Na Mwandishi Wetu WAKATI huu wa msimu wa sikukuu za Krismas na Mwaka mpya, gazeti lako ulipendalo la Uwazi linakuletea zawadi bomba na bab’ kubwa kama vile kompyuta mpya, simu, ‘Music system’ na runinga mpya kupitia mfumo wa kadi maalumu ya zawadi itakayowekwa ndani ya gazeti hilo kuanzia Jumanne ya Desemba 8, 2009...
KUMRADHI: Wiki tatu zilizopita tulikuwa tukichapisha mfululizo wa maneno kutoka hotuba iliyotoka kwenye kitabu cha Nyerere kilichoitwa ‘TUJISAHIHISHE’ kilichotolewa Dar es Salaam Mei 1962, tulipomaliza, kwenye sehemu ya kutambua kazi hiyo, hatukueleza kwamba ndani ya machapisho hayo tulibadili maneno TANU, WanaTANU na wasio WanaTANU kwenda CCM na WanaMtandao na wasio WanaMtandao. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika hilo.Mhariri...
Mpenzi msomaji, kijana Mohamed Geni mkazi wa Dumila Kilosa mkoani Morogoro ambaye katika safari yake ya maisha anadai amekumbana na mkasa wa kubambikiwa kesi ya kubaka na kujikuta akitupwa gerezani alikotakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30, anaendelea mkasa uliomkuta uliosababishwa na wema aliomtendea dada mmoja aliyefika Dumila akitokea Singida na baadaye kudaiwa alimbaka. Ilikuwaje? Ungana na MWANDISHI WETU KULWA MWAIBALE katika mkasa huu wa kweli…
BAADA ya Theresia kuwaua kichawi wanafunzi wenzake aliokuwa akisafiri nao kwenda mbugani Hwangwe kwa safari ya mafunzo akanusurika Albert peke yake kwa sababu alikuwa anampenda, wazazi wa watoto hao wanashikwa na hasira na kuamua kuchoma wodi aliyolazwa Theresia, akateketea kabisa ndani ya moto na mabaki yake kusafirishwa kwenda kuzikwa Tanzania.
Albert ambaye tayari alimpenda sana Theresia, aliumizwa sana na kifo hicho cha kikatili, ingawa Theresia mwenyewe alikiri kuwa mchawi pasipo hiari yake, bado alimpenda na alitamani angekuwa mke wake maishani! Anachanganyikiwa kabisa, akawa hataki tena shule, jambo hili lilifanya wazazi wake wamtafutie mtaalamu wa saikolojia ya vijana ili amrejeshe katika hali ya kawaida, kwa miezi mitatu mtaalamu huyo alifanya kazi mpaka akafanikiwa na Albert kurejea shuleni.
Katika hali ambayo Albert hakuitarajia, siku moja anapokea simu kutoka kwa rafiki yake Shadrack na kuomba afungue Televisheni kwenye stesheni ya CNN ajionee, akafanya hivyo na hakuamini macho yake alipoona taswira ya Theresia runingani, akidaiwa ni msichana aliyekamatwa na polisi nchini Kongo kwa tuhuma za mauaji ya kichawi ya watu kumi katika kijiji cha Chipole! Alichokifanya Albert ni kupiga kelele akiita jina la Theresia.
Je, nini kitafuata? Aliyekamatwa nchini Kongo ni Theresia kweli au msichana mwingine anayefanana naye? SONGA NAYO…
ILIPOISHI WIKI ILIYOPITA •Mambo mengi hutokea au hutegemea na mitazamo uliyonayo. Maamuzi mengi tufanyayo hutegemea na mitazamo tuliyonayo maishani. Kama mtazamo wako ni wakujutia kila kitu au kulaumu wengine, basi utalaumu na kujutia kila utakachowahi kukifanya, mfano; utajutia na kulaumu kozi unayosoma, kazi unayofanya, biashara unayofanya, mke au mume mliyeoana nae, watoto uliowazaa nk...
KUACHWA ni jambo linalotia uchungu usioelezeka katika mapenzi hasa pale wanaoachana mmoja anakuwa bado angali dimbwini kwenye mahaba. Wanaoachwa huku wanapenda hukonda kwa mawazo na wakati mwingine hutamani kufa kuliko kuishi mbali na wapenzi wao...
Picha tatu hapo juu zinaonyesha gari aina ya Cadillac Escalade ambalo Tiger Wood alipata nalo ajali nje ya nyumba yake mapema tarehe 27, Novemba 2009
* Hakuripoti ajali hiyo polisi hadi siku tatu baadaye KATIKA taarifa aliyotoa kwenye tovuti yake, nguli wa mchezo wa golf duniani, Mmarekani Tiger Woods amemsifia mkewe, Elin Nordegren, kwa kumsaidia wakati alipopatwa na ajali nje ya nyumba yake ambapo aligonga bomba kubwa la maji ya kuzimia moto huko Isleworth, Orlando...
Novemba 30, 2009 Babu Seya na wanawe walipanda tena kizimbani ili kusikiliza hatma ya rufaa yao ambayo ingeamua maisha yao gerezani ambako wamekuwa wakisota kwa miaka mitano sasa. Hata hivyo mambo hayakuwa kama walivyotarajia badala yake kesi yao imepigwa kalenda hadi Desemba 3 itakapoanza kusikilizwa rasmi. Bonyeza Player ilikujionea video hii inayoonyesha sehemu ya mambo yaliyojili mahakamani leo. Video: Christopher Lissa /GPL
Novemba 30, 2009 ndiyo siku iliyopangwa kusikiliza rufaa ya Babu Seya na wanae waliohukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kunajisi. Lakini kesi hiyo haikuendelea baada ya wakili wa awali, Hubert Nyange kujitoa dakika za mwisho. Kesi sasa imeshikwa na wakili Mabere Marando na imepigwa kalenda hadi kesho kutwa Alhamis Desemba 3 ili wakili mpya apate muda wa kuipitia...hali ilikuwa ni ya simanzi kwa ndugu na jamaa wa familia hiyo ingawa wao wenyewe walionekana kuchangamka kidogo ingawa ndani ya macho yao wamejaa hali ya kukata tamaa na maisha.....
Familia ya Nguza ikiingia ndani ya jengo la Mahakama Kuu mapema leo
..hali ya wasiwasi..(kutoka kushoto) Babu Seya, Paii Kocha, Mbangu na mdogo wao wa mwisho Francis
..unaweza kuhisi anachowaza Papii..!
..akiwapa mkono wa pole ni binamu yao..Grace Francis
..ndani ya majonzi makubwa...Monica Nguza ambaye ni dada wa akina Papii
....wakiwa kizimbani
Mzee Nguza akipeana mkono wa matumaini na wakili wake mpya, Mabere Marando.
Shemu ya hotuba ya Malkia Elizaberth aliyoitoa wakati akihutubia viongozi wa nchi za Jumuiaya ya Madola..baadhi ya watu wamemtaka asijiingize kwenye siasa... wewe unaonaje? ..soma baadhi ya comments zao hapo chini....
Kila Jumamosi katika viwanja vya Leaders huwa kunafanyika bonanza kubwa linalowakutanisha wasanii wa fani mbalimbali ambao ubadilishana mawazo na kufanya onesho la pamoja.
Wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamisi Ramadhan 'H. Baba' (kulia) na Tundaman wakiweka mikakati ya kufanya kazi za nguvu 2010.
Msanii wa sanaa za Maigizo, Jackline Wolper akipozi ili apigwe picha katika viwanja vya Leaders siku ya Bonanza hilo.
Wasanii wa Bendi ya muziki wa dansi ya Minofu wakitoa burudani katika bonanza hilo.
*Asema muda si mrefu wataugua kisukari, shinikizo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka India, Dk. Pujar Suresh, amesema idadi kubwa ya Watanzania wananyemelewa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu kutokana na kula bila mpangilio...
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe
*YADAIWA KUWASAIDIA SILAHA WAASI DRC, MEMBE AWAKA, ATAKA IOMBWE RADHI WAKATI Umoja wa Mataifa (UN) ukiitupia shutuma nzito Tanzania kuwa inasaidia kusafirisha silaha kwenda kikundi cha waasi nchini Congo, serikali imekanusha na kutaka iombwe radhi...