arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 11.11.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Yanga yaikimbia Simba, ...
» Mpenzi wako anavyoweza ...
» EBWANAEEE, KUMBE CHUO ...
» MISS KIBAHA KUFANYIKA K ...
» Baba alinitoa kafara kw ...
» Profesa Jay atatoka na ...
» KUELEKEA UCHAGUZI MKUU ...

 

Ukimuamini mpenzi wako na kupuuza maneno ya watu, mtadumu milele!

Mahaba  
Ukimuamini mpenzi wako na kupuuza maneno ya watu, mtadumu milele!

KWANZA namshukuru Mungu kwa kunijaalia afya njema na pia kwa kunipa mwangaza wa kuandika hiki ninachokusudia. Lakini pia niwashukuru wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tuliweza kuwasiliana na kushauriana hili na lile katika tasnia hii adhimu ya mapenzi...
    (11 November 2009)
Views: 247 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Kwa nini watu huongea au kufanya mambo wakiwa usingizini?

Saikolojia na maisha  
KUNA watu ambao hutembea, hutazama, hukaa, huzungumza na kufanya baadhi ya mambo huku wakiwa wamelala. Mwanamuziki kutoka Uganda Jose Chamelion aliwahi kuripotiwa kudondoka kutoka ghorofani kwa kile kilichotajwa kuwa ni kutembea huku akiwa usingizini...
    (11 November 2009)
Views: 175 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Niliukubali mkoba wa kichawi ili niwe tajiri!

Mikasa ya kusisimua  
MPENZI msomaji, kabla sijaanza kuwaletea mkasa uliomkuta kijana Kafumu aliyefundishwa uchawi na bibi yake aliyetokea kumpenda sana bila yeye kuelewa sababu za kupendwa sana tofauti na watoto wenzake, nitakueleza baadhi ya mambo aliyofundishwa ili ujue uchawi unavyofanya kazi...
    (11 November 2009)
Views: 613 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Knocked Down? You can stand up 18

hadithi za Shigongo  
Kelvin kijana wa Kitanzania aliyefanikiwa sana katika soka mpaka kujikuta akichezea timu ya Liverpool, kila kitu maishani mwake kinaparanganyika! Kwanza mama yake anagundulika kuwa na kansa ya damu na baadaye kufariki dunia, yeye mwenyewe anapatwa na ajali mbaya ya gari akiwa nchini Uganda alikokwenda kumpokea mchumba wake Martina Weston, mtoto wa tajiri nchini Uingereza, ajali hii ilimfanya apooze kuanzia shingoni hadi miguuni, akawa mtu wa kulala tu.

Baadaye jumba lake la kifahari alilolijenga akicheza mpira linateketea kwa moto yeye akiwa ndani baada ya mfanyakazi wake aliyemtoroka kuacha pasi inawaka, bila kuokolewa na bibi Regina angefia humo maana hapakuwa na mtu mwenye taarifa! Kama vile hiyo haitoshi soko la hisa la Uingereza alikowekeza mamilioni ya Paundi linaporomoka ghafla sababu ya mtikisiko wa uchumi na kujikuta anapoteza kila kitu na kuwa masikini mpaka kujikuta akiishi nyumbani kwa bibi Regina, rafiki wa marehemu mama yake, mwenye kibanda cha mbavu za mbwa akilala kwenye kitanda cha kamba!

Huku ni kuporomoka kwa hali ya juu, inavyoonekana Kelvin atakufa upesi jambo ambalo analikataa kabisa, yeye anaamini ipo siku atanyanyuka kitandani na kucheza soka tena kisha kurudisha utajiri wake uliopotea.
Je, hilo linawezekana? kama aliifahamu vizuri historia ya mama yake mzazi. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (11 November 2009)
Views: 748 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

HABARI ZA KUSIKITISHA

Habari mbalimbali  
Habari za kusikitisha zilizotufikia mapema leo ni maporomoko ya ardhi yaliyosababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kufikia 25, yaliyotokea katika kijiji cha Goha, wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, tukio hilo limetokea baada ya kunyesha mvua kubwa usiku wa kuamkia leo ambayo ilisababisha maporomoko yaliyozikumba nyumba saba zilizokuwa na watu, yumkini wakiwa usingizini.

Hadi mchana huu, jumla ya maiti 15 zimeshapatikana na miongoni mwao 10 ni za kike na 5 ni wa kiume. Jitihada za kunasua maiti nyingine bado zinaendelea. Hili ni tukio la kwanza kutokea katika kijiji hicho na limeacha majonzi makubwa kwa wakazi wake.
    (11 November 2009)
Views: 120 | Maoni (4) |

 

GOLIKIPA ROBERT ENKE AJIUA

Habari mbalimbali  
GOLIKIPA ROBERT ENKE AJIUA

GOLIKIPA ROBERT ENKE AJIUA
Picha mbili hapo juu ni Robert Enke enzi za uhai wake

Golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Ujerumani, Robert Enke amejiua mwenyewe kwa kujigongesha kwenye treni lilikokuwa kwenye spidi kali. Golikipa huyo wa Ujerumani na timu ya Hannover inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, amefariki dunia jana jumanne baada ya kugongwa na treni wakati aliposimama kwenye reli mbele ya treni lililokuwa kwenye spidi ya kilomita 160 kwa saa!
    (11 November 2009)
Views: 162 | Maoni (5) |

 

ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB

photos  
Uongozi wa Maisha Club ambayo mwishoni mwa wiki iliyopita iliteketea kwa moto, leo mchana ulizungumza na vyombo vya habari na kuwatoa hofu wapenzi wa burudani na kuwataka wasiwe na wasi wasi kwani licha ya jengo hilo kuteketea kwa moto, lilikuwa limekatiwa bima ya moto.

Wakati mkutano ukiendelea, kundi la vichekesho la Orijino Komedi lilivamia mkutano huo na kujichanganya na wanahabari ambapo baadaye walirekodi igizo la tukio la ajali iliyotokea mjengoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Klabu hiyo, Hellen Sweya, aliwataka wapenzi wa burudani kuwa na subira wakati uchunguzi wa Jeshi la Polisi, Shirika la Umeme (Tanesco) na wakandarasi wa jengo hilo ukiendelea.

Hellen alisema hivi karibuni wanatarajia kutangaza sehemu nyingine ambayo wataendeshea burudani kabla ya kukamilika kwa ukarabati wa jengo hilo lililoteketea.

ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB
Mkurugenzi wa Maisha Club, Hellen Sweya, akiongea na waandishi wa habari.

ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB
Sehemu ya mabaki ya Maisha Club kama ilivyochukuliwa picha leo mchana.

ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB
Sehemu ya wanahabari wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB
Jokofu la vinywaji likiwa nyakanyaka baada ya ajali hiyo.

ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB
Kundi la Orijino Komedi wakati likivamia mkutano huo.

ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB
Mmoja wa wadau wa ukumbi huo, Malcolm Libaba a.k.a Ras Makuchila, (kushoto) akilia kwa uchungu wakati akihojiwa na Mwandishi Muandamizi wa Mtandao huu, Christopher Lissa.


ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB
Wasanii wa Orijino Komedi, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ (kushoto) na Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkagandamizaji’ wakiwa katika mishemishe kwenye mkutano huo.

ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB
Baada ya kutoka kwenye mkutano wa waandishi wa habari, wasanii hao pichani walianza kurekodi igizo la tukio hilo hapohapo.

ONYO KALI
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo imetoa tangazo linalopiga marufuku mambo mbalimbali ikiwemo kujisaidia, kutupa taka
ovyo na kadhalika ambapo limesema kwamba watakaokiuka amri hiyo watakiona cha mtema kuni. Tahadhari hiyo imekuja baada ya wazoa taka wa maeneo ya Posta kulalamikia kitendo cha kuzoa zaidi ya tolori mbili za kinyesi kila siku.

ZE KOMEDI WAVAMIA MKUTANO WAANDISHI WA HABARI MAISHA CLUB
Sehemu ya tangazo hilo lililobandikwa katika Idara ya Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam.
PICHA: RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA /GPL
    (11 November 2009)
Views: 134 | Maoni (1) |

 

WALIMWENGU WAKUMBUKA KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA

Habari mbalimbali  
WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Mpiga tarumbeta (buruji) kutoka Bendi ya Polisi ya New South Wales huko Sydney, Australia, akipuliza wimbo wa 'Kituo cha Mwisho' katika Siku ya Kumbukumbu ya kusainiwa kwa makubaliano ya kuacha mapigano katika Vita vya Kwanza vya Dunia yaliyofanyika saa 11 (kwa saa za GMT nchini Uingereza, ambayo ni saa tano asubuhi), siku ya 11 na mwezi wa 11 mwaka 1918. Nchi za Jumuiya ya Madola na nyingine duniani, huadhimisha dakika mbili za kukaa kimya ambapo majeshi ya Ujerumani yalisaini Mkataba wa Kusimamisha Mapigano, mkataba ambao ulimaliza Vita vya Kwanza vya Dunia. Siku hii inatumiwa kwa kuwakumbuka askari na raia wote walioangamia katika vita mbalimbali vilivyotokea na vinavyoendelea kutokea duniani.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Bendi ya Polisi ya New South Wales ikitumbuiza katika kumbukumbu hiyo.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Kasisi wa jeshi la Uingereza akiwa tayari kwa sala maalum kwa Siku ya Kumbukumbu kwenye makaburi ya askari wa Uingereza mjini Kabul, Afghanistan, tarehe 11 Novemba mwaka huu.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Baadhi ya makaburi ya Askari wa Uingereza waliofariki nchini Afghanistan.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Kasisi wa jeshi la Uingereza akiendesha sala katika makaburi ya askari wa Uingereza waliofariki Afghanistan.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Askari wa Uingereza wakipigana picha mjini Kabul katika kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu mwaka huu.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Baadhi ya askari wa Uingereza walioshiriki Siku ya Kumbukumbu kwenye makaburi ya askari wa Uingereza mjini Kabul.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Mpiga buruji akiwa katika maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu mjini Melbourne, Australia kwenye Uwanja wa Kingston Heath Golf Club.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Wapiganaji hao maveterani wa Ufaransa wakikumbukia siku hiyo iliyokuwa muhimu sana katika historia ya Vita vya Kwanza vya Dunia mjini Sydney.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Mpiganaji wa zamani katika vita hivyo, akiweka shada la maua katika maadhimisho ya mwaka wa 91 wa Siku ya Kumbukumbu wakati wa sala maalum katika eneo la Cenotaph Martin mjini Sydney, Australia.

WALIMWENGU WAKUMBUKA  KUMALIZIKA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA
Huko Caniberra, Australia, Siku ya Kumbukumbu pia iliadhimishwa kwa shughuli mbalimbali kama inavyoonekana pichani.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA GETTY IMAGES NA REUTERS
    (11 November 2009)
Views: 99 | Maoni (2) |

 

JWTZ, Magereza, Muhimbili, UDSM kugawiwa bure samaki wa 'Magufuli'

Habari mbalimbali  
JWTZ, Magereza, Muhimbili, UDSM kugawiwa bure samaki wa 'Magufuli'

Tani 296.32 za samaki wa ‘Magufuli’ waliokamatwa katika kina kirefu cha bahari ya Hindi, eneo la Tanzania, Machi, mwaka huu, wamepangwa kugawiwa bure keshokutwa...
    (11 November 2009)
Views: 310 | Maoni (10) | Soma Zaidi

 

Dowans matatani

Habari mbalimbali  
KAMPUNI ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Limited (DTL) haitakuwa na kazi kwa siku 10 kuanzia jana.
Hatua hiyo inatokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia dalali wake, Majembe Auction Mart Ltd, kuifungia kwa kuzuia mali zake kwa muda huo hadi kampuni hiyo itakapolipa deni lake la kodi la Sh bilioni 9.1. ...
    (11 November 2009)
Views: 114 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

CNN MULTICHOICE AFRICAN JOURNALIST AWARDS 2010

photos  
CNN MULTICHOICE AFRICAN JOURNALIST AWARDS 2010

CNN International and MultiChoice this week officially launched the CNN MultiChoice African Journalist 2010 Awards. The winners of these prestigious annual Awards will be announced at a gala ceremony to be held in Kampala, Uganda in May 2010.

Tony Maddox, Executive Vice President and Managing Director of CNN International, said: ““It is with great pleasure that we announce the 2010 CNN MultiChoice African Journalist Awards are returning to East Africa. And it is fitting that now in its fifteenth year, the awards are being held in Uganda, a country that has produced so many success stories and winners in the competition’s history. “ Collins Khumalo, [/b]

    (11 November 2009)
Views: 107 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

NI VIONGOZI WAWILI WA KITAIFA. ZITTO APINGA VIKALI

Habari mbalimbali  
NI VIONGOZI WAWILI WA KITAIFA. ZITTO APINGA VIKALI

HATIMAYE yule bundi wa kisiasa ambaye alikuwa akiinyemelea Chadema, sasa ametua rasmi baada ya chama hicho kutangaza kuwatimua maafisa waandamizi wawili ambao ni washirika wakubwa wa naibu katibu mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, ambaye ameeleza bayana kutofautiana na maamuzi hayo...
    (11 November 2009)
Views: 762 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

HAYA KWA WANAOWANIA VISA YA OBAMA!

photos  
HAYA KWA WANAOWANIA VISA YA OBAMA!


New Visa Process for Frequent Travelers

October 2, 2009

Beginning on November 2, 2009, the U.S. Embassy will waive the interview requirement for frequent travelers (B1/B2 visa). and also for students (F visa) and exchange participants (J visa) who are continuing their studies. Visa applicants who meet the requirements listed below may receive a visa by submitting their applications directly to the U.S. Embassy, without a personal interview. The requirements are as follows:

For B1/B2, F, and J visa categories:

* the previous visa was issued on or after November 1, 2007;
* all ten fingerprints were captured at a prior visa interview;
* the previous visa is valid or has expired within the last twelve months;
* the applicant is applying for exactly the same type of visa;
* the previous visa was issued by the U.S. Embassy in Dar es Salaam;
* the applicant’s name is currently the same as on the previous visa; and
* the previous visa does not have “clearance received” written on it.

Additionally for F and J visa categories:

* the applicant must have the same SEVIS number as on the previous visa, and the applicant must submit his/her official transcript.

Visa applications for applicants who meet all of these requirements will be accepted at the Consular Section only on Monday and Wednesday afternoons from 2:00pm to 4:00pm. A courier may submit the applications on behalf of the applicant.

Applicants using this process must complete all necessary forms, submit one photograph, and pay the application fee at Citibank. See the U.S. Embassy website, usembassy.tanzania. gov, for more detailed information on the application process.

If the applicant is qualified, in most cases, the applicants may pick up their passport at the Embassy two days after submission. For example, a successful application submitted on Monday will result in the passport with new visa being ready for pick-up on Wednesday. This new process is a continuation of the U.S. Embassy’s commitment to “secure borders, open doors.”

Please Note: The use of this process does not guarantee visa issuance. In some cases, the Embassy may still require an applicant to appear for an in-person interview, especially if an application is incomplete or inaccurate.
    (11 November 2009)
Views: 132 | Maoni (2) |

 

IRENE UWOYA AZITWANGA KUMGOMBEA KALALA JR

risasi mchanganyiko  
IRENE UWOYA AZITWANGA KUMGOMBEA KALALA JR

Na Waandishi Wetu
La kuvunda halina ubani, mwaga manukato ya gharama lakini harufu itaendelea kuwepo na hiyo inashabihiana na habari yenye mshtuko kwamba, Miss Tanzania namba tano 2006-07, Irene Uwoya ‘amezichapa’ laivu kugombea penzi la Kalala Junior...
    (11 November 2009)
Views: 3475 | Maoni (20) | Soma Zaidi

 

Vunja mbavu

Vichekesho na Udaku  
ZIZINI KWAMPONZA
Kijana mmoja alikuwa na tabia ya kukojoa zizini kila asubuhi.
Kama kawaida siku hiyo asubuhi aliamka na kwenda zizini kumbe alikuwepo baba yake. Baba akamuuliza; ‘Unafanya nini humu zizini saa hizi?
Kijana akajibu; ‘Naangalia kama yule ng’ombe jike mwenye mimba amezaa.’ Akaona akisema anataka kujisaidia mzee wake atamgombeza. Baba yake alimwangalia aliona zipu iko wazi, akamuuliza, ‘ Na hiyo zipu vipi?
Kijana; Nilikuwa nataka kukojoa.
Baba; Hebu kojoa nione kama kweli ulikuwa unataka kukojoa kutokana na ule mshituko na wasiwasi mkojo ukashindwa kutoka. Baba yake akafoka na kutoa onyo.
Baba; Pumbavu unanifanya mimi mjinga! Usirudie mchezo wako huo mchafu, umehangaika sasa umehamia kwenye mifugo yangu.
Kijana alijisikia aibu kwa kudhaniwa alitaka kubaka ng’ombe!

FUNDI CHEREHANI NA BIBLIA!
Fundi cherehani mmoja alikuwa hoi baada ya kuingia mteja wake mmoja mrembo sana! Mrembo huyo alikuja kupima kitambaa ili ashonewe gauni; Ile kumtazama jinsi alivyoumbika, fundi uchu ukamshika.
Basi wakati anampima akawa anaitumia nafsi hiyo kumshikashika mara kifuani, mara hips huku akijichelewesha kumpima taratibu. Yule mrembo kuona vile hakuvumilia, ndipo akamwambia Fundi; We, fundi kumbuka Mathayo 7;7, kusikia hivyo fundi akaogopa kwa kudhani amekutana na mlokole ikabidi kwa hofu asitishe mchezo wake.
Basi alipomaliza kumpima, yule mrembo aliondoka. Fundi haraka sana akachukua Biblia na kuanza kusoma Mathayo 7; 7. Lahaula alikutana na maneno haya; “Ombeni nanyi mtapewa! Pale pale aliitupa Biblia mezani na kutimua mbio kumfuata yule mrembo.
    (11 November 2009)
Views: 116 | Maoni (0) |
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com