Na Saleh Ally KOCHA Mkuu wa yanga, Kosta Papic amefungua milango kwa wachezaji wenye uwezo ambao wanaamini wanaweza kuwa msaada mkubwa iwapo watasajiliwa katika kikosi chake wakati wa dirisha dogo la usajili...
Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa tovuti ‘blog’ ya www.mohammeddewji.com/blog, Mohammed Dewji ambaye ni Mbunge wa Singida Mjini (CCM) amesema blog yake imekuwa haraka haraka na kufikia kupata watu 5000 wanaotembelea kila siku...
Na Mwandishi Wetu DAKTARI anayemtibu kipa namba moja Yanga, Obren Cuckovic amemtaka kupumzika nje ya uwanja wa wiki sita kabla ya kuanza mazoezi ya taratibu...
Na Saleh Ally Klabu nyingine mbili zimemuomba kiungo mshambuliaji aw Simba, Haruna Moshi 'Boban' kujumuika nazo na kufanya majaribio kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Akizungumza na Championi Jumatano juzi saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Boban alisema anatarajia kumaliza majaribio leo katika klabu ya Kalmar FF na kuna klabu nyingine mbili zimempa nafasi...
Na Saleh Ally KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema atasikia faraja kubwa iwapo kikosi chake kitashinda mchezo wa mwisho mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar na mingine minne baada ya kuanza kwa mzunguko wa pili ili afikie na baadaye kuivunja rekodi yake aliyowahi kuiweka nchini Zambia...
Josia, Janeth na Vivian wamefanikiwa kuipata fimbo ya Bunge kwenye jumba la kumbukumbu liitwalo Mysore Palace, lililoko katika jiji la Mysore na kuondoka nayo mpaka kwenye nyumba waliyofikia nje kidogo ya jiji la Bangalore.
Muda mfupi baada ya hakufika hapo wanawapigia simu Nilesh na Kumar, Wahindi waliomtapeli Josia na kuondoka na fimbo hiyo kwenda kuiuza Mysore kwa mamilioni ya dola, wao wakiwa wamempa dola bandia! Bila kujua ambacho kingetokea Wahindi hao walikwenda mpaka kwenye nyumba hiyo wakijua wanakutana na wafanyabiashara wa madini kutoka Kongo, wakajikuta wanatekwa na Vivian, Josia na Janeth ambaye alifyatua risasi mbili hapo hapo, zikawapata mapajani.
Muda mfupi baadaye magari yakaunguruma nje ya nyumba, Vivian alipofungua alikutana na wazungu walioongozana na maaskari wa Kihindi, alipotaka kujua walikuwa ni akina nani, wakamjibu “Scotland Yard” wapelelezi kutoka Uingereza. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Wanasema "Picha moja ina maneno Elfu Moja".....angalia hii picha jinsi Eliza alivyopagawa mara baada ya 'kumuona' huyo kijana,,,sijui ni huyo mwenye dread kichwani au mwenye kipara...sijui...wewe unafikiri kilichompagawisha hapa ni nini? Ni wakati akitoka mjengoni Jumapili iliyopita!
Kufuatia kuongezeka kwa watu omba omba katika maeneo mbalimbali Mkoani Morogoro huku wengine wakiwa hawana vigezo vya kufanya hivyo, wananchi wameamua kuwageuzia kibao kwa kuwaondoa kwa nguvu katika maeneo wanayofanyia kazi hiyo.
Pichani ni ombaomba mmoja ambaye alilazimika kutumia mbinu ya kujilaza barabarani ili kuwashinikiza watu kumpa msaada lakini janja yake ya nyani hiyo haikuzaa matunda baada ya watu kuamua kumbeba mzobemzobe na kumtupa pembeni mwa daraja la Shani katika barabara ielekeayo Dar es Salaam. Picha: Dastan Shekidele /GPL
Staa wa filamu ‘The Big Name’ Bongo Steven Kanumba ‘The Great’, amedhihirisha kuwa pamoja na fani ya uigizaji, pia anaweza kuwa bonge la mwanamitindo ‘Model’ kama ataamua kufanya hivyo.Msanii huyo aliudhihirishia mtandao huu baada ya’kuvunja’ kabati lake na kuanza kubadili pamba za nguvu kiasi cha kuonekana Model wa ukweli. Hebu cheki picha hizi jinsi mtu mzima anavyong’ara.
Kama kuna suti ambayo mzee Hamis Gabriel Chifupa, ambaye ni baba wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), hayati Amina Chifupa Mpakanjia (wapili kushoto) anaizimia , basi ni hii aliyoivaa pamoja na Sendozi zake. Mara kadhaa akiwa kwenye shughuli maalum Mzee Chifupa hupenda kuvaa nguo hizi, hata hivyo leo amesahau kidogo kifimbo chake kama kile cha Nyerere.Unajua anamwigiza nani? Suti isiyo na kola pamoja na kifimbo humuigiza hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere. Picha hii ilinaswa wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Clouds FM , Alex Kusaga, kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Polisi wa kuzuia ghasia ‘FFU’ maarufu kama Tigo wanaotumia Pikipiki, wakiimarisha doria maeneo ya Kinondoni karibu na Ubalozi wa India kama walivyonaswa na kamera yetu leo mchana. Polisi hawa wamekuwa wakisifika mno kwa utendaji wao mzuri hali iliyosaidia kudhibiti tatizo la uporaji wa magari pamoja na kuimarisha usalama barabarani.
Staa wa muziki wa Hip Hop Bongo, Kala Pina, mwenye fulana nyekundu akiwa na jamaa yake wakiwa katika harakati zao mitaa ya Kinondoni kama walivyonaswa na mpiga picha wetu. PICHA:CHRISTOPHER LISSA NA ISMAIL MANG’OLA /GPL
Mimi ni yule yule Christian Magic wa Austria (mweusi mwenye dread), just to say that I follow ur newspaper by internet everyday, bcs nilikuwa mpenzi wa magazeti ya Global Publishers long time, meseji imporntant kwa musician wote wa Tanzania, muziki si uhuni, muziki ni kazi kama doctor ama mwalimu ect...., ninge waomba wenzetu musician, especially ndugu zangu Wacongo , acheni malumbano, fanyeni kazi kwa umojo, wenzetu pande hii hu fanya kazi kwa umoja, ingawa kila mtu ana company yake. Ma featuring kwa wingi, angalieni vijana wa bongo fleva hu jaribu ku ungana kikazi some times that's why wana endeleya zaidi yetu wazee wazima, featuring I mean, why not band za dansi,...., twanga Fm Academia just nyimbo moja pamoja, Fm, Akudo, ect.. bila iyo bad.o twa cheza apo apo kama myaka zote. Asanteni sana Global Publisher, nilikuwa nimesahauliuka..!
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba
*Yasema Reginald Mengi mwanachama wao halali *Katibu Dar akana kuukataa uanachama wake Siku chache tu baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, kuibuka ndani ya kamati ya kusaka suluhu ya uhasama miongoni mwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kumbeza Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, kuwa si mwanachama wao, Katibu wa chama hicho, mkoani Dar es Salaam, Kilumbe, Ng’enda, amesema Mengi ni mwanachama halali...
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, amepanga kukutana na viongozi wa mitaa, kata na watendaji wa halmashauri za manispaa kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo, kwa ajili ya kujadili pamoja na mambo mengine, kuhusu maandalizi ya kukabiliana na mvua za El Nino...