arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 04.07.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» BARUA KUTOKA KWA MAREHE ...
» Yanga yaua, Simba safi
» Shigongo kumvaa Rostam ...
» Nancy kuolewa na Msauzi
» Papic amtwika Mghana zi ...
» DIAMOND: AITEKA BONGO F ...
» Jeshi la Polisi, Tanesc ...

 

DESKTOP SASA NI Zoom Polytechinic

photos  
[center]Chuo maarufu cha kozi za ufundi wa kompyuta, graphics designing, utalii n.k, cha Desktop Computer Technology, leo kimezinduliwa rasmi kikijulikana kwa jina jipya la Zoom Polytechinic ambapo makao makuu yake sasa yatakuwa Magomeni Usalama, jijini Dar es salaam. Zamani kilikuwa na maskani yake kule KAMATA eneo la gerezani.

DESKTOP SASA NI Zoom Polytechinic
Mkurugenzi wa Chuo cha Zoom Polytechinic Bw. Gadius S. Shija (kushoto) akimuonyesha baadhi ya madarasa ya chuo hicho Makamau Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) Profesa Tory Mbwete, kabla ya uzinduzi wa chuo hicho uliofanyika chuoni hapo mapema Jumamosi

DESKTOP SASA NI Zoom Polytechinic
Profesa Mbwete akiwasisitizia wanafunzi wa chuo hicho kujitutumua kimasomo ili waweze kufika na kuonyesha uwezo wa hadi katika Chuo Kikuu cha Mlimani.

DESKTOP SASA NI Zoom Polytechinic
Hizi ni moja ya madarasa likiwa imesheheni Kompyuta za kujifundishia wanafunzi , kila darasa litakuwa na zaidi ya Kompyuta hamsini na tayari Chuo kina zaidi ya kompyuta 120.

DESKTOP SASA NI Zoom Polytechinic

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Zoom Polytechinic wakisikiliza kwa makini risala iliyokuwa ikisomwa na Profesa Mbwete aliyemuwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Shamsa Mwangunga.
PICHA ZOTE NA ISMAIL MANG’OLA / GPL.[/center]
    (4 July 2009)
Views: 156 | Maoni (2) |

 

MFUGO MTAANI!!

photos  
MFUGO MTAANI!!

MFUGO MTAANI!!
Tatizo la mifugo kuzurura mitaani katika jiji la Dar es salaam, bado linaendelea na limekuwa sugu, kama g'ombe hawa walivyokutwa wakiranda pembezoni mwa Barabara ya Mandela maeneo ya kituo cha mafuta cha MT MERU huki wakionekana hawana msimamizi. City Fathers mko wapi?
PICHA ZOTE NA ISMAIL MANG’OLA / GPL.
    (4 July 2009)
Views: 147 | Maoni (0) |

 

IFM KIDEDEA MISS HIGHER LEARNING

photos  
Chuo cha Usimamizi wa fedha cha IFM cha jijini Dar, kimeibuka kidedea katika Shindano la kumsaka mlimbwende wa Vyuo Vikuu nchini, Miss Higher Learning, baada ya Mwanafunzi wa chuo hicho, Betrice Lukindo, kutwaa taji hilo usiku wa kuamkia leo.
Wakati Betrice akibatizwa umalkia wa Vyuo Vikuu nchini, Linda Mzinga kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama amechukua nafasi ya pili na Doris Donatus kutoka Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) akiibuka mshindi wa tatu.
Kwa ushindi huo, Magreth amepata tiketi ya moja kwa moja ya kujiunga na Kambi ya Miss Tanzania msimu huu, tayari kwa kuwania taji la Miss Tanzania, 2009/10.
Shindano hilo lilifanyika ndani ya viunga vya Karimjee katikati ya jiji la Dar es Salaam, lililosababishwa kwa udhamini mkubwa wa Mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom, Global Publishers Ltd, Clouds FM, Ndege Insuarance, kinywaji cha Overmeer na wadhamini wengine kibao.

IFM  KIDEDEA MISS HIGHER LEARNING
Miss Vodacom Higher Learning 2009/10, Betrice Lukindo (katikati) akiwa katika picha ya pozi na mshindi wa pili, Linda Mzinga (kulia) na kushoto ni Doris Donatus, mshindi wa tatu.

IFM  KIDEDEA MISS HIGHER LEARNING
Hii ndiyo ilikuwa Top 5.

IFM  KIDEDEA MISS HIGHER LEARNING
Majaji, kutoka kushoto ni Miss Tanzania mwaka juzi , Jokate Mwegelo, Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga ‘Anko’ na Miss Tz mwaka jana, Nasreen Mohamed, wakiwa makini kutazama warembo (hawapo pichani).

IFM  KIDEDEA MISS HIGHER LEARNING
Warembo wakicheza staili ya Mugongo Mugongo jukwaani baada ya kupanda kwa mara ya kwanza.

IFM  KIDEDEA MISS HIGHER LEARNING
Kundi la sanaa la International Youth Ferowship, likikonga nyoyo za wadau wa urembo kwa ngoma ya kichina kabla ya mrembo kutangazwa.

IFM  KIDEDEA MISS HIGHER LEARNING
Wanenguaji wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ wakivamia jukwaa wakati wa shindano hilo.

IFM  KIDEDEA MISS HIGHER LEARNING
Nani amesema wanenguaji siyo masister Duu? Hawa mamiss ila ni wanenguaji wa Twanga wakiwa chobingo wakijipodoa kwa ‘Mapouda’

IFM  KIDEDEA MISS HIGHER LEARNING
Staa wa Kundi la ucheshi la Orijino Komed ‘Masanja Mkandamizaji” akiinama kukwepa kamera baada ya kubambwa ukumbini hapo akishuhudia mchuano mkali wa walimbwende hao.
PICHA:CHRISTOPHER LISSA/GPL
    (4 July 2009)
Views: 435 | Maoni (7) |

 

MBILI ABEL APAGAWISHA DAR

photos  
Usiku wa kuamkia leo mkongwe wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbili Abel alifanya makamuzi ya kufa mtu katika onesho lililofanyika Ukumbi wa Police Oficers Mess Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Katika onesho hilo mwanamuziki huyo alisindikizwa na ‘Wazee Sugu’ The Akapitale Band chini ya mkongwe, Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kikii'

MBILI ABEL APAGAWISHA DAR
Mbili Abel akifanya majambozi jukwaani

MBILI ABEL APAGAWISHA DAR
Hapa akiserebuka na wacheza shoo wake

MBILI ABEL APAGAWISHA DAR
Mashabiki wakichizika na vibao vilivyowahi kutamba enzi hizo

MBILI ABEL APAGAWISHA DAR
Wazee Sugu wakipagawisha na kitambaa cheupeee... Ishara ya upendo

MBILI ABEL APAGAWISHA DAR
Mashabiki wakichizika kwa kibao cha Wazee Sugu, ‘kitambaa cheupe’
PICHA: RICHARD BUKOS /GPL
    (4 July 2009)
Views: 315 | Maoni (2) |

 

Alifumaniwa, akavuliwa nguo

risasi jumamosi  
Alifumaniwa, akavuliwa nguo
Na Mwandishi Wetu

Sakata la mchekeshaji mwenye uwezo mkubwa nchini kulawitiwa, sasa linaweza kuchambuliwa na Risasi Jumamosi baada ya kupata ÔdataÕ za uhakika kutoka kwa vyanzo vyake...
    (4 July 2009)
Views: 5758 | Maoni (15) | Soma Zaidi

 

Maajabu maziko ya Michael Jackson

risasi jumamosi  
Maajabu maziko ya Michael Jackson
Na Mwandishi Wetu

Ni maajabu makubwa, maziko ya Mfalme wa muziki wa Pop duniani, Michael Jackson ambapo inasemekana yatahudhuriwa na watu wapatao milioni 1 huku wengine milioni 750 wataangalia kwa njia ya runinga...
    (4 July 2009)
Views: 2612 | Maoni (11) | Soma Zaidi

 

Ukijua siri hizi, mpenzi wako hakutesi

Mahaba  
Ukijua siri hizi, mpenzi wako hakutesi

Katika mapenzi, kila mmoja huwa na hisia zake moyoni, kwa bahati mbaya hisia hizo haziwezi kuonekana kwa macho na ni vigumu sana mtu kutoa hisia zake za siri. Mara nyingi imekuwa ikitokea wapenzi kuzungumza kwa vitendo zaidi kuonesha kilichopo moyoni mwao...
    (4 July 2009)
Views: 977 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Msitu wa pande -37

hadithi za Shigongo  
Jacob ametoka gerezani baada ya msamaha wa Rais, alinusurika na kifo cha kunyongwa Rais aliposoma kitabu chake kiitwacho Give me another chance Êalichokiandika akiwa gerezani! Hukumu yake ikabadilishwa kuwa kifungo cha maisha ambacho nacho kimefutwa baada ya kuugua kifua Kikuu akiwa gerezani.

Hakuamini alipoambiwa yuko huru, kwa msaada wa nauli aliyopewa na Mkuu wa Gereza alisafiri hadi katikati ya jiji la Dar es Salaam ambako alipanda basi jingine lililompeleka mpaka stendi karibu na nyumba iliyowahi kuwa yake lakini akamwachia mfanyakazi wao wa ndani baada ya kuhukumiwa kifungo, sababu mke na mtoto wake walishauawa.

Kwenye nyumba hiyo anagonga, lango linafunguliwa na badala ya kumkuta Diana, aliyewahi kuwa mfanyakazi wao wa ndani, macho yake yanakutana na msichana mwingine ambaye baada ya kujitambulisha alimtukana na kuamini ni mwizi sababu taarifa alizonazo ni kwamba Jacob alikuwa gerezani akitumikia kifungo cha maisha, msichana huyo akalibamiza lango kwa nguvu na kuondoka zake akimwacha Jacob ameduwaa.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (4 July 2009)
Views: 647 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

Sura ya mtu, roho ya shetani - 6

Mikasa ya kusisimua  
Sueya anajikuta njia panda baada ya mganga kukataa dhamira yake ya kumdhuru wifi yake, nini kitakachofuata baada ya mganga wa kwanza kukataa kumdhuru wifi yake? ili kuyajua yote. KANYAGA TWENDE...
    (4 July 2009)
Views: 722 | Maoni (0) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com