Na Saleh Ally SIMBA jana iliendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kufanikiwa kuichapa Mtibwa Sugar ya Manungu kwa jumla ya mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, hivyo kuandika rekodi mpya ya kumaliza mzunguko wa kwanza kwa kushinda mechi zote 11..
Na Saleh Ally KOCHA Mkuu wa Yanga, Kosta Papic amesema hakuna anachohitaji leo dhidi ya Prisons ya Mbeya zaidi ya pointi tatu na amewaambia wachezaji wake, “tubebe pointi tatu, au tumalize mzunguko na aibu”...
Na Saleh Ally ZIMEBAKI angalau asilimia 20 tu ya mambo kabla ya Haruna Moshi ‘Boban’ kuweka rekodi ya aina yake kwa wachezaji wa Tanzania hasa kuanzia miaka ya 1980 hadi leo baada ya viongozi wa benchi la ufundi la timu ya Gefle FF ya Sweden kusema, wana kila sababu ya kumuingiza katika kikosi chao...
Khadija Mngwai na Leah Kweka KOCHA mkuu wa Azam FC, Itamar Amourim amesema kuwa anahitaji nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kwa kutwaa ubingwa au kushika nafasi ya pili...
Ni hitaji lenye kuuma, Vivian, Josia na Janeth wamepambana kufa na kupona na hatimaye kuirejesha fimbo ya Bunge nyumbani lakini pamoja na juhudi hizo Josia na Janeth ni wahalifu wanashtakiwa kwa mauaji ya wapelelezi waliyoyafanya huko nyuma kabla.
Kesi inaunguruma kwa muda mrefu na Janeth anapata msamaha kwani hakuhusika kwa namna yoyote ile na mauaji ila kwa Josia mambo si shwari anahukumiwa kwenda jela na hatimaye kunyongwa, Janeth analia mno, msamaha aliopewa hakika haikuwa na maana kwake, alitamani yeye pia angehukumiwa kifo kama ilivyotokea kwa kaka yake.
Wakiwa nje ya mahakama Josia anaigundua huzuni waliyonayo Janeth na Vivian lakini anawapa moyo kwa kuwambia kwamba yeye asingekufa kwa sindano ya sumu wala kunyongwa mpaka siku yake ya kufa ikatapofika.
Wakiwa katikati ya mazungumzo maaskari wanafika na kumchukua, anabebwa na kupandishwa kwenye gari la magereza na muda mfupi baadaye safari kwenda gereza la Ukonga kusubiri siku ya kunyongwa ifike! Cha kushangaza uso wake umejaa tabasamu, ingawa dada zake na baadhi ya watu waliomwona walikuwa wakilia kwa huruma. Je, nini hatima ya Josia gerezani? Atanyongwa? Kitatokea nini kwa Janeth na Vivian? SONGA NAYO…
Vijana wa mavipaji kutoka THT wakiongozwa na Lady Jaydee, wakiwakilisha Bongo kwenye onesho maalumu la Mo Foundation lililofanyika Jumamosi iliyopita, Mlimani City jijini Dar es salaam ambako wasanii wengine wa kimataifa Youssou N'dour kutoka Senegal na Anjelique Kidjo kutoka Benin wali perform.
Rais JK akiwa 'mtu kati' ya Lady Jaydee na mumewe Gadner (kushoto) mara baada onesho lake.
Rais JK akiongea na mwanamuziki Youssou N'dour (kati) huku Jide akifuatilia..we mzee Youssou mkono huo.......mke wa mtu huyo, OH HOO!
Mkuu wa wilaya ya Nanihii (kulia) akiwa ndani ya suti ya 'kufa mtu' alipata nafasi pia ya 'kuuza sura' na msanii Emmanuel kutoka Sudan na bibie Angelique Kidjo ambaye licha ya ku perform alikuwa MC wa shughuli hiyo iliyohudhuriwa na vigogo wa Bongo.