arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » uwazi » WAUAWA KIKATILI!

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» The Spring of Sadness! ...
» DAR HOI MISS TZ ‘08’
» ZIARA YA MBANGU NA FRAN ...
» Jalada la E.P.A
» SHOGA WA KIJAPANI ANASW ...
» The assassination -72
» Miss Tanzania kesho kut ...

WAUAWA KIKATILI!

uwazi

usafiri huo umekuwa wa mashaka, usiyo wa uhakika zaidi na wenye kutatanisha si kwa abiria tu ambao wengi wao wamejikuta wakiutegemea kutokana na unafuu wake pia uwezo wa kupenya maeneo yasiyo na barabara imara bali pia madereva ambao wamekuwa wakichinjwa na kunyongwa na baadhi ya wakodishaji kisha kupokwa mali na pikipiki zao.

Moja ya matukio makubwa yaliyotokea hivi karibuni, ni lile la maeneo ya Mbezi wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo madereva wawili wa pikipiki, Jimmy Shirima na Deo Mushi, waliuawa kikatili na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Taarifa zilizopatikana katika eneo la tukio zilieleza kwamba, madereva hao waliingia katika mtego wa majambazi hayo baada ya kuwakodisha huku wakijifanya ni abiria wema na walipofika katika eneo liitwalo Mbezi Muhimbili, sehemu iliyoandaliwa kwa mauaji, madereva hao walielezwa wasimame kwa madai kwamba walishafika lakini ghafla, walishtukia wakikamatwa kisha kuanza kupigwa kwa magongo hadi kufa.

WAUAWA KIKATILI!
Huyu ameuawa

Waandishi wetu walishuhudia nyasi katika eneo hilo zikiwa zimevurugwa na inasemekana kwamba marehemu kabla ya kuuawa walikuwa wakijaribu kujinasua toka mikononi mwa majambazi hayo bila mafanikio kabla ya kuzidiwa nguvu na hatimaye kuuawa kisha pikipiki zao kuchukuliwa.

Mwenyekiti wa madereva wa pikipiki, wa maeneo ya Mbezi Shule, James John Mrema, alisema kwamba, vifo vya vijana hao vimewasikitisha sana na hali hiyo inawajengea hofu kubwa juu ya usalama wao.


Aliendelea kusema kwamba, tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Juni 16, mwaka huu ni la kipekee na endapo wahusika hao ambao kwa sasa wanaonekana kujipanga vilivyo hawatakamatwa na kudhibitiwa, hali ya usalama katika eneo hilo itaendelea kuwa tete hivyo kujenga uwezekano wa huduma hiyo tegemeo kwa wakazi wa Dar es Salaam, kuyumba sana.

Alieleza kuwa, maiti za madereva hao zilionwa na mwenzao majira ya alfajiri wakati akiwa katika shughuli za kusafirisha abiria ambapo mwili wa Shirima ulikutwa hatua sita toka ulikokutwa ule wa Mushi huku damu zilizotokana na majeraha zikiwa zimetapakaa katika eneo hilo.

“Baada ya dereva huyo kuona miili hiyo, aliita majirani na madereva wa pikipiki ambao waliwataarifu polisi waliofika muda mfupi baadaye na kuipeleka miili katika Hospitali ya Tumbi huku wakiahidi kuendelea na uchunguzi,” alisema Mrema.

WAUAWA KIKATILI!
Huyu ameuawa

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa, tangu usafiri huo uhalalishwe kumekuwa na mfululizo wa matukio ya mauaji ya kikatili dhidi ya madereva na kuongeza kuwa, hivi karibuni, mwenzao aitwaye Masudi Mohamed (35) alishambuliwa vikali na majambazi yaliyojifanya abiria kabla ya kufariki kutokana na kuvuja damu nyingi kwenye majeraha akiwa Hospitali ya Tumbi.

Katika kile kinachoonesha kuwa pikipiki ni ‘kaburi’ la madereva hawa, Uwazi likiwa bado limepiga kambi eneo la tukio, lilipata taarifa za kuchinjwa kisha kuchomwa na kitu chenye ncha kali dereva wa pikipiki aitwaye Ramadhan Kusena (24) katika eneo la Mbezi King’ong’o, saa 1.15 jioni usiku wa kuamkia jana (Jumatatu) ambaye kama ilivyokuwa kwa wenzake, alikuwa amekodiwa.

Uchunguzi zaidi uliofanywa na Uwazi katika maeneo mbalimbali jijini hasa yale ya Makumbusho, Mwenge, Sinza Africa Sana, Kunduchi na Msasani na mikoa ya Kanda ya Ziwa ambako usafiri huu ni tegemeo, umebaini kuwa, matukio kama hayo hutokea mara kwa mara, hali ambayo inafanya usafiri huo uwe wa hofu tupu.

Aidha, aina ya uendeshaji wa baadhi ya madereva imekuwa ikisababisha ajali ambapo takwimu zilizopo zinaonesha kwamba, ajali zinazosababishwa na pikipiki zimeongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita.

WAUAWA KIKATILI!
Huyu ameuawa

Kinachosababisha ajali hizo ambazo zimekuwa zikiua na kujeruhi raia (kama baadhi yao wanavyoonekana pichani ukurasa wa mbele) ni pamoja na kugongwa kwa pikipiki hizo na magari zinapokuwa barabarani, uendeshaji usiofuata taratibu hasa wa bila kuvaa ‘helmet’ kichwani, uwepo wa madereva wasiokuwa na leseni na sababu zingine nyingi.

Gazeti hili limebaini kwamba, Bajaj na pikipiki zimekuwa zikiibwa na kwenda kuuzwa kwa bei za juu katika mikoa mbalimbali nchini na kuna taarifa za uhakika kwamba injini za pikipiki hizi zimekuwa zikitumika kuendesha boti za uvuvi katika maeneo ya wavuvi kutokana na kuwa na nguvu kubwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbezi (OCD), Bw. Ndaki alitoa amri kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi kusimamia kikamilifu na kutunga sheria ndogondogo zitakazoweka muda maalum wa biashara hiyo kufanyika.


 (Votes #: 10)
    (23 June 2009)
Soma Zaidi: 2422 | Maoni Yako (9)

Udaku Mwingine

uwazi
 
  • NINI KIFANYIKE?
  • Tukio la ujambazi Dodoma wamo madereva taksi
  • Mauaji makubwa ya kutisha Dar
  • Mwendesha pikipiki anusurika katika ajali
  • MADEREVA WA MABASI TANZANIA WAGOMA
  •    

    #1 Author: RABY (23 June 2009 01:41)

    mmmmmmmmhhhh
     
    fast    

    #2 Author: MARK.MUSHI WA ITALY (23 June 2009 02:40)

    KWA KWELI VIFO VYAO VIMENIUMA SANA SINA ZAIDI YA KUSEMA,ILA NAOMBA MNIPATIE NAMBA YA NDUGU ZA MAREHEMU DEO MUSHI ILI NIWEZE KUTUMA MCHANGO WANGU WA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA AU UKOO WA DEO MUSHI,BWANA AMETOWA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIABUDIWE MILELE,NA MWANGA WA MILELE UWAANGAZIE MILELE,KWA BWANA YESU KILA GOTI LITAPIGWA-BWANA NDIYO MCHUNGAJI WETU...MUNGU AIBARIKI FAMILIA YA MUSHI,WENU MARK MUSHI AKIWA ITALY,
     
    fast    

    #3 Author: sauda (23 June 2009 07:55)

    ok poleni sana
     
    fast    

    #4 Author: mimi (23 June 2009 09:31)

    jamani mngetuwekea na hiyoo habari ya huyo jamaa wa zeutamu plzz,tunataka sana kujua imekuwaje,ila tunaona heading tu huku kwa mtandao hamna habari zake plzzzzz
     
    fast    

    #5 Author: kisimilu (23 June 2009 21:25)

    Naona Tanzania wanunue mashine za uchunguzi kama nchi nyingine duniani zinavyofanya, katika nchinyingine wakisema wanaendelea na uchunguzi inakuwa kweli,sio utani na wanamkamata mhalifu.

    sisi tutaisha kwa kuwa hawakamatwi hata siku moja, naona wanamwaga dawa inang'arisha sehemu alizopita na wanachunguza hadi kiatu cha aliyekanyaga pale na anapatikana hadi nyumbani kwake, wawa ulize wamarekani/ waingereza na nchi nyingine wanafanya nini kuwakamata wauwaji, kulikoni kununua rada isiyo na kazi.
     
    fast    

    #6 Author: nicole (23 June 2009 22:23)

    kusema kweli Mark una upendeleo,mbona hujaomba anwan ya Jimmy Shirima nae si ni mchaga mwenzako?au kwa vile Deo jina lake la pili ni kama lako,acha ubaguzi tuma na kwa kina Shirima.au ungetuma kwa wote waliouwawa.
     
    fast    

    #7 Author: hery (26 June 2009 03:16)

    very sorry!
     
    fast    

    #8 Author: john (26 June 2009 11:48)

    Tanzania ime2chosha na amani nipora ya kuwa kama rwanda kwani hakuna tofauti ya rwanda mauaji kama hayo si mchezo nimeumia sana kwa upande wangu Mungu warehemu
     
    fast    

    #9 Author: Gachson (20 July 2009 08:47)

    Mwenyezi mungu azilaze roho zao pema peponi. Amina
     
    fast    

    Add comments

    Name:
    E-mail:

    Code:
    Include security image CAPCHA.
    to renew the code
    Enter Code:

     

    Kura Yako / Poll

    Habari Katika Picha


    Gazeti la Uwazi


    Nani Yupo / Alikuwepo


    Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

     hit counter

    counters

    2008 © globalpublisherstz.com