
Imedaiwa kuwa, kigogo huyo amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo na kwamba, licha ya wafanyakazi wengine kugundua na kushangaa, bado mhesimiwa huyo hakuona sababu ya kuukatisha, bali penzi lao lilizidi kunoga na kushamiri.
Habari zaidi za kiudaku zinadai kuwa, mzito huyo mbali na kubanjuka na ‘stafu’ wake huyo pia ni mume wa mtu na mkewe alishautilia wasi wasi uhusiano huo haramu.
Kabla ya picha hizo kunaswa, inadaiwa siku moja wawili hao walipanga chumba kwenye hoteli moja ya kisasa kisha kula bata ndani ya chumba hicho huku wakifurahia uhusiano wao wa siri.
Habari za ndani zinazidi kudai kuwa, wakiwa katika ‘malavu’ walianza ‘kufotoana’ picha kwa zamu kwa kutumia kamera ya simu ya mkononi lakini utunzaji wao ukawa mbaya kiasi cha kuzifanya picha hizo kuvuja na kuwafikia wadaku.
Miongoni mwa watu waliofikiwa na picha hizo ambazo nyingine hazitazamiki, inadaiwa ni mabosi wenzake mnene huyo, wakiwemo pia ‘mastafu’ wa chini ambao walipigwa butwaa.
Katika kuonesha kuwa, kampuni hiyo ‘haifugi’ ujinga kama huo, mhesimiwa huyo alilazimishwa ‘kuchora’ barua ya kuacha kazi katika kipindi cha saa ishirini na nne na hivi sasa yuko ‘benchi.’
Hata hivyo, Amani lilifika makao makuu ya kampuni inayodaiwa kuwa ndiyo kigogo huyo alikuwa akifanyia kazi ambapo baadhi ya ‘stafu’ walikiri kusambazwa na kuziona picha hizo chafu, lakini bila kukubali au kukataa kama wanamfahamu mthumiwa huyo.
