Hukumu hiyo, ilitolewa na hakimu wa mahakama hiyo, Bw. Gadiel Malick ambaye alisema kuwa baada ya kusikiliza pande zote mbili, mashtaka na utetezi, imethibitika kuwa watuhumiwa hao wana hatia.
Waliokumbwa na zahama hiyo ni Anicet Edward (30) na Job Mulama (30) wote wakiwa ni wafanyakazi wa kampuni ya utafiti wa madini, Barrick East Africa Expollation, pamoja na Shija Madata (18) aliye mkazi wa Kijiji cha Sota, Sengerema, Mwanza.
Akisoma hukumu hiyo Mei 4, 2009, Malick alisema kuwa Shija atatumikia kifungo cha miaka 55 jela kwa kuwa kitendo alichofanya hakistahili katika jamii iliyostaarabika ya Kitanzania.
Alisema, katika kosa la kwanza la mshitakiwa kumrubini mtoto huyo na kumpeleka kwenye kambi ya utafiti wa madini ya Sota inayomilikiwa na Barrick, kwa nia ya kumfanyisha mapenzi na mbwa, atatumikia kifungo cha miaka 15 jela.
Malick alisema, katika kosa la pili washitakiwa wote, Shija, Job na Mulama, watatumikia kifungo cha miaka 20 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumshawishi mwanafunzi huyo na kumfanyisha mapenzi na mbwa.
Hakimu huyo aliongeza kuwa washitakiwa wote kwa pamoja watakaa jela kwa miaka 20 mingine kwa kosa la kumlazimisha kwa nguvu mtoto huyo kufanya ngono na mbwa, kitendo ambacho ni kinyume na haki za binadamu.
Mbali na kutoa hukumu hiyo, Hakimu Malick aliagiza kuwa mbwa aliyetumika kufanya kitendo hicho akabidhiwe kwa Jeshi la Polisi, Mwanza ili amilikiwe na serikali na kufanya kazi ya kulinda usalama wa raia.
“Naamuru uongozi wa Kampuni ya Barrick, umkabidhi mnyama huyo (mbwa) aliyehusika kufanya kitendo cha ngono na mtoto kwa Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai (RCO) ili atumike kwa mazuri badala ya kile akichokitenda,” alisema.
Hata hivyo, hakimu huyo alisema washitakiwa wana haki ya kukata rufaa endapo wataona hukumu hiyo haikuwatendea haki.
Ijumaa Wikienda mwaka jana, liliripoti tukio hilo ambapo lilieleza kuwa mtoto aliyetendewa unyama huo ni mwanafunzi aliyekuwa Darasa la Nne kwenye Shule ya Msingi Sota, Sengerema.
|