arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 19.11.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» Aina 10 ya vyakula vinavyoo ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» Nilioa Mwanamke kumbe J ...
» Kama kweli mnapendana k ...
» NAFASI ZA KAZI NA ZABUN ...
» HATUACHA VIMINI NG'OOO ...
» Bodi ya Utalii ing’olew ...
» Binti wa kigogo Dar amu ...
» Dada kamuambukiza ukimw ...

 

PICHA YETU YA LEO!

Vichekesho na Udaku  
JE? HUYU JAMAA HUKO JUU ALIFUATA NINI? TOA MAONI YAKO TAFADHALI!

PICHA YETU YA LEO!
    (19 November 2009)
Views: 241 | Maoni (5) |

 

HE! LIYUMBA AMETOKA LINI MAHABUSU?

photos  
HE! LIYUMBA AMETOKA LINI MAHABUSU?
Mwenye fulana yenye mistari ni Katibu Mkuu wa timu ya Yanga Iman Madega. Kama hujamtazama kwa makini mtu aliye mbele yake aliyevaa shati lenye mikono mirefu unaweza kumdhania kuwa ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba ambaye anasota mahabusu kwa takribani mwaka mmoja na nusu sasa.
Picha hapo chini ni Amatus Liyumba (original) jaribu kuwafananisha na Pacha wake hapo juu.
HE! LIYUMBA AMETOKA LINI MAHABUSU?
Amatus Liyumba (original), akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

TUKO TAYARI KWA FIESTA ‘ONE LOVE’
HE! LIYUMBA AMETOKA LINI MAHABUSU?
Watangazaji na Ma-DJ wakali wanaopiga mzigo katika kituo cha Redio Clouds FM cha jijini Dar es Salaam, DJ B12 (kulia) na DJ-Mully B a.k.a Mully Bringbring wakiwa katika picha ya pamoja. Ma-DJ hao walisema kuwa wako tayari ‘kukimbiza’ wakati wa Bonanza kubwa la Fiesta ‘One Love’ linalotarajiwa kufunika ndani ya viwanja vya Chuo cha Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Jumamosi (Novemba 21) mwaka huu.

MLIMA KILIMANJARO WAHAMIA DAR
HE! LIYUMBA AMETOKA LINI MAHABUSU?
Ukitazama kwa makini picha hii utaona kama vile kwa mbali unaona kilele cha Mlima Kilimanjaro. Hii ni moja ya mfano wa mlima huo iliyopo katika viunga vya jengo moja jipya lililopo kando ya Barabara ya Mandela, jijini Dar es Salaam.Mfano huu wa kilele umekuwa kivutio kikubwa kwa wapiti njia licha ya kuonekana kwa mbali ukiwa ndani ya uzio.

MASILIANO HOUSE HIYOO
HE! LIYUMBA AMETOKA LINI MAHABUSU?
Ujenzi wa majumba makubwa na ya kisasa unazidi kuendelea jijini Dar es Salaam na kufanya mandhari ya jiji kubadilika sana na kuwa ya kuvutia. Pichani ni jengo kubwa la Mawasiliano House lililopo kando ya barabara ya Sam Nujoma likiwa limekamilika.

PHARMACY YA DAWA ZA ASILI
Utafiti wa dawa za asili a.k.a Mitishamba, unaozidi kujipatia sifa nchini Tanzania, umepelekea kuibuka kwa maduka mengi makubwa yanayouza dawa za asili huku wateja kibao wakimiminika kununua dawa hizo.
HE! LIYUMBA AMETOKA LINI MAHABUSU?
Pichani ni moja ya duka la dawa lililonaswa na mpiga picha wetu maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam likiwa na dawa mbalimbali za mitishamba.

PICHA:CHRISTOPHER LISSA/GPL
    (19 November 2009)
Views: 84 | Maoni (2) |

 

KOMBE LA DUNIA LA SOKA KUTUA BONGO LEO MAJIRA YA SAA 10 JIONI

photos  
KOMBE LA DUNIA LA SOKA KUTUA BONGO LEO MAJIRA YA SAA 10 JIONI
Kombe lenyewe ndo hili

KOMBE LA DUNIA LA SOKA KUTUA BONGO LEO MAJIRA YA SAA 10 JIONI
Ndege aina ya Boeing 727 inayosafirisha kombe hilo

KOMBE la Dunia la soka linawasili jijini Dar es Salaam leo saa 10:00 jioni likitokea Addis Ababa, Ethiopia na kupokelewa na viongozi wa serikali ya Tanzania kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Kapteni George Mkuchika ndiye atapokea kombe hilo ambalo litapelekwa moja kwa moja kwenye Uwanja wa Taifa na kukabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete.

Burudani zaidi pamoja na kupiga nalo picha vitafanyika siku ya Jumamosi.


    (19 November 2009)
Views: 95 | Maoni (5) |

 

Sauti za Busara 2010

photos  
Sauti za Busara 2010
The seventh edition of the Sauti za Busara music festival will take place in Zanzibar, 11-16 February 2010; admission is free to all EA Residents before 5pm. Sauti za Busara (Sounds of Wisdom) is an international festival celebrating East African music taking place around the second weekend of February each year in Zanzibar.
    (19 November 2009)
Views: 117 | Maoni (1) |

 

Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu

Habari mbalimbali  
Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu
Rais mstaafu Benjamin Mkapa

Rais mstaafu Benjamin Mkapa, amesema yote yanayosemwa juu yake, anamwachia Mungu...
    (19 November 2009)
Views: 696 | Maoni (14) | Soma Zaidi

 

Kikwete abatilisha adhabu za vifo

Habari mbalimbali  
Kikwete abatilisha adhabu za vifo

RAIS Jakaya Kikwete amesema, hivi karibuni alibatilisha hukumu 75 za vifo kuwa vifungo vya maisha...
    (19 November 2009)
Views: 518 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

‘Mume wangu unaniua’

Amani  
‘Mume wangu unaniua’

TUKIO la kusikitisha, kutisha na kuogopesha limetokea Dar es Salaam, ambapo mwanaume mmoja mkazi wa Mbagala Charambe Machinjioni, jijini, Sharifu Hassani Kondo (45), anadaiwa kumchoma visu hadi kumuua mkewe wa ndoa, Bi. Khadija Daudi (22), Amani lina ‘fulu’ data kutoka kwa ndugu, wazazi na watu wa karibu wa wanandoa hao...
    (19 November 2009)
Views: 1912 | Maoni (5) | Soma Zaidi

 

Masanja Mkandamizaji azimika kwa Mademu wawili kwa mpigo

Amani  
Masanja Mkandamizaji azimika kwa Mademu wawili kwa mpigo

Comedian ‘kiraka’ Bongo ndani ya Kundi la Orijino Komedi, Emmanueli Mgaya ‘Masanja MKandamizaji’, ameibuka na kudai anawamis kinoma flowers aliokuwa akikutana nao pale Club Maisha Masaki, jijini Dar es Slaam, ambayo iliteketea kwa moto hivi karibuni...
    (19 November 2009)
Views: 1093 | Maoni (7) | Soma Zaidi

 

Akon katika ufunguzi wa kombe la dunia Sauzi

Amani  
Akon katika ufunguzi wa kombe la dunia Sauzi
Akon

Nyota wa Pop na R&B toka pande za USA, Aliaune Badara Akon Thiam a.k.a Akon, ni mmoja wa staa barani Afrika watakaopiga shoo wakati wa ufunguzi wa michuano ya soka ya Kombe la Dunia huko Bondeni mapema mwakani...
    (19 November 2009)
Views: 190 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Dullayo achomwa visu akitoka Club

Amani  
Dullayo achomwa visu akitoka Club

Msanii wa Kizazi Kipya, Abrahamu Kasembe‘Dullayo’, mwisho wa wiki iliyopita alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuchomwa visu na watuwasiojulikana alipokuwa akitoka Club ya Pop Life iliyoko Maeneo ya Uwanja wa Ndege, jijini Dar...
    (19 November 2009)
Views: 494 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Ripoti A-Z ya Skendo za ngono vyuoni

Amani  
Ripoti A-Z ya Skendo za ngono vyuoni

Taasisi za elimu ya juu nchini zinatajwa kuwa nambari wani kwa skendo za ngono zinazofanywa na ‘madenti’ ambao huishia kwa kuteketezana wao kwa wao, Amani lina ripoti kamili...
    (19 November 2009)
Views: 2041 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Knocked Down? You can stand up 19

hadithi za Shigongo  
Maisha ya Kelvin kijana aliyepata mafanikio makubwa sana kwa kucheza soka kuliko Mtanzania mwingine yeyote katika historia kwani alifikia mpaka kuchezea klabu kubwa kama Liverpool ya Uingereza, yanaporomoka kwa kasi ya ajabu na kujikuta masikini wa kutupwa akiishi kwenye kibanda kidogo cha mwanamke aitwaye Regina, rafiki wa mama yake mzazi (Kokubanza)

Mambo haya yalianza akiwa kwenye kilele cha mafanikio, kwanza mama yake aliyekuwa akiishi naye nchini Uingereza aligundulika kuwa na Saratani ya damu na madaktari kusema angekufa baada ya miaka mitatu, jambo hili lilimfanya Kelvin akatishe mkataba wake wa mamilioni ya Paundi na kurejea nyumbani kumuuguza mama yake mpaka atakapokufa. Hakujua kwamba mama yake huyo huyo ndiye baadaye angemuuguza yeye!

Miaka miwili ilipopita, mama yake akijua alikuwa amebakiza mwaka mmoja tu wa kuishi, alimtaka Kelvin aoe ili amwone mjukuu wake kabla hajaondoka duniani! Wazo hili lilimfanya Kelvin amrejee msichana aliyemkatalia mapenzi kwa muda mrefu (Martina Weston) raia wa Uingereza, mtoto wa familia tajiri ya watengeneza mashine na karatasi za kuchapia magazeti ambaye alitegemewa kuwa mrithi wa utajiri wote baba yake akifa.

Wazazi wa Martina walikataa kabisa mtoto wao kuolewa Afrika, ndipo binti huyo akatoroka mpaka Entebbe ambako Kelvin alimpokea, mbele wakiwa njiani kuelekea Bukoba kabla hawajaondoka Kampala, gari lao liligongana uso kwa uso na lori kubwa, huo ndio ukawa mwisho wa kila kitu! Kelvin akapooza kuanzia shingoni mpaka miguuni, mama yake akaanza kumuuguza mpaka alipokufa wakiwa Beijing, China na kurejeshwa nyumbani kwa mazishi. Kelvin alilia mno, akiamini amebaki duniani peke yake.

Akajikuta mikononi mwa bibi Regina, rafiki mkubwa wa mama yake, ambaye alimchukua na kumpeleka kwenye kibanda chake kidogo cha nyasi, kufuatia nyumba yake kuungua kwa moto na kufilisika pale soko la Hisa la Uingereza ambako Kelvin aliwekeza fedha nyingi lilipoanguka na fedha zake zote kupotea! Mwanamke huyo alimsimulia historia ya maisha yake ambayo Kelvin hakuwahi kuisikia na kugundua kumbe mama yake hakuwa Mtanzania bali raia wa Rwanda, aliyeingia nchini mwaka 1959.
Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO…
    (19 November 2009)
Views: 778 | Maoni (0) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com