arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 01.07.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» T.I. atoka jela
» (Siri za Mapenzi) Waiju ...
» Msitu wa pande -24
» ZAWADI NI ZAWADI
» WANANCHI WAMFYEKA VIDOL ...
» HARDMAD: Nimeimba sana ...
» VITA dhidi ya Ufisadi; ...

 

MTAANI LEO

photos  
MTAANI LEO
Wazungu hawa hawakuona tabu kuburuza begi laola nguo na kukatiza mitaa ya jiji la Dar es salaam kama walivyonaswa na kamera yetu leo mitaa ya Sokoine.

MTAANI LEO
Kufuatia Tangazo la Halmashauri ya Jiji la Dar la kuwataka wamiliki wa majengo kulipia kodi ZA MAJENGO, hivi sasa kumekuwepo misululu mirefu katika ofisi za TRA, karibu kila tawi.

MTAANI LEO
..Manati mjini hutumika kuwindia nini? Kijana akipita kwenye rodi akijiuzia manati yake!

MTAANI LEO
Unaweza usiamini, lakini anayeingia ndani ya gari hii ni Mohamed Mpakanjia kama alivyokutwa na mpiga picha wetu mitaa ya Magomeni Mapipa alipokuwa akiongea na pedeshee mwenzie Papa Msofe.

PICHA: ISMAIL MANG'OLA/GPL

    (1 July 2009)
Views: 442 | Maoni (5) |

 

TOLLYWOOD TAYARI KWA USAILI

photos  
Kufuatia matangazo yaliyokuwa yakitolewa na kuchapishwa kwenye magazeti mbalimbali ya Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises yaliyohusiana na kuomba nafasi ya kushiriki kucheza filamu yaTears On Valentine Day, hatimaye usaili kwa ajili ya kuwapata wasanii watakaofaa kuigiza katika filamu hiyo umeanza katika ofisi za Tollywood zilizoko Sinza Bamaga, jijini Dar es Salaam. Katika usaili huo, waombaji kibao wamejitokeza kama wanavyoonekana pichani.

TOLLYWOOD TAYARI KWA USAILI
Wasanii wakiwa nje ya ofisi za Tollywood wakisubiri zamu yao kufanyiwa usaili.

TOLLYWOOD TAYARI KWA USAILI
Washiriki wakiwa ndani ya ofisi hizo kwa pamoja wakiteta jambo muda mfupi kabla ya kufanyiwa usaili.

TOLLYWOOD TAYARI KWA USAILI
Mratibu wa shughuli hiyo, Hammie Rajab na msaidizi wake, Deborah Sanga wakimfanyia usaili mshiriki
Picha zote:Musa Mateja/GPL
    (1 July 2009)
Views: 307 | Maoni (4) |

 

DANGURO

risasi mchanganyiko  
DANGURO
Issa Mnally na Dege Masoli, Tanga

Maafande wa Kituo Kikuu cha Polisi cha Chumbageni, jijini Tanga wakiwa ndani ya ‘Difenda’ walivamia Danguro ‘alwatani’ lijulikanalo kwa Jina la Majestiki na kuwanasa makahaba kadhaa, wakiwemo wake za watu ambao walikuwa wakiendesha biashara ya kuuza miili.
Tukio hilo la aibu ya karne, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika barabara ya 5 jijini hapa ambapo pia ilielezwa kuwa, jengo hilo lina baa kwa chini na vyumba vya kulala ghorofani...
    (1 July 2009)
Views: 1897 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Mainda awachana Thea, Riyama

risasi mchanganyiko  
Mainda awachana Thea, Riyama
Na Mwandishi Wetu

Msanii wa maigizo nchini, Mwanaid Suka ‘Mainda’ hivi karibuni, na yeye aliibuka na kukemea kwa nguvu zote, tabia ya wasanii kujiachia mwili kwa kula ‘maugali’ na hivyo kunenepeana...
    (1 July 2009)
Views: 1756 | Maoni (14) | Soma Zaidi

 

Mbilia Bell anaswa Bongo

risasi mchanganyiko  
Mbilia Bell anaswa Bongo
Na Musa Mateja

Mwanamuziki nyota wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbilia Bell amenaswa kwenye duka moja la vipodozi akinunua dawa zinazodaiwa huongeza ukubwa wa makalio ‘wowowo’ na matiti...
    (1 July 2009)
Views: 1623 | Maoni (12) | Soma Zaidi

 

Jahazi taarab yasambalatika

champion  
Jahazi taarab yasambalatika
Musa Mateja na Issa Mnally

Kundi la miondoko ya muziki wa mwambao, Jahazi Morden Taarab linadaiwa kusambaratika kutokana na kile kinachosemekana kuwa, ni kukithiri kwa majungu ambayo yamepelekea baadhi ya wasanii wake kutokuwa na uhuru kama ilivyo kwa makundi mengine...
    (1 July 2009)
Views: 950 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Msitu wa Pande-34

hadithi za Shigongo  
Kwa mauaji aliyoyafanya kama kisasi kufuatia mke na mtoto wake kuuawa kikatili, Jacob anajikuta akihukumiwa kifo na kupelekwa gerezani ambako miaka mingi baadaye alinusurika kunyongwa baada ya Rais kukisoma kitabu chake kiitwacho Give Me Another Chance, akiomba apewe muda wa kuishi sababu alikuwa amebadilika. Kitabu hiki alikiandika akiwa gerezani.

Pamoja na kunusurika kifo kisha kuhukumiwa kifungo cha maisha, hali ya Jacob imekuwa mbaya gerezani, anaugua ugonjwa wa kifua na homa kali lakini hataki kupewa matibabu zaidi ya maombi! Hali ilipokuwa mbaya zaidi ilibidi apelekwe hospitalini ambako daktari aliyempokea alitokea kuwa mmoja wa waumini wa Madhehebu yake ya Freedom for all International.
Je, atapona? Nini kinafuata? SONGA NAYO…
    (1 July 2009)
Views: 667 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Utaidhulumu nafsi yako mpaka lini?-2

Mahaba  
Ni Jumatano nyingine tena nikiwa mwenye furaha na afya tele, nipo katika uwanja wangu wa kujidai, Uwanja wa Huba. Nikukaribishe kwa moyo mkunjufu, nikiamini kwamba utajifunza kitu kipya katika mada hii...
    (1 July 2009)
Views: 260 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Sura ya mtu, roho ya shetani-4

Mikasa ya kusisimua  
Sueya anapewa mawazo ya kupelekwa kwa mtaalamu wa dawa za asili ili amdhuru wifi y ake. Je, atafanikiwa? ili kuyajua yote twende sassa...
    (1 July 2009)
Views: 9 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Sura ya mtu, roho ya shetani-4

Mikasa ya kusisimua  
Sueya anapewa mawazo ya kupelekwa kwa mtaalamu wa dawa za asili ili amdhuru wifi y ake. Je, atafanikiwa? ili kuyajua yote twende sassa...
    (1 July 2009)
Views: 901 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Kimanda acziba nafasi ya Cammavaro Yanga SC

champion  
Kimanda acziba nafasi ya Cammavaro Yanga SC
Julius Kihampa na Khadija Mngwai

KUSAINI kuichezea klabu ya Yanga kwa mchezaji Eric Kimanda raia wa Rwanda mwenye asili ya Jamhuri ya watu wa Congo, kumeibua faraja mpya kwa uongozi na wanachama wa timu hiyo hasa bada ya mlinzi wao wa kutumainiwa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuhitajika katika majaribio nchini Canada...
    (1 July 2009)
Views: 358 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Walioula Yanga, Simba

champion  
Na Julius Kihampa

WAKATI jana ilikuwa ni siku ya mwisho kwa klabu za Ligi Kuu hapa nchini kuwasilisha usajili wao katika ofisi za Shirikisho la Soka, TFF, wachezaji wapya wa timu 14 zitakazoshiriki ligi hiyo wanatarajiwa kuanikwa hii leo...
    (1 July 2009)
Views: 308 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Phiri atua Simba na wawili tu

champion  
Na Khadija Mngwai

Kocha mkuu wa Timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Patrick Phiri, anatarajia kuwasili leo nchini leo (Jumatano) akiwa na wachezaji wawili akitokea nyumbani kwake Zambia alikokuwa amekwenda kwa ajili ya mapumziko mafupi baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita...
    (1 July 2009)
Views: 275 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

The Painful demand (Hitaji lenye kuuma)

hadithi za Shigongo  
Kulikuwa na ukimya wa ajabu ndani ya chumba hicho chenye ukubwa wa mita za mraba hamsini, mwanga uliowaka ulikuwa ni wa chini sana lakini mtu yeyote asingeweza kusema kulikuwa na giza ndani ya chumba hicho, ilivyoonekana mwanga huo ulikuwa umepunguzwa makusudi ili kilichotarajiwa kutokea ndani ya chumba hicho kisiweze kuonekana na watu waliokuwa wakipita nje...
    (1 July 2009)
Views: 472 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Jalada la E.P.A -55

hadithi za Shigongo  
Baada ya Jimmy Master na Bernadetha kufa gerezani, Rais Adrian na mkewe Nandi aliyewahi kutolewa mfuko wa uzazi baada ya kutoa mimba, wanamchukua mtoto aitwaye Huruma, ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Bernadetha pamoja na Edward Lonjino ambaye yuko gerezani ambako yeye na rafiki yake Paul Kitumbi waliowahi kuwa mawaziri katika serikali ya nchi hiyo, wanasubiri siku ya kunyongwa kwao kufuatia mauaji na utesaji walioufanya.

Mtoto Huruma anakua akiwafahamu kama wazazi wake, lakini baadaye walimu wake wa shule ya msingi anaitoboa siri ya kila kitu kilichotokea na kwamba baba yake mzazi bado yu hai gerezani akisubiri siku ya kunyongwa! Maneno hayo ya mwalimu yanamtesa Huruma kwa muda mrefu, hapendi kuwauliza wazazi wake juu ya kilichotokea, anaogopa.

Juhudi za Rais Adrian na mkewe kumshawishi Huruma aseme kinachomsumbua zinashindwa kuleta mafanikio, mpaka miaka michache baadaye Huruma alipofanikiwa kuendelea na masomo yake ya kidato cha kwanza, hapo ndipo akaamua kumuuliza mzazi wake juu ya jambo alilolisikia akiwa mdogo.

Rais Adrian anashindwa kutoa jibu na kumfuata mkewe chumbani, wote wawili waliporudi sebuleni walijadiliana na kuamua kumwambia mtoto kilichokuwa kikiendelea ili afahamu ukweli, wakamsimulia kila kitu huku Huruma akibubujikwa na machozi ya uchungu sababu ya mateso ambayo Rais Adrian alipewa na Edward Lonjino na usaliti aliofanyiwa na mama yake Bernadetha! Mtoto akajikuta ana mapenzi makubwa na Adrian pamoja na Nandi kuliko Bernadetha na Edward Lonjino.

Baada ya hapo akapelekwa Afrika Kusini kuendelea na masomo yake ya sekondari katika shule ya Oliver Thambo Academy ambako watoto wengi wa matajiri na wanasiasa wakubwa walisoma, Huruma akapewa heshima ya mtoto wa Rais.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
    (1 July 2009)
Views: 663 | Maoni (5) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com