arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 02.11.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KARIBU KATIKA ULIMWENGU ...
» My Black Chapter -33
» UAMINIFU, KUPUUZA MANEN ...
» (SIMULIZI LA CHUMBANI) ...
» Zijue faida za kufunga ...
» DIAMOND MUZIKA YAMTANGA ...
» Wasanii Jumba la dhahab ...

 

REVENGE OF THE DEAD -18

hadithi za Shigongo  
Theresia na Albert wameokolewa kutoka msituni wakiwa na maaskari wengine walioumwa na nyoka mwenye sumu ndani ya maji, kwa helikopta wakachukuliwa na kupelekwa mpaka hospitali ya Perirenyatwa ambako walilazwa na kuanza kupewa dawa ya kupambana na sumu ya nyoka! Siku chache baadaye Albert alirejewa na fahamu zake lakini Theresia aliendelea kubaki katika hali hiyo, matumaini ya yeye kupona yakazidi kupungua!

Kihistoria, Theresia ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Steven Kunjumu ambaye alijihusisha na nguvu za giza katika utafutaji wa utajiri wake, akawa anaua watu na kuuza viungo vyao! Mwisho wa siku watu aliowaua wakaamua kulipa kisasi, hii ndiyo Revenge of the Dead! Kisasi hiki kikaanza na yeye Steven na mke wake, wakafa na kumwacha mtoto wao Theresia ambaye mizimu inaendelea kumtumia kuua watu ili ipate damu kama chakula chao.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
    (2 November 2009)
Views: 777 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

JINSI YA KUUJENGA NA KUUKUZA UJASIRI WETU (BOASTING YOURSELF CONFIDENCE)

Saikolojia na maisha  
KATIKA kufanikiwa katika jambo lolote unahitaji walau mambo yafuatayo:
1. Kujua kile unachokitaka
2. Shauku ya hali ya juu ya kupata kile unachokihitaji.
3. Kuamini kwamba unaweza kukipata kile unachokihitaji, yaani kuuamini uwezo ulionao katika kuhakikisha unakipata unachokilenga.
4. Kuamini kuwa unastahili kukipata unachokihitaji. Namanisha kujiamini kuwa unathamani kabisa kukimiliki unachokitaka.
Ujasiri ninaokwenda kuuzungumzia hapa unahusika moja kwa moja na jambo la tatu na la nne. Tuanze na jambo la tatu: Amini kwamba unaweza kukipata au kuwa nacho kile unachokihitaji...
    (2 November 2009)
Views: 222 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

NILIBAMBIKIWA KESI YA UBAKAJI NIKAFUNGWA MIAKA 30

Mikasa ya kusisimua  
KATIKA safari ya maisha, binadamu ukumbana na mitihani ya kila aina kwani wapo waliofiwa na watu wao muhimu kama watoto na wazazi, kuugua maradhi ya kutisha na kufilisika. Ukiacha hao, wapo ambao wamedhurumiwa mali na watu wengine na wapo ambao wanatumikia vifungo magerezani bila hatia yaani kwa kubambikiwa kesi za mauaji au makosa mengine.

Miongoni mwa watu wanaodai kukumbwa na kesi ya kubambikiwa ni kijana Mohamed A. Geni mkazi wa Dumila Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Hebu ungana na Mwandishi Wetu katika mkasa uliomkuta kijana huyo ambaye anaanza kuelezea kilichomsibu na kujikuta akihukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kubaka lakini alitumikia miaka 9 tu na kuachiwa baada ya kubainika hakutenda kosa hilo…
    (2 November 2009)
Views: 420 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Matatizo ya wanawake wazuri na jinsi ya kuyakabili

Mahaba  
Matatizo ya wanawake wazuri na jinsi ya kuyakabili

KARIBUNI katika safu yenu hii mpya yenye lengo la kutoa mwanga katika masuala yahusuyo mapenzi na maisha...
    (2 November 2009)
Views: 449 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

TAKUKURU YAKOMAA NA POSHO YA WABUNGE

photos  
TAKUKURU  YAKOMAA NA POSHO YA WABUNGE
Richard Bukos na Christopher Lissa

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), imeendelea kulikomalia suala la wabunge wa Jamhuri ya Muungano kupokea posho mara mbili na kuwataka waheshimiwa hao kuiacha taasisi hiyo ifanye kazi yake kwa mujibu wa sheria...
    (2 November 2009)
Views: 318 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

KITUO KIKUU CHA MABASI UBUNGO SHWARI!!!

photos  
KITUO KIKUU CHA MABASI UBUNGO SHWARI!!!
Siku chache baada ya serikali kuchukua uendeshaji wa kituo kikuu cha mabasi ya mikoani na nchi jirani cha Ubungo jijini Dar es Salaam, hali ni shwari kabisa eneo hilo ambapo mapaparazi wetu walipatembelea mapema leo na kukuta shughuli za usafiri zikiendelea vyema kama inavyoonekana pichani.
PICHA: CHRITOPHER LISSA NA RICHARD BUKOS /GPL
    (2 November 2009)
Views: 93 | Maoni (0) |

 

KESI YA KINA MRAMBA: MASHAHIDI WAANZA KURINDIMA

photos  
Bw. Nyelo Godwin kutoka kampuni ya Madini ya Euronets TZ Ltd, ambaye ni shahidi wa kwanza upande wa Serikali katika kesi ya ufisadi inayowakabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Pesambili Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Grey Mgonja, ameanza kutoa ushahidi wake leo katika kesi hiyo inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
KESI YA KINA MRAMBA: MASHAHIDI WAANZA KURINDIMA
Kutoka kulia ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Basil Pesambili Mramba, Daniel Yona na Grey Mgonja wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
    (2 November 2009)
Views: 96 | Maoni (1) |

 

Dr Hoseah wa PCCB awaka

photos  
Dr Hoseah wa PCCB awaka

(4 hours ago)

Nimetoka kwenye mkutano wa Dr Edward Hoseah ambao umemalizika muda mchache uliopita katika ofisi za makao makuu ya TAKUKURU Upanga jijini Dar es Salaam.

Katika Mkutano huo, kwanza Dr Hoseah kaanza kwa kusema "Sijiuzulu ng'o, maana toka asubuhi ninapokea simu za watu wakiuliza kama nimejiuzulu tayari" hayo yalikuwa maneno yake wakati anaingia ukumbi wa mikutano kabla hata ya kusamiliana na wanahabari.

Dr Hoseah anasema "kuna nini mpaka wabunge waogope kuchunguzwa na TAKUKURU? kinachomshangaza ni kuwa hata sheria inayotekelezwa na TAKUKURU imepitishwa na bunge lenyewe tena na wabunge hao hao, iweje leo waanze kulalamika kuwa hawatendewi haki? haki wanayoitaka waheshimiwa wabunge ni ipi?" anahoji Hoseah.

Aidha anasema , barua ya bunge ya tarehe 26/02/2009 iliyokuwa imeelekezwa kwake, ilikitaka chombo chake kufanya uchunguzi ili kujiridhisha maana kulikuwa na minong'ono ya wabunge kulipwa posho mbili, huku wanalipwa na bunge pamoja na taasisi wanayokwenda kuitembelea!

Amewataka wabumge ambao wamekuwa na sifa kubwa ya kupinga vitendo vya kifisadi watoe ushirikiano ili chombo hicho kiweze kuwafanyia 'natural justice' maana katika detection tayari makachero wa TAKUKURU walishapata kila kitu kuhusu posho hizo mbili za wabunge.

Aidha amewataka wabunge ambao wanaona anafanya makosa kuwachunguza, wapige kura ya kutokuwa na imani naye, na yupo tayari kwa lolote litakalotokea, huku akijiganba kuwa TAKUKURU sio mwisho wa maisha yake hata kidogo, "there is life after PCCB" anasema Dr Hoseah.
(NA MKINGA)
    (2 November 2009)
Views: 92 | Maoni (1) |

 

Nigeria, Zimbabwe na Namibia zatamba ‘2009 Channel O Music Video Awards’

photos  
Nigeria, Zimbabwe na Namibia zatamba ‘2009 Channel O Music Video Awards’
Gal Level kutoka Namibia

• Washindi wanyakua tuzo mbili kila mmoja

USHINDI wa wasanii watatu kutoka Nigeria, Zimbabwe na Namibia ambapo kila mmoja wao alishinda tuzo mbili katika mashindano ya tuzo bora za video za muziki kwa mwaka huu, yaani ‘2009 Channel O Music Video Awards’, zilidhihirisha nguvu kubwa waliyo nayo wasanii hao katika fani hiyo...

    (2 November 2009)
Views: 177 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

D'Banj Surprises the housemates

photos  
Day 54 on M-Net’s Big Brother Revolution and Nigerian superstar D’Banj surprises the housemates! Tune in to Big Brother Revolution on DStv channel 198 or 199 and for more information, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother.
D'Banj Surprises the housemates
D’Banj and series host IK.
    (2 November 2009)
Views: 208 | Maoni (2) |

 

Mitambo ya IPTL yakwama kuwashwa

photos  
Matumainia ya kumalizika haraka kwa tatizo la mgawo wa umeme ulioikumba nchi kwa takriban mwezi sasa, yamefifia, baada ya mitambo ya kufua nishati hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), kushindwa kuwashwa jana, kama ilivyotangazwa awali na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja...
    (2 November 2009)
Views: 163 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Mc Regan, Wakuvanga, nani zaidi?

photos  
Mc Regan, Wakuvanga, nani zaidi?
Na Joseph Shaluwa

Baada ya mtangazaji Aboubakar Sadick kuibuka mshindi dhidi ya Abdallah Mwaipaya wiki iliyopita, sasa vumbi linatimka ndani ya Kundi la Orijino Komedi, ambapo wasanii Alex Chalamila ‘Mc Regan’ na mwenzake Isaya Mwakilasa ‘Wakuvanga’...
    (2 November 2009)
Views: 511 | Maoni (11) | Soma Zaidi

 

Nine Tanzanian students arrested in India

photos  
*They are accused of attacking three police officers

Nine Tanzanian students and one from Kenya have been arrested in India for allegedly attacking three police officers and cause public nuisance...
    (2 November 2009)
Views: 170 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Akina Kingunge waenguliwa rasmi Ubungo Stendi

photos  
Akina Kingunge waenguliwa rasmi Ubungo Stendi
Mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru

*Jiji waanza kukusanya ushuru wenyewe
Halimashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza rasmi kukusanya mapato katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) baada ya mkataba wa kampuni binafsi inayomilikiwa na familia ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, iliyokuwa ikifanya kazi hiyo kukatishwa...
    (2 November 2009)
Views: 499 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

Mbunge afariki dunia!

photos  
Mbunge afariki dunia!
Marehemu Sigifrid Ng'itu

WABUNGE wa Bunge la Tanzania wapo katika maombolezo, mwenzao, Sigifrid Ng’itu (55) ameaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam...
    (2 November 2009)
Views: 789 | Maoni (6) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com