Hali si shwari ndani ya Kundi la Kaole Sanaa la Dar es Salaam na hivi sasa linawaka moto chini kwa chini, baada ya kikundi kidogo kutaka mabadiliko ya haraka ya uongozi...
Msichana mrembo mwenye umri kati ya miaka kumi na saba na kumi na nane hivi, anakutwa kando ya barabara ielekeayo Bagamoyo maeneo ya Zinga, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Anavuja damu nyingi kiasi kwamba aliyemwokota anaamini amegongwa na gari lililokuwa likiendeshwa kwa kasi na dereva hakusimama.
Haelewi ukweli kwamba msichana huyo hakugongwa na gari bali alikuwa mjamzito na alikwenda porini kwa ajili ya kukatisha uhai wake, lakini alipofikiria kiumbe alichokuwa nacho tumboni aliamua kuahirisha na kuruka kutoka mtini! Kitendo hiki ndicho kilianzisha maumivu makali ya tumbo ambayo baadaye yalikuwa uchungu, akiwa ameamua kutokufa, msichana huyo alianza kutembea na maumivu yake kuelekea barabarani.
Njiani akianguka mara nyingi, chupa ikiwa imepasuka na maji mengi kumwagika mtoto akachungulia na hatimaye kumzaa akiwa peke yake porini! Kitendo hiki cha kujifungua kilifuatia na kuvuja damu nyingi isivyo kawaida, mwili ukaishiwa nguvu na macho kuanza kuona giza, akiwa amedhamiria kutokufa binti huyo alimwacha mtoto wake hapo hapo na kuanza kutambaa kuelekea barabarani huku akivuja damu mfululizo.
Mbele kidogo alishangaa alipopata maumivu makali tena, akajikuta anaanza kusukuma na mtoto wa pili akatoka, kumbe alikuwa na watoto pacha! Akiwa hana nguvu kabisa aliendelea kutambaa mpaka barabarani ambako alianguka na kupoteza fahamu kabisa, muda mfupi baadaye ndipo kijana mmoja alifika na kumwona, akasimamamisha gari na wakamchukua mpaka hospitali ya Bagamoyo bila kufahamu alikuwa amejifungua watoto wawili pacha porini kabla ya kufika barabarani. Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO…
Furaha yote aliyokuwa nayo Dk. Laurian Lwambo ambaye amegundua chanjo ya ugonjwa wa Chinese Encephalitis na anatarajia kulipwa dola milioni hamsini na moja, inapotea!
Akiwa mbioni kuelekea katika jiji la Kinshansa kutoka porini alikokuwa akifanya utafiti, tena akiwa na mkewe Clara ambaye amekutana naye porini katika mazingira ya kutatanisha, gari alilokuwa nalo linaanza kutoka moshi mwingi mbele! Anasimama na kushuka kwenda kufungua boneti, katika hali ambayo hakuitarajia kabisa, akiwa hajui kwamba rejeta imechemka kupita kiasi, anashangaa kuona mfuniko wa rejeta unafunguka na maji yenye nyuzi joto mia moja yanaruka na kummwagikia usoni na kifuani! Anaanguka chini na kuanza kupiga kelele.
Mke wake ana hali mbaya, amepatwa na ugonjwa aliokwenda kuufanyia utafiti porini (Chinese Encephalitis) kama ilivyomtokea Dk. Laurian akaokolewa na dawa iitwayo Immuno Booster, jambo ambalo Dk. Laurian alfianya kabla hajapatwa na ajali ya maji ya moto ni kumchoma mke wake sindano hiyo ndipo akaanza safari kuelekea Kinshansa, lakini safari hii imekomea hapa! Je, nini kitatokea? SONGA NAYO…
Sueya anajikuta sehemu asiyoijua akiwa kwa mganga wa kienyeji, baada ya kupata nafuu kutokana na kuugua wendawazimu kwa miaka mitano. Mganga anamsimulia vitu ambavyo vinaufanya moyo wake kuuma na kutamani dunia immeze kwa ubaya alioutenda. Nini hatma ya yote? TUWE PAMOJA...
Ni siku nyingine tena, tunakutana katika Uwanja wa Huba, kwa ajili ya kupeana mawili matatu juu ya mambo ya mapenzi. Ni imani yangu kwamba mtakuwa wazima wa afya njema tangu tulipoachana Jumamosi ambapo nilimalizia mada ya jinsi ya kudumisha penzi la mbali...
HUENDA mambo yakawa mazuri na historia kwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ iwapo ‘atakaza buti’ baada ya kupata nafasi nyingine nchini Sweden ambayo akiitumia vizuri, basi atakuwa ameula...
KOCHA wa makipa wa timu ya taifa, Taifa Stars, Juma Pondamali amemtaka kocha mkuu wa Yanga, Kosta Papic kuiga mfano wa kocha wa Simba, Patrick Phiri, kuibadili timu yake kutoka kwenye ziro hadi 100...
BAADA ya kipigo cha Simba, Kocha Mkuu wa Yanga, Kosta Papic ameamua kuigawa timu yake katika vipande vitatu na kila mchezaji atakuwa akiingia kwenye kundi husika kutokana na juhudi zake...
WAKATI kikosi cha Taifa Stars kinaondoka leo kwenda katika mji wa Aswan nchini Misri kuwavaa wenyeji, Kocha Mkuu, Marcio Maximo amewaonya mabeki wake wa kati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Salum Sued kwamba wanapaswa kuwa makini na ushindani wa namba...
Mpelelezi Vivian anafanikiwa kuwatorosha Josia na Janeth kwenda hadi Bangalore, India baada ya kugundua kuwa ni ndugu zake. Watu hao wawili ndio walikuwa wamekabidhiwa jukumu la kuwasaka wakituhumiwa kwa wizi wa fimbo ya Bunge iliyotengenezwa kwa madini yenye thamani kubwa. Akafanikiwa kuwakamata na wakakiri.
Katika maongezi yao ndipo ilithibitika kuwa vijana hao wawili ni watoto wa Aminatha, ambaye siku za nyuma aliwahi kuitwa Mwajuma lakini alipopewa mimba na mwalimu wake shule ya msingi alikimbilia mjini na kujifungua mtoto lakini akamtelekeza, huyo ndiye Vivian ambaye baadaye alilewa kwenye kituo cha watoto yatima na kuchukuliwa na familia ya Kijerumani kwenda kuishi huko, huko ndiko alisoma mpaka kuwa mpelelezi.
Hitaji lenye kuuma (Painful Demand) ambalo Josia na Janeth wamemwomba Vivian ni kutowafikisha mbele ya sheria ingawa kweli waliiba fimbo hiyo ikiwa njia ya kupata haki yao, kwani baba yao mzazi mzee Emmanuel Lugoye, aliitumikia serikali ya Jamhuri kwa uaminifu wa hali ya juu bila kuiba mpaka alipopatwa na ugonjwa wa Kiharusi na baadaye kufa akiwa masikini.
Josia na Janeth wako Bangalore, wamefichwa kwenye shamba la Jonti wakimsubiri Vivian afike ndipo waanze zoezi la kuwasaka wezi wa fimbo, wanaamini wako nchini India lakini hawafahamu katika jimbo gani! Vivian amelazwa hospitali akitibiwa majeraha ya risasi aliyojipiga mwenyewe pajani na kusingizia alitekwa na Josia pamoja na Janeth ndipo wakatoroka, jambo ambalo halikuwa ukweli na ameahidi kuungana nao nchini India kwa ajili ya kazi moja tu ya kuwasaka wezi wa fimbo siku kumi na nne baadaye. Je, nini kitaendelea? Watakamatwa? SONGA NAYO…
Naomba mnisaidie jambo moja ambalo linanitatiza sana. Hivi mnaposema wabunge tutazibwa midomo kwa kuhojiwa mna maana gani? Kama mbunge ni msafi na akaenda kuhojiwa na takukuru na kutoa ushirikiano ni lipi litamziba mdomo kuendeleza libeneke la kupambana na ufisadi? Atakaezibwa mdomo ni yule tu mwenye makosa/dhambi na akakubali kubadilishana dhambi na serikali - yaani Mbunge ambaye ana mdomo sana, anaitwa na serikali na kuonyeshwa faili lake lenye madhambi na madudu yake. Wanakubaliana kaa kimya na
Kombe la dunia Ramani ya ziara kamili ya kombe hilo Ndege aina ya Boeing 727 inayosafirisha kombe hilo
Na Hemed Kisanda SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limetangaza kuwa ziara ya Kombe la Dunia kwa nchi za Afrika inaendelea vizuri na kwamba hakuna matatizo yoyote yaliyotokea tangu kuzinduliwa kwake nchini Uswiss na kuanza ziara katika bara hilo nchini Misri...
Serikali ya Marekani imeahidi kuipatia Tanzania dola milioni 37.7 za nchi hiyo kwa ajili ya kuimarisha uchumi ambao uliathiriwa na mtikisiko wa uchumi duniani...
MKAZI wa kijiji cha Kindo, Kibosho mkoani Kilimanjaro, Tadeus Joseph (38), anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Rariki Mushi, kwa kumkatakata kwa shoka kichwani kisha kumpasua tumbo na kumla nyama...