arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for May 2009 Year

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» AY ALIVYOFUNIKA MALAYSI ...
» Simba mwanzo mwisho
» Nizar Khalfan apiga 529 ...
» BARUA KUTOKA KWA MAREHE ...
» 4; UTEKELEZAJI WA MPAN ...
» Niliukubali mkoba wa ki ...
» PINDA NA WALIMU MBEYA

 

MISS UNIVERSE 2009 APATIKANA

photos  
Usiku wa kuamkia leo warembo 20 walipanda jukwaani katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kugombea taji la Miss Universe ambapo mrembo Iluminata James ndiye aliyeibuka mshindi.

MISS UNIVERSE 2009 APATIKANA
.Iluminata akiwa na furaha baada ya ushindi

MISS UNIVERSE 2009 APATIKANA
Illuminata (kushoto) akikabidhiwa tuzo na muandaaji wa mashindano hayo, Maria Sarungi, baada ya kunyakua taji hilo.

MISS UNIVERSE 2009 APATIKANA
Miss Universe akiwa kwenye picha ya pozi na mshindi wa pili Eveline Almasy (kulia) na Hidaya Maeda (kushoto)

MISS UNIVERSE 2009 APATIKANA
Vimwana wa Diamond Musica wakitoa burudani wakati majaji wakifanya mahesabu ya kumpta mshindi.

MISS UNIVERSE 2009 APATIKANA
Mzee Kitine (kulia) licha ya kuwa Jaji katika shindano hilo lakini naye alikuwa paparazi na kuchukua picha mbili tatu alizoona zinamfaa.


PICHA:RICHARD BUKOS /GPL



    (31 May 2009)
Views: 401 | Maoni (2) |

 

Profesa Jay kidume!

photos  
Profesa Jay kidume!
Hatimaye ule mpambano wa Nani Zaidi, kati ya wakali wa Bongo Fleva, Juma Kassim Kiroboto ‘Juma Nature’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’, uliokuwa ukiendeshwa na mtandao huu, umefikia tamati wiki hii baada ya Jay kuibuka kidedea alipopata asilimia 55 dhidi ya Nature mwenye asilimia 45 ya kura 548 zilizopigwa na wasomaji. Ulikuwa mpambano mgumu kuliko yote iliyowahi kutokea tangu kuanzishwa kwa vuta-nikuvute hiyo. Ilibaki kidogo tu, mpambano urudiwe tena, lakini tunashukuru hatimaye mshindi amepatikana. Tunawashukuru sana wadau ambao wanaozidi kulikuza shindano hilo ambalo halina maana nyingine yoyote zaidi ya kukuza vipaji na kuwapa sapoti wasanii wetu. Wasanii wanaochuana wiki hii ni Marlaw na Ali Kiba.
    (30 May 2009)
Views: 375 | Maoni (4) |

 

KUNDI LA WELAWELA LIMEENDELEZA LAANA!!!

photos  
Kundi la wamwaga radhi maarufu Dar es Salaam, Welawela, leo alfajili, liliendeleza laana hiyo, wakati likichuana vikali na wanenguaji wa Bendi ya African Stars, 'Twanga Pepeta International' ndani ya Ukumbi wa Africentre uliopo Ilala jijini.

KUNDI LA WELAWELA LIMEENDELEZA LAANA!!!
KIONGOZI wa Welawela, Mamaa Shifo, akiwa manuuu... katika hekaheka mpambano huo.

TWANGA WAKIPAMBANA NA WELAWELA
KUNDI LA WELAWELA LIMEENDELEZA LAANA!!!
Wanenguaji wa Twanga nao wakijikwinya kupambana na Welawela leo alfajili.

AISHA MADINDA ANYWEA BAADA YA KUFUTUKA
KUNDI LA WELAWELA LIMEENDELEZA LAANA!!!
Mnenguaji wa Twanga, Aisha Madinda amenywea baada ya kufutuka mpaka kudaiwa kuwa mjamzito kutokana na alivyonenepa, mnenguaji huyo aliyepotea ghafla usiku wa kuamkia leo aliibukia Ukumbi wa Africentre na kuonekana mwembambaaa... kama Betina wa Dr. Love Pimbi.

WEE DIOUF, IMBAA MACHO 'KODO' KWA MAPEDESHEE!!!
KUNDI LA WELAWELA LIMEENDELEZA LAANA!!!
Mwanamuziki wa Twanga Msafiri Abdullah 'Diouf' katika onesho hilo yeye kila alipopata nafasi ya kukamata kipaza sauti alikuwa 'macho kodo' kuwakodolea mapedeshee na kuwarusha kwenye wimbo ili wampe mambo fulani.
PICHA: RICHARD BUKOS /GPL.
    (30 May 2009)
Views: 595 | Maoni (1) |

 

Pinda kwenye sherehe za 'utamaduni'

photos  
Pinda kwenye sherehe za 'utamaduni'
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Helena Adrian wa Ngara kuhusu vyakula asili vya kabila la Wahangaza na Washububi katika sherehe za siku ya Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Washubi na Wahangaza alizozifungua kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam May 29, 2009.
(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu).
    (30 May 2009)
Views: 231 | Maoni (1) |

 

Pinda ndani ya maongezi mazito

photos  
Pinda ndani ya maongezi mazito
9626 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shrika la Kimataifa la Concern World Wide, Bw. Tom Arnold, Ofisini kwake jijini Dar es salaam, May 29, 2009.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    (30 May 2009)
Views: 213 | Maoni (0) |

 

Kanumba muuaji?

risasi jumamosi  
Kanumba muuaji?
Na Imelda Mtema
Muigizaji ‘bitozi’ wa filamu za Bongo, Steven Kanumba ‘The Great’ juzi (Alhamisi) usiku aliwatishia kwa bastola vijana wawili waliomtaka atoe gari lake barabarani ili wapite, Risasi limenyakishwa...
    (30 May 2009)
Views: 1869 | Maoni (22) | Soma Zaidi

 

Maimartha abondwa nusu atolewe jicho

risasi jumamosi  
Maimartha abondwa nusu atolewe jicho
Na Mwandishi Wetu
Mtangazaji mwenye jina kubwa nchini, Maimartha Jesse a.k.a Oprah wa Bongo almanusura atolewe jicho katika ugomvi mkubwa kati yake na mchumba wake, Perfect Kagisa ‘P. Diddy’...
    (30 May 2009)
Views: 2588 | Maoni (14) | Soma Zaidi

 

Mil. 300 zamrejesha uraiani kula bata

risasi jumamosi  
Mil. 300 zamrejesha uraiani kula bata
Na Richard Bukos

Dhamana ya shilingi Mil. 300, imemuwezesha kurejea tena mtaani aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, baada ya jana (Ijumaa) Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kukubali ombi la mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya kuiingizia hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 200 benki hiyo kuomba kwa miezi kadhaa bila mafanikio...

    (30 May 2009)
Views: 630 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

BABA ALINITOA KAFARA KWA MAJINI-2

Mikasa ya kusisimua  
ILIPOISHIA JUMATANO...
Na kama haiwezekani kwanini alikuwa akiinua gauni langu juu na kuzungumza maneno ambayo sikuyaelewa? Baba alikuwa na siri nzito sana, siri ambayo pengine kama ningezungumza naye, angenieleza ukweli. Nabaki na maswali yangu kichwani. Endelea...
    (30 May 2009)
Views: 704 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Inakuwaje kila siku unaishia kuachwa? -2

Mahaba  
Inakuwaje kila siku unaishia kuachwa? -2

Nitakuwa situmii busara kama nitaacha kumshukuru Mungu wangu wa Mbinguni kwa mema yote anayoyafanya katika maisha yangu. Nasema ahsante sana baba! Ndugu zangu, kumshukuru Mola wako ni kujiongezea baraka katika ndoa yako na maisha yako ya kiuhusiano kwa ujumla...
    (30 May 2009)
Views: 463 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Msitu wa pande -26

hadithi za Shigongo  
Jacob amelipa kisasi kwa mauaji ya kikatili yaliyofanywa kwa mke na mtoto wake na baadhi ya watu waovu ndani ya serikali, amemuua Dk. Pandya Kumar, ASP John Kirumo na Waziri wa Afya Martin Lupingu baada ya kuteka Bunge! Watu hawa ndio waliopandikizwa na Shirika la Kijasusi la CIA ili kufanikisha zoezi la majaribio ya chanjo ya ugonjwa hatari uitwao Chinese Encephalitis ambao unazidi kushambulia dunia.

Chanjo hii ilitengenezwa kwa kuchanganya wadudu wawili hatari waliopunguzwa nguvu, hata hivyo kitendo hicho kilipingwa sana na shirika la Afya la Duniani kwa madai kwamba ilikuwa ni hatari iwapo wadudu hao wangepata nguvu. Mtoto wa Jacob, Natalia akawa miongoni mwa watoto waliopewa chanjo hiyo kwa siri, yeye na watoto wengine watano wakaugua ugonjwa wa Ini na kufa.

Ili kuficha siri Jacob, mke wake pamoja na wazazi wa watoto wengine walitekwa na kupelekewa kwenye Msitu wa Pande ambako walipigwa risasi na baadaye kutangazwa kwamba walikuwa ni majambazi waliokuwa wakipambana na Polisi! Bahati nzuri Jacob hakufa kwa risasi aliyopigwa, akaambaa na kujiokoa.

Kazi aliyoamua kuifanya baada ya hapo ni kulipa kisasi ambacho hivi sasa amekikamilisha na kukimbilia nchini Rwanda ambako amefichwa na rafiki yake David Kanyankore, huku serikali ya Rwanda ikimlinda kwa sababu ni yeye aliyetoa siri kuwa mzigo mwingine wa chanjo ya majaribio ulikuwa ukipelekwa nchini humo, Rwanda ikazuia kutolewa na watoto kuokolewa.

Serikali ya Tanzania inamhitaji Jacob kwa gharama yoyote, viongozi wamewasiliana na serikali ya Rwanda kuitaka wamkabidhi Jacob mikononi mwao ili ashtakiwe kwa makosa ya mauaji jambo ambalo Serikali ya Rwanda imelikataa kwa madai kuwa Jacob hayupo nchini humo jambo ambalo Serikali ya Tanzania linaamini ni uongo! Umetokea msuguano mkubwa unaoweza kusababisha vita.
Je, nini kitatokea? Jacob atakabidhiwa? SONGA NAYO…
    (30 May 2009)
Views: 660 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

UWOYA ATEMBELEA GLOBAL

photos  
UWOYA ATEMBELEA GLOBAL
Aliyekuwa mshiriki wa kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2007/8, Irene Uwoya, akiingia kwenye gari wakati akiondoka baada ya kutembelea ofisi za Global Publishers leo jioni.
PICHA: RICHARD BUKOS /GPL.
    (29 May 2009)
Views: 862 | Maoni (8) |

 

LIYUMBA AKUBALIWA DHAMANA

photos  
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa BoT, Bw. Amatus Liyumba, baada ya kunyimwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu, kwa miezi kadhaa katika kesi inayomkabili ya kuiingizia hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 200 benki hiyo, hatimaye leo Mahakama hiyo imekubali kumpa dhamana kwa shilingi Milioni 300.

Liyumba amepewa nafasi hiyo ya dhamana, na kutakiwa masharti mengine ambayo ni kutotoka nje ya jiji la Dar es Salaam, pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani hapo.

Kutokana na ufinyu wa muda Mawakili wa Liumba, wamemuomba Hakimu mpya anayeendesha kesi hiyo Bi. Nyigulila Mwaseba, kuahirisha kesi hiyo mpaka Jumatatu Juni, 1 mwaka huu, ili wakamilishe mipango ya kumdhamini.

LIYUMBA AKUBALIWA DHAMANA
Amatus Liyumba akirudishwa mahabusu mpaka Jumatatu, baada ya ombi la kumdhamini kukubaliwa leo mchana.
PICHA: RICHARD BUKOS /GPL.
    (29 May 2009)
Views: 198 | Maoni (0) |

 

JK AWAPIGA TAFU WAKAZI WA RUKWA

photos  
JK AWAPIGA TAFU WAKAZI WA RUKWA
Rais Jakaya Kikwete akiteta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa katika harambee hiyo.

JK AWAPIGA TAFU WAKAZI WA RUKWA
Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar es salaam May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa. Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    (29 May 2009)
Views: 290 | Maoni (4) |

 

MAPAPARAZI WAPEWA MIKOBA KUPAMBANA NA UKIMWI

photos  
Zaidi ya waandishi wa habari 50, kutoka vyombo mbalimbali nchini, wamemaliza mafunzo ya siku 3, yaliyokuwa na lengo la kuwapa stadi mbalimbali za kupambana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI, hususan unyanyapaa katika jamii.

Mafunzo hayo yalifanyika kuanzia Mei, 25 hadi 27 katika Hoteli ya Morogoro, mkoani Morogoro ambapo wahusika walikuwa ni waelimishaji rika kutoka katika vyombo hivyo na yaliandaliwa na Shirika la kimatifa la Misaada la Marekani (USAID).

MAPAPARAZI WAPEWA MIKOBA KUPAMBANA NA UKIMWI
Mtaalamu wa ushauri kutoka shirika la Fetures Group Bi.Asha Mtwangi, akiongea na washiriki wa semina hiyo mjini Morogoro.

MAPAPARAZI WAPEWA MIKOBA KUPAMBANA NA UKIMWI
Watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI, kutoka Chama cha Watu waishio na Virusi Vya UKIMWI mkoani Morogoro, (WAVUMO) Bi. Fatuma Japhari, (aliyejitanda Kanga kulia) Bw. Bugia Uhondo (katikati) na Bi. Keren Mpesa aliyevaa Kanga (kushoto) wakitoa ushuhuda wao kwa wanasemina hiyo.

MAPAPARAZI WAPEWA MIKOBA KUPAMBANA NA UKIMWI
Mkufunzi wa Semina hiyo Dr. Lucas Munaku (kushoto ) akitoa maelekezo kwa wanasemina.

MAPAPARAZI WAPEWA MIKOBA KUPAMBANA NA UKIMWI
Mwakilishi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, katika semina hiyo Christopher Lissa (kushoto mwenye tai) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanasemina.

MAPAPARAZI WAPEWA MIKOBA KUPAMBANA NA UKIMWI
Wanasemina wakiwa katika picha ya pamoja.
PICHA: CHRISTOPHER LISSA/GPL.
    (29 May 2009)
Views: 204 | Maoni (0) |
Back  <<  1 2 3 ... 18 19 20  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com