Ligi Kuu Tanzania Bara jana iliwakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga katika Uwanja wa Taifa ambapo mpaka kipenga cha mwisho Yanga ilikuwa imebamizwa bao 1- 0. Bao hilo lilifungwa na Mussa Hassan Mgosi baada ya kupokea krosi kutoka kwa Danny Mrwanda.

Kikosi cha Simba kilichoanza mchezo jana.

‘Jeshi’ la Yanga lililoanza mashambulizi dhidi ya Simba.

Mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega, wakiwapa ‘Hai!’ mashabiki wa timu yake kabla ya mpambano.

Sehemu ya mashabiki wa Simba waliohudhuria mtanange huo.

Licha ya kuwa wamechapwa bao, mashabiki wa Yanga waliendelea kuwapa moyo wachezaji wao kwa kuwashangilia wakati wote wa mchezo.

Beki wa Simba, Salum Kanoni (kushoto) akiwa hewani kumdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa.

Amir Maftah, mlinzi wa Yanga (kulia), akimdhibiti mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.

Mshambuliaji wa Simba, Danny Mrwanda, akimtoka Nurdin Bakari wa Yanga (aliyekaa).

Simba wakishangilia bao.

Kocha mpya, Yanga Kosta Papic, alijaribu kubadili kila mfumo katika mchezo huo, lakini hapakuwa na mafanikio yoyote.

Meneja wa Top Band, Hamis Dakota (mwenye fulana ya njano) pamoja na mashabiki wengine wa Yanga wakichana fulana ya mmoja wa mashabiki wa Simba (hayupo pichani).

Mhariri Kiongozi wa magazeti ya Championi, Saleh Ally, (kushoto) akiwa na mapaparazi wa kituo cha Super Sports cha Afrika kusini, waliofika uwanjani hapo kuripoti mechi hiyo.

Shabiki wa Yanga (jina lake halikuweza kupatikana) akilia baada ya mpira kumalizika.

Kocha wa Simba, Patrick Phiri (kulia), akihojiwa na waandishi wa habari. Mwenye miwani kichwani ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally.
PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL