
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, akiwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kesi yake akidaiwa kuitia hasara serikali mabilioni ya fedha.Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa mapema leo.
MATESO YA WANAFUNZI MPAKA LINI?
Baadhi ya makondakta wa basi la abiria jijini Dar es Salaam (daladala) linalofanya safari zake kati ya Tandika na Mwenge, wakimsulubu mwanafunzi mmoja ambaye jina lake na la shule anayosoma halikufahamika mara moja baada ya mwanafunzi huyo kushuka katika kituo cha Usalama Chang’ombe, Temeke na kulipa Sh. 100, nauli ambayo ilikataliwa na makonda hao wakimtaka alipe Sh. 250 nauli ya mtu mzima, hivyo kumlazimisha kurudi kwenye basi hilo ili kumbana zaidi.
DINI ZIPO NYINGI DUNIANI
Viongozi wa taasisi ya kidini ya Iskon Hare Krishna, Umapati Dasa (kushoto), kutoka Temple Resident, Nairobi nchini Kenya, akiwa na Kevin Gagnier kutoka Canada (kulia) wakiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam mapema leo juu ya dini yao.
HUJAFA HUJAUMBIKA!
Msanii nguri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Liso Katama Ibrahimu (Jita Man) kushoto, akiongea na mwandishi wetu, Christopher Lissa, juu ya ajali mbaya iliyompata jijini Mwanza miezi kadhaa iliyopita na kuzushiwa kuwa ameaga dunia. Msanii huyo ambaye hivi sasa hujiita Teminator, kufuatia sura yake kuharibika vibaya kwa mishono huku akivuta mguu wake wa kulia ambao ulivunjika, aliibukia katika ofisi za gazeti hili jijini Dar es Salaam, na kusimulia mkasa wa kutisha uliomkumba hadi kudaiwa kufa, ingawa alisema kwa mapenzi ya Mungu yuko hai na ataendelea kufanya muziki.

Sura ya Jita inavyoonekana kwa sasa.
Mtandao huu unampa pole mdau huyo.RETURN OF ‘SUNCHE NA KAPETO’
Wasanii marufu wa vichekesho nchini, Hassan Abdul ‘Sunche’ na Hussein Abdul ‘Kapeto’, hujulikana zaidi kama ‘Sunche na Kapeto’ (wapili na watatu kutoka kulia) wakiongea na mwandishi wetu Christopher Lissa (kulia) juu ya kurudi kwao kwenye ‘game’ baada ya kujichimbia kwa kipindi kirefu jijini Nairobi nchini Kenya.Kulia ni swahiba wao, James Almasi ‘Kivu’.

Sunche na Kapeto ambao ni mapacha wakiwa katika picha ya pozi.
‘FIESTA ONE LOVE’ INANUKIA!Maandalizi ya kufunga zana za burudani wakati wa pati kubwa la Fiesta One Love linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wengi yameanza katika viwanja vya Chuo Cha Posta , Kijitonyama nyuma ya Makao Makuu ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zain, kama inavyoonekana pichani.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Novemba 21 mwaka huu, ambapo msanii nyota kutoka Marekani, Busta Rymes, atapiga shoo ya kufa mtu!

Mkali huyu, Busta Rymes ndiye atakayesindikiza burudani hiyo