arrowMake Homepage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » photos » MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Picha Ya Week ...

Nani Yupo / Alikuwepo

 


 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» JIDE HOI
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» HUKUMU YA BABU SEYA!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» Jinsia ya Aunt Ezekiel ...
» MISS GLOBAL PUBLISHERS ...
» Kimwana manywele
» AHSANTENI SANA KWA KUWA ...
» Nilizaa na dada na mama ...
» Eti Maureen yuko bize, ...
» Meja wa Jeshi

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE

photos
Eneo la Kinyerezi, Tabata jijini Dar es Salaam, Novemba 12 mwaka huu lilikumbwa na tukio la aina yake kufuatia vita kubwa kuzuka kati ya baadhi ya watu wanaojiita walokole kutoka Kanisa la International Pentecoste Hollyness Church Ebenezer na watu wanaojihusisha na nguvu za giza ‘wachawi’ kupambana uso kwa uso mtaani mchana kweupe.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, walishuhudia vitu vya ajabu vikiruka angani huku nyoka waubwa na wadogo wakitoka katika nyumba ya kijana mmoja aitwaye Kafumu Moto ambaye inadaiwa ni mganga wa jadi tishio katika eneo hilo.
Walisema, tukio hilo lilianza majira ya mchana wakati kundi la walokole zaidi ya 18 likiongozwa na mhubiri maarufu katika eneo hilo aliyetajwa kwa jina moja la Kefa ambaye amepachikwa jina la Jesus, waliposambaa mtaani na kuanza kupiga injili ambayo ililenga kuangamiza uchawi, mapepo na kuleta wokovu katika eneo hilo.

Mashuhuda hao walisema kuwa, pitapita hizo za walokole, ziliishia katika nyumba ya Kafumu Moto ambapo walianza kupiga neno la mungu kisawasawa kitendo kilichomkera mganga huyo kijana na kumfanya naye kuingia ndani na kuvaa magwanda yake ya kazi ya kichawi, kisha kuchukua silaha zake za uchawi wakiwemo nyoka wakubwa na wadogo kisha kutoka nje akiwa na wapambe wake na kuanza kushambuliana na walokole hao.

Inadaiwa kuwa, Kafumu Moto aliamrisha majoka yake kuwashambulia walokole, ambao walitimua mbio na kutawanyika mtaani, huku baadhi yao wakienda kuweka kambi katika kilima kimoja porini kuendelea na maombi yao kwa sauti ya juu.

Mtandao huu ulifika eneo la tukio na kukuta mtafutano kati ya walokole na kundi la mganga huyo ukiendelea vichakani, huku watu wengine wakitimua mbio kuponya nafsi zao .

Hatimaye wahubiri watatu wakiongozwa na Kefa walikutana uso kwa uso na Kafumu ambaye alikuwa amevirigwa na nyoka mdogo shingoni huku akiwa amesheheni silaha zake ambazo ilidaiwa ni tunguli na hirizi.

Walokole walikuwa wakikemea kwa nguvu huku Mganga Kafumu naye akikemea kwa kutaja mizimu yake akiiomba iwaangamize kabisa walokole wale ambao yeye aliwaita ni wachawi wanaotumia neno la Mungu kumuangamiza.

Katika hali ya kushangaza mlokole mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Lazaro Daniel alianza kufuka moshi mkubwa ulioanzia kwenye mifuko yake ya suruali ambapo alianza kupiga kelele na kuvua suruali hiyo kisha kubakia na nguo yake ya ndani.

Baada ya Kefa kuona mwenzake akiwaka, alitimua mbio akifuatiwa na Daniel ambaye alikuwa na ‘kufuli’ aina ya Boxer huku akiomba msaada kwa watu ambao nao walianza kukimbia kuokoa nafasi zao.

Waandishi wetu walifanya jitihada za kuongea na Daniel ambaye alisitiriwa kwa kufungwa shati kwa chini, ambapo alikiri suruali yake kushika moto kimiujiza na kueleza kwamba huenda Kafumu alimwekea kiberiti.

TUKIO LENYEWE LILIKUWA HIVI.
MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Kefa (kushoto) akiwa na Daniel juu ya kilima wakipiga injili

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Mganga wa jadi Kafumu Moto akiwasili eneo la maombi kilimani.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Mganga Kafumu Moto akimwekea hirizi Daniel mfukoni.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Baada ya kuweka hirizi mfukoni kwa Daniel Mganga aliomba aombewe ili aokoke ikiwa ni hatua ya kupima uwezo wa wahubiri hao ambao walihisiwa kuwa ‘Feki’.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Ghafla Suruali ya Daniel ikaanza kuungua

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Danieli akiwa amepagawa ilibidi avue suruali yake, wakati huo mganga alikuwa akiendelea kumuombea dua ya mashetani ili azidi kukolea moto. Kushoto anayeonekana ni Mhubiri Kefa a.k.a Jesus akitimua mbio baada ya mwenzake kuanza kuwaka moto.
MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Baada ya wahubiri kutimua mbio , kilima kitakatifu cha maombi kikatekwa na kigagula Kafumu Moto.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Danieli (katikati) akiwa amejisitiri kwa kujifunga shati la mhubiri Kefa baada ya ‘kutoka nduki’. Kulia ni raia mmoja akiwa amekaa juu ya tofali mkao wa kujihami.

MGANGA WA JADI AWAZULIA TIMBWILI WALOKOLE
Kafumu Moto akiendelea kuchimba biti mtaani

MGANGA HUYO AKITOA MAELEZO BAADA YA KUMALIZIKA KWA MCHAKATO HUO


WALOKOLE WAKITOA MAELEZO YAO BAADA YA MCHAKATO HUO

PICHA:CHRISTOPHER LISSA NA ISMAIL MANG’OLA



Dear Guest you have enter our site without being Registered. We recommend to register to view more...
"Mgeni wetu unatakiwa Kuregista kupata Udaku Wote..."
 (Votes #: 3)
    (14 November 2009)
Soma Zaidi: 659 | Maoni Yako (14)

Udaku Mwingine

photos
 
  • My God
  • Nilivyolazimishwa kuwa mchawi-6
  • Nilikubali mkoba wa kichawi ili niwe tajiri-14
  • Nilikubali mkoba wa kichawi ili niwe tajiri-7
  • Nilikubali mkoba wa kichawi ili niwe tajiri-13
  •    

    #1 Author: MZALENDO (14 November 2009 08:51)

    Hii nayo ni aina yake.
    Kwa kanisa, hili linaonyesha kuwa kuna kazi mmeianza na kamwe msiiache maana ni neno la Mungu lina uwezo kuliko nguvu zote. Mchungaji Mrema, na wainjilisti tumeni watu waliojazwa na ROHO wakaimalize kazi.
    Kazi imeanza
     
    fast    

    #2 Author: mm (14 November 2009 09:40)

    JAMANI WALOKOLE HAKUNA UCHAWI WALA UGANGA JUU YA WATU WA MUNGU,MKIENDA KAZINI VAENI SALAHA ZA MUNGU KWELI KWELI WALA MSICHANGANYE NA MAMBO MENGINE KABISA,MKIWA HAMPO IMARA SHETANI ANAWEZA KUJITUTUMUA NA KUWASHINDA,MCHUNGAJI UNAKIMBIA MGANGA?THIS IS FUNNY,HEMBU WAPELEKWE WAUMINI WAWILI WALIOJAA NENO TOKA FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP WAONE KAMA HUYO MGANGA ATAKAA NA KUJITAMBA,HII NI AIBU KWA UFALME WA MUNGU.TUOMBE NDUGU ZANGU.
     
    fast    

    #3 Author: shushuna (14 November 2009 13:27)

    Hao walokole ni matapeli tu wamekubaliana n huyo mganga kuitangaza biashara ya uchawi ili kumpa soko huyo mganga.Waache kutumia jina la MUNGU kinyume cha matakwa yake.
     
    fast    

    #4 Author: chichi (14 November 2009 19:18)

    hahaha uwiiiiii , mbavu zangu . lakini huyo mchawi mbona hivyo ashindwe na alegee kwa jina la yesu yesu atabakia juu
     
    fast    

    #5 Author: mio (14 November 2009 19:27)

    Yaani nimecheka sina mbavu, sasa kweli wewe inayesema unamwamini Mungu kwanini ukatize mbuga, kama ni kweli ni Neno la Mungu unahubiri na umejaa Roho Mtakatifu ungetakiwa uendelee kuhubiri na kwa nguvu zote - Damu ya Yesu iliita aise si utani .. inafanya kazi na pia wewe unatakiwa uwe msafi wa roho kwanza - yaani sina mbavu
     
    fast    

    #6 Author: bonge (15 November 2009 01:57)

    duh! jamaa kuona mwenzake anaungua hakutaka hata kugeuka nyuma, kumsaidia mwenzake....kweli mganga namuaminia ... mganga unatisha kaka
     
    fast    

    #7 Author: Musa Kidichi (15 November 2009 02:15)

    kutokujua nini wanachokifanya,imani na mila potofu tu!
     
    fast    

    #8 Author: MKOSOAJI (15 November 2009 03:19)

    NAOMBA MKAE ATTENSION WATANZANIA WENZANGU HUO WOTE NI USANII ULIYOFANYWA KUMTANGAZA MGANGA, MWANDISHI ALIJUAJE KAMA KUNA TUKIO KAMA HILO MPAKA AKAENDA NA VYOMBO VYA KUCHUKUA SCENE?, haya yote ni ujanja wa business, nimefatlia mambo yote kuanzia tabata, kuanguka kwa rama kanisa la mama RWAKATARE, NIKAONA WOTE NI USANII, nilisoma kitabu cha UCHAWI WA MCHUNGAJI STEPHANO, anasema wachawi huanga wakiwa uchi sasa vipi watu wanakamatwa wakiwa na nguo?, NAOMBA WABONGO TUWE EXPLICABLE, TUUMALIZE HUO USANII, KAZI KWENU MNAOENDEKEZA POWER OF DARKNESS
     
    fast    

    #9 Author: achaar (15 November 2009 04:58)

    Inaonekana vita ilikuwa kali sana
     
    fast    

    #10 Author: krogs (15 November 2009 05:25)

    jamani mie naombeni simu ya huyo mganga nataka kuwasilana nae...nawasihi jamani kama mnajua namba yake.....udaku nisaidieni kupata namba yake ya simu
     
    fast    

    #11 Author: IM (15 November 2009 06:21)

    IGNORANCE, yote haya ni dalili za umaskini unaosumbua watu,laiti walio wengi wangekuwa na kazi kwa ajili ya kujikimu kimaisha pasingekuwa na mambo haya ya kupumbaza watu. badala la kutafuta maendeleo wengi wanakuwa ni waumini,wainjilisti,sijui nn mnafikiri MUNGU atawashushia mahitaji yenu?acheni ujinga jishugulisheni na kazi yenye manufaa kwenu,na taifa kwa jumla, vinginevyo itafikia hatua watu wote wanataka kuwa wachungaji maana kuwa mchungaji siku hizi ni *deal* hebu fikiria itakuwaje iwapo kila mtu ataanzisha kanisa lake? itakuwa ni CHAOS.
     
    fast    

    #12 Author: mtamboni (15 November 2009 07:43)

    huyo mchungaji mwenyewe mbona anaonekana kama konda halafu kama amelewa vile
     
    fast    

    #13 Author: moyo (15 November 2009 13:25)

    hawa wote wako kundi moja,wanataka tu kumpandisha chat huyo mchawi,
     
    fast    

    #14 Author: disminder (16 November 2009 00:41)

    TURUDI KATIKA BIBLIA NA QURAN.
    Mwenyezi Mungu amesema siku za mwisho kutakuwa na magonjwa ya ajabu, dini za uzushi, Manabii wa uongo na Ibilisi atashinda iman dhaifu.

    TUWE MAKINI NA WATU HAWA.
     
    fast    

    Add comments

    Name:
    E-mail:

    Code:
    Include security image CAPCHA.
    to renew the code
    Enter Code:


    Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

    hit counter

     

    2008 © globalpublisherstz.com