arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » uwazi » SIRI YAFICHUKA

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» ZITO LAIBUKA
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Serikali: `Mvua za Lowa ...
» HATIMAYE WAPANDISHWA KI ...
» Mgosi amaliza mkataba w ...
» The Blood Deal! -48
» GROUP SEX
» Vunja mbavu
» Jini Mahaba linanitesa ...

SIRI YAFICHUKA

uwazi

Taarifa za kiuchunguzi ambazo zimethibitishwa na watu wa karibu wa pande zote mbili (ya Marehemu na Mtuhumiwa), zinaeleza kwamba, mtuhumiwa wa mauaji Masamba Musiba (27) ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho, alichukua uamuzi huo kufuatia kusononeshwa na uwepo wa kigogo wa TRA Makao Makuu ya jijini Dar es Salaam (jina halikupatikana) aliyekuwa akitembea na marehemu enzi za uhai wake.

Vyanzo vyetu hivyo vya habari ambavyo viko ndani ya Hosteli za Mabibo zinazomilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, vinasema kwamba, kigogo huyo wa TRA alikua akifika mara kwa mara majira ya jioni akiwa kwenye gari lenye rangi ya bluu aina ya Toyota RAV 4 muundo wa kisasa (New Model) na kumpakia kisha kuondoka naye kusikojulikana.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, kigogo huyo wa TRA alikua akifika na gari hilo lenye vioo vyeusi (tinted) kuanzia majira ya saa 2 jioni na wakati mwingine alikua akimuachia fedha za kukodi teksi kwa lengo la kumfuata anakokuwa na kurudi kesho yake.

“Huwa tulikuwa tunamuona huyo jamaa wa TRA akija hapa jioni na kuondoka naye.Lakini mara nyingine alikuwa akimwachia hela ya teksi na yeye kumfuata,” alisema mmoja wa wasichana walio jirani na kilichokuwa chumba cha Beatha.

Hata hivyo, chanzo kimoja cha habari kimeliambia Uwazi kuwa,Beatha (Marehemu) alianza kuwa na uhusiano na kigogo huyo baada ya kutokea mgogoro wa kimapenzi kati yake na Musiba.

Kimezidi kueleza kuwa, mgogoro huo ulisababishwa na Beatha kutoa kauli ya mwisho kwa mpenzi wake Musiba (mtuhumiwa) ikimtaka aache mara moja tabia ya ulevi na uvutaji bangi kupindukia aliyokuwa nayo ambapo mtuhumiwa alikubali kubadilika na kuahidi kutorudia tena ingawa siku chache baadaye alirejea katika tabia hiyo chafu hali iliyomuudhi Beatha na kusisitiza kuachana naye.

Habari zaidi zinasema kuwa, mtuhumiwa alikua akihisi vibaya pale Beatha alipoendeleza azma ya kusitisha penzi lao, hali iliyomfanya kuwa katika majaribu ya kujiua kwa kujitupa kutoka ghorofani kwenye Hosteli za Mabibo mara kwa mara ingawa ilishindikana baada ya kuokolewa na wanafunzi wenzake.

Baadhi ya waliokuwa marafiki wa marehemu enzi za uhai wake waliohojiwa na gazeti hili walisema kwamba, uhusiano baina ya wawili hao ulianza zamani ingawa hata hivyo matumizi ya vilevi halali na haramu yalikuwa yakitia doa raha ya penzi lao na ilifikia hatua ya Beatha kumpa muda wa kujirekebisha mpenzi wake huyo vinginevyo angesitisha mapezi.

Waliendelea kusema, baada ya Musiba (mtuhumiwa) kushindwa kutumia muda huo kujirekebisha, Beatha aliamua kuchukua maamuzi magumu ambayo yalihitimisha penzi lao na yeye kuhamisha mapenzi yake kwa kigogo huyo wa TRA ambaye imeelezwa kwamba anafedha ‘chafu’ zilizokuwa zikimpa kiburi marehemu.

Katika kile kinachoonesha kuwa kigogo huyo wa TRA alikolea kwa penzi la Beatha, hivi karibuni alichukua likizo kazini kwake iliyompa wasaa wa kujivinjari mara kwa mara hivyo kuzidi kulifanya jina la Masamba kufutika kwenye mawazo ya Beatha kitendo kilichomkera na kuchukua uamuzi wa kinyama.

Mmoja wa Wanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha DUCE (hakutaka jina liandikwe) ambaye alidai kuwa rafiki wa Masamba, ameliambia Uwazi kuwa, migogoro baina ya wawili hao ilichukua sehemu kubwa ya muda wao wa masomo hali iliyosababisha warudi nyuma kitaaluma.

Musiba anakabiliwa na tuhuma ya kumuua mpenzi wake, Beatha kwa kumshambulia kwa kisu hivi karibuni nje ya chumba chake namba C 250 kilichoko Block C katika Hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mbapo kifo kilimpata wakati akikimbizwa hospitalini.

Kwa sasa mtuhumiwa amefunguliwa kesi ya mauaji iliyosomwa wiki iliyopita katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.


 (Votes #: 11)
    (16 June 2009)
Soma Zaidi: 5674 | Maoni Yako (16)

Udaku Mwingine

uwazi
 
  • Denti aliyeuawa chuo kikuu, yadaiwa Chanzo ni simu
  • MWANAFUNZI CHUO KIKUU ALIVYOUAWA
  • NINI KIFANYIKE?
  • Inasikitisha
  • Kijana auawa akigombea demu
  •    

    #1 Author: inye (16 June 2009 01:57)

    kwahiyo sie tufanyeje? huyo kaka wa TRA hakuingilia penzi bali marehemu alishamuonya huyo muuaji... mie sioni cha kushangaza hapo.

    Poleni wafiwa.. sheria ichukue mkondo wake
     
    fast    

    #2 Author: mabomba (16 June 2009 04:24)

    Naomba muache kumtoa huyu dada kwani mnatuzidishia uchungu wafiwa, Na huu sio muda wakuanza kusema alifanya nini kibaya na walasio muda wakudiscuss alikuwa na mabwana wangapi..Kilichobaki tumuombee alale mahali pema peponi,, Amina.
     
    fast    

    #3 Author: lieutenant2003 (16 June 2009 06:28)

    Dont use your money and your time to find girls/women, instead use your time to find money and girls/women will find you automatically.
    We ukiwa na Hela hata uvute bangi to infinite wala asingekuacha. Hizo nguvu ulizotumia kumuua marehemu ni sawa na nguvu alizotumia mwenzako wa TRA kutafuta hela, aafu marehemu akam'find'automaticaly.
    Wewe unafaa unyongwe mpaka ufe. Kwani demu ni huyo mmoja tuu?, au unafikiri we ndio a kwanza kuachwa?, watu walisomesha na wakaachwa lakini hawakuua. Demu uliyenay level moja ukishafika nae mabibo sio wako tena, kwanini hutaki kukubali? Ndugu yangu watu walishamwagwa hadharani na maneno mazito kama vile;- 'u r not of my type',
    'our families dont match', I need a graet man & r not a great man' na maneno mengi ya dharau. Uliza sasa hivi wako wapi na maneno yao, wanaishia kusema ningejua, wakikuona wanakuomba na lift. Nyie akina musiba be a man and dont let your hasira tawala wewe.
    NB
    Unyongwe mpaka ufe.
     
    fast    

    #4 Author: maua (16 June 2009 06:50)

    Mabomba pole sana ukishakufa kifo ambacho si cha kawaida tayari wewe ni maarufu no matter ulikuwa nani ? hata mimi nilikuwa na hamu sana uya kujua chanzo cha kifo cha huyo Dada maana ameniuma kama Mdogo wangu wa kuzaliwa tumbo moja hivyo nataka kukwambia mengi sana yataandikwa wala usijali ni jambo la kawaida sana

    Mungu amurehemu na amlaze mahali pema peponi Amina..

    Wooote tutafuata tu tatizo staili ya kuondokea
     
    fast    

    #5 Author: JIWE (16 June 2009 07:21)

    i think this serves as an example to both men and women that we should not take/make decision as we are mad.i either laud musiba nor beartha but what i am trying to say is,take your time to think before making a step,not only that but also,you students have to focus on your future instead of squandering your time doing unsensible things.biblia inasema msiyachokoze mapenzi,ushauri wa bure.
     
    fast    

    #6 Author: upende (16 June 2009 07:32)

    mtazamo wangu ni kwamba huu ni wakati mzuri sana kujifunza na kubadilika maana matatizo ya namna hiyo ,bado yapo katika maisha ya watu.
    bangi zinavutwa sana, zinaa kwa sana,uongo kwa sana na habari za Mungu bado hatuzipi uzito wa kutosha.We learn through others mistakes
     
    fast    

    #7 Author: kimavi (16 June 2009 07:39)

    huyo bwana muuaji alishaonywa ajirekebishe na marehemu akakaidi, akaamua kuendelea na mtu aliyestaarabika kigogo wa TRA hapo sijaona kosa lake ni mawivu tu ya kijinga.

    heheee atachemka mura unakuja na jembe mujini utarima rami?
     
    fast    

    #8 Author: azzle (16 June 2009 10:49)

    labda tufikirie hivi: ok tabia ni kama ngozi kuiacha inataka muda na nafasi, ok umemuacha men wako au gel wako, vip 1.unajichunga naye kwa lolote baya,kumbuka binadamu kukuchekea siyo kufurahi nawe, 2.unamringishia kwamba unamwingine bomba zaid anayeweza kuja hadi kukuchukua na kukupeleka popote unapotaka.ulifikiria hatua kama hiyo itamuuzi au laa ikilinganishwa ''kiwango cha mapenzi yenu'' jichukulie ni wewe men au dem kakupiga chini then anajipitisha na mwaume mwingine ili umuone ingekuaje.
    3. kwani hali kama hiyo ya kutoswa ilianza kwako tuu wako wengi walizaa hata watoto wametengana,



    ushauri wangu mimi: mlioachana muwe makini sana kwa kila mmoja wenu, musioneshane kwamba mmoja wenu hakufaa hata kidogo ndo maana mmeachana, mifanyiane mambo yatayomuudhi mmoja wenu.


    mapenzi daa
     
    fast    

    #9 Author: MARK.MUSHI WA ITALY (16 June 2009 14:56)

    BADO NIKO HEWANI ATA MKINIPONDA VIPI,MIMI BADO NAULIZA HIVI-ENDAPO YULE ALIYEBAKA KAFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA JE SASA UYU ANAYEUWA ATACHUKULIWA ADHABU GANI 10YEARS ALAFU ATATOKA?KAMA NIIVYO MNANICHEKESHA SANA,SIJUWI SHERIA ZA UKO BONGO ZINASEMAJE LAKINI ZA APA ITALY UKIUWA KWA KUKUSUDIA YANI KWA MAKUSUDI KAMA ALIVYOFANYA MUSIBA-BASI UTAFUNGWA MIAKA30KISHA UTATOKALAKINI UMEUWA KWA BAATI MBAYA BILA KUKUSUDIA BASI UTAFUNGWA KWA MIAKA 10AU15KWISHA MCHEZO UMETOKA,ALIYEBAKA NI MIAKA15AU20JELA,WE MISS YOU PAPI KOCHA MTOTO WA MFALIME,NINA MAWAZO YA KUFUNGUA KITUO CHA KUSAIDIA YATIMA UKO BONGO,SIYO KUWALEA TU ATA WAPATE ELIMU BORA NA MAITAJI MUHIMU KAMA KUNA MTU MWENYE MAWAZO KAMA YANGU ANIANDIKIE,CHELSEAFORTE1@YAHOO.IT,AU ANIPIGIE,+393336989592,MTAFUTAJI MARK IN ITALY,YULE ALIYENIANDIKIA KUWA NIMTUMIE EURO3000ASINIANDIKIE TENA UYO NI TAPELI,WAZO LA LEO UKIWA NA MTOTO MMOJA ONGEZA MWINGINE,CIAO,
     
    fast    

    #10 Author: Bob Sambeke (16 June 2009 20:28)

    Hi All,

    Mbana BC hamuellewi? Kipi ndo Chanzo cha Kifo cha Bertha mwarabu? Mwanzo Mmesema Ni Simu Ya Mkononi ,Leo Mnasema Chanzo Ni Bosi Wa TRA,Tuamini Lipi? Kuweni Makini Na Taaluma Yenu,co wote wanaopitia site yenu ni Kinamaimuna Kuna wengine wanaupeo mkubwa!

    Bob Sambeke!
     
    fast    

    #11 Author: mpiluka (17 June 2009 14:51)

    POLENI SANA WAFIWA.YAANI MARK MUSHI COMMENT ZAKO NI PUMBA,WE NI BONGE LA MSHAMBA JAPO SIKUFAHAMU UNAANDIKA MAMBO AMBAYO HATA HAYAHUSIANI NA MADA,HEBU OMBA USHAURI WAKATI UNAANDIKA ILI UREKEBISHWE,WATU WOTE HAWAWEZI KUKUCHUKIA NA KUKUSEMA BURE YAANI UNABOA KICHIZI YAANI USIVYOJIAMINI NA UTANZANIA MPAKA UMEONA UJIBANDIKIZE KWAMBA UPO ITALIA,MAMBO YA HIVYO YAMEPITWA NA WAKATI HIZO NI NDOTO ZA MCHANA,UNAMDANGANYA NANI KWAMBA UPO ITALIA KAMA SI MWENYEWE
     
    fast    

    #12 Author: Nyeura (18 June 2009 06:35)

    adhabu ya musiba sio kifo mie naona adhabu yake ahasiwe kama makisai bila ganzi na hukumu miaka 30 kama atakua bado yuko hai.over
     
    fast    

    #13 Author: akiba (19 June 2009 10:21)

    Ni mawivu tu hayo,ok,hakuna pametulia tu hapo.
     
    fast    

    #14 Author: MZEE (23 June 2009 04:39)

    POLENI WAFIWA,...SI KILA KIFO KINATOKANA NA MAPENZI YA MUNGU,...LAKINI SASA TUSEME NINI....KWA KUJIFARIJI TUSEME TU...SIKU ZAKE ZILIKUWA ZIMEFIKA.....MUNGU AWAFARIJI WAFIWA.....
     
    fast    

    #15 Author: easy (24 June 2009 03:19)

    mpiluka nimekupata yaani huyo charlie anani -bore mpaka basi, yaani yeye kuishi Italy ni kama ameshafika peponi!kwanza hata vimaandishi vyake anavyotumia utajua nia kashamba fulani hivi!huyu si mchagga,anatumia hilo jina tu, wachagga hawana muda mchafu kama huo wa ku ji proud all of the time,,,,Mark will you stop blabbering,your sentiment is always irk me!your type of clueless life you'r living in Italy make you to belabor the name every time on you'r sentiments, am fed up for your evangelizing, will you find a college to back up your mind instead of the crappy job u'r doing there?
     
    fast    

    #16 Author: hongera (5 July 2009 23:32)

    siyo poa hata kidogo
     
    fast    

    Add comments

    Name:
    E-mail:

    Code:
    Include security image CAPCHA.
    to renew the code
    Enter Code:

     

    Kura Yako / Poll

    Habari Katika Picha


    Author: admin


    Gazeti la Uwazi



    Nani Yupo / Alikuwepo


    Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

     hit counter

    counters

    2008 © globalpublisherstz.com