Majengo yenye muonekano wa kizamani yaliyopo mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, yanazidi kubomolewa kila kukicha kama mafundi hawa walivyonaswa na kamera yetu Mtaa wa Nyamwezi mchana huu, wakibomoa jengo la zamani kwa ajili ya kujengwa jengo la kisasa.
‘MTEJA MFALME’ Mchuuzi wa biashara ya machungwa (kulia) alinaswa na kamera yetu maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam, mchana huu, akimhudumia mteja wake kwa kumuhifadhia machungwa aliyonunua kwenye mfuko wa plastiki kwa ajili ya kuondoka nayo.
Mzee Rwakatare anapata ajali mbaya sana ambayo inamuondoa duniani katika mazingira ya kutatanisha ambayo yanaonyesha dhahiri kuwa ilikuwa ni ajali ya kupangwa. Rais anapatwa na mshtuko mkubwa sana baada ya kusikia kuwa gari alilolitoa kwenda kumchukua Mzee Rwakatare usiku ule limepata ajali mbaya sana.
Anaingiwa na hofu kubwa kwa kudhani kwamba wananchi wake wangehisi kuwa yeye ndiye aliyepanga mpango ule wa kumpoteza mzee Rwakatare. Bi Patricia naye anapoteza fahamu baada ya kusikia habari ya ajali mbaya alioyopata mumewe anaamini kuna mikono ya watu nyuma ya matukio yote yanayoikumba familia yao na mambo yote yanaonekana kubadilika... Je nini kinaendelea? Twende pamoja…
Ilianza kama nukuu nyepesi na hakuna aliyewaza kwamba lingezuka jambo kubwa lakini hivi sasa linatengeneza vichwa vingi vya habari Afrika Kusini, ni kuhusu maandalizi ya mazishi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela a.k.a Madiba...
Afya ya muigizaji ‘photogenic’, Yvonne-Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ si bukheri na sasa amelazwa kwenye wadi namba saba ya Hospitali ya Mikocheni Mission (MMH), Dk. Hubert Kairuki, Dar es Salaam...
Ni kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo waumini wa imani ya Kiislamu wanafunga, lakini Ijumaa Wikienda nalo, halikusita kuzama mitaani kuangalia ‘live’ matukio mbalimbali yaliyojiri siku ya Ijumaa usiku katika Jiji la Dar es Salaam...
Picha ‘sexy’ walizopiga Miss Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha TBC 1, Masoud Kipanya zimezua maswali mengi huku baadhi ya watu wakidhani kwamba, wawili hao wako katika uhusiano wa kimapenzi uliojificha...
Kiongozi wa Kundi la Bongo Dar es Salaam linalorusha kipindi chake kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Kulwa Kikumba ‘Dude’, hivi karibuni alitiwa mbaroni katika Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar es Salaam akidaiwa kumtorosha mtuhumiwa Ester Eliyakimu ambaye ni msanii wake...
Dona anafanikiwa kutoroka nyumbani kwa bilionea Bahati alikokuwa ameolewa bila kijana huyo kugundua kwamba mwanamke aliyekuwa akiishi naye ndani bila kufahamu kwamba ndiye aliyekuwa akisakwa dunia nzima kwa mauaji, yeye anamfahamu kwa jina la Christine Jackson, raia wa Marekani, jina ambalo Dona alilitumia baada ya kubadilisha sura yake huko Canada.
Anasafiri kwa ndege ya kukodi mpaka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro ambako alikodisha gari na dereva akampeleka mpaka Marangu ambako alishuka barabarani na kuanza kutembea kwenda nyumbani kwa bibi yake mgongoni akiwa amembeba mtoto wake na mkononi ameshikilia begi lenye dola nyingi.
Moyoni mwake anahisi akiwa kwa bibi yake anaweza kujificha bila kugundulika, alipofika aligonga na bibi akafungua mlango baada ya kugundua sauti ilikuwa ni ya mjukuu wake lakini walipokutana macho kwa macho bibi alishtuka alipoona sura ni tofauti na ya Dona, hilo lilimfanya Dona aanze kujieleza huku akimwonyesha bibi yake makovu ya upasuaji wa plastiki ili kumhakikishia yeye alikuwa Dona lakini alifanyiwa upasuaji huo kubadili sura jambo ambalo bibi hakukubaliana nalo.
Hata hivyo, baada ya kujieleza sana, hatimaye bibi alimruhusu aingie ndani kulala mpaka asubuhi alipoamka na kuaga anakwenda dukani kununua mahitaji, muda mfupi baada ya kuondoka Dona aliamua kutoka nje kwenda kuchimbia begi lake la fedha katikati ya migomba, akimwacha mtoto wake chumbani.
Akiwa huko alishangaa kumwona bibi anawasili na maaskari, moyo wake ukashtuka na kujua amekamatwa! Alichokifanya alijibanza katikati ya migomba na kujifunika na majani yake huku mwili wote ukitetemeka, akiwa hapo alimsikia mmoja wa maaskari akiwaonyesha wenzake nyayo za mtu aliyetembea kutoka ndani ya nyumba, Dona akahisi mkojo unamtoka hasa alipowasikia maaskari wakitembea kuelekea kwenye mgomba aliokuwa amejificha katikati yake. Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO…
Nimshukuru Manani kwa kunikutanisha nanyi tena wiki hii nikiwa mzima bukheri wa afya huku nikiendelea na majukumu yangu ya kila siku kama kawaida. Natumaini wewe pia umzima kabisa na uko tayari kuisoma mada ambayo nimekuandalia...
Ilipoishia wiki iliyopita Alisema: “Nilipofika tu na wao kuondoka, nilipitiwa na usingizi lakini baada ya muda nilishtuka na kusikia maumivu makali. Mwili ulikuwa hauna nguvu na nilibaki kama mgonjwa. Hata hivyo, kilichonishangaza zaidi ni pale nilipojiangalia miguuni. Huwezi kuamini kwamba sikuwa na jeraha hata moja. Endelea kusoma…
MKE wa Kocha Mkuu wa Yanga, Dusan Kondic aitwaye Rosa, ametua jijini Dar es Salaam na kumshauri mumewe mambo kadhaa yanayoweza kuwasaidia mabingwa hao wa Tanzania Bara kuzinduka na kuondokana na ukame wa mabao...
SHUJAA wa Simba katika mechi ya juzi dhidi ya Tanzania Prisons mjini hapa, David Tevelu Naftal, atakuwa akicheza namba yoyote, ulinzi, kiungo au ushambuliaji kulingana na aina ya mechi, amesema Kocha Mkuu wa Msimbazi, Patrick Phiri...
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, ameomba ulinzi kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa washambuliaji wake Danny Mrwanda na Mussa Hassan Mgosi...
Baada ya kutengana kwa muda mrefu hatimaye Josia na Janeth, watoto wa bwana na bibi Emmanuel Lugoye ambao wote ni marehemu, wamekutana! Josia ambaye baba yake alikuwa Spika wa Bunge, mtumishi wa Umma mwaminifu, ambaye hakuwahi kuiba au kujilimbikizia mali, alitoroka nyumbani kwao kwenda kuishi kusikojulikana baada ya maisha yao kuporomoka kufuatia kifo cha baba yao na mama yao mzazi, kujikuta amekuwa mamantilie.
Walihama kutoka Masaki kwenda kuishi Buguruni, wakatolewa shule ya Kimataifa ya Kilimanjaro na kutakiwa kujiunga shule ya msingi Buguruni kwa sababu mama yao hakuwa na kipato cha kutosha kulipa ada ya shule! Hali hii ya kuporomoka kiuchumi ndio ilimfanya Josia aamue kutoroka nyumbani kwao akiacha ujumbe kwamba anakwenda kufuatilia haki ya baba yake.
Miezi michache baada ya yeye kuondoka nyumbani, mama yake mzazi alifariki kwa kugongwa na gari! Josia hakuhudhuria mazishi, dada yake Janeth akalia peke yake na kwa msaada wa babu yake Mzee Mwinyimkuu na majirani, alizikwa na baada ya hapo Janeth akachukuliwa kwenda kuishi kijijini Mvumi ambako aliendelea na masomo yake ya shule ya msingi akijihesabu yu peke yake duniani.
Akafaulu kwenda shule ya sekondari ya Kilakala ambako alisoma na kufanya vizuri sana katika masomo yake mpaka akafika kidato cha sita, siku ya mahafali ya kumaliza, akiamini hakuna mtu kwenye familia yake aliyekuja kushiriki, alishangaa kumwona mwendawazimu akisonga mbele na shada la maua mikononi, alipomwangalia usoni alimtambua kwamba ni Kaka yake Josia. akaanguka chini na kupoteza fahamu.
Alipozinduka na kuulizia kama watu walimwona, hakuna aliyeelewa ni wapi alikoelekea mwendawazimu huyo baada ya Janeth kupoteza fahamu, akajitahidi kuwaeleza kwamba ni kaka yake waliyepotezana naye muda mrefu na akaamini huenda alikuwa marehemu! Watu wote walishangaa na kuamua kumsaidia kumtafuta lakini Josia hakuonekana, Janeth akarejea kwa babu yake ambako aliishi mpaka matokeo yakatoka na kuchaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alifurahi sana ushindi huo na akatamani angalau wazazi na kaka yake wangekuwepo, lakini haikuwa hivyo! Alipojiunga na Chuo, siku moja alishangaa kuona Bajaj ikiwa imeegesha mbele yake, mwendawazimu akiwa amesimama nje akitabasamu, alipomwangalia vizuri alikuwa ni Josia! Hakuamini macho yake. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Jana jioni timu za Yanga na Manyema Rangers za jijini Dar es Salaam, zilimenyana katika Uwanja wa Uhuru kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika kipute hicho, Yanga waliwagaragaza Manyema kwa bao 3-0 ambapo bao la kwanza na la tatu yalifungwa na mshambuliaji Jerry Tegete na bao la pili lilifungwa na Mike Barasa kwa njia ya penati baada ya kipa wa Manyema, Oddo Nombo, kumchezea vibaya mshambuliaji wa Yanga, Kabongo Honore. Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Manyema Rangers.
‘HAPA HUPITI’ Beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa (kulia) akimkaba mshambuliaji wa Manyema, Ally Mohamed ‘Gaucho’.
‘WEE MTOTO VIPI!’ Nsajigwa alimkamata Gaucho asilete madhara
‘KABARI’ YA NGUVU Baada ya kuona haitoshi, Nsajigwa aliamua kumkumbatia kabisa Gaucho.
BAADA YA KUPONYOKA Katika mbilinge hilo, Gaucho alipata nafasi ya kuponyoka na kuachia shuti golini mwa Yanga lakini halikuzaa matunda.
Mshambuliaji wa Yanga, Kabongo Honore (kulia aliyelala) akiugulia maumivu baada ya kuchezewa rafu eneo la hatari na kipa wa Manyema, Oddo Nombo, na kusababisha penati iliyozaa bao la pili.
Mike Barasa akijiandaa kupiga penati hiyo iliyozaa goli la pili.
Hii ni sehemu ya mashabiki waliofika uwanjani hapo.