Tembelea... |
 |
Kalenda |
 |

Marafiki wetu |
 |
Habari Zilizopita |
 |



|
|
 |
|
|
 |
 |
JOYCE KIRIA: Nimekula uroda na wanaume wengi sana!
|
ijumaa |
|
 |
TQ: Nipo hapa kwa niaba ya wasomaji wa gazeti la Ijumaa ambao wanataka kujua maisha yako ndani na nje ya kazi. Bila kupoteza muda anza kwa kutueleza ni kitu gani hasa kilikufanya ukaamua kuingia katika fani ya utangazaji hasa ya kuchambua filamu za kibongo?
Joyce: (Akiwa makini) Napenda sanaa ya maigizo, lakini kila kukicha matatizo yamekuwa hayaishi kwenye filamu zetu, nikaona ni bora niingie niweze kuwakosoa na kuwapongeza waliofanya vizuri kama njia ya kuikuza. TQ: Kazi yako ya utangazaji umewahi kuifanya nje ya Bongo?
Joyce: Zaidi ya Clouds Fm, Channel Ten na sasa EATV, sijavuka mipaka ya nchi yetu ingawa ni moja ya ndoto zangu za baadaye. TQ: Nini mafanikio yako katika kazi yako?
Joyce: Mafanikio yapo ingawa siyo ya moja kwa moja. Kubwa zaidi ni kufahamiana na watu wa nyanja mbalimbali. TQ: Unaweza kukumbuka idadi ya wanaume uliokuwa nao kabla ya kukutana na mumeo Dj Nelly?
Joyce: (Huku akicheka) Hapa lazima niseme ukweli...sikumbuki idadi kamili maana nimetembea na wanaume wengi sana! Uzuri wangu ndiyo unaowachanganya kwahiyo nikajikuta nikiwa na wanaume wengi sana, lakini baada ya kukutana na toto la Kihaya, Nelson Nkongo (Dj Nelly) nimetulia kwa raha zangu, maana ananipa kila ninachokihitaji.
TQ: Mh! Hujatulia wewe, enhee nini kilisababisha ukachaana na wapenzi wako wa nyuma? Joyce: Unajua mimi nilikuwa natafuta mume wa kuishi naye, kwahiyo kila nilipogundua mtu ana nia ya kunitumia, niliachana naye haraka sana, ndiyo sababu nikawa na wanaume wengi.
TQ: Sasa wanaume wote hao jamani, hukukanyaga miwaya kweli? Joyce: Nilikuwa makini sana, mara zote nilikuwa nikitumia kinga. Hata hivyo niliwahi kupima na kukuta nipo poa.
TQ: Unataka kuniambia baada ya kukutana na Dj Nelly mlipima? Joyce: Kwakweli hapana, lakini najiamini maana sijawahi kutoka nje ya penzi letu, na hata yeye namuamini pia.
TQ: Kuna nyepesi zinasema kwamba, Dj Nelly alikuwa mume wa mtu na wewe uliingilia ndoa ya watu. Hilo unalizungumziaje? Joyce: Hakuwa mume wa mtu bali alikuwa akiishi na mwanamke, lakini baada ya kuridhika na mimi ndiyo akaamua kunichukua jumla kwa ndoa halali ya Kanisani.
TQ: Sasa naomba kukuuliza swali la chumbani zaidi. Ni kitu gani ukifanyiwa na mpenzi wako faragha unajisikia raha zaidi? Joyce: Mi’ napagawa zaidi na romance, hapo tu, ndipo panaponiacha hoi mtoto wa kike.
TQ: Halafu kuna tetesi mjini kwamba huo weupe wako ni wa dukani, nikimaanisha kwamba unajichubua. Hiyo nayo imekaaje? Joyce: Naona maswali yamekuishia sasa...kifupi weupe wangu ni wa asili, kwaheri bro!
|
|
 |
|
|
 |
Kura Yako / Poll |
 |
Habari Katika Picha |
|
 |

Nani Yupo / Alikuwepo |
 |
|