arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 17.11.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» ZITO LAIBUKA
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» MAHARUSI WASAIDIA YATIM ...
» Ni Mdogo Mno Kufa - 32
» Boban: Maximo utajuta k ...
» MY HEART IS BLEEDING( M ...
» SILENT FOREVER (26)
» Spika Sitta aipuuza Tak ...
» Nyota wa Cape Verde aio ...

 

Mama Eliza afanyiwa kitu mbaya Big Brother

risasi mchanganyiko  
Mama Eliza afanyiwa  kitu mbaya Big Brother

Hamida Hassan na Imelda Mtema
Mama Mzazi wa aliyekuwa Mwakilishi wa Tanzania katika Shindano la Big Brother 2009, Elizabeth Gupta ‘Queen’, Mama Eliza, amefanyiwa kitu mbaya na ‘The Big Boss’ wa kinyang’anyiro hicho, gazeti namba moja la mastaa Bongo linaandika...
    (17 November 2009)
Views: 2988 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Just hang me -6

hadithi za Shigongo  
Tracy Martin Matetere, binti mrembo kupita kiasi akiwa mjamzito anaamua kwenda kujinyonga kwenye msitu wa Zinga, wilayani Bagamoyo! Kabla hajafanya hivyo anamwonea huruma mtoto aliyeko tumboni na kuamua kuruka kutoka mtini hadi chini, kitendo hicho ndicho kilianzisha uchungu.

Akitambaa kuelekea barabarani alizaa mtoto mmoja na kumwacha hapo hapo kisha kusonga mbele, kabla hajatokeza barabarani akazaa tena mtoto wa pili na kumwacha hapo hapo, moyoni akiamini mara akifika barabarani na kukutana na msamaria mwema angemwambia juu ya watoto wake lakini haikuwa hivyo, kwani akiwa barabarani alipoteza fahamu.

Baadaye aliokotwa na wapita njia kisha kupelekwa hospitali wakiamini aligongwa gari, daktari alipompima alithibitisha amekwishakufa, siku chache baada ya ndugu kutojitokeza akazikwa na halmashauri ya mji na miezi michache baadaye, tajiri mmoja mjini Bagamoyo alikufa na kaburi lake kujengwa juu ya kaburi laTracy, hivyo binti huyo akawa amepotea milele!

Historia yake inaonyesha ni binti wa mfanyabiashara tajiri jijini Dar es Salaam mzee Martin Matetere aliyemilika viwanda vya kutengeneza plastiki, akiwa na watoto wanne, Tracy pekee ndiye alikuwa mtoto wa kike! Mzee huyu alimpenda mtoto wake kupindukia, kiasi cha watu kuhisi kulikuwa na kitu cha ziada, baadaye akaamua kumpeleka Uingereza kwa masomo, huko ndiko nia yake ilithibitika baada ya kumnywesha mwanae mvinyo na kumwingilia kimwili bila ridhaa yake kwa kitisho kuwa siku akifungua mdomo angekuwa kichaa, sababu mambo hayo yalikuwa ni ya kishirikina.

Tracy alilia mno, mama yake alipoongea naye kutoka Tanzania alifikiri alikuwa analia kwa sababu ya kukumbuka nyumbani, akamfokea na kumtaka atulie ili aendelee na masomo mpaka mwisho. Je, nini kinaendelea leo? SONGA NAYO…
    (17 November 2009)
Views: 1023 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Mpenzi wangu kapewa mimba na mwanaume mwingine, nifanyeje?

Mahaba  
Mpenzi wangu kapewa mimba na mwanaume mwingine, nifanyeje?

Bila shaka kwa uwezo wa aliye juu, Muumba wa Mbingu na Dunia mtakuwa wazima wa afya njema na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku salama kabisa. Karibuni katika uwanja wetu wa kupeana elimu maridhawa juu ya uhusiano na mapenzi...
    (17 November 2009)
Views: 398 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Ushuhuda kabla ya kifo changu-4

Mikasa ya kusisimua  
Nilizinduka baada ya muda na kwenda bafuni kuoga baada ya kuoga nilijitahidi kupata chakula japo sikuwa na hamu nacho, nilifanya hivyo kutokana na njaa kunisumbua tangu asubuhi. Baada ya chakula nilijipumzisha, kila nilipokumbuka roho iliniuma sana...
    (17 November 2009)
Views: 1013 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Mba aikomba Yanga Sh milioni 50

champion  
Mba aikomba Yanga Sh milioni 50

Na Saleh Ally
MSHAMBULIAJI Robert Jama Mba ni kati ya waliotupiwa virago na Kocha Mkuu wa Yanga, Kosta Papic hali inayoufanya uongozi wa Jangwani kulazimika kusaka kitita cha dola 50,000 ili kuvunja mkataba Mba...
    (17 November 2009)
Views: 446 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Majimaji yamwaga machozi TFF

champion  
Na Khadija Mngwai
UONGOZI wa Majimaji ya Songea umelilaani Shirikisho la Soka TFF kufuatia hatua yao ya kuwatoa kushiriki kwenye michuano ya kombe la Tusker itakayoanza Desemba 14 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam...
    (17 November 2009)
Views: 142 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Boban aula Ulaya, Waswidi watangaza dau

champion  
Na Saleh Ally
UONGOZI wa klabu ya Gefle FF, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Sweden umetangaza rasmi kwamba, kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ amefanikiwa katika majaribio ya kucheza soka ya kulipwa...
    (17 November 2009)
Views: 625 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Tenga: Fuateni mwendo wa Simba

champion  
Na Chausiku Omar
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF Leodegar Tenga ameipongeza timu ya Simba kwa kutopoteza mechi hata mmoja katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu na kuzitaka timu nyingine kufuata nyayo zao...
    (17 November 2009)
Views: 171 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Nizar, Henry kuongeza nguvu Stars

champion  
Nizar, Henry kuongeza nguvu Stars

Na Mwandishi Wetu
VIUNGO wawili, Henry Joseph na Nizar Khalfan wana nafasi kubwa ya kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars wakati wa michuano ya Challenge...
    (17 November 2009)
Views: 172 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

The Painful Demand- 59

hadithi za Shigongo  
Baada ya kugundua kwamba Janeth na Josia ni ndugu zake, mpelelezi Vivian anaamua kufanya kila linalowezekana kunusuru maisha yao na kifo cha kunyongwa kwa makosa ya mauaji waliyoyafanya. Anawatorosha nchini Tanzania hadi India, ambako baadaye walibaini kwamba ndiko fimbo ya Bunge ilikopelekwa baada ya kuibiwa Dodoma na kuuzwa kwa wahindi Kumar na Nilesh wanaoishi katika jiji la Bangalore, ambako ndiko Josia na Janeth wamejificha.

Tukio hili linamfanya Vivian asafiri hadi India ambako aliungana na Janeth, Josia na rafiki zake wawili aliosoma nao Urusi ambao hivi sasa wanafanya kazi ya upelelezi nchini humo (Jonti na Rajesh) katika kazi ya kuifuatilia fimbo hiyo mpaka wakaipata kwenye jumba liitwalo Mysore Palace ambako ilikuwa imeuzwa ikiwa vipande vipande na ilionyeshwa kama vyombo vya makumbusho ya kale.

Hawakuipata fimbo peke yake bali pia waliwakamata Nilesh na Kumar na kurejea nao nchini Tanzania ambako Josia, Janeth na Vivian walipokelewa kama mashujaa waliofanikiwa kuikomboa fimbo ya Bunge! Tofauti na matarajio ya Vivian kwamba Josia na Janeth wangesamehewa, haikuwa hivyo, badala yake walipandishwa kizimbani kwa mauaji ya watu nane.

Kesi ikaunguruma kwa kipindi kirefu na Janeth akaachiwa huru lakini Josia akahukumiwa kunyongwa kwani ndiye aliyehusika na mauaji moja kwa moja, akapelekwa gerezani kusubiri siku yake mpaka ilipowadia ndipo akachukuliwa na kuingizwa kwenye chumba cha kunyongewa.

Upande wa pili unaonyesha Kombe la Dunia limeingia nchini Tanzania katika safari zake za kutembezwa nchi mbalimbali, watu wamefurika kwenye ukumbi wa Golden Jubilee kulishangaa kombe hilo na kupiga nalo picha, ghafla walianza kusinzia na kuanguka sakafuni, ndipo kikundi cha watu kumi walipitia kwenye dari la jengo hilo wakiwa wamevalia kininja na kulichukua kombe.

Polisi waliokuwa doria wakatoa taarifa na mapambano yakaanza, kilichowashangaza polisi ni uwezo wa majambazi hao kutumia silaha, walikuwa na shabaha za ajabu! Hii ililazimisha kikao cha dharura kiitishwe, hasa baada ya Jeshi la wananchi kushindwa kutumia mabomu ili mtu mwenye sabaha sana atafuwe, hapo ndipo sauti ya kike kwenye kikao ikadai kulikuwa na mtu gerezani mwenye uwezo wa ajabu katika kulenga shabaha!

Je, ni nani huyo? Nini kitatokea? SONGA NAYO…
    (17 November 2009)
Views: 828 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

WANANCHI TUTAENDELEA KUPORWA MPAKA LINI?

photos  
Jeshi la polisi nchini linatakiwa kuwa imara katika kukabiliana na wahalifu ambao wamekuwa wakiwavamia watu na kuwapora pesa na mali zao, kisha kuwajeruhi kwa vipigo.

HUYU KAKUMBANA NA WAHALIFU HAO
WANANCHI TUTAENDELEA KUPORWA MPAKA LINI?
Mkazi huyu wa Kijitonyama ambaye jina lake halikufahamika, alikumbwa na dhahama la vibaka akiwa amejipumzisha barazani mwa nyumba anayoishi ambapo licha ya kumpora simu yake, walimcharanga kwa mapanga.

PICHA: ISSA MNALY NA ISMAIL MANG’OLA /GPL

    (17 November 2009)
Views: 145 | Maoni (5) |

 

Vituko

Vichekesho na Udaku  
Mambo ya kupiga mbizi hayo
Vituko

Undugu kufaana si kufanana
Vituko

Car-wash yageuka Cow-wash
Vituko
Katika hali isiyokuwa ya kawaida jamaa huyu alimleta ng’ombe wake ‘Car-wash’ na kuanza kumuogesha

Umoja ni nguvu
Vituko

Raha jipe mwenyewe
Vituko
Baada ya pilikapilika za siku nzima Paka huyu aliamua kwenda kula 'good- time' kama anavyoonekana pichani

Mambo ya ubunifu hayo
Vituko
    (17 November 2009)
Views: 123 | Maoni (2) |

 

Askari wa kike akataa kwenda kupigana Afghanistan

Habari mbalimbali  
* Kisa? Hakuna wa kulea kichanga chake cha miezi 10
Askari wa kike akataa kwenda kupigana Afghanistan
Askari, Alexis Hutchinson, akiwa na mwanaye wa kiume

SAVANNAH, Georgia, Marekani
MPISHI mmoja katika jeshi la Marekani ambaye ni mwanamke asiye na mume huenda akakabiliwa na mashitaka ya jinai kwa kukataa kuandikishwa jeshini kwenda kupigana Afghanistan akisema kwamba hapana mtu wa kumlelea mtoto wake mchanga wakati akiwa nje ya nchi hiyo...
    (17 November 2009)
Views: 677 | Maoni (7) | Soma Zaidi

 

MAPACHA WATENGANISHWA BAADA YA OPERESHENI YA KIHISTORIA YA MASAA 25

Habari mbalimbali  
MAPACHA WATENGANISHWA BAADA YA OPERESHENI YA KIHISTORIA YA MASAA 25
Timu ya Madaktari ikiwafanyia operesheni Mapacha hao

MAPACHA WATENGANISHWA BAADA YA OPERESHENI YA KIHISTORIA YA MASAA 25
Baada ya upasuaji walikuwa kama inavyoonekana hapo juu

MADAKTARI nchini Australia wamefanikiwa kuwatenganisha mapacha wa kike -- Trishna na Krishna -- waliokuwa wameungana vichwa vyao...
    (17 November 2009)
Views: 509 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

UTALII WA NDANI

photos  
Mji wa Bagamoyo ni wa Kihistoria ambao una mambo mengi ya kuvutia na kustaajabisha. Ni vizuri kila Mtanzania akatembelea mji huo japo mara moja katika maisha yake. Ni eneo ambalo lilikuwa soko la mababu zetu ambapo walikusanywa kama Watumwa. Kuna makaburi ya viongozi maarufu wa eneo hilo, kuna kisima cha maji yasiyokauka wala kuongezeka na mambo mengine ya kuvutia. Zifuatazo ni picha za eneo la Kaole mjini Bagamoyo ambazo zimetumwa kwetu na mwanafunzi wa STD VI wa Diamond Primary School ya jijini Dar es salaam, Lulu Abdallah, ambaye pamoja na wanafunzi wenzake walikuwa na Study tour mjini humo mwishoni mwa wiki iliyopita...

KABURI LA SHARIFAT
UTALII WA NDANI

UTALII WA NDANI

UTALII WA NDANI
Hili ni kaburi maarufu eneo hilo (pichani juu), linaelezwa kuwa ni kaburi la Sharifat aliyefariki karne kadhaa zilizopita, ambalo watu huenda kuomba na kusema shida zao na kwa mujibu wa imani zao hutatuliwa matatizo yao mbalimbali ya kimaisha. katika picha ya katikati utaona kwa ndani kuna kitezo cha ubani ambacho hutumika kufukiza ubani wakati wa kuomba dua. Picha ya juu ni makaburi ya watoto.


UNAKUMBUKA NOTI HIZI?

UTALII WA NDANI
Hizi ni noti za shilingi 100 za enzi hizo za mwalimu ambazo zilikuwa na thamani sawa na dola mia..!

UNAJUA ASILI YA PICHA YA NOTI HII?
UTALII WA NDANI

UTALII WA NDANI
Angalia vizuri picha iliyopo kwenye noti za shilingi 1000 za sasa utaona kuna picha ya jengo, unajua asili ya hilo jengo? Kwa taarifa yako jengo hilo lipo Bagamoyo kama linavyoonekana pichani ambalo ndiyo yalikuwa makao makuu ya waarabu waliokuwa wakifanya biashara ya watumwa.


KISIMA CHA AJABU

UTALII WA NDANI
Hiki ni kisima cha ajabu kilichopo Kaole. Hakijawahi kukauka wala kujaa maji hata mvua inyeshe vipi, licha ya kuwa karibu na bahari, maji yake siyo ya chumvi, watu hunywa na wengine kujipaka mwilini kuondoa maradhi mbalimbali yakiwemo ya ngozi!!

RANCHI YA MAMBA
UTALII WA NDANI
Hawa ni mamba wa kufugwa, ambao huuzwa kama samaki, wateja wakubwa ni Wachina ambao huwanunua kwa ajili ya kitoweo...!

KARIBU KAOLE
UTALII WA NDANI

UTALII WA NDANI
...baadhi ya wanafunzi wa Diamond walikokuwa katika ziara hiyo ya kimasomo.

WITO: UTALII WA NDANI UANZE NA MTANZAIA MWENYEWE NA ELIMU HII IANZIE SHULE ZA MSINGI...

PICHA: LULU ABDALLAH/ DIAMOND PRIMARY SCHOOL
    (17 November 2009)
Views: 96 | Maoni (1) |
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com