arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for September 2009 Year

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» ZITO LAIBUKA
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Richard Mshindi BBA
» THE LAST HOPE (tumaini ...
» MCHUANO WA MVUTO UNAPAM ...
» UKWELI KUHUSU NDOTO
» MIMI SIO CHURA
» Simba afadhali...
» Ufuska laivu Pasaka!

 

MAANDAMANO YA CUF

Videos  
    (30 September 2009)
Views: 108 | Maoni (0) |

 

MAANDAMANO CUF YATIKISA DAR

photos  
CHAMA cha Wananchi (CUF), leo kimefanya maandamano makubwa yenye lengo la kudai tume huru na ya haki ya chaguzi nchini. Maelfu ya wananchi, hususan wanachama wa CUF, walijitokeza kushiriki maandamano hayo ambayo yamelitikisa jiji la Dar es Salaam.
Maandamano hayo yalianzia Buguruni kupitia baraba za Uhuru, Bibi Titi, Lumumba na kuishia viwanja vya Kidongo Chekundu, Mtaa wa Lumumba ambapo Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, aliyapokea na kuyahutubia, sambamba na Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba, Makamu Mwenyekiti, Juma Duni Haji na Katibu Mkuu, Self Sharif Hamad.
Polisi wakiwa katika mavazi maalum ya kutulizia ghasia pamoja na magari ya kumwaga maji ya kuwasha, maarufu kama ‘Vikojozi’, walitanda katika maeneo mbalimbali ya jiji ambamo maandamano hayo yalipita ili kuimarisha ulinzi.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Baadhi ya waandamaji wa CUF wakiwa eneo la Msimbazi Kariakoo.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Vikosi vya Polisi vikiimarisha ulinzi eneo la Mnazi Mmoja ambapo vurugu zilikuwa zinanukia baada ya waandamanaji kuwekewa kizuizi wasielekee eneo la Posta zilipo Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Magari ya kumwaga maji ya kuwasha (Vikojozi) yakiwa yamewekwa tayari eneo la Mnazi Mmoja kuthibiti ghasia zozote wakati wa maandamano hayo.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Moja ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Wafuasi wa CUF wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa (kulia), akiwa na Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba (katikati) na Maalim Self Hamad (kushoto )wakiwa katika mkutano wa chama hicho viwanja vya Kidongo Chekundu mara baada ya kupokea maandamano hayo.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Maalim Self (kushoto) akihutubia.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Profesa Lipumba akimkaribisha John Tendwa kuhutubia.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Tendwa akwaihutubia wafuasi wa CUF.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Kutoka kushoto ni Lipumba, Tendwa na Maalif Self wakiondoka katika viwanja hivyo baada ya mkutano kumalizika.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Mapaparazi wakiwa wameparamia mnara wa saa uliopo katika makutano ya barabara za Uhuru na Msimbazi ili kupata picha bora za maandamano hayo.

MAANDAMANO CUF YATIKISA  DAR
Mtoto wa wafuasi wa CUF akishiriki maandamano kwa kibaiskeli chake.
PICHA:CHRISTOPHER LISSA NA RICHARD BUKOS/GPL
    (30 September 2009)
Views: 158 | Maoni (0) |

 

SERIKALI YASALIMU AMRI KWA WANAFUNZI WA KIBASILA

Videos  


Hatimaye serikali imesikia kilio cha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam kwa kuagiza kuwekwa matuta katika barabara ya Mandela na Chang'ombe kwenye makutano ya barabara hizo jirani na kiwanda cha Bia cha Serengeti. Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya wanafunzi wa shule hizo kukaa barabarani kwa saa tano wakiishinikiza serikali kuweka matuta baada ya wanafunzi watatu kugongwa kwa siku tofauti kutokana na mwendo kasi wa magari yanayotumia barabara hiyo kutozingatia usalama wao

Akizungumza na baadhi ya wanafunzi hao katika eneo la tukio leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi amesema kuwa, yeye binafis amesikitishwa na kitendo cha madereva ambao wasiojali usalama wa watu wanaotumia barabara hiyo hasa watembe kwa miguu na badala yake wao hutumia kama ni yao pekee. Mh. Lukuvi ameitaka sekta husika kuhakikisha wanaweka matuta kabla ya wiki hii kumalizika kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

VIDEO NA: ISMAIL MANG'OLA/ GPL

    (30 September 2009)
Views: 130 | Maoni (2) |

 

PAMOJA TUNAWEZA!

photos  
PAMOJA TUNAWEZA!
Tuungane kuwasaidia wenzetu, watoto kwa wakubwa wenye matatizo hayo mdomono...mpe taarifa jirani yako au mtu mwenye tatizo hili unayemfahamu - UPASUAJI UNAFANYWA BURE!
    (30 September 2009)
Views: 142 | Maoni (0) |

 

AIBU YA MWAKA

risasi mchanganyiko  
AIBU YA MWAKA
Na Waandishi Wetu

Masikini Tanzania! Wimbi la mmomonyoko wa maadili linaendelea kuchukua nafasi pana nchini, makahaba wanapanua wigo kwa kubuni viwanja zaidi vya kunasa mabuzi, ushoga unasimama lakini kali iliyo ‘ndani ya karatasi’ ni kituo cha ngono cha vigogo...
    (30 September 2009)
Views: 5816 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

JIde ashambuliwa na gonjwa baya

risasi mchanganyiko  
JIde ashambuliwa na gonjwa baya
Na Mwandishi wetu

Nyota wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Judith Wambura ‘Jide’ ameshambuliwa na gonjwa baya baada kula nyama ya kuku wa kisasa mfulilizo, ishu hiyo ameifafanua mwenyewe...
    (30 September 2009)
Views: 2529 | Maoni (14) | Soma Zaidi

 

Rose Ndauka atemana na Richie

risasi mchanganyiko  
Rose Ndauka atemana na Richie
Na Musa Mateja

Mcheza filamu ‘seksistigel’ nchini, Rose Donatus Ndauka anadaiwa ‘kutemana’ na msanii mwenzake nyota, Single Mtambalike ‘Richie Richie,’ Risasi lina data zote...
    (30 September 2009)
Views: 1514 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Mainda auchapa ulabu, atapika!

risasi mchanganyiko  
Mainda auchapa ulabu, atapika!
Na Christopher Lissa

Nyota wa kike wa ‘muvi’nchini, Mwanaid Ruth Suka ‘Mainda’ hivi karibuni alipatwa na fedheha kubwa ukumbini baada ya kulewa pombe kupita kiasi na kuanza kujitapikia hovyo...
    (30 September 2009)
Views: 1249 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Msitu wa Pande-62

hadithi za Shigongo  
Hatimaye Mohamed Al-Kharaf, kijana ambaye familia yake yote iliteketea akiwa mdogo baada ya meli waliyokuwa wakisafiria kupigwa bomu, yeye peke yake ndiye akanusurika na kusukumwa na maji akiwa na boya mpaka kwenye kisiwa cha Lonely ambacho watu waliogopa kukitembelea kwa imani kwamba kulikuwa na majini.

Ni kwenye kisiwa hicho ndiko Diana pia alipelekwa na maji baada ya ndege aliyokuwa amepanda kuanguka baharini na watu wote kufa, yeye pia akaaminika kwamba alikufa! Jacob mchumba wake akamtafuta kwa muda rmefu bila mafanikio hatimaye kumuoa msichana aitwaye Jaine na kuzaa naye mtoto mmoja ambaye walimwita Diangela, kumbukumbu ya Diana na Angela.

Mohamed akamfanyia Diana ukatili wa kutisha, akimfanya mtumwa wa ngono na kumzalisha watoto watatu mpaka alipookolewa na Jacob bila kufahamu kuwa alikuwa Diana sababu ya uvimbe aliokuwa nao usoni, baadaye walipofahamiana, Jaine aliamua kujiua baada ya kugundua Jacob alikuwa na mapenzi na Diana!

Kilichofuata baada ya hapo ni kwenda kisiwani kuwakomboa watoto pamoja na Mohamed ambaye alipelekwa moja kwa moja nyumbani kwao Kuwait na kurithishwa utajiri wote wa familia ya Al-Kharaf, akawa bilionea ghafla! Alipotembelea Dubai ambako pia kulikuwa na mali nyingi za familia, alimtafuta Diana, Jacob na watoto na kuwagawia utajiri mkubwa wa mali zote zilizoko Dubai na visima vya mafuta nchini Kuwait! Diana alizimia.

Baadaye wakiwa hotelini ambako Mohamed aliwataka walale, kwani hoteli hiyo ilikuwa yao, Jacob alizinduka usingizini na kumkuta mke wake hayupo, akazunguka huku na kule akimtafuta bila mafanikio, moyoni akaamini Mohamed alikuwa amemfanyia ushenzi wa kumchukua kwenda kufanya naye ngono! Je, ni kweli? Nini kitatokea? Diana yuko wapi? SONGA NAYO…
    (30 September 2009)
Views: 775 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Sura ya mtu, roho ya shetani -30

Mikasa ya kusisimua  
Baada ya mganga kuyaweka maovu yake nje na kusababisha Sueya kujiona akiumbuka mbele ya mganga na kupoteza fahamu. Ni kweli siri ya Sueya kila mmoja ataielewa? Ili kuyajua yote TUWE PAMOJA...
    (30 September 2009)
Views: 751 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Mvuto pekee ni kipimo cha kuwa mwenzi bora?

Mahaba  
Mvuto pekee ni kipimo cha kuwa mwenzi bora?

Nianze kwa kuwashukuru wote wanaonipongeza kwa kazi hii, lakini pia sitaacha kuwashukuru hata ambao mmekuwa mkiuliza maswali mbambali juu ya mapenzi na uhusiano. Nawashukuru sana kwa ujumla wake na nawakaribisha kwa moyo mkunjufu katika safu hii ambayo hukupata darasa maridhawa...
    (30 September 2009)
Views: 345 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Yanga: TFF njooni Kaitaba muone kifo

champion  
Yanga: TFF njooni Kaitaba muone kifo
Na Saleh Ally

KINACHOIPELEKA Yanga Mjini Bukoba ni kuhakikisha inaondoka na pointi tatu muhimu na Kocha wake Mkuu, Dusan Kondic amesema anataka kubomoa rekodi ya kupoteza mchezo msimu uliopita...
    (29 September 2009)
Views: 278 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Chelsea yaitibua rekodi ya Simba

champion  
Na Saleh Ally

KIPIGO cha kwanza kwa Chelsea katika Ligi Kuu ya England, kimemfanya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri kuongeza tahadhari zaidi ili kuepuka kutibua rekodi yao ya kutofungwa hata mechi moja katika Ligi Kuu ya Vodacom...
    (29 September 2009)
Views: 213 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Chuji: Ngrrrrrr…Boban, mikosi hii ndugu yangu

champion  
Chuji: Ngrrrrrr…Boban, mikosi hii ndugu yangu
Na Saleh Ally

KIUNGO wa Yanga, Athuman Idd ‘Chuji’ anayetumikia adhabu ya kutocheza soka kwa miezi mitatu, juzi alimpigia simu kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ anayetumikia adhabu ya kutocheza mechi moja na kumweleza, “ndugu yangu, mikosi hii”...
    (29 September 2009)
Views: 364 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

The Painful Demand-39

hadithi za Shigongo  
Josia anafanikiwa kuiuza fimbo aliyoiiba Bungeni kwa Wahindi (Kumar na Nilesh) ambao wamekambidhi kitita cha dola milioni moja! Lakini baada tu ya biashara hiyo anapigiwa simu na Kamishina Masimbi akimtaaarifu kwamba mambo yameharibika na kuna wapelelezi hatari watatu wamekabidhiwa kazi ya kufuatilia mpaka fimbo ipatikane.

Kamishina huyo akamtaka Josia awaue wapelelezi hao, akamtaarifu kwamba amewaita ofisini kwake, Josia akaenda huko akiwa na gari lake lenye namba za Serikali, mlinzi akamfungulia bila kujua ni mtu hatari, akamuua mlinzi na kukata breki kwenye magari yote ya wapelelezi watatu walioitwa na Kamishina Masimbi akiwemo Vivian Lyimo.

Josia alizipata taarifa za vifo ya wapelelezi hao akiwa mjini Dodoma alipokwenda kumchukua dada yake, amefika nyumbani kwake na kuanza kugonga lakini hakuna aliyeitikia, akapiga simu yake, akasikia kabisa ikiita ndani ya nyumba bila mtu kuipokea! Hapo ndipo akaamua kuvunja mlango na kuingia mpaka ndani, ALICHOKIKUTA KILIMSIKITISHA. Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO…
    (29 September 2009)
Views: 644 | Maoni (4) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2 3 ... 26 27 28  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com