Tembelea... |
 |
Kalenda |
 |

Marafiki wetu |
 |
Habari Zilizopita |
 |



|
|
 |
|
|
 |
 |
|
 |
   sherehe hiyo ilitawaliwa na vilio na majonzi, hasa pale Bibi harusi alipoingia kwenye eneo la wazi lililoandaliwa kwa shughuli hiyo akiwa amekaa kwenye baiskeli ya gurudumu (Wheel Chair). Aidha, vilio vilisita baada ya kukaa kwenye kiti kilichoandaliwa ‘spesho’ kwa Bibi harusi, lakini vilianza tena baada ya maharusi hao kuimba wimbo kwa pamoja unaoelezea mapenzi yalivyo. “Mke wangu sitakuacha, wewe ni mahabuba wangu, sitakuacha,” Sajuki aliimba wimbo huo. “Mume wangu unilinde, unipende, usiniache…,” Wastara naye alijibu na kusababisha vilio kutoka kwa wageni waalikwa. Aidha, yeye mwenyewe alishindwa kuendelea kuuimba wimbo huo na kujikuta akilia kwa uchungu mkubwa. Habari zinasema wimbo huo pia waliuimba kwenye filamu ya Mboni ya Jicho Langu ambayo iliwashirikisha wote. Msanii wa kike wa filamu nchini, Aunt Ezekiel ambaye alikuwa miongoni mwa waalikwa, alishindwa kuvumilia na kuporomosha machozi huku akisema: “Kwa kweli kwa namna hii huwezi kuvumilia hata uwe na roho ya aina gani ni uchungu mno, lakini Sajuki ameonesha upendo wa ujasiri.” Ukumbi huo ulizidi kutawaliwa na simanzi ingawa na makofi kwa mbali, pale bwana harusi aliposhika ‘maiki’ na kuwatangazia waalikwa kuwa, Wastara ni mkewe wa maisha, kamwe hatomwacha. “Nimesimama hapa kwa ajili ya kumhakikishia nyonga mkalia ini wangu (Wastara) kuwa mimi ni wake milele sitomuacha mpaka kifo,” alisikika Sajuki. Baada ya Shamrashamra hizo, Sajuki alimbeba Wastara huku akicheza naye wimbo wa mwanamuziki wa Sauzi, Yvonne Machaka ‘Chakachaka’ uitwao ‘Mkomboti’ huku akielekea naye kwenye gari kwa ajili ya kuondoka. Tukio hilo lilisindikizwa na wasanii kibao kwa nyuma huku wakicheza mpaka maharusi hao walipopanda gari na kwenda kwenye Fungate lao Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Baadhi ya watu waliohudhuria harusi hiyo walisema kuwa, hawakutegemea kama Sajuki angemuoa Wastara, hasa baada ya kukatwa mguu na kwamba kwa tukio hilo ameonesha upendo wa hali ya juu. Wasanii waliohudhuria sherehe hiyo ya ndoa ni Steven Kanumba ‘Kanumba’, Vincent Kigosi ‘Ray’, Aunt Ezekiel, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, na Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo.’ Wengine ni Hisan Muya ‘Tino’, Adam Kuambiana, William Mtitu ‘Mtitu’ na Hawa Mkama.        PICHA:IMELDA MTEMA
|
|
 |
 |
#15 Author: Rach! (8 June 2009 03:34)
|
|
 |
 |
hongereni sana na Mungu azidi kuwalinda katika maisha yenu na awajalie kheri na fanaka! usijali dada wastara yote ni mipango ya mungu pia Mungu anakupenda sana thats'y umishuhudia siku ambayo ulikuwa unaingoja kwa hamu sana! pia sajuki big up sana kaka yangu umonyesha mfano kwa wanaume wengine kukubali mabadiliko yanapo tokea!Mungu akuzidishie ujasiri zaidi!!!!!!!!! ha ha ha ha ha ha!!! endeleeni kupendana sana tuu! |
|
|
 |
|
|
 |
Kura Yako / Poll |
 |
Habari Katika Picha |
|
 |

Nani Yupo / Alikuwepo |
 |
|