arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 14.11.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» BONGO YAZIZIMA KWA SIMA ...
» MAFISADI EPA WABURUZWA ...
» Afande Sele atangaza ku ...
» HII NDIO BONGO, KARIBU ...
» China yawanyonga waliou ...
» WAZIRI MKUU AKUTANA NA ...
» Waziri Mkuu wa Italia a ...

 

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE

photos  
Eneo la Kinyerezi, Tabata jijini Dar es Salaam, Novemba 12 mwaka huu lilikumbwa na tukio la aina yake kufuatia vita kubwa kuzuka kati ya baadhi ya watu wanaojiita walokole kutoka Kanisa la International Pentecoste Hollyness Church Ebenezer na watu wanaojihusisha na nguvu za giza ‘wachawi’ kupambana uso kwa uso mtaani mchana kweupe.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, walishuhudia vitu vya ajabu vikiruka angani huku nyoka waubwa na wadogo wakitoka katika nyumba ya kijana mmoja aitwaye Kafumu Moto ambaye inadaiwa ni mganga wa jadi tishio katika eneo hilo.
Walisema, tukio hilo lilianza majira ya mchana wakati kundi la walokole zaidi ya 18 likiongozwa na mhubiri maarufu katika eneo hilo aliyetajwa kwa jina moja la Kefa ambaye amepachikwa jina la Jesus, waliposambaa mtaani na kuanza kupiga injili ambayo ililenga kuangamiza uchawi, mapepo na kuleta wokovu katika eneo hilo.

Mashuhuda hao walisema kuwa, pitapita hizo za walokole, ziliishia katika nyumba ya Kafumu Moto ambapo walianza kupiga neno la mungu kisawasawa kitendo kilichomkera mganga huyo kijana na kumfanya naye kuingia ndani na kuvaa magwanda yake ya kazi ya kichawi, kisha kuchukua silaha zake za uchawi wakiwemo nyoka wakubwa na wadogo kisha kutoka nje akiwa na wapambe wake na kuanza kushambuliana na walokole hao.

Inadaiwa kuwa, Kafumu Moto aliamrisha majoka yake kuwashambulia walokole, ambao walitimua mbio na kutawanyika mtaani, huku baadhi yao wakienda kuweka kambi katika kilima kimoja porini kuendelea na maombi yao kwa sauti ya juu.

Mtandao huu ulifika eneo la tukio na kukuta mtafutano kati ya walokole na kundi la mganga huyo ukiendelea vichakani, huku watu wengine wakitimua mbio kuponya nafsi zao .

Hatimaye wahubiri watatu wakiongozwa na Kefa walikutana uso kwa uso na Kafumu ambaye alikuwa amevirigwa na nyoka mdogo shingoni huku akiwa amesheheni silaha zake ambazo ilidaiwa ni tunguli na hirizi.

Walokole walikuwa wakikemea kwa nguvu huku Mganga Kafumu naye akikemea kwa kutaja mizimu yake akiiomba iwaangamize kabisa walokole wale ambao yeye aliwaita ni wachawi wanaotumia neno la Mungu kumuangamiza.

Katika hali ya kushangaza mlokole mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Lazaro Daniel alianza kufuka moshi mkubwa ulioanzia kwenye mifuko yake ya suruali ambapo alianza kupiga kelele na kuvua suruali hiyo kisha kubakia na nguo yake ya ndani.

Baada ya Kefa kuona mwenzake akiwaka, alitimua mbio akifuatiwa na Daniel ambaye alikuwa na ‘kufuli’ aina ya Boxer huku akiomba msaada kwa watu ambao nao walianza kukimbia kuokoa nafasi zao.

Waandishi wetu walifanya jitihada za kuongea na Daniel ambaye alisitiriwa kwa kufungwa shati kwa chini, ambapo alikiri suruali yake kushika moto kimiujiza na kueleza kwamba huenda Kafumu alimwekea kiberiti.

TUKIO LENYEWE LILIKUWA HIVI.
MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Kefa (kushoto) akiwa na Daniel juu ya kilima wakipiga injili

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Mganga wa jadi Kafumu Moto akiwasili eneo la maombi kilimani.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Mganga Kafumu Moto akimwekea hirizi Daniel mfukoni.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Baada ya kuweka hirizi mfukoni kwa Daniel Mganga aliomba aombewe ili aokoke ikiwa ni hatua ya kupima uwezo wa wahubiri hao ambao walihisiwa kuwa ‘Feki’.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Ghafla Suruali ya Daniel ikaanza kuungua

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Danieli akiwa amepagawa ilibidi avue suruali yake, wakati huo mganga alikuwa akiendelea kumuombea dua ya mashetani ili azidi kukolea moto. Kushoto anayeonekana ni Mhubiri Kefa a.k.a Jesus akitimua mbio baada ya mwenzake kuanza kuwaka moto.
MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Baada ya wahubiri kutimua mbio , kilima kitakatifu cha maombi kikatekwa na kigagula Kafumu Moto.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Danieli (katikati) akiwa amejisitiri kwa kujifunga shati la mhubiri Kefa baada ya ‘kutoka nduki’. Kulia ni raia mmoja akiwa amekaa juu ya tofali mkao wa kujihami.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Kafumu Moto akiendelea kuchimba biti mtaani

MGANGA HUYO AKITOA MAELEZO BAADA YA KUMALIZIKA KWA MCHAKATO HUO


WALOKOLE WAKITOA MAELEZO YAO BAADA YA MCHAKATO HUO

PICHA:CHRISTOPHER LISSA NA ISMAIL MANG’OLA
    (14 November 2009)
Views: 660 | Maoni (14) |

 

AKUDO YATAMBULISHA KIFAA KIPYAAA…

photos  
Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ usiku wa kuamkia leo imemtambulisha mnenguaji wake mpya, anayefahamika kwa jina la Queen Angel, katika onesho la bendi hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam.

MANJONJO YA ‘QUEEN ANGEL’
AKUDO YATAMBULISHA KIFAA KIPYAAA…
Hivi ndivyo alivyoanza

AKUDO YATAMBULISHA KIFAA KIPYAAA…
Mara mtoto akachanika msamba

AKUDO YATAMBULISHA KIFAA KIPYAAA…
Baada ya kuinuka aliubeba mguu mmoja na kuanza kucheza nao.

AKUDO YATAMBULISHA KIFAA KIPYAAA…
Vimwana wa Stone Mayiyasika katika pozi la ukweli.

PICHA:RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA /GPL
    (14 November 2009)
Views: 118 | Maoni (1) |

 

Chadema hali tete wenye viti mikoa 11 wapinga uamuzi wa Dk Slaa

Habari mbalimbali  
Chadema hali tete wenye viti mikoa 11 wapinga uamuzi wa Dk Slaa
Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa

UAMUZI wa katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wa kuwatimua maafisa wawili wa sekretarieti, umekifanya chama hicho kugubikwa na wingu zito baada ya wenyeviti wa mikoa 11 kumpinga, akiwemo katibu wa Kigoma, Msafiri Wamarwa ambaye amejitokeza kutangaza kuwatambua waliotimuliwa...
    (14 November 2009)
Views: 291 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Maiti za mume, mke zakutwa zimefukiwa kifusi kitandani

Habari mbalimbali  
Maiti za mume, mke zakutwa zimefukiwa kifusi kitandani
Baadhi ya wananchi wakitoa moja kati ya miili miwili iliyopatikana jana katika kijiji cha Goba, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro kwa masaada wa mbwa na Polisi.

Miili ya watu wawili, mume na mke, jana zilifukuliwa kutoka katika kifusi baada ya kutokea maporomoko yaliyotokana na mvua zilizonyesha katika kijiji cha Goha wilayani Same mkoani Kilimanjaro na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20.
Maiti nyingine za watu 20 waliofariki dunia katika mafuriko hayo yaliyotokea usiku wa kuamkia Jumatano ziliopolewa na kuzikwa juzi karibu na eneo la tukio....
    (14 November 2009)
Views: 285 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

WABONGO WAMKARIBISHA ELIZABETH

photos  
Usiku wa kuamkia leo mshiriki wa Big Brother Africa (BBA) Elizabeth Gupta, alifanyiwa sherehe ya kukaribishwa 'home' iliyoenda sambamba na kumpongeza kwa kwa ushiriki wake. Sherehe hiyo ilifanyika ndani ya Club Billicanas na iliudhuriwa na mashabiki kibao. Akiongea na waandishi wa habari ukumbini hapo, Eliza alisema kuwa amefurahishwa sana na kitendo cha MultiChoice Tanzania kumwandalia sherehe hiyo ambayo imemwezesha kujumuika tena na Watanzania wenzake.

WABONGO WAMKARIBISHA ELIZABETH
Eliza akiwa katika picha ya pamoja na kaka na mama yake mzazi huku akiwa ameshika bendera ya Tanzania.

WABONGO WAMKARIBISHA ELIZABETH
Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim (Kushoto) akicheza muziki na Jokate Mwegelo katika sherehe hiyo

WABONGO WAMKARIBISHA ELIZABETH
Eliza akiongea na mashabiki waliojitokeza kumpongeza.


WABONGO WAMKARIBISHA ELIZABETH
Lucy Kihwele akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim (Kushoto) na Jokate Mwegelo.

WABONGO WAMKARIBISHA ELIZABETH
Wanamuziki wa Kizazi kipya Ambwene Yesaya 'AY' (kushoto) Joseph Haule 'Profesa J' wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe hiyo.

WABONGO WAMKARIBISHA ELIZABETH
Mara baada ya kuongea na waandishi wa habari na mashabiki waliojitokeza kumpongeza, Eliza alijumuhika na baadhi ya mashabiki hao kucheza muziki.

WABONGO WAMKARIBISHA ELIZABETH
Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim (kulia) akipata kinywaji na Seven.

WABONGO WAMKARIBISHA ELIZABETH
Mshiriki wa BBA Eliza akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mashabiki waliojitokeza katika sherehe hiyo ya kumpongeza.

Picha: Issa Mnally GPL
    (14 November 2009)
Views: 222 | Maoni (5) |

 

Aunt Ezekiel afumaniwa

risasi jumamosi  
Aunt Ezekiel afumaniwa

Na Waandishi Wetu
Kila mkataa pema pabaya panamwita, hivyo ndivyo ngano ya wahenga inavyosema, pia hiyo inaweza ikawa inashabihiana na tukio la Aunt Ezekiel Grayson kufumaniwa na ‘mista’ wa watu, asubuhi ya Alhamisi (juzi, Novemba 12, 2009) Kinondoni, Dar es Salaam...
    (14 November 2009)
Views: 4090 | Maoni (24) | Soma Zaidi

 

‘Nilikuwa tishio ndani ya mjengo wa BBA’

risasi jumamosi  
‘Nilikuwa tishio ndani ya mjengo wa BBA’

Hamida Hassan na Imelda Mtema
Mshiriki wa Bongo kwenye mjengo wa Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta ‘Queen’ amepaza sauti na kuweka bayana kuwa, yeye alikuwa tishio ndani ya jumba hilo ndiyo maana alipigiwa kura za kuingia kwenye mchujo mara nne...
    (14 November 2009)
Views: 841 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

Busta kuwasha moto Novemba 21 Dar

risasi jumamosi  
Busta kuwasha moto Novemba 21 Dar

Na Kyalaa Seheye
Baada ya kusitishwa kutokana na msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Clouds Entertainment, Alex Kusaga lile tamasha lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa la Fiesta ‘One Love’ linatarajia kufanya makamuzi Jumamosi ya Novemba 21, 2009 ambapo Busta Rhymes atafanya makamuzi kama kawa...
    (14 November 2009)
Views: 171 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Babu Ayubu ajaribu ‘zali’ kwenye Mipasho

risasi jumamosi  
Babu Ayubu ajaribu ‘zali’ kwenye Mipasho

Na Richard Bukos
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya na vichekesho nchini, Babu Ayubu baada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye fani hizo hatimaye ameibukia kwenye muziki wa Mipasho na wimbo wake Chaja ya Kobe...
    (14 November 2009)
Views: 280 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Modo Uniq yazidi kupamba moto

risasi jumamosi  
Modo Uniq yazidi kupamba moto

Na Imelda Mtema
Shindano ambalo la aina yake nchini linalokwenda kwa jina la Modo Uniq linazidi kupamba moto baada ya usaili wa kwanza kufanyika wiki iliyopita katika Ukumbi wa Billicanas, jijini Dar...
    (14 November 2009)
Views: 177 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Mchizi Mox sasa alilia Mkali wa Rhymes

risasi jumamosi  
Mchizi Mox sasa alilia Mkali wa Rhymes

Na Christopher Lissa
Mkali wa muziki wa Hip Hop Bongo, Taikun Ally ‘Mchizi Mox’ ameibuka na kulilia shindano lililowahi kuzoa mashabiki lukuki ambalo lilikuwa likiwashindanisha wanamuziki kibao wa muziki wa kizazi kipya la Mkali wa Rhymes ambapo alidai likiboreshwa linaweza kuwatoa wasanii kimaisha na kimuziki...
    (14 November 2009)
Views: 158 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Kimwana Manywele agoma kuachia sinia la Pilau

risasi jumamosi  
Kimwana Manywele agoma kuachia sinia la Pilau

Na Mwandishi Wetu
Kimwana Manywele mwaka 2008, Halima Haroun amejikuta akijikwaa kwenye tukio dogo tu la kung’ang’ania sinia lenye msosi huku wenzake wakimtolea macho kutaka kujua kama atamaliza kutokana na wingi wa chakula hicho, Risasi limemdaka...
    (14 November 2009)
Views: 712 | Maoni (3) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com