Kushoto ni Afisa Rasilimali Watu wa Tigo Bennett Kakorozya akikabidhi zawadi ya Laptop kwa mshindi wa PILI wa promosheni ya TIGO CHEMSHA BONGO HASSAN MOHAMED wa MBAGALA, katikati ni Tawonga Mpore Ofisa huduma za ziada Tigo na Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando wakishuhudia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo ofisi za Tigo makao makuu. kushiriki Mteja alitakiwa kutuma neno SWALI kwenda 15550 na kisha alianza kupokea maswali mbalimbali kutoka Tigo kwa mwezi mmoja uliopita.
Kulia ni Afisa Rasilimali Watu wa Tigo Bennett Kakorozya akikabidhi zawadi ya Plasma TV Inch 26 kwa mshindi wa kwanza wa promosheni ya TIGO CHEMSHA BONGO JAMAL JUMBE wa KINONDONI, katikati ni Tawonga Mpore Ofisa huduma za ziada Tigo na Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando wakishuhudia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo ofisi za Tigo makao makuu. kushiriki Mteja alitakiwa kutuma neno SWALI kwenda 15550 na kisha alianza kupokea maswali mbalimbali kutoka Tigo kwa mwezi mmoja uliopita.
Tarehe 16 Novemba 2009, Kampuni ya simu za mkoni Tigo leo imekabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa promosheni ya Tigo Bingwa iliyokuwa ikichezeshwa kwa kipindi mwezi mmoja uliopita. Zawadi zilizokuwa zikishindaniwa katika mchezo huo ni pamoja na 1Plasma TV 26 Inch-LCD mshindi wa Pili
Na Igenga Mtatiro, Tarime JAMAA awliyefahamika kwa jina la Sinda Saidi mkazi wa Mtaa wa Saronge wilayani hapa, amenusurika kuuawa baada ya kubainika ana tabia ya kuwauzia watu nyama ya mbwa akidai kuwa ni ya mbuzi...
Haruni Senchawa na Aziz Hashim KISA cha tukio la askari polisi, PC Chediel George, wa Kituo cha Stakishari jijini Dar es Salaam kumuua kwa kumpiga risasi mfanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, George Jackson Demzee Nyanda (24), (pichani) kimetajwa...
Na Dege Masori, aliyekuwa Same NYUMA ya pazia la maafa ya mlima wa mawe na udongo uliofunika Kitongoji cha Manka, kilichopo katika kijiji cha Goha, Kata ya Myamba, wilayani Same, Kilimanjaro na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 24, kuna maajabu mengi, Uwazi linaandika...
Mpenzi msomaji, kijana Mohamed Geni mkazi wa Dumila Kilosa mkoani Morogoro ambaye katika safari yake ya maisha anadai amekumbana na mkasa wa kubambikiwa kesi ya kubaka ambayo hatoisahau iliyosababisha kukaa gerezani miaka 9 akitumikia kifungo bila hatia, anaendelea kusimulia alivyojikuta katika kifungo hicho baada ya kumsaidia dada mmoja aliyefika Dumila akitokea Singida na baadaye kudaiwa alimbaka. Ilikuwaje mpaka akajikuta akitupwa lupango ili atumikie kifungo cha miaka thelathini? Ungana na MWANDISHI WETU KULWA MWAIBALE katika mkasa huu wa kweli…
HUU ni ubinafsi mbaya sana. Ni kweli kwamba demokrasia haiwezi kudumu ikiwa wachache hawatakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo ya wazi wazi...
Theresia anamsimulia Albert kila kitu kilichotokea maishani mwake, namna alivyochukuliwa na mizimu na kupelekwa chini ya bahari ambako alipewa kazi ya kukusanya damu ambayo ni chakula cha mizimu hiyo! Jambo pekee ambalo hakulielezea vizuri ni namna alivyoua, kwani hali hiyo ilitokea bila yeye mwenyewe kujitambua lakini fahamu ziliporejea alikuta watu wamekufa na akatupiwa lawama kwa mauaji hayo.
Maongezi hayo yanasikiwa na wazazi waliokuwa nje ya chumba cha hospitali alimolazwa Theresia, walipoingia baadaye, mama yake Albert akiwa na hasira nyingi alianza kumfokea Theresia akimwita mchawi na kumwambia angezisambaza habari za uchawi wake kwa Zimbabwe nzima ili kila mtu aelewe ni nani aliyewaua watoto wa Zimbabwe.
Theresia anaruka kutoka kitandani na kupiga magoti mbele ya mama huyo akimbembeleza asifanye hivyo, Albert akamnyanyua na kumrudisha kitandani tena, yeye akiwa amechukua jukumu la kumbembeleza mama yake asichukue hatua aliyotaka kufanya, mama huyo hakusikia, alizidi kufoka. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakichezewa na kuumizwa moyo bure...
Kundi la Jahazi Modern Taarabu usiku wa kuamkia leo liliwashindanishwa mashabiki wake kuimba nyimbo za kundi hilo ambapo mashabiki 14 waliweza kuonesha vipaji vyao kwa kuiga sauti za waimbaji wa kundi hilo.
Katika mashabiki hao, walipatikana washindi watatu ambao watatoa burudani kwenye sherehe za miaka mitano ya kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Times FM.
MLEMAVU MWENYE KIPAJI CHA MIPASHO Shabiki mwenye ulemavu wa macho, Pili Salum (kulia) akionesha ujuzi wake wa kuiga nyimbo za kundi la Jahazi ambapo alifanikiwa kuingia kwenye tatu bora. Kushoto aliyemshikia kipaza sauti ni muimbaji wa kundi hilo, Miriam Amour.
UHONDO UNAPOKOLEA Kundi la mashabiki likitimbwilika wakati, Bi. Pili akipagawisha.
‘MWANAUME MASHAUZI’ Mtoto wa kiume (kulia) kidomo cha tabasamu, kiuno cha kubinuka akiserebuka kimtindo katika shoo hiyo.
MRITHI WA HADIJA YUSUPH Shabiki huyu aitwae Munira Juma, naye aliwapagawisha mashabiki kwa kuiga kibao kilichoimbwa na Khadija Yusuph enzi hizo kiitwacho ‘Mkuki kwa nguruwe’.
BADO NIPO NIPO Mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini, Hassan Bitchuka, usiku wa kuamkia leo alinaswa na kamera yetu akiendelea kufanya makamuzi na bendi yake ya Mlimani Park Orchestra (Sikinde ngoma ya ukae) katika uwanja wake wa nyumbani, DDC Kariakoo ‘Old Trafford’, jijini Dar es Salaam.
‘NAMI BADO NAPAGAWISHA’ Mkali wa muziki wa dansi hapa Bongo, mzee wa enzi hizo, Maalim Muhidin Gurumo wa Msondo Music Band (kushoto), usiku wa kuamkia leo alinaswa ukumbi wa Africentre jijini Dar es Salaam akiendelea kupagawisha mashabiki katika onesho la bendi hiyo lililofanyika ukumbi huo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni mmoja wa mashabiki wa bendi hiyo aliyeshindwa kuvumilia na kuamua kwenda kuchezea jukwaani, sambamba na mkongwe huyo.
Wikiendi hii, mapaparazi wa mtandao huu walitua pande za Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam nyumbani kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes a.k.a Mr.Misifa. Bahati mbaya hawakuweza kumkuta lakini waliishia nje ambako walivutiwa na hali ya jiko lake pamoja na dishi la Runinga yake. Hebu cheki ilivyokuwa...
Huu ndio muonekano wa picha ya jiko la staa wetu Dully Sykes’ Handsome Boy’ ambaye picha yake inaonekana hapo juu
Hapa ni mahali anapotumia kupikia chakula chake.
Baada ya kula huhifadhi vyombo vyake juu ya kochi hili la ‘mbavu za mbwa’ bila kuviosha ambapo nzi hufanya tafrija kwenye makombo. Hapa ni baada ya kupata kifungua kinywa.
Hili ndio kabati lake la kuhifadhia vifaa vyote vya jikoni.
Ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni.Hili ndiyo Dish ambalo 50 Cent wa Bongo, Dully Sykes hulitumia kwenye Runinga yake, ambalo ameligeuza kamba ya kuanikia nguo.
Pembeni ya nyumba ameegesha ‘ mkoko’ (gari) wake wa maana ambao hata hivyo ulikuwa na pancha katika tairi lake la mbele upande wa kulia.
Katika hali inayoonekana kuwa ni mmomonyoko wa maadili uliopitiliza , dada mmoja mkazi wa mtaa wa Mandala, Buguruni jijini Dar es Salaam ambaye jina lake halikufahamika mara moja, hivi karibuni amemshushia kichapo kikali mama yake mzazi anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 60 na kumuumiza vibaya.Chanzo cha tukio hilo la aina yake inaelezwa kuwa ni mvutano uliokuwepo kati ya binti huyo na mama yake kuhusu mtoto wa binti huyo.
Imeelezwa kuwa alikuwa akimtaka mwanae akatembee naye mitaani ambapo mama yake alikuwa akikataa kwa madai kuwa binti yake huyo ni kiruka njia na hastahili kuondoka na mtoto mdogo kutokana na tabia yake ya uzururaji. Binti huyo alianza kumshushia kipigo mama yake mzazi ambapo watu wenye hasira waliingilia kati na kuanza kumfunza adabu binti huyo kwa kumshushia kichapo kikali.
Pichani, binti akiwa hoi kwa kipigo kutoka kwa watu wenye hasira
Hapa akiangua kilio huku raia mmoja akimshika kinguvu ili apigwe picha
WANAFUNZI katika vyuo vikuu kadhaa nchini wanadaiwa kuishi maisha ya kubahatisha kutokana na fedha wanazozitegemea kutoka Bodi ya Mikopo kutowafikia kwa wakati mwafaka...
Siku zote usalama ni jambo la muhimu sana katika maisha yetu, kutokana na kutambua hilo denti huyu ambaye hakufahamika jina lake wala shule anayosoma jijini Dar, aliamua kuuchapa usingizi juu ya benchi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Lakini kama ingekuwa sehemu ingine isiyo salama, naamini asingethubutu kufanya hivyo kwa kuhofia ‘dungadunga.’
Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amesema hakuna masharti waliyowekeana katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, katika kumaliza mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar...