Tafadhali wajulishe wote wanaohusika kwamba kuna kundi kubwa la majambazi wenye silaha kali, ambao wameingia Jijini Dar es salaam hivi karibuni. Wahalifu hao ni pamoja na Wakenya ambao wana tabia ya kupora fedha katika taasisi kubwa kama,mabenk,kampuni za mafuta na sehemu zenye biashara kubwa n.k .
Aidha watu hawa wana mbinu ya kula njama na watumishi wasiokuwa waaminifu.Ni muhimu mkafuatilia mienendo mbalimbali katika benk zenu na sehemu zilizotajwa hapo juu pamoja na kuimarisha usalama julisheni kwa message kupitia namba hii
0783034224 . au kwa simu ya mdomo
0754-034224 . 0787034224 .
zote ni namba za Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam. Namba zingine za simu ni
0754- 276217 0776880000
namba hizi ni za mkuu wa Upelelezi Kanda maalum. Lengo la maelezo si vitisho kwenu bali ni tahadhari muhimu , inayofaa kuzingatiwa, S. H. Kova - SACP KAMANDA WA KANDA MAALUM DAR ES SALAAM
Kufuatia uhalifu uliofanywa na majambazi katika Benki ya NMB tawi la Temeke, imebaki stori kwa jinsi wanaume hao walivyofanya kitu ambacho hakitasahaulika kwa staili waliyotumia kuingia wakiwa wamevalia hijabu pamoja na wigi kichwani na kufanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali.
WAMECHUKUA ZAIDI YA MILIONI (150)
Meneja wa Benki ya NMB, Shy-rose Bhanji (kushoto) akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo la ujambazi lilivyotokea na kusema kiasi cha pesa kilichochukuliwa hakijafahamika ila ni zaidi ya shilingi milioni 150 za kitanzania. Majambazi hayo yanadaiwa yalitumia gari aina ya Prado lililokuwa na namba za Serikali STK.
SIJUI KAMA LEO NITAPATA USINGIZI
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (Kulia) akiteta jambo na ‘Bodigadi’ wake huku akionyesha kukerwa na uvamizi huo uliosababisha kifo cha askari mmoja wa Kampuni ya Moku Security Servises Ltd na kujeruhi watu 13 wakiwemo askari polisi wawili na kisha majambazi hayo kutokomea zao na kitita cha pesa.
SIJAWAHI KUONA
Mmoja wa waliojeruhiwa na majambazi hayo, akielezea jinsi mkasa ulivyompata wakati alipokuwa ndani ya benki hiyo akichukua vijisenti vyake na kusema hajawahi kuona jinsi majambazi wanavyofunga mtaa.
HII ILIKUWA BAB KUBWA HADI WAZIRI NDANI!
Gari la Waziri wa Mambo ya Ndani likiwa nje ya Jengo la Benki ya NMB Temeke dakika chache baada ya majambazi hayo kufanya uhalifu huo na kutimka zao.
WANATISHA!
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, wakijadiliana mambo kadha wa kadha jinsi gani majambazi hayo yalivyofunga mtaa wa Sterio na Temeke huku wawili waliokuwa na jinsia ya kike wakitamba nje ya geti walikokuwa wameegesha gari lao lililokuwa katika ‘sailensa’ tayari kwa kuondoka mara baada ya kukamilisha kazi yao.
JAMANI UTAFIKIRI KACHINJWA NG’OMBE!
Damu ikiwa imetapakaa baada ya majambazi yaliyovamia benki hiyo kuwamiminia risasi maaskari waliokuwa wakilinda benki hiyo na kusababisha kifo cha Askari wa Kampuni ya Moku Security Sevirces Ltd ya jijini Dar es Salaam ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja.
HAPA KAZI IPO
Baadhi ya makamanda wa polisi wakijaribu kubadilishana mawazo kukabiliana na majambazi hayo ambayo yalitokomea baada ya kufanikiwa kupora mamilioni hayo ya fedha na kutokomea maeneo ya Tandika, wakijaribu kutafuta njia mbadala ya kuweza kuyanasa majambazi hayo popote pale.
MASKINI MGONJWA HUYU WA KIFAFA!
Mkazi wa jijini akiwa ameanguka chini katika maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kudaiwa kuwa alianguka kutokana na ugonjwa wa Kifafa unaomsumbua, hapa wanaonekana wasamaria wema wakimsaidia lakini hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja kama walikuwa wote au la maana walionekana kutoa msaada wa karibu zaidi.
SASA AMEPATA AHUENI
Mkazi huyo wa jijini aliyeanguka kwa Kifafa akinyanyuliwa na wasamaria wema baada ya kupata ahueni ambapo aliweza kunyanyuka kwa kushikwa mkono na kukaa kitako.
Kesi ya matumizi mabaya ya ofisi inayowakabili mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Grey Mgonja, ambayo inaunguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo iliingia hatua mpya baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha mbele ya kiongozi wa jopo la mahakimu wanaoendesha kesi hiyo, John Utamwa, vielelezo mbalimbali vinavyodaiwa kuonesha makosa yalivyotendwa na washtakiwa. Mpaka tunaelekea mitamboni vielelezo zaidi ya sita vilikuwa havina pingamizi mbele ya mawakili wa utetezi ambao walikuwa na kazi ngumu ya kuvihakiki kabla ya kuviruhusu kuwasilishwa mbele ya jopo la mahakimu watatu wanaoendesha kesi hiyo ili viweze kutumiwa na mahakama hiyo.
NGOMA NZITO! Mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Basil Mramba (kulia) na Daniel Yona wakiteta jambo kabla ya kesi yao kuanza kusikilizwa. Kushoto ni mshitakiwa wa tatu, Grey Mgonja. PICHA:RICHARD BUKOS /GPL
Usiku wa kuamkia leo warembo wanaotarajiwa kushiriki kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Ilala 2009 walitoana jasho katika pambano la kuwatafuta warembo wenye vipaji (Miss Talent) lililofanyika Ukumbi wa Hotel ya Lamada jijini Dar es Salaam. Katika mchujo huo warembo watano walifanikiwa kushinda na hivyo kuiwakilisha Wilaya ya Ilala katika kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka huu.
Warembo walioshiriki kinyang'anyiro hicho wakipita kwa madaha mbele ya watazamaji (hawapo pichani).
Doris Jimmy, mmoja wa walimbwende hao, akionesha kipaji chake cha kuigiza.
Majaji wakiwa kazini katika kinyang’anyiro hicho. Kutoka kushoto ni Manka Mushi, Gerald Hando na Victor Rwehumbiza.
Hawa ndiyo warembo waliofanikiwa kuwa wawakilishi wa Miss Talent katika fainali za Miss Tanzania mwaka huu. Kutoka kushoto ni Zena Rashid, Silyvia Shao, Margaret Peter, Husna Mohamed na Doris Jimmy. PICHA:RICHARD BUKOS /GPL
Wasanii wanaocheza filamu ya 'Tears on Valentine' inayotarajiwa kutoka hivi karibuni, jana walitembelea ofisi za Kampuni ya Global Publishers watoaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Championi, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda na kujionea shughuli mbalimbali zinavyoendeshwa kwenye kampuni hiyo.
Wasanii hao pichani wakimsiliza mhariri wa Gazeti la Risasi, Oscar Ndauka (wa pili kulia), aliyekuwa akiwafahamisha kazi za Mhariri Msaidizi wa gazeti hilo, George Kayala (aliyekaa).
Hamida Hassani, (kulia) na Imelda Mtema, waliokaa, wakiwaonyesha wasanii hao jinsi wanavyotumia mtandao wa Internet katika kazi za kampuni hiyo.
Mhusika mkuu wa filamu hiyo Joanita (katikati) akiwa na Mzee Magali, ambaye ni Baba Joanita na Mama Joanita walioshiriki katika filamu hiyo.
Katika ziara hiyo wasanii hao walitembelea pia upande wa uchoraji katuni na kupata maelezo ya kina kutoka kwa mchoraji wa magazeti hayo, Aloyce James, aliyekaa. PICHA:RICHARD BUKOS /GPL
Staa wa TAKEU, Hamis Ramadhan a.k.a H-Baba yawezekana yupo katika kipindi kizuri kimapenzi, akila ‘goodtime’ na kimwana mpya, kamera za Ijumaa zinaweka kitu ‘laivu bila chenga’...
Mlimbwende wa Tanga, 2006, Chuchu Hans ambaye kwa sasa amejikita kwenye tasnia ya filamu, amekanusha vikali madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mshindi wa Pili wa Big Brother II, Mwisho Mwampamba...
Zoezi la kumsaka Miss Temeke 2009-2010 kwa njia ya gazeti limekamilika kwa mrembo namba 9 kushika nafasi ya kwanza, hivyo dalili zipo wazi kwamba kesho ndiye atavalishwa taji...
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Philipo Nyandindi a.k.a O-Ten ameibuka na kutoboa siri ya ‘kufulia kimuziki’ kuwa ni kutokana na majukumu ya kifamilia yaliyokuwa yanamkabili...
Aliyekuwa msanii wa kundi la Kidedea Professional Art, Anna Maiko maarufu kama ‘Sina’ amefariki dunia nyumbani kwao Kigogo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi...
Kimwana wa Manywele, Halima Harun ameibuka na kumlamba miguu Mtangazaji wa Kituo cha East Africa Radio na TV , Maimartha Jesse kuwa, bila kampuni yake asingeweza kuendesha gari maishani mwake...
Miss Ruvuma 2007, Neema Chande amefanyiwa unyama wa kutisha na mpangaji mwenzake ambaye pia hapo awali walikuwa marafiki kufuatia kumpiga na kitu chenye ncha kali jichoni na kumsababishia kuharibika kwa mimba...
Jengo la Mlimani City leo litakuwa ‘vere bize’ wakati ambapo shindano lenye nguvu kuelekea Miss Tanzania, Miss Kinondoni litakapokuwa linafikia tamati kwa mwaka huu wa 2009...
Niaje wadau wangu wa safu hii ya TQ? Naamini mko poa kabisa na bila kuwachosha, niwafahamishe tu kwamba, wiki hii nimeibukia pande za Tabata jijini Dar es Salaam na kukutana uso kwa uso na msanii wa filamu nchini ambaye pia ni mjasiriamali...
Dona au Christine Jackson kama anavyoitwa hivi sasa baada ya kubadilisha sura na hati yake ya kusafiria, ameshindwa kumuua Bahati ingawa wako ndani ya chumba pamoja na kisu chake kimefichwa chini ya mto! Unajua kilichofanya ashindwe kumuua ni nini? Utaalam wa Bahati katika masuala ya mapenzi, kijana ni mzuri, anaiweza kazi na tena kwa sababu ni miaka mingi hajakutana na mwanamke kimwili, amemkuna Dona mahali ambapo hakuwahi kukunwa kabla.
Dona amechanganyikiwa kabisa na kujikuta akiweweseka kwa kusema maneno mengi mbele ya Bahati huku akibubujikwa machozi, anasema wazi kuwa, kwa jinsi ambavyo Bahati amemfanyia, hakika ameahirisha mipango yote aliyokuwa nayo, hasemi mipango hiyo ni ipi pamoja na Bahati kumdadisi kwa kina.
Historia ya jambo hili ni kwamba, Dona ni mtoto wa marehemu James Ngalo na mke wake Rachel, wazazi ambao pamoja na Dana pacha wa Dona waliuawa kikatili kwa mkono wa mzee Ahmed Mwinyi, baba wa Bahati.
Dona aliyashuhudia mauaji hayo na baadaye kuamua kulipa kisasi kwa kuwaua wote walioshiriki kufanya unyama huo, akaanza na ASP John Lukiko, rafiki wa Ahmed Mwinyi ambaye alishirikiana naye kufanya mauaji hayo. Baada ya hapo akaanza kumsaka mzee Ahmed Mwinyi lakini kabla hajamuua mzee huyo akapata ajali mbaya ya gari na baadaye kufa.
Pamoja na kufa, hasira ya Dona haikwisha, akaihamishia kwa mtoto wake Bahati, akiamini kumuua huyu ingekuwa ni sawa na kumuua baba yake, mzee Ahmed Mwinyi, akamsaka kwa muda mrefu mpaka kufanikiwa kumwingiza Bahati chumbani, kabla hajamuua akakubali kufanya naye tendo la ndoa, hapo ndipo alipogundua kwamba kumbe chumbani hakuwa na mwanaume tu bali mwanaume mwenye PhD ya kufanya tendo hilo.
Mambo aliyoyafanyiwa akabaki akilia tu, hasira yote ikayeyuka! Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…