo bila kutiwa mikononi mwa Vyombo vya Sheria.

Usiku huo, Priscilla hakutaka kulala anamwambia Wairimo anatamani kuanza kazi hiyo mapema, wanakubaliana na kumuacha Miloslov chumbani na kuvaa nguo za kimahaba zinazoshawishi wanaume. Kila mmoja anaridhika kuwa amependeza ndipo anapochukua teksi iliyowapeleka hadi Manzese Tip Top katika baa moja inayopiga muziki siku za mwisho wa wiki. Je, atafanikiwa kunyonya damu au atatiwa mikononi mwa Polisi? SONGA NAYO...
    (31 March 2009)
Views: 1022 | Maoni (3) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com