arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for October 2009 Year

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» Aina 10 ya vyakula vinavyoo ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» Zijue faida za kuuanda ...
» CCM yamkingia kifua Ric ...
» Chadema hali tete wenye ...
» Kabla ya kifo chake
» Watu 73 wafa maji katik ...
» JE, NI WAKATI GANI HASA ...
» MTIKILA ARIPUKA TENA!

 

UZINDUZI JAHAZIMODERN TAARAB ZIIII

photos  
Haikutarajiwa, lakini ndivyo ilivyotokea usikuwa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo kundi la muziki wa mwambao la Jahazi Modern Taarab ‘Wana wa nakshi nakshi’ waliposhindwa kurudia historia yao ya kujaza nyomi ukumbi huo na kujikuta ikizindua albamu yake mpya ya Daktari wa Mapenzi huku mashabiki wakiwa nusu.Hii ni kutokana na maasi yaliyofanywa na waliokuwa wasanii nyota wa kundi hilo ambao walianzisha kundi lao liitwalo Five Stars Modern Taaarab lenye upinzani mkali na Jahazi kwa sasa.

UZINDUZI JAHAZIMODERN TAARAB ZIIII
Mkurugenzi wa kundi la Jahazi , Mzee Yusuf akimpagawisha shabiki jukwaani wakati wa uzinduzi

UZINDUZI JAHAZIMODERN TAARAB ZIIII
Mtu mfupi huyu alikuwa kivutio ukumbini humo baada ya kujimwaga na kujiachia kwa raha zake huku akikatika nyonga katikati ya watu warefu hasa wanawake.

UZINDUZI JAHAZIMODERN TAARAB ZIIII
Baunsa huyu aliyekuwa akilinda usalama jukwaa kuu, alijikuta akisahau majukumu yake baada ya kuvamiwa na vimwana ambao walianza kumkatia mauno hadi akawa legelege wakati wa uzinduzi huo.

UZINDUZI JAHAZIMODERN TAARAB ZIIII
Ghafla ukumbi wa Diamond Jubilee uligeuka ulingo wa ndondi. Mabaunsa wakimdhibiti kijana ambaye alikuwa akitishia usalama ukumbini humo baada ya kulewa ‘nyapinyapi’na kuanza tabia ya ukorofi wa kupigana na kufurumisha matusi mazito.

UZINDUZI JAHAZIMODERN TAARAB ZIIII
Mwimbaji nyota wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’ Jesus Katunzi, akitoa burudani usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya kisasa ya Johannesburg, iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.

UZINDUZI JAHAZIMODERN TAARAB ZIIII
Bingwa wa kuandaa nyama choma, ndizi na mapochopocho mengine katika hoteli ya Johannesburg Sinza, Daudi Tryphone akiwajibika kuwaandalia wateja ‘mnuso’ usiku wa kuamkia leo.

UZINDUZI JAHAZIMODERN TAARAB ZIIIIDuh!Wabongo bwana.Hebu mcheki huyu ‘ mama nanihi’ mzima aitwaye Sara ambaye alinaswa mitaa ya Sinza akiwa amekalia kwa pozi la kimitego kiti cha plastiki cha mtoto, huku mmiliki wa kiti hicho ‘dogo’ flani hivi akiwa presha juu kuhofia kiti chake hicho kuvunjika.

UZINDUZI JAHAZIMODERN TAARAB ZIIIIAma kweli ajali haina kinga. Daladala linalopiga ‘ruti’ zake kati ya Mwenge na Kigogo lilinaswa likiwa limetumbukia katika mfereji wa barabara ya Kawawa jijini Dar es Salaam jana. Uzembe huchangia zaidi ajali za namna hii.
    (31 October 2009)
Views: 104 | Maoni (1) |

 

We mama mbavu zangu..!

Vichekesho na Udaku  
ALITAKA RUSHWA KUBWA
Jamaa mmoja alikwenda nchini Kenya kwenda kutembea. Kwa bahati mbaya alikamatwa na askari wa nchi hiyo kwa kosa uzururaji. Jamaa huyo alikuwa na uwezo wa kifedha na aliona njia nyepesi ya kuachiwa huru ni kutoa rushwa. Hata hivyo askari alikataa hongo hiyo na kumpeleka kituoni na kumfungulia mashtaka mawili moja la kuzurula na pili kutaka kutoa rushwa.
Mkuu wa kituo alimuuliza yule jamaa:
Mkuu wa kituo: Ni kweli asemayo afande?
Jamaa: Ni kweli lakini hakusema ukweli kuwa nimempa rushwa na kupokea, ila alitaka zaidi nikakataa na kuamua kunileta hapa.
Mkuu wa kituo: Umempa kiasi gani?
Jamaa alitamka kiasi cha pesa alizokuwa nazo yule askari na kumfanya aje juu lakini Mkuu wa kituo aliagiza askari apekuliwe na kukutwa na kiasi cha pesa alizosema yule jamaa.
Pesa alirudishiwa yule Mtanzania huku askari akiwekwa ndani na jamaa akaachiwa na faida ya pesa za askari. Kweli mjini shule... (bonyeza soma zaidi kuendelea)
    (31 October 2009)
Views: 622 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

GLOBAL PUBLISHERS YAWAMWAGIA ‘MSHIKO MADENTI’

photos  
Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, wachapishaji wa magazeti pendwa ya Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda, Amani, Uwazi, Championi na wamiliki wa mtandao huu, leo imewamwakabidhi kitita cha jumla ya Shilingi Milioni 1.1 wanafunzi wa tano wa kidato cha nne kutoka shule ya Sekondari Tirav, iliyopo Yombo Machimbo, Temeke jijini Dar es Salaam ambao walifanya vizuri katika masomo yao mbalimbali. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Bamaga, Mwenge mchana huu.

GLOBAL PUBLISHERS YAWAMWAGIA  ‘MSHIKO  MADENTI’
Mhariri Mkuu Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Richard Manyota (kushoto) akimkabidhi kitita cha Sh. 500,000/ Omary Kabono ambaye ni mshindi wa masomo ya Historia, Uraia, Jiografia, Book Keeping na Biashara, ambapo kila somo alipewa laki moja.

GLOBAL PUBLISHERS YAWAMWAGIA  ‘MSHIKO  MADENTI’
Mpiga picha Mkuu wa Global Publishers Ltd, Richard Bukos (kushoto), ambaye pia ni mdau wa mtandao huu, akimkabidhi kitita cha Sh. 200,000/ , mwanafunzi Mwanahamis Mramba ambaye ni mshindi wa masomo mawili ya Kiswahili na English.

GLOBAL PUBLISHERS YAWAMWAGIA  ‘MSHIKO  MADENTI’
Msanifu kurasa wa Global Publoshers Ltd, George Alphonce “MC George’(kushoto) akimkabidhi, Kiumbe Mlile kiasi cha Sh. 200,000/ baada ya kushinda masomo ya Kemia na Baiolojia.

GLOBAL PUBLISHERS YAWAMWAGIA  ‘MSHIKO  MADENTI’
Mhariri wa gazeti la Ijumaa, Amran Kaima (kushoto) akimkabidhi Sh. 100,000/ Hysein Kangambili ambaye ni mshindi wa somo la Hesabu.

GLOBAL PUBLISHERS YAWAMWAGIA  ‘MSHIKO  MADENTI’
Wanafunzi hao wakiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wao (watatu kushoto) wakifurahia ‘mahela’ yao.

KAMA HUYAJUI MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS LTD SOMA HAPA
GLOBAL PUBLISHERS YAWAMWAGIA  ‘MSHIKO  MADENTI’
Picha: Christopher Lissa /GPL
    (31 October 2009)
Views: 129 | Maoni (1) |

 

NI VILIO

risasi jumamosi  
NI VILIO
Na Mwandishi Wetu

Jiji lenye mastaa wengi, Dar es Salaam, Jumatano iliyopita lilitikisika na baadhi ya watu kusimamisha shughuli zao kwa muda, baada ya kusoma habari ya kihistoria, kuhusu mnyororo wa mapenzi wa mastaa kwa kuanzia kwa Wema Sepetu.
    (31 October 2009)
Views: 3981 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Mama Mjata: Sanaa haina umri

risasi jumamosi  
Mama Mjata: Sanaa haina umri
Na Imelda Mtema

MKONGWE wa sanaa ya maigizo nchini ,Techla Mjata (Mama Mjata) amesema kuwa licha ya umri wake kuwa mkubwa, bado anaimudu vema fani hiyo na wakati mwingine anafanya vyema kushinda wale wanaoibuka sasa katika tasnia ya filamu...]
    (31 October 2009)
Views: 241 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Waimbaji maarufu wa Injili nchini kumwombea afya JK

risasi jumamosi  
Waimbaji maarufu wa Injili nchini kumwombea afya JK
Na Mwandishi Wetu

WAIMBAJI maarufu wa muziki wa Injili nchini, Upendo Nkone, Upendo na Amon Kilahiro, Victor Arone, Christina MwangÕonda na Joseph Nyuki watapanda jukwaa moja katika kumwombea afya njema Rais Jakaya Kikwete sambamba na uzinduzi wa Albamu ya Yesu ni Bwana na Tenda Wema ya muimbaji Margaret Somy...
    (31 October 2009)
Views: 199 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Kelvin alazimisha kula denda la Eliza

risasi jumamosi  
Kelvin alazimisha kula denda la Eliza
Mshiriki wa shindano la kumsaka mkali wa Big Brother kutoka nchini Nigeria, Kelvin juzi alilazimisha kwa nguvu kumbusu bila mafanikio, Elizabet Gupta kama inavyoonekana pichani hali iliyopelekea binti huyo wa Kitanzania kumjia juu na kumzuaia asiendelee kumsogelea...
    (31 October 2009)
Views: 744 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Kiongozi Chadema amjeruhi muuguzi

risasi jumamosi  
Kiongozi Chadema amjeruhi muuguzi
Ismail MangÕola na Makongoro Oging

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Yangeyange, Kata ya Msongola, Ilala jijini Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Colman Marwa Waisokera, anadaiwa kumjeruhi Muuguzi wa Zahanati ya eneo hilo, aliyetajwa kwa jina maarufu la Mama Marwa...
    (31 October 2009)
Views: 236 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Asha Baraka: Hili nalo litapita

risasi jumamosi  
Asha Baraka: Hili nalo litapita
Na Mwandishi Wetu

Baada ya vitisho vya kuuawa, Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET), inayomiliki Bendi ya Muziki wa Dansi ya African Stars ÔTwanga Pepeta InternationalÕ, Asha Baraka ÔThe Iron LadyÕ amesema, Ôhili nalo litapita tuÕ kufuatia kile alichodai ni kuandamwa na wabaya wake...
    (31 October 2009)
Views: 568 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Just hang me! -1

hadithi za Shigongo  
Hii ni hadithi yangu mpya, yenye mafundisho makubwa kwa watu waliofanya makosa na kuamini hawawezi kusamehewa! Pili kwa binadamu wengine ambao kazi yao kubwa ni kuhukumu na hawako tayari kusamehe, hawa huwahukumu hata watu waliokwishakufa! Ni vyema wakati mwingine kumwachia Mungu kazi yake. Nawakaribisheni muisome mwanzo mpaka mwisho, hakika hakuna atakayejuta kwamba alipoteza muda wake, kazi yangu mimi si kuburudisha tu bali kufundisha pia.
ANZA NAYO...
    (31 October 2009)
Views: 775 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Kutafuta cheo kazini kulinifikisha hapa- 14

Mikasa ya kusisimua  
Eflazia baada ya kutafuta dawa ya kuongezwa cheo anajikuta akiingia katika matatizo mengine kupaja ujauzito wa ndotoni. Nini kitaendelea TUWE PAMOJA...
    (31 October 2009)
Views: 1198 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Sura ya mtu, roho ya shetani - 39

Mikasa ya kusisimua  
Sueya baada ya kumtendea ubaya wifi yake na kushiriki katika mbinu za kumuondoa duniani mama Kiota kibao kinamgeukia na kujikuta amekuwa wendawazimu. Alipozinduka alijikuta kwa mganga akitibiwa bila kujua aliletwa lini na ugonjwa wake umechukua muda gani mpaka kurudiwa na akili timamu. Ili kutajua yote TUWE PAMOJA....
    (31 October 2009)
Views: 661 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Fahamu jinsi ya kudumisha penzi la mbali!-3

Mahaba  
Fahamu jinsi ya kudumisha penzi la mbali!-3

Hii ni Jumamosi nyingine tena tunakutana katika safu yetu nzuri kabisa ya kupeana elimu mahususi juu ya mambo ya mapenzi. Sina shaka wote mtakuwa wazima wa afya njema na mpo tayari kupata kitu kipya...
    (31 October 2009)
Views: 368 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Msitu wa Pande -71

hadithi za Shigongo  
Dk. Clara ameamua kwenda porini kumsaka mume wake, lakini akiwa huko naye anaugua ugonjwa wa Chinese Encephalitis. Hataki kufia porini tena, anaingia ndani ya gari ili awahi Kinshansa, wakati anaingia barabarani, gari jingine linatokea upande wa pili na kumgonga! Akashuka mwanaume na kwenda kumkaba akiwa na hasira. Lakini mwanaume huyo alipiga kelele akisema ÒClaraaaaaa!
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (31 October 2009)
Views: 562 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Michuano ya Shimiwi yapamba moto

photos  
Wachezaji wa timu ya Rasi kutoka Mbeya wenye (Jezi nyekundu) na wenzao wa Rasi ya Dar es salaam wenye (Jezi ya njano) wakiwania mpira kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo Rasi ya Mbeya waliibuka na ushindi wa bao 2-1.

Michuano ya Shimiwi yapamba moto

Michuano ya Shimiwi yapamba moto


Wachezaji hao walikuwa wakimenyana vikali katika michuano ya Idara na Wizara za serikali (SHIMIWI) inayoendelea mkoani Morogoro.

Michuano ya Shimiwi yapamba moto
Georgia Gervase akimnyonyesha mtoto wake kabla ya kuingia uwanjani.

Michuano ya Shimiwi yapamba moto
Georgia Gervase mchezaji wa timu ya Ras Kagera kutoka mkoani Kagera mwenye jezi iliyoandikwa GD akijarubu kumzuia mchezaji wa timu ya Rasi ya Mwanza ili asipeleke madhara katika lango la timu yake.

Michuano ya Shimiwi yapamba moto
Mashambilizi makali yakiendelea.
Picha: Dustan Shekidele /GPL
    (30 October 2009)
Views: 100 | Maoni (2) |
Back  <<  1 2 3 ... 31 32 33  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com