arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for April 2009 Year

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» ZITO LAIBUKA
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Nilivyobakwa na baba ya ...
» JAMANI NARUDI TENA KUWA ...
» Maximo: Ngasa gumzo Bra ...
» Mai afanyiwa Kitu Mbaya
» GAMBOSHI- 4
» Mapenzi na pesa ni chan ...
» MSIBANI KWA BALOZI DARA ...

 

HALI BADO TETE MBAGALA

photos  
Hali bado ni tete kwa wakazi wa eneo la Mbagala Wilayani Temeke na katika Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla, kufuatia tukio lililotokea jana la kulipuka kwa mabomu makubwa katika ghala la Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na kusababisha maafa makubwa. Watu kumi wamethibitishwa kupoteza maisha hadi leo, wakiwemo askari 5 wa JWTZ - kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam. Asubuhi ya leo, mtandao huu ulishuhudia wananchi, wakihaha kuwasaka ndugu na jamaa zao hasa watoto ambao walipotea jana. Vituo vingi vya Polisi, Msalaba Mwekundu, kambi za kijeshi na Hospitali, hasa Wilayani Temeke, mamia ya watu walijazana kutambua ndugu zao, huku vilio na mayowe vikitawala.

Askari wa Jeshi la Wananchi, JKT, Polisi, Scouts, wauguzi na watoa huduma ya kwanza walionekana wakiendelea kutoa huduma kwa watoto katika vituo huku zoezi la utambuzi likiendelea katika kambi za Mbagala Kizuiani na JKT Mgulani na katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke. Kwa ujumla, Mbagala bado inazizima ambapo asilimia kubwa ya wakazi wake hawakwenda kwenye shughuli za kawaida na badala yake walizidi kuzagaa mitaani kusaka ndugu zao. JWTZ imeweka kizuizi kwa waandishi wa habari wa kawaida kuingia eneo la tukio (kambini) ambapo wanaoruhusiwa ni waandishi wa habari wanajeshi tu.

HALI BADO TETE MBAGALA
Hawa ni baadhi tu ya watu wanaoishi karibu kabisa na kambi ambayo kulikuwa na ghala lililolipuka wakiwa wamehifadhiwa katika kambi ya JKT Mgulani baada ya kukosa mahali pa kuishi.

HALI BADO TETE MBAGALA
Wananchi wakijiandikisha kwa ajili ya kutambua ndugu zao katika kambi ya JKT Mgulani leo.

HALI BADO TETE MBAGALA
Hawa ni watoto waliokusanywa baada ya kushindwa kurejea makwao, wakipata kifungua kinywa katika kambi ya msalaba mwekundu Kizuiani leo asubuhi.

HALI BADO TETE MBAGALA
HAWA SIYO MAHABUSU: Wananchi wakiingia kwenye kwenye gari ambalo hubebea mahabusu ‘Karandinga’ katika kituo cha Polisi Kizuiani Mbagala kwa ajili ya kwenda kambi ya JKT Mgulani kutambua ndugu zao waliopotea asubuhi leo.

HALI BADO TETE MBAGALA
Scout akisaidia kumnywesha uji mtoto mwenye umri wa kati ya miaka miwili anayehifadhiwa katika kambi ya Msalaba mwekundu Kizuiani.

HALI BADO TETE MBAGALA
Mama huyu akilia baada ya kumkosa mwanaye katika kambi ya JKT Mgulani, ikiwa ni baada ya kuhangaika sana kumtafuta.

HALI BADO TETE MBAGALA
Mmoja wa skari wa JWTZ ambaye alijeruhiwa na mabomu akiwa nje ya kambi ya jeshi Mbagala akielekezwa jambo na askari mwenzie.

PICHA: CHRISTOPHER LISSA
    (30 April 2009)
Views: 309 | Maoni (1) |

 

VUNJA MBAVU

Vichekesho na Udaku  
VUNJA MBAVU
Mchaga na dili la pesa
Jamaa mmoja wa kichaga alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni. Ndugu zake wakaamua kumpeleka hospitali, akatakiwa afanyiwe operesheni.
Gharama za Matibabu zilitakiwa milioni mbili.Ndugu na jamaa wakahangishana wakapata pesa hizo kisha wakampatia Dokta ili amfanyie upasuaji ndugu yao.
Ile ndugu wanaondoka tu hospitalini pale, mazungumzo kati ya mgonjwa na daktari yakawa hivi:
Mgonjwa: Dokta nataka tufanye dili la pesa. Mimi naona huu uvimbe achana nao, nishone tu ili wakija wajue umenifanyia operesheni. Kwenye hizo milioni mbili chukua laki tano niachie moja na nusu , nipate za kunywea bia! Msingi wa biashara hawataki kunipatia ila pesa ya kunitibia wanatoa, huu si ujinga Dokta.
Dokta akabaki ameduwaa...
    (30 April 2009)
Views: 918 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

A - Z YAMLIPUKO DAR

Amani  
A - Z YAMLIPUKO DAR
Na Waandishi Wetu

Jiji la Dar es Salaam, jana (Jumatano) lilitikiswa na mabomu yaliyolipuka kimakosa kutoka ndani ya ghala la Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ lililopo Mbagala Kizuiani na kuzua tafrani kubwa miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.
Mlipuko mkubwa na wa aina yake ulisikika kwa mara ya kwanza majira ya saa 5:30, asubuhi na kutikisa paa za nyumba sehemu mbalimbali za jiji, jambo lililowafanya watu watoke majumbani na maofisini wakiweweseka kwa hofu ya tukio hilo lisilo la kawaida...
    (30 April 2009)
Views: 1602 | Maoni (14) | Soma Zaidi

 

MAUREEN BADI UNABISHA?

Amani  
MAUREEN BADI UNABISHA?
Na Mwandishi Wetu

Binti maarufu jijini Dar es Salaam, aliyepata kushiriki mashindano ya kuwania Taji la Miss Tanzania 2005, Maureen Gislary amefumwa laivu tena akifanya mchezo mchafu yeye na msichana mwenzake aitwaye Cheshije Hamisi, kamera yetu imenasa ishu nzima...
    (30 April 2009)
Views: 4222 | Maoni (29) | Soma Zaidi

 

BEYOND LOVE – 31

hadithi za Shigongo  
Tom, kijana aliyesotea maisha, akiishi maisha ya dhiki na matatizo tupu, huku akishuhudia baba yake mzazi akifa mbele ya macho yake, tatizo kubwa likiwa ni fedha! Alikuwa fukara wa kutupwa, kama ufukara ungekuwa na harufu, basi Tom alikuwa ananuka ufukara, tena wenye harufu kali sana!

Pamoja na ufukara wake akatokea kumpenda mtoto wa kitajiri Mariam, ambaye wazazi wake walikuwa wakimkataza kabisa kuwa naye. Siku moja ambayo baba yake Tom alipozidiwa sana, Mariam huyo huyo ndiye aliyeiba gari la wazazi wake na kumkimbiza baba yake Tom hospitalini. Yote hayo ikiwa ni kwasababu alikuwa akimpenda sana.

Kwa bahati mbaya, wakati Mariam anarudi nyumbani anapata ajali inayomlaza kitandani kwa miaka kadhaa akiwa hajitambui kabla ya kupata nafuu na kurudi chuoni kuendelea na masomo. Hapo ndipo walipokutana kwa mara nyingine katika Ukumbi wa Nkurumah ambapo Tom alikuwa akitoa Semina ya Ujasiriamali. Machozi yanarejea tena katika maisha yake, hasa baada ya Tom kumtambulisha Mariam kwa mchumba wake mpya, Juliana.

Hata hivyo baada ya kushauriwa na Wataalamu wa Saikolojia, anaamua kukubaliana na hali halisi na kuendelea na maisha yake kama kawaida. Lakini katika hali ya kushangaza sana, siku ambayo Tom alipanga kufunga ndoa na Juliana, ndiyo siku anayomvalisha pete ya uchumba Mariam kabla ya kufunga naye ndoa wiki chache baadaye.

Uamuzi huo unasababishwa na mpenzi wake Juliana ambaye alitegemea kumuoa, kumfumania akimsaliti tena na rafiki yake kipenzi. Furaha kwa Mariam inakuwa ya msimu tu, kwani baadaye Tom anamletea Mariam mwanamke mwingine aliyeitwa Mayasa! Hapo ndipo mwanzo mpya wa machozi kwa Mariam.

Mariam ananyanyaswa, anateswa na kulazimishwa kulala chumba cha wageni, mambo yalivyomshinda akaamua kurudi nyumbani kwao, lakini kwa bahati mbaya akaanguka na kupoteza fahamu. Alipotibiwa na kupona, akawaomba wazazi wake waende kuzungumza na Tom, lakini walipoenda Tom na Mayasa, walifukuzwa kama mbwa!

Mariam anaamua uamuzi mpya, anakwenda kuishi kijijini Matombo, Morogoro, kwa bibi yake kwa nia ya kukaa mbali na Tom pamoja na vyombo vya habari. Hakutaka kusikia kabisa habari za Tom. Wakati hayo yote yakitokea, shetani wa pesa anamwingia Mayasa, anapanga mipango ya kumuua Tom ili aweze kurithi mali zote!
Je, atafanikiwa? Vipi maisha ya Mariam huko kijijini Matombo? SONGA NAYO....
    (30 April 2009)
Views: 991 | Maoni (11) | Soma Zaidi

 

WANAWAKE HUISHI MIAKA MINGI ZAIDI YA WANAUME!

Saikolojia na maisha  
Inaweza ikawa ni mada ngumu kuikubali kutokana na sababu kadha wa kadha, lakini ukweli unabaki kuwa wanawake wamebainika kuwa na uwezo wa kuishi miaka mingi zaidi ya wanaume. Hii ni kwa mujibu wa tafiti nyingi zilizofanywa hivi karibuni ulimwenguni, ukiwemo ule ulioendeshwa na wanasayansi wa Chuo cha Liverpool John Moores (LJMU) nchini Uingereza...
    (30 April 2009)
Views: 736 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

KUTAFUTA MAISHA KUMENIFANYA NIWE MCHAWI – 41

Mikasa ya kusisimua  
Mpenzi msomaji, kijana Beka anaendelea kusimulia mkasa uliomkuta huko Bububu Zanzibar alikofundishwa uchawi. Wiki iliyopita nilielezea alivyomfanyia ndumba mrembo mmoja aliyekuwa akiutesa moyo wake ambaye kila alipomtongoza alimkataa kwa madai hakuwa na sifa za kuwa mpenzi wake. Kitendo hicho kilimuumiza sana Beka ndipo aliamua kutumia uchawi ambao ulizaa matunda kwani baada ya dada huyo aliyekuwa akiishi katika familia ya kilokole kuruka ndumba ambazo Beka alizichimbia ardhini kwenye mlango wa ofisi aliyokuwa akifanya kazi, mrembo huyo alipagwa na kwenda ofisini kwa Beka na kuonesha dalili za kumtaka kimapenzi.

Hata hivyo, ili kumalizia kumroga dada huyo, Beka alilazimika kwenda nyumbani anakoishi dada huyo usiku wa manane. Beka alipofika nyumbani kwa dada huyo akiwa na matunguri yake alishindwa kufanikisha kazi yake baada ya ndugu wa dada huyo ambao ni walokole kufanya maombi. Hata hivyo, kwa kushirikiana na mganga mwenzake aitwaye mzee Mohamed wanamua kufanya ndumba zaidi ili kumnasa msichana huyo. Je, watafanikiwa? Ungana na Mwandishi Wetu KULWA MWAIBALE katika mkasa huu wa kweli…
    (30 April 2009)
Views: 931 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

UFANYEJE MPENZI WAKO ANAPOAMUA KUKUACHA GHAFLA?

Mahaba  
UFANYEJE MPENZI WAKO ANAPOAMUA KUKUACHA GHAFLA?

Kuachwa ni jambo linalotia uchungu usioelezeka katika mapenzi hasa pale wanaoachana mmoja anakuwa bado anampenda mwenzake kwa dhati. Wanaoachwa huku wanapenda hukonda kwa mawazo na wakati mwingine hutamani kufa kuliko kuishi bila wapenzi wao.

Wapenzi wengi huuliza “nifanyeje baada ya kuachwa au nitumie mbinu gani ili kurudiana na mpenzi wangu kwani siwezi kuishi bila yeye na kwamba bado namhitaji maishani.” Katika maswali haya wahusika hutaka kujua mambo mawili tofauti lakini yote yanatokana uchungu wa kuachwa.

Moja, ni namna gani wanaweza kufanya ili warudishe uhusiano na waliowaacha ili mioyo yao ipate tiba na pili wanawezaje kuepukana na uchungu wa kuachwa ambao huwakaa moyoni kiasi cha kuwatesa? Majibu ni kama ifuatavyo:
    (30 April 2009)
Views: 2676 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

TIGO YAFADHILI KUANZISHWA KWA MRADI WA KUWEKA NA KUKOPA

photos  
TIGO YAFADHILI KUANZISHWA KWA MRADI WA KUWEKA NA KUKOPA
Dodoma Kampuni ya simu za mkononi ya tigo Tanzania kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali CODERT imetangaza ushirika maalum wa kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa kwa mfumo kwa mfumo wa kuweka hisa ndani ya kikundi ili kusaidia wananchi wa Tanzania kujikomboa kiuchumi na kuimarisha maisha yao kwa jumla kwenye jamii wanazoishi.
    (29 April 2009)
Views: 310 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

MAAFA MAKUBWA MBAGALA!

photos  
MAAFA MAKUBWA MBAGALA!
...askari wa Kikosi cha zimamoto wakielekea eneo la tukio

MAAFA MAKUBWA MBAGALA!
..eneo la Mtoni Kwa Azizi Ally kuelekea mabomu yanakolipuka

MAAFA MAKUBWA MBAGALA!
...baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani wakiwa juu ya Daraja la Mbagala wakiangalia sekeseke hilo

MAAFA MAKUBWA MBAGALA!
...familia ikihama makazi kukimbia milipuko ya mabomu.


PICHA: ISSA MNALLY/GPL
    (29 April 2009)
Views: 461 | Maoni (0) |

 

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO

photos  
HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
Wakazi wa eneo la Mto Mzinga, kilomita 15 kutoka ghala la siliha lililoripuka wakiwa wameokota bomu lililoangukia Mto Mzinga baada ya kuripuka.

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
..moja ya vipande vya mabomu hayo

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
..kijana huyu alikuwa hajiwezi kutembea hivyo kupakiwa kwenye mkokoteni baada ya kuvunjwa mguu wake wa kulia na bomu.

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
..Kamishna wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja akiongea na BBC eneo la tukio

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
...mama na mtoto wake akikimbia makazi yake kwa muda

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
..wasamaria wema wakimbeba mwanadada huyu aliyepoteza fahamu kwenye mkokotena ili kumuwahisha hospitali

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
...mtoto wa shule ya awali akiwa kituo cha polisi Mbagala Kizuiani akiwa ni miongoni mwa watoto wengi waliopoteana na familia zao

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
DCI Manumba (kulia) nae aliwasili eneo la tukio kujionea hali halisi

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
...mama huyu anaangua kilio baada ya kumpoteza mtoto wake mdogo wa MIEZI MINNE wakati wa hekaheka ya kukimbia milipuko ya mabomu!

HEKA HEKA ZA MABOMU MBAGALA LEO
..ilikuwa ni hekaheka ya kila mtu kuokoa nafsi yake

PICHA: ISSA MNALLY/GPL
    (29 April 2009)
Views: 712 | Maoni (16) |

 

BREAKING NEWS: MABOMU YALIPUKA MBAGALA!!

photos  
Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyoko Mbagal Kizuiani, inalipuka na nyumba zilizopo jirani na kambi hiyo zimeshika moto!! Habari kutoka kwenye eneo la tukio zinasema kuwa, mabomu hayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye ghala la silaha la kambi hiyo na yamekuwa yakiripuka kila baada ya sekendu chache na yanendelea kulipuka hadi wakati huu tunawaletea taarifa hii. Kishindo cha milipuko ya mabomu hayo, ambayo yameleta hofu kubwa katika jiji la Dar es salaam, hasa maeneo ya Mbagala, Mtoni kwa Azizi Ally na maeneo ya Temeke, kimekuwa kikisikika hadi maeneo ya Mwenge.

Kwa mujibu wa habari za Radio One, mtu mmoja hadi sasa ameripotiwa kufa katika kadhia hiyo ya aina yake baada ya bomu moja kuangukia ndani ya nyumba yake na kuiteketeza na kwa sasa barabara ya Kilwa imefungwa, magari kutoka Kongowe kuja Mbagala, yamezuiwa. Waandishi wetu wako eneo la tukio na tutawajia baadae na picha za tukio hili la kwanza na la aina yake kutokea nchini.

    (29 April 2009)
Views: 945 | Maoni (12) |

 

MAITI YAKUTWA IKIELEA MTONI DAR

photos  
Maiti ya mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 35 na 40, leo asubuhi imekutwa ikielea katika Mto Msimbazi karibu na daraja linalozitenganisha wilaya ya Ilala na Kinondoni jijini Dar es Salaam, maeneo ya Kigogo njia panda. Kufuatia tukio hilo wakazi wanaoishi jirani na eneo hilo walitoa taarifa Polisi ambao walifika na kuuchukua mwili huo kisha kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati uchunguzi ukindelea. Mpaka mwili huo unaondolewa eneo hilo, hakuna aliyejitokeza kumtambua marehemu.

MAITI YAKUTWA IKIELEA MTONI DAR
Mwili wa marehemu ukitolewa kutoka mtoni

MAITI YAKUTWA IKIELEA MTONI DAR
Wasamaria kwa kushirikiana Askari kanzu wakiwa na mwili wa marehemu katika barabara ya Kawawa wakienda kuupakiza kwenye 'Difenda'

MAITI YAKUTWA IKIELEA MTONI DAR
Marehemu akiwa ndani ya 'Difenda'


PICHA: RICHARD BUKOS/GPL
    (29 April 2009)
Views: 398 | Maoni (1) |

 

Wema anaswa

risasi mchanganyiko  
Wema anaswa
Na Waandishi Wetu
Siku chache baada ya ‘kumwagana’ na Jumbe Yusuf Jumbe (aliyedaiwa kuwa ni mpenzie), Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu amenaswa katika Hoteli ya Coral Beach, Masaki, jijini Dar es Salaam, akiwa na Mbunge ‘yanki’ wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Zuber Kabwe, Risasi lina ‘ fulu muvi’.
    (29 April 2009)
Views: 4717 | Maoni (29) | Soma Zaidi

 

Nataka kichwa chamwanangu-28

Mikasa ya kusisimua  
ILIPOISHIA...
Ikingi amempa lifti msichana aliyejitambulisha kwa jina la Jasmini. Walipofika Sinza ya Makaburini, anashangaa kumuona yule msichana akiwa barabarani, alipogeuza shingo yake upande wa pili, hakumuona. Ikingi akapiga kelele. Je, nini kitaendelea? Mwandishi Wetu JOSEPH SHALUWA anaendelea...
    (29 April 2009)
Views: 676 | Maoni (2) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2 3 ... 17 18 19  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Author: admin


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com