Na Saleh Ally KOCHA Mkuu wa Yanga, Kosta Papic ametoa pendekezo kikosi chake kiweke kambi nje ya Tanzania kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom na Afrika Kusini ndiyo chaguo lake la kwanza...
Khadija Mngwai na Samira Phillip WAKATI Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Joel Bendera akishindwa kutoa maoni yoyote juu ya kipigo cha mabao 5-1 cha Taifa Stars dhidi ya Misri, Kocha wa zamani wa timu hiyo, Syllersaid Mziray amesema kukosekana kwa wachezaji Haruna Moshi ‘Boban’ na Athumani Idd ‘Chuji’ ni sehemu ya tatizo lililosababisha kipigo hicho...
Na Saleh Ally MECHI ya leo dhidi ya Mjolden na ile ya marudiano ya Jumamosi ijayo ndiyo itakayotoa jibu iwapo kikosi cha Kongsvinger anayochezea Mtanzania, Henry Joseph Shindika kitakuwa kimepanda hadi Ligi Kuu nchini Norway au la...
Na Khadija Mngwai KOCHA Mkuu wa timu ya Maji maji ya Songea, David Mwamwaja amempigia debe mlinda mlango wake Said Mohammed kuwa ni mmoja kati ya makipa bora nchini na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo amtupie jicho...
Na Mwandishi Wetu KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Vasalund ya Sweden, Athuman Machuppa amesema ana imani na matumaini ya juu kuwa timu yake hiyo itapigana nla kurejea hadi Ligi daraja la kwanza msimu ujao...
Na Shufaa Lyimo UONGOZI wa timu ya soka ya JKT Ruvu unatarajia kuongeza wachezaji wanne ili kuimarisha kikosi chao itakapofika wakati wa dirisha dogo inayoanza Novemba 20...
Vivian anawaongoza Josia na Janeth pamoja na kijana mmoja wa Kihindi waliyepewa na Jonti hadi Mysore Palace ambako wamezima umeme kwenye Main Switch na kufanikiwa kumfunga kamba mfanyakazi aliyekuwa kwenye chumba cha Vito, ambamo fimbo ya Bunge ikiwa imevunjwavunjwa imewekwa na kuichukua hadi nje kisha kuondoka na gari lao kurudi kwenye nyumba waliyofikia.
Muda mfupi tu baada ya kuingia wanaona kwenye luninga picha zao zikionyeshwa, kumbe kila mtu ambaye aliingia ndani ya jumba hilo hupigwa picha, ndizo zinazoonyeshwa kwenye luninga wakitafutwa kwa udi na uvumba, zawadi ya dola elfu kumi imetangazwa kwa yeyote atakayewezesha kukamatwa kwao. Je, watakamatwa? SONGA NAYO…
Ukumbi maarufu kwa burudani jijini Dar es salaam, Club Maisha uliyopo Oysterbay umeteketea kwa moto mchana huu. Habari zilizopatikana muda mfupi uliyopita kutoka eneo la tukio zinasema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa nane adhuhuri na ukumbi mzima wa disco umeteketea kabisa!!! Ukumbi huo ulifanyiwa ukarabati mkubwa hivi karibuni na ulikuwa ni ukumbi unaochuana na Club Billicanas kwa viwango na upigaji disco. Picha za tukio zima ni kama zifuatazo:.
Bi. Hellen Swai
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka, ambaye bendi yake ya African Stars imekuwa ikipiga muziki wa dansi katika ukumbi huo mara kwa mara, akimfariji mmiliki wa disco hilo Bi. Hellen Swai ambaye alionekana kuwa na majonzi mazito kwa kupatwa na janga hilo ambalo hadi sasa chanzo chake hakijajulikana.