Na Saleh Ally KOCHA Mkuu wa Yanga, Kosta Papic amesema Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Marcio Maximo hakumtendea haki yule wa Simba, Patrick Phiri kwa kitendo chake cha kumuita kipa wake namba mbili, Ally Mustapha ‘Barthez’...
Na Saleh Ally WAKATI Yanga inahaha kujua kiungo mshambuliaji mkongwe, Mike Baraza yuko sehemu gani hasa, Championi limeng’amua kila kitu baada ya kugundua anaishi katika hoteli ya Lamada iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam huku kila kitu kikigharimiwa na mmoja wa wanachama wa kundi la Friends of Simba...
Na Phillip Nkini LIGI Kuu ya Tanzania Bara mzunguko wa kwanza inamalizika Jumatatu ijayo huku kwa Yanga kucheza na Prisons, lakini Simba itakuwa na kibarua kigumu keshokutwa Jumapili itakapocheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru...
Na Saleh Ally MLINZI wa kati wa timu ya Memphis Grizzlies inayoshiriki Ligi Maarufu ya Mpira wa Kikapu ya Marekani, NBA, Hasheem Thabeet amesema yuko katika hali nzuri na wala hajavunjika taya kama ambavyo imeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari likiwamo shirika kubwa la habari duniani la CNN...
Na Saleh Ally PAMOJA na kufanikiwa kufanya vizuri majaribio ya kucheza soka ya kulipwa nchini Sweden, viungo kutoka Brazil na Jamhuri ya Kidemokarasia ya Kongo (DRC), wameonekana kuwa kikwazo kwa Mtanzania, Haruna Moshi ‘Boban’...
Na Eunice Macha BAADA ya kufanikiwa kumnasa kipa wa zamani wa Yanga, Ivo Mapunda, klabu ya African Lyon imesema sasa ina uhakika wa kufanya vizuri chini ya mlinda huyo...
Na Mwandishi Wetu MSHAMBULIAJI Thomas Morris ametimuliwa katika klabu ya Majimaji ya Songea kutokana na suala la utovu wa nidhamu na tayari kazi ya kusaka atakayeziba pengo lake imeanza...
Mpelelezi Vivian, Josia na Janeth wanaendesha upelelezi mkali nchini India mpaka kufanikiwa kuipata fimbo ya Bunge katika jiji la Mysore, kwenye jengo liitwalo Mysore Palace, ambako iliuzwa na vijana wawili wa Kihindi waliomtapeli Josia na kumpa dola za bandia (Nilesh na Kumar)
Baada ya kuipata fimbo hiyo wanarejea Bangalore, ambako waliwapigia Nilesh na Kumar simu wakijifanya wafanyabiashara wa madini kutoka nchini Kongo, Wahindi hao wakaingia kichwa kichwa na kujikuta wakiwekwa chini ya ulinzi! Muda huo huo magari yakasikika nje ya nyumba waliyofikia, Vivian akatoka nje na kukutana na wapelelezi wa Scotland Yard wakiwa na maaskari wa India, wakakamatwa na kupelekwa kituo cha polisi.
Huko mawasiliano yalifanyika na kuthibitika kuwa Vivian alikuwa mpelelezi aliyekwenda nchini humo kuwasaka Josia, Janeth, Kumar na Nilesh waliokuwa wakitafutwa kwa wizi wa fimbo ya Bunge kazi ambayo pia Scotland , Kumar na Nilesh waliokuwa wakitafutwa kwa wizi wa fimbo ya Bunge kazi ambayo pia Scotland Yard walikodishwa na serikali ya Tanzania kwenda kuifanya.
Hapakuwa na jambo jingine zaidi ikabidi wasafirishwe mpaka Tanzania ambako walipokelewa kama mashujaa na kupelekwa moja kwa moja makao makuu ya jeshi la Polisi, huko wakakutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ambao waliwapongeza kwa kazi waliyoifanya lakini mwisho Mkuu wa jeshi la polisi aliamuru Josia na Janeth wafungwe pingu na kupelekwa kituo cha polisi kuunganishwa na Nilesh na Kumar ambao tayari walishatangulizwa.
Jambo hili lilimfanya Vivian aanze kujieleza kwa wakuu wake wa kazi juu ya uhusiano uliokuwepo kati yake na Vijana hao, jambo lililowashtua kabisa viongozi wake ni aliposema kwamba ni yeye aliyefanya mpango mzima wa kuwatorosha na baadaya kujipiga risasi ili ionekane kwamba alitekwa. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Na Ally Mbetu Naam, tumekutana tena leo hii ili kupeana machache kuhusiana na mahaba ambayo yametawala maisha yetu ya kila siku. Ukipata bahati ya kumpenda akupendae utajiona hakuna mwenye bahati kama wewe katika dunia...
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Malipula eneo la Chamwino mkoani Morogoro wakiangua vilio baada ya kuwaona wafanyaka wa kikosi cha Zimamoto wakimuopoa mtoto Hawa (1.5) aliyetumbukia juzi Jumanne majira ya saa moja usiku katika shimo lililochimbwa jirani ya nyumba yao kwa lengo la kujenga choo. Wananchi wa mtaa huo waliofurika katika eneo la tukio walijipanga barabarani kwa uchungu na kuangalia gari la Polsi likiondoka na mwili wa marehemu. Mmiliki wa nyumba yenye shimo hilo, Bw. Azani Ngata, anashikiliwa na Polisi kuhusiana na tukio hilo. Mwandhishi wetu alifanikiwa kuzungumza na mtuhumiwa huyo kabla ya kupanda katika gari la polisi.
Katibu Mkuu wa Simba Sports Club, Mwina Kaduguda ‘Simba wa Vita’, akiwa amejibwaga mavumbini baada ya kukosa sehemu nzuri ya kukaa wakati akifuatilia mpambano wa kirafiki wa Simba na Azam uliofanyika Uwanja wa Uhuru hivi karibuni. Wadau wa soka waliokuwa uwanjani hapo walisikika wakilalamikia kitendo cha kutowatengea sehemu maalum ya kuangalia soka viongozi wakuu katika soka kama Kaduguda.
MIJUMBA CHAKAVU ‘CITY CENTRE’ !!! Licha ya Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kupiga vita majengo ya chakavu katikati ya jiji, baadhi ya maeneo hayo yameendelea kuonekana kuwa na majengo hayo ambayo huharibu mandhari ya jiji kama jengo hili lilivyonaswa na kamera leo mchana, Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo jijini.
MWANAMKE ‘ANGEL FACE’ Muimbaji nyota wa kundi la East African Melody, Miriam Allawi akiwa katika pozi na sura yake iliyokolea ‘Angel Face’ na kumfanya aonekana bonge la toto. Miriam alinaswa na kamera yetu hivi karibuni katika onesho la bendi yake lililofanyika ukumbi wa Hotel ya Travertine, Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Mnyange huyo akiwa katika hoteli ya City Paradise ambapo aliongea na waandishi wa habari juu ya shindano la BBA na mafanikio yake kwa ujumla.
Elizabeth akifurahia swali aliloulizwa na waandishi wa habari kuwa ni kwanini alikuwa akichukiwa na washiriki wengine na kupigiwa kura za kutoka nje ya njengo la mashindano mara nne, ambapo alilijibu kwa ufasaha na kusema kuwa yote hayo yalitokea kwa kuwa alikuwa ni tishio kwa wengi.
Akiwa ameshika gazeti pendwa la ‘Amani’ moja ya magazeti yanayochapishwa na kampuni ya Global Publishers, lililokuwa na habari kuhusu fahari ya Watanzania kuhusu ushiriki wake BBA.
Mrembo akiyarudi “magoma” wakati bendi ya Diamond Musica ilipokuwa ikiwapa raha wakazi wa Tabata katika ukumbi wa New Green Park uliopo Mawenzi jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, binti huyo alikuwa chakari baada ya “kunyonya mvinyo” kiasi cha kutosha na kuridhika na hivyo kuonekana kutokwenda sambamba na mirindimo ya muziki husika.
MAJI YANAPOFUATA MKONDO Mnenguaji wa bendi ya muziki wa dansi ya Diamond Musica anayefahamika kwa jina la Hatia na ambaye ni mtoto wa mwanamuziki Rehema Tajiri, anaonekana kufuata njia aliyopita mama yake kwa “kujichimbia” pia katika sanaa ya muziki ambapo ni mnenguaji tishio katika fani hiyo.
USANII KATIKA OMBAOMBA! Mtu huyu anayeonekana kuwa ni mlemavu kwa kujifanya mguu wake mmoja umekatika, ni mzima wa bukheri akiwa na miguu yake yote miwili ambayo huificha kwa kukaa chini wakati wote na kuomba apewe chochote na wapita njia. Usanii huu ni moja za changamoto kwa mamlaka za jiji hili la Lukuvi ambazo zinabidi kutafutiwa ufumbuzi wa mara moja na wa kudumu.
MIKE Tyson, bondia maarufu duniani kutoka Marekani, ametiwa mbaroni kwa kudaiwa kumtwanga konde usoni mpiga picha na mwandishi wa habari (paparazzi) na kumsababishia maumivu na majeraha ambapo alivuja damu nyingi jana jioni katika uwanja wa ndege wa LAX nchini Marekani....