Ajabu nilijikuta nikimchukia sana tofauti na zamani, sikupenda kumwona pale siku ile. Bila kunielewa nilimuuliza swali, hata sijui nililitokea wapi na kupita mdomoni mwangu...
Sueya baada ya ubaya wake aibu imemkuta, baada ya matibabu anarejea nyumbani na kushangazwa na watoto ambao anaelezwa historia yake inayochubua jeraha moyoni mwake na kuwa kielelezo cha ubaya wake. Ni kielelezo gani? TUWE PAMOJA...
Kwa mara nyingine gazeti lako la Risasi linakuletea simulizi nyingine yenye kukusisimua na kukupa mafunzo ili usirudie makosa aliyofanya mwenzako. Ni kweli kila mwanadamu ameumbwa akiwa si kamili ndiyo maana hufanya makosa ambayo kutokana na ufahamu aliopewa na Mungu ni vigumu kurudia kosa kwa vile hata muumba humsamehe asiyejua kama anatenda kosa...
Binti aitwaye Tracy anapanda basi kutoka jijini Dar es Salaam mpaka kijiji kiitwacho Zinga ambako anazama porini kwenda msituni kwa lengo la kujiua! Msichana huyo ni mjamzito wa miezi tisa, akiwa mtini amekwishavaa kamba shingoni anamkumbuka mtoto aliyemo tumboni mwake na kuamua kuahirisha kitendo hicho, akashuka mtini na baadaye kuruka, mtikisiko wa tumbo ndio uliosababisha uchungu uanze.
Mbele akitembea kwenda barabarani, maumivu yanazidi akashindwa kabisa na kuamua kulala chini, baadaye akaamua kutambaa mpaka mbele ambako alijifungua mtoto mmoja na kuamua kumwacha porini kwa sababu mwili wake haukuwa na nguvu.
Akaendelea na safari yake kwa kutambaa, huku akivuja damu nyingi kupita kiasi, mbele tumbo likaanza kumuuma tena na kujikuta akisukuma na kuzaa mtoto wa pili! Hakujua alikuwa na watoto pacha. Akazidi kusonga mbele akimwacha pia mtoto huyo porini kwa imani kwamba akipona atakakuja kufuatilia watoto wake au akikutana na msamaria mwema atamwelezea jambo ambalo halikutokea kwani alipofika barabarani alikuwa taaban, akaanguka chini na kupoteza fahamu.
Mtu mmoja alifika na kumwona, akadhani amegongwa gari akasimamisha gari na kumchukua hadi hospitali ya Bagamoyo ambako iligundulika amekwishakufa! Hakuna aliyejitokeza kutambua maiti, wala aliyeelewa Tracy alizaa watoto pacha porini kabla ya kufika barabarani. Akazikwa na Halmashauri ya Jiji la Bagamoyo bila kuelewa alikotokea. Huo ndio ukawa mwisho wake. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
Hatimaye Dk. Laurian na mke wake Dk. Clara aliyeamua kuchukua kazi ya utafiti wa ugonjwa wa Chinese Encephalitis kwa lengo la kwenda kumtafuta mume wake wanakutana porini, hali ya Clara ikiwa mbaya kwa ugonjwa huo huo, Dk. Laurian anamchoma sindano ya Immuno Booster ili kuziamsha kinga zake angalau ziweze kupambana na virusi vya ugonjwa huo, ndio mbinu aliyoitumia yeye kujiokoa na kifo baada ya kugundua kinga ya ugonjwa huo porini.
Baada ya hapo akambeba kwenye gari lake na kuendesha kwa kasi akijaribu kuwahi Kinshansa ambako anaamini watapata msaada, lakini kilometa chache mbele anashangaa kuona gari lake likitoa moshi mwingi, akashuka na kwenda kufungua boneti bila kujua rejeta ilikuwa imechemka kupita kiasi baada ya gari kuishiwa maji! Mfuniko wake ukafunguka na maji ya moto kummwangikia usoni na kifuani, Dk. Laurian akaanguka chini akipiga kelele kuomba msaada lakini hakuwepo mtu wa kumsaidia.
Alilala hapo mpaka siku iliyofuata ndipo akajitahidi kunyanyuka na kupapasa mpaka kwenye gari ambako alichukua boksi la Immuno Booster na kutoa chupa moja pamoja na bomba la sindano, maumivu yake yalikuwa makali na hakuwa na uwezo wa kufumbua macho, uso wote ulikuwa umevimba! Akavuja dawa hiyo na kumchoma Dk. Clara, akashangaa kusikia akipiga kelele na baadaye kumuuliza alikuwa nani, Dk. Laurian akataja jina lake, Dk. Clara alipofumbua macho yake kumwangalia hakuamini, kwani sura ilikuwa imevimba na uso wote umeungua ingawa sawa ilikuwa ni ya Dk. Laurian, akamuuliza kama alikuwa Laurian kweli.
Simu yangu ilikuwa na wakati mgumu sana mara baada ya gazeti la Risasi Mchanganyiko kutoka Jumatano iliyopita. Wasomaji wengi sana waliamua kuchangia mada hii. Kwa bahati nzuri (kama nilivyotarajia awali), wachangiaji wengi walikuwa mastaa na walio katika uhusiano na mastaa...
Chama cha michezo ya jadi nchini (CHAMIJADA), kimepata mwaliko wa kushiriki tamasha la mashindano ya kucheza mchezo wa bao nchini Italy kuanzia Novemba 21 mpaka 22 mwaka huu.
Timu ya wacheza bao sita na viongozi watatu, wanatarajiwa kuingia kambini kesho kwenye kambi iliyopo Wapi Wapi Bar, Temeke, Chang’ombe, jijini Dar es Salaam, kabla ya kuondoka nchini Novemba 18 mwaka huu.
Mwenyekiti wa CHAMIJADA, Monday Likwepa, akisistiza jambo wakati akiwajuza taarifa hizo waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari, MAELEZO, jijini Dar es Salaam.
ZA MWIZI AROBAINI! Mlinzi wa jengo la IPS lililopo eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam (kulia) akimtia mbaroni mwanadada anayedaiwa kujihusisha na shughuli haramu za utapeli kwenye jengo hilo leo mchana. PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL
Unaweza ukadhani hapa ni Darfur nchini Sudan lakini ukweli hili ni eneo la makazi katikati ya jiji la Dar es Salaam lilipo eneo la Chang’ombe, wilayani Temeke .Wakazi wa eneo hili wamekuwa wakiishi maisha duni baada eneo hilo kuchukuliwa na mwekezaji mmoja na pesa zao za fidia zilizotolewa awali na mwekezaji huyo kutafunwa na vigogo hali iliyosababisha wakazi wa eneo hilo na mwekezaji kuwa katika mgogoro mkubwa. Sakata hilo limedimu kwa zaidi ya miaka kumi na tisa sasa. Mbali na kuishi maisha duni wakazi hao pia wapo katika eneo la hatari kwani wamezungukwa na matanki ya mafuta ya Petroli pamoja na kemikali zinazotoka katika viwanda vinavyozunguka eneo hilo.Hebu tazama picha hizi 8,9,10 na 11 ujionee jinsi watu hawa wanavyoteseka. ...8
Lile sakata la mishahara mipya kwa wafanyakazi nchini, linaendelea kutikisa ambapo hii leo wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza Nondo cha QUAIM STEEL MILS LTD Chang’ombe jijini Dar es Salaam wamegoma kuendelea na kazi wakiushinikiza uongozi wa kiwanda hicho kuanza kuwalipa mishahara yao mipya kama ilivyotangazwa na Serikali. Jumla ya wafanyakazi 150 walihusika na mgomo huo kuanzia asubuhi ambapo Polisi wa kutuliza ghasia walifika kiwandani hapo na kuwatawanya. Muda mfupi baada ya mgomo kuanza uongozi wa kiwanda hicho ulitoa tangazo la kuwataka wafanyakazi wote wenye msimamo wa kugoma kuchukua barua za kuacha kazi mara moja na kuondoka kiwandani hapo na wale wanaotaka kuendelea na kazi kujiorodhesha. Zaidi ya wafanyakazi 35 walisaini barua za kuacha kazi huku wengine wakiwa hawaelewi cha kufanya na wengine wakirejea kiwandani kuendelea na kazi. Pande zote mbili yaani uongozi wa kiwanda na wafanyakazi waliogoma wamekilaumu Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda (TUICO) mkoa maalum wa Temeke kwa madai ya kuchochea mgomo huo.
Sehemu ya kiwanda cha Nondo.
Tangazo maalum la onyo kwa wafanyakazi
Mabosi wa kiwanda hicho, (kulia) ni Meneja Mkuu wa kiwanda hicho Mohamed Bharvan akiwa pamoja na Afisa Utawala Bw. Kara Remtullah wakitoa ufafanuzi wa mgomo huo kwa waandishi wa habari hii (hawapo pichani) leo.
Baadhi ya wafanyakazi waliogoma wakiwa katika mkutano wa pamoja kwenye baa moja jirani na kiwanda hicho kujadili hatma yao.
Kufuatia mgomo huo uzalishaji kiwandani umedorora.
Baadhi ya wafanyakazi hao waliogoma wakiwa nje ya ofisi za TUICO Chang’ombe Maduka mawili Dar kufuatilia haki zao.
Hii ni sauti ya Wanyonge ambayo ni sawa na kilio cha samaki Je, nani atawasaidia?
PICHA NA VIDEO: CHRISTOPHER LISSA NA ISMAIL MANG’OLA/GPL
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema, Baraza la Mawaziri litajadili hali ya uendeshaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ili Serikali ifanye uamuzi. Rais Jakaya Kikwete ni mwenyekiti wa baraza hilo...
SAFARI ndefu ya mjadala mzito wa kashfa ya Richmond iliyotikisa nchi , sasa inakaribia ukingoni baada ya taarifa ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kupangwa kuwasilishwa kesho kwenye chombo hicho...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba.
*Aporomosha matusi dhidi ya Anne Kilango *Mpendazoe amchambua anavyoenzi mafisadi *Kikwete, Pinda wapongezwa kwa kumvumilia *Amtukana pia Mengi aliyempa Sh. 5m za uchaguzi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, ametia aibu. Hali hiyo imedhihirika kutokana na kauli za matusi ya nguoni alizozitoa mbele ya Kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, kuchunguza uhasama miongoni mwa wabunge wa CCM na dhidi ya serikali yao ilipokutana na wabunge wa chama hicho juzi...
Na Mwandishi Wetu Tafsiri nyepesi ya uhusiano wa mapenzi kwa mastaa ni ìhuyu leo yupo na yule kesho kamdaka mwingine ndani ya bwawa mojaî ndiyo maana majina mengi yanajirudia katika kila mtandao wa ngono, hivyo kuzidi kuibua shaka ya kuibuka kwa maumivu ya wengi kama matumizi ya kondomu hayatazingatiwa...