MSANII nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khaleed Mohamed ‘TID’ ameibuka hivi karibuni na kusema kuwa mkali mwenzake, Abubakar Katwila ‘Q-Chilla’ alitaka kumuangamiza kwa kumzushia sifa mbaya zilizolenga kumharibia jina hapo awali...
UMOJA wa kundi lolote ni sawa sawa na umoja wa viungo mbalimbali vya mwili au mtambo. Viungo vya mwili havina budi vitii kanuni zinazoviwezesha kufanya kazi yake sawa sawa, lakini haviwezi kutii kanuni hizo kama haviko katika hali ya afya njema. Mara kiungo kimoja kinapokuwa hakina afya nzuri, huanza kuvunja kanuni za kazi na mwili mzima hupata tabu...
Mpenzi msomaji, wiki iliyopita nilianza kuwaletea mkasa mpya unaomhusu kijana Mohamed Geni mkazi wa Dumila Kilosa mkoani Morogoro ambaye katika safari yake ya maisha, anadai amekumbana na mkasa wa kubambikiwa kesi ya kubaka ambayo hatoisahau maishani kwani imemuharibia maisha yake msaidia dada huyo aliyekuwa akizongwa na wahuni na kumpeka katika gesti moja alikolala na siku dada huyo aliendelea na safari yake. Ilikuwaje mpaka akajikuta akitumikia kifungo cha miaka 30 gerezani? Ungana na MWANDISHI WETU KULWA MWAIBALE katika mkasa huu wa kweli…
Mizimu walemavu wa ngozi ambao Steven Kunjumu (baba wa Theresia) aliwaua na kuuza viungo vyao, inaamua kulipa kisasi kwa kumuua Steven na mke wake na baadaye kumwingia mwanae Theresia na kumfanya awe akiua watu kwa nguvu za kichawi bila yeye kufahamu ili kuipatia mizimu hiyo chakula chake ambacho ni damu.
Theresia bila kujielewa anaua wanafunzi wenzake katika shule alizokuwa akisoma, ana nguvu katika macho ambazo akikuangalia sana, unaanguka chini na kufa! Hili limefanya shule nyingi nchini Tanzania zimkatae, ndipo akahamishiwa Zimbabwe wasikomfahamu ambako pia amewaua wanafunzi wenzake wote isipokuwa Albert mpenzi wake, aliokuwa akisafiri nao ndani ya basi kwenda kwenye mbuga ya Hwangwe kwa safari ya mafunzo.
Alijigeuza Popo na kuua mwanafunzi mmoja baada ya mwingine, alipotakiwa na mizimu kumuua Albert alikataa katakata, wakatembea porini wakikimbia mpaka baadaye walipookolewa na maaskari wakiwa wameumwa na nyoka na kukimbizwa hadi Harare ambako walilazwa kwenye hospitali ya Perirenyatwa na kupatiwa matibabu, Albert akawa wa kwanza kuzinduka na baadaye kuruhusiwa kwenda nyumbani, akimwacha Theresia bila fahamu.
Watu hawakuelewa kwamba katika muda aliokuwa hana fahamu, kilichokuwa kikimsumbua sio sumu ya nyoka bali mizimu ilimchukua na kumpeleka chini ya bahari ambako alitakiwa kumuua Albert lakini Theresia alikataa kabisa na kuwa tayari kufa yeye kama mizimu iliona inafaa kufanya hivyo! Mwisho aliachiwa na kutakiwa kutekeleza suala hilo, hapo ndipo akafumbua macho yake na kujikuta yuko wodini, kando yake akiwepo Albert, bibi yake na ndugu wengine.
Kila mmoja alifurahi, baadaye Theresia na Albert waliketi chini na kuongea, kijana huyo akijaribu kumuuliza Theresia kama yeye ndiye alikuwa Popo aliyeua wanafunzi wote porini, kwani kwa kumbukumbu zake Albert alimsikia Theresia akitamka maneno hayo kabla hajapoteza fahamu kando ya mto! Theresia aliposikia maneno hayo badala ya kujibu alianza kulia kwa uchungu, akamwangalia Albert na kumkazia macho, mwanga mkali ukatokeza baada ya macho yake kubadilika na kufanana kama Paka, sauti nzito ilisikika ndani ya Theresia ikisema “Tunahitaji damu yake, huu ndio wakati kabla hajatoboa siri, vinginevyo wewe ndio utakufa maana tulikuambia usimwambie mtu yeyote siri hii lakini ukakiuka” Je, nini kitatokea? Hatimaye Theresia kaamua kumuua Albert ampendaye? SONGA NAYO…
MANENO haya ya ukiri wenye kujenga na kutia moyo yako mengi, yaweze kuwa ni maneno yaliyosemwa na watu mashuhuri, au wahenga (nahau), yaweza kuwa maneno kutoka vitabu vitakatifu au nyimbo fulani n.k. Nitajaribu kutoa mifano michache hapa...
WENGI wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema kwamba, idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni...
Kibaka mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Omary Nuru mkazi wa Msasani jijini Dar es Salaam, Hatimaye amebadilisha useme wa zamwizi arobaini na kufanya watu waone zake ni 80 usemi huo ulikuja ghafla mara baada ya kukwapua simu na fedha kwenye duka la jamaa aliyejitambulisha kwa jina moja la Mudy mkazi wa Sinza Makaburini na kuchezea kichapo kikali kutoka kwa wananchi waliokuwa na hasira na kisha kuachiwa huru!!
Kibaka huyo akiwa amekalishwa chini na wananchi muda mfupi baada ya kula kumkong’oto wa kutosha.
Baadhi ya wananchi wakijaribu kumpeleleza alikoficha ‘kilongalonga’ na fedha alizoiba muda mfupi kabla ya kunaswa.
Wananchi wenye hasira kali wakiwa wamemuweka mtu kati baada ya kupokea kichapo.
Uchunguzi usio rasmi umebaini kuwa idadi ya ndege aina ya Tausi waliokuwa wanafugwa katika bustani mbalimbali jijini Dar es Salaam imepungua. Hii ni tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa ni kawaida kuona ndege hawa wenye mvuto wakiruka kwenye bustani hizo hasa maeneo ya Ikulu na kuwa kivutio kikubwa kwa wapita njia. Pichani ni Tausi aliyenaswa na kamera yetu akitembea peke yake kama mkiwa katika bustani za Karimjee tofauti na awali ambapo ilizoeleka kuwakuta wakitembea kwa makundi.
BONGO MSOTO MKALI! Kijana huyu anayedaiwa kufanya shughuli za vibarua alinaswa na kamera yetu leo mchana akiwa hoi kwa uchovu na kuamua kuuchapa usingizi chini ya mti baada ya kufanya kazi nzito mchana kutwa katika jumba la Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari jijini Dar es Salaam leo wamechuana vikali katika mashindano ya Chemsha Bongo kuhusu masuala ya kodi. Shindano hilo limefanyika katika ukumbi wa Karimjee na liliandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Tanzania Youth Cultural Organisation (TAYCO).
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika shindano hilo.
Msanii anayekuja kwa kasi katika muziki wa kizazi kipya, Angelis Faber 'Enji' (katikati) akiwa na wanafunzi wenzake wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Green Acres High School. Kushoto ni Mujuni Mukolera na kulia ni Rose Lawrence wakiwa ndani ya ukumbi wa Karimjee wakishiriki shindano hilo.
Miss Tanzania namba mbili 2006/7, Jokate Mwegelo (kushoto) ‘akipiga chabo’ kumtafuta mwenzake aliyepotezana naye ndani ya jengo la Karimjee. Mrembo huyo alifika katika jengo hilo kama mmoja wa wageni waalikwa katika shindano hilo.
Jengo la Ukumbi wa Karimjee ambamo shindano hilo limefanyika. PICHA: RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA /GPL
Salamu zangu nataka ziwafikie wapenzi wangu wote, enzi za Stono Musica wajela jela original...., ni mimi mwenyewe mzee wakukaanga chips, Christian Magic a.k.a mai mai, kutoka Austria...
• Ajabu wanaopiga vita ufisadi ndiyo wenye kusakamwa Na Walusanga Ndaki
DHORUBA inayoendelea hivi sasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni dhahiri imevutia nadhari za Watanzania wengi –- wanachama wa chama hicho, watu wanaokiunga mkono na watu wengine ambao hawahusiki na chama hicho bali wamekuwa wakifuatilia matukio hayo katika chama hicho ambacho kimeitawala nchi hii tangu mwaka 1961 hadi sasa...
Msanii wa muziki wa kizazi kipya na vichekesho, Mc Babu Ayub, jana alitangaza rasmi kuingia kwenye muziki wa mipasho baada ya kuzindua kibao chake kiitwacho ‘Chaja ya Kobe’. Babu Ayub alikizindulia kibao hicho ukumbi wa Travertine uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam.
Babu Ayubu akizindua kibao chake jukwaani.
KAMA NI VIMINI HII BALAA! Wanenguaji wa bendi mbalimbali hapa nchini wanazidi kujianika nusu-uchi jukwaani kama kamera yetu ilivyomnasa mnenguaji wa Bendi ya Akudo Impact, Nancy Lohuma, alivyokuwa akijiachia jukwaani katika bonanza lililofanyika Msasani Beach Club jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mashabiki wa Akudo Impact, wakiserebuka katika bonanza la bendi hiyo lililofanyika Msasani Beach Club.
Uonevu, mateso,manyanyaso,chuki na roho mbaya anavyofanyiwa mtu huhifadhiwa katika mfumo mkuu wa akili na kumbukumbu zake huendelea kujirudiarudia katika kipindi chote cha maisha ya mtu aliyetendewa yote haya. Kumbukumbu hizi hupelekea nafsi ya mtendewa kuwa na ari kubwa ya kulipa kisasi, na kisasi kinapokomaa huwa kisasi cha damu…The Blood Revenge.
Kijana Khaleed anapitia mateso makubwa sana maishani mwake baada ya familia yao kusambaratishwa na watu wenye uchu wa pesa na kumiliki mali. Wazazi wake wote wawili Bwana Khalfan na Bi Miriam wanauliwa kikatili na anashuhudia yote haya kwa macho yake.
Wadogo zake nao wanakufa vifo vya kikatili sana huku kaka yake wa hiyari Girbons akikatwa mkono na watu wanaotafuta viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi. Matukio haya ambayo yanamtokea akiwa bado kijana mdogo kabisa yanamfanya Khaleed kutoroka kutoka nchi yake aliyozaliwa na kukimbilia Tanzania kutafuta amani wakati akijipanga upya kurudi kulipa kisasi.
Anajikuta akifika katika machimbo ya madini ya Tanzanite huko Mererani mkoani Arusha ambako kama bahati anafanikiwa kutoroka na jiwe kubwa la madini ya Tanzanite. Licha ya kuonekana na walinzi wa mgodi, akiwa na rafiki yake mwenye asili ya kimasai wanafanikiwa kutoroka mpaka mbali kabisa na machimbo.
Kwa bahati mbaya wakiwa njiani, rafiki yake anakamatwa na wale walinzi kwa kushirikiana na polisi na anawekwa chini ya ulinzi mkali. Khaleed anajitosa na kuruka kwenye bonde kubwa lakini kama muujiza anajikuta akinasa kwenye matawi ya miti iliyoota kwenye ukuta wa bonde lile la kutisha. Anafanikiwa kujinasua lakini baada ya kufika juu kabisa anajikuta akiangukia mikononi mwa mtu hatari. Malizia sehemu hii ya mwisho ya Part I…
Mahakama ya Rufani wiki hii, inaweza kueleza chochote kuhusu rufani ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake nane, waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi...
WAFUASI wa Chama cha Wananchi (CUF) wa kisiwani Pemba, wameungana na wenzao wa Unguja kutounga mkono hatua ya chama hicho kuikubali Serikali ya Rais Amani Abeid Karume ikiwa na lengo la kumaliza tofauti za kisiasa baina ya chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM)...