Ajabu siku ya pili tuliamka saa mbili asubuhi na si kawaida yetu, nilikuwa wa kwanza kuamka baada ya kupigwa na mwanga mkali wa jua la nje kupitia upenyo katika kuta za nyasi...
Bugumba baada ya maisha mazuri na kuiona ndoa kama pepo ya duniani ghafla inambadilikia na kuiona kumbe ule ulikuwa mwanzo wa ndoa kwake uligeuka na kuwa jehanamu iliyomchoka kila kukicha. Anamchanganya na kumfanya kupandwa na presha na kupoiteza fahamu. Nini kitaendelea? TUWE PAMOJA...
Ni swali gumu sana kulijibu haraka, lakini jepesi kwa mtazamo. Wengi wamekuwa wakiingia katika mjadala huu bila kujua kwamba, suala lenyewe lina sura mbili tofauti. Hili halipingiki hata kwa hoja gani...
Fedha nyingi alizopewa na baba yake zinamfanya Tracy ajiingize kwenye masuala ya starehe na makundi yasiyostahili, akajikuta akiacha shule na kuingia mitaani ambako alikutana na kijana wa Kitanzania ambaye alijihusisha na kazi ya wizi wa magari, hii ilisababisha Tracy na kijana huyo kujikuta wako polisi kwa wizi.
Walipotoka mahabusu baada ya juhudi kubwa za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Tracy na kijana huyo walipelekwa moja kwa moja uwanja wa ndege ambako walipandishwa kwenye ndege na kurejeshwa Tanzania ambako kila mmoja alipokelewa na wazazi wake na hawakutakiwa tena kurejea katika nchi hiyo.
Familia yote ya Tracy ilikuwepo uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alipotoka nje na kugonganisha macho na mama yake mzazi, Tracy aliinamisha kichwa chini! Hakuweza kabisa kumwangalia kwa aibu ya kufanya tendo la ndoa na baba yake mzazi ambaye hakuonekana kuwa na wasiwasi wowote.
Ndani ya gari lawama zilianza kumiminika kwa Tracy kutoka kwa mama na kaka zake, lakini mzee Matetere alimtetea Tracy kupita kawaida, kama vile hakufanya kosa lolote na aliwagombeza watu wote waliojaribu kumwonyesha vidole. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
Mwekahazina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Amos Makalla ameendelea kumwaga neema kwa wakazi wa Wilaya ya Mvomero, Morogoro kwa kuwezesha kupatikana kwa vifaa vya michezo.
Hivi karibuni, Makalla kwa ushawishi wake, aliwezesha safari ya Rais wa Kent Football Association, Kent Masters wa Uingereza wilayani Mvomero ambaye alitoa msaada wa vifaa hivyo vya michezo kwa kata zote za wilaya hiyo.
Kent, alikabidhi vifaa hivyo kwa kila diwani kutoka kata zote 17 za Mvomero katika bonanza kubwa la michezo ambalo liliandaliwa na Makalla.
Akizungumza kwenye bonanza hilo, Kent alisema kuwa ameanza kwa kutoa msaada wa vifaa vya michezo na kwamba kitakachofuata ni kusaidia kwenye upande wa elimu.
Alisema, atatoa vitabu vitakavyowezesha kila mwanafunzi kumiliki kitabu chake kwa kila somo.
Makalla alipozungumza na mtandao huu alisema kwamba anafanya yote ili kuwatumikia wananchi kwa sababu Mvomero ni nyumbani kwao kwa kuwa ndiko anakoishi baba yake mzazi, Gabriel Makalla.
“Pia nafanya yote kwa ajili ya kutekeleza ilani ya chama changu,” alisema Makalla.
Mwekahazina wa CCM, Amos Makalla akihutubia wananchi wakati wa bonanza kubwa la michezo aliloliandaa wilayani Mvomero hivi karibuni ambapo alimwalika Rais wa Kent Football Association, Kent Masters ambaye alitoa msaada wa vifaa vya michezo.
Rais wa Kent Football Association, Kent Masters wa Uingereza akisalimiana na waamuzi, wakati wa bonanza kubwa la michezo lililofanyika hivi karibuni wilayani Mvomero.
Rais wa Kent Football Association, Kent Masters (mwenye shati jeupe) akifuatilia jambo kwenye bonanza kubwa la michezo wilayani Mvomero hivi karibuni, kulia kwake ni Mwekahazina wa CCM, Amos Makalla ambaye ndiye aliyemwalika Rais huyo.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini (C.A.G) Ludovick Otouh leo ametoa ripoti juu madai mbalimbali ya walimu nchini na kueleza kuwa katika uchunguzi wao wamebaini kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwa baadhi ya walimu ambao wengi walithubutu kughushi baadhi ya nyaraka ili kujipatia fedha kutoka serikalini. Alisema waliogundulika kughushi nyaraka watachukuliwa hatua za kisheria na kwamba wale ambao nyaraka zao zimeonesha hazina kasoro watalipwa madai yao kama inavyostahiki.
C.A.G Otouh akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha ripoti ya uchunguzi wa ofisi yake juu ya madai ya walimu nchini mapema leo katika mkutano uliofanyika Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
C.A.G Otou akiteta jambo na Emmanuel Kalibashubaro, ambaye ni Mkaguzi wa Mahesabu wa Kanda (Zonal Auditor) mara baada ya mkutano wao na waandishi wa habari kumalizika.
PICHA YA MPIGA PICHA! Kutokana na mkutano wa C.A.G kuhudhuriwa na watu wengi, ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo ulionekana kuwa mdogo kiasi cha kuwalazimu baadhi ya mapaparazi kuamua kukaa chini. Hata hivyo, baada ya mtandao huu kuwamulika baadhi ya mapaparazi hao, walijikuta wakificha sura zao. Kilikuwa ni kisa cha “Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu uchungu”! Kupiga picha wenzao sawa, lakini si wao!
Mdau wetu, John Bukuku, anayemiliki ‘blog’ ya full shangwe.com (mwenye kofia) akiwa ndani ya Idara ya Habari Maelezo pamoja na mapaparazi wenzake wakifuatilia ishu mbalimbali.
ULINZI NA USALAMA Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania, Almas Maige, akiongea na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam juu ya masuala mbalimbali yanayohusu sekta hiyo na mkutano wao mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Isaya Maisela. PICHA:CHRISTOPHER LISSA NA RICHARD BUKOS /GPL
RAIS Jakaya Kikwete jana alizindua ziara ya Kombe Dunia la Shirikisho la Kimataifa Duniani (FIFA) nchini sherehe iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kombe hilo liliwasili jana uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo lilipokelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. Joel Bendera na kasha kulipeleka Uwanja wa Taifa.
Wasanii wa kikundi cha Simba Theatre wakitoa burudani kabla ya kombe hilo kuwasili uwanja wa ndege.
Mh. Bendera (katikati) akipiga stori wakati wa kusubiri ujio wa kombe.
Msanii wa Simba Theatre akionyesha manjonjo kwa kupiga filimbi akitumia pua.
Dege lililoleta kombe likiwasili uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere.
Wasanii wa kundi la Tanzania House of Talent (THT) wakitoa burudani Uwanja wa Taifa ambapo ziara ya kombe hilo ilizinduliwa.
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwasili Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuzindua kombe hilo. Kushoto ni mkewe, Mama Salma Kikwete, na kulia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Mh. Joel Bendera.
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Leodgar Tenga (kushoto), akimueleza jambo Rais Kikwete dakika chache kabla ya kuzindua kombe hilo.
Hivi ndivyo ‘JK’ alivyoanza uzinduzi wa kombe la FIFA.
Rais akiwa amefunikwa na maua wakati akizundua kombe hilo.
Kombe likipata busu la Rais baada ya kulizindua. Kulia ni mmoja wa maofisa wa FIFA aliyekuwa kwenye msafara wa kombe hilo.
Rais Kikwete akitabasamu wakati ameshikilia kombe hilo.
Aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana (kushoto) naye alikuwepo katika uzinduzi huo.
Hii ni sehemu ya watu waliofika uwanjani hapo kulishuhudia kombe hilo.
Kundi la THT likitoa burudani baada ya Rais Kikwete kumaliza uzinduzi.
*Sasa aomba Watanzania wampime *Ajigamba alichapa kazi akiwa Ikulu *Aambiwa aombe radhi asamehewe Kuna kila dalili kwamba Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ameanza kulegea juu ya msimamo wake wa kutokujibu tuhuma dhidi yake za kupoteza uadilifu akiwa madarakani...
*Wataka hatua zaidi dhidi ya ufisadi zichukuliwe *Vinginevyo hawatatoa fedha zao mwakani Nchi wahisani zimeiambia serikali iongeze nguvu zaidi katika kupambana na ufisadi vinginevyo watafikiria upya iwapo kuna haja ya kuendelea kuchangia bajeti ya serikali...
Christopher Lissa na Ismail Mang'ola Mpambano wa aina yake kati ya wafuasi wa madhehebu ya kilokole, wanaosali Kanisa la International Pentecost Holiness Ebenezer dhidi kijana anayedhaniwa kuwa ni mchawi, yamefanyika na kuacha mtikisiko mkubwa wa kiimani kwa walioshuhudia...
Sisi kama ShowBiz tumewahi kushuhudia muvi kibao za Kibongo nzuri lakini kwa upande wa Septemba 11 ambayo imeshuka kitaani hivi karibuni inaweza ikawa zaidi kutokana na kazi iliyogongwa na mastaa wengi waliopata nafasi ya kushiriki kunako mzigo huo...
Kupitia mpambano huu wa kumtafuta staa wa kiume mwenye mvuto wa kimahaba, Ijumaa Sexiest Bachelor wiki iliyopita tuliwataarifu kuwa leo tutashuka na Top 3, lakini kutokana na washiriki wawili kufungana kwa kupata idadi sawa ya kura huku Jerry Tegete akiambulia kura chache zaidi, imebidi wanne waingie kwenye Top 4 ambapo baadaye itatafutwa tatu bora kwa ajili ya kumpata mshindi mmoja...
Na mwandishi wetu Msanii wa filamu nchini, Aunt Ezekiel ameibukia ‘midia’ nyingine akidai kuwa, fumanizi aliloandikwa kupitia gazeti la mastaa wa Bongo, Risasi Jumamosi si la kweli na wala hana uhusiano usiyofaa na mwanaume huyo...