arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 24.11.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» JIDE HOI
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» HUKUMU YA BABU SEYA!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» MBINU ZA KUFANYA MTIHAN ...
» SHE IS TOO YOUNG TO DIE ...
» Mkali Wa Bongo Ampachik ...
» I am Back From Hell (31 ...
» Mchungaji afumaniwa aua ...
» Ushoga, usagaji, ukahab ...
» Kwa mafanikio 2008, taf ...

 

Mkenya ataka Sh 60m atue Simba

champion  
Na Mwandishi Wetu
KIUNGO Ahmed Jamal raia wa Kenya, amesema yuko tayari kutua Simba, lakini ametaka kitita cha dola 50,000 ili kujiunga na kikosi cha Msimbazi kwa ajili ya mzunguko wa pili...
    (24 November 2009)
Views: 120 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Manji ambakiza Mba Yanga

champion  
Na Mwandishi Wetu
HATUA ya mfadhili mkuu wa Yanga, Yusuf Manji kugoma kutoa kitita cha zaidi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya kumlipa mshambuliaji, Robert Jama Mba raia wa Cameroon, kimeifanya timu hiyo kushindwa kumuacha...
    (24 November 2009)
Views: 123 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Boko aipeleka Azam Caf

champion  
Na Khadija Mngwai
MSHAMBULIAJI wa nyota wa Azam FC, John Boko amesema atafanya kila juhudi kuhakikisha kikosi cha timu hiyo kinatimiza adhima yake ya kucheza michuano ya Kimataifa iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), msimu ujao...
    (24 November 2009)
Views: 61 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Manyema wahamishia nguvu kwa vijana

champion  
Na Samirah Phillip
UONGOZI wa Klabu ya Manyema Rangers baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom, wameelekeza nguvu zao kukinoa kikosi cha timu B kujiandaa na michuano ya Uhai inayotarajia kufanyika Novemba 29 jijini Dar es salaam...
    (24 November 2009)
Views: 41 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Mtibwa wataka Kombe la Tusker lihamie kwao Manungu

champion  
Na Samirah Philip
KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga amesema wataitumia mikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom kufanya vizuri na kulibeba kwa mara ya pili mfululizo kombe la Tusker...
    (24 November 2009)
Views: 37 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Maximo akiri kulindwa na JK

champion  
Samira Phillip na Leah Kweka
KOCHA mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars, Mbrazil, Marcio Maximo amesema anawashukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Kikwete na yule ya TFF, Leordegar Tenga kwa kuwa wanamuunga mkono katika maendeleo ya timu hiyo...
    (24 November 2009)
Views: 78 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Dalali atanua mbawa kwenye kiti Simba

champion  
Na Khadija Mngwai
MWENYEKITI wa Simba, Hassan Dalali amesema anajiamini kwa asilimia mia moja kuibuka na ushindi tena kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Desemba mwaka huu...
    (24 November 2009)
Views: 57 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Mtangazaji atamba na kikapu kwa watoto

champion  
Na Mwandishi Wetu
MMOJA wa wagombea katika Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Selemani Semunyu amesema iwapo atapata nafasi ya uongozi atajikita zaidi katika kusaka, kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto katika mchezo huo...
    (24 November 2009)
Views: 42 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Boniface Ambani arejea Yanga

champion  
Na Saleh Ally
MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita, Boniface Ambani amesema anatarajia kurejea Yanga ndani ya wiki hii kuzungumza na uongozi wa klabu hiyo na mwisho kuchukua malipo yake baada ya mkataba wake kuvunjwa...
    (24 November 2009)
Views: 107 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

The Painful Demand- 62

hadithi za Shigongo  
Amepandishwa juu ya ghorofa lililo jirani kabisa na ukumbi wa Golden Jubilee akiwa na bunduki yake aina ya AK47 na mikanda ya risasi, hapo alipo ni umbali wa mita mia mbili mpaka mahali walipo majambazi, maaskari na wanajeshi wanaamini si rahisi kumlenga mtu kwa risasi na kumpata lakini Josia amewaomba wamwachie kazi hiyo yeye! Muda mfupi baadaye helkopta ilionekana ikishuka taratibu juu ya paa la ukumbi wa Golden Jubilee ambako majambazi wamesimama wakijiandaa kupanda ili waondoke.

Walichokiona maaskari waliokuwa chini wakiwa wamekata tamaa na kuamini kombe limeondoka, ni jambazi akidondoka juu ya paa la ukumbi, yeye ndiye alikuwa amebeba kombe, likaanza kuporomoka juu ya bati na kwenda moja kwa moja hadi chini! Wakaelewa tayari Josia alikwishaanza kazi yake, jambazi mwingine tena akajaribu kuishika kamba lakini yeye pia akadondoka chini na kulala juu ya paa, hivyo ndivyo ilivyotokea kwa majambazi wote kumi, hatimaye helkopta ikaamua kuondoka.

Kwa Josia kazi ilikuwa imemalizika, akashuka haraka hadi chini ambako alikimbia mpaka mbele ya ukumbi wa Golden Jubilee na kunyanyua mikono yake juu akiwaita maaskari wamsogelee, wakafanya hivyo, kwa pamoja wakaingia ndani ya ukumbi na kukuta maelfu ya watu wamelaliana! Hakuna jambazi aliyekuwepo.

Josia na Vivian wanapanda hadi darini lengo lao likiwa ni kupita sehemu ile ile waliyopitia majambazi kuingia ndani ya ukumbi, hapo Josia alisita na kumwacha Vivian atangulie kwanza, moyoni mwake alijua hapakuwa na tatizo lolote, majambazi walishakufa lakini Vivian alipotokeza nje tu mlio wa risasi ulisikika.
Je, Vivian amekufa? Josia atafanya nini? SONGA NAYO..
    (24 November 2009)
Views: 585 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

WAFUNGWA NA THRILLER!

---  

Wafungwa wa Philipines wakijiliwaza kwa kuigiza uchezaji wa wimbo Thriller wa hayati Michael Jackson...ni mambo ya kuburudani tu!
    (24 November 2009)
Views: 41 | Maoni (0) |

 

RAIS WA UFILIPINO ATANGAZA HALI YA HATARI

Habari mbalimbali  

RAIS WA UFILIPINO ATANGAZA HALI YA HATARI

RAIS WA UFILIPINO ATANGAZA HALI YA HATARI

RAIS WA UFILIPINO ATANGAZA HALI YA HATARI
Juu ni picha za matukio zinazoonesha miili ya watu waliopoteza maisha kwenye vurugu za kisiasa huko nchini Ufilipino

RAIS WA UFILIPINO ATANGAZA HALI YA HATARI
Ramani ya Ufilipino kuonesha eneo lililokumbwa na machafuko

AMPATUAN, UFILIPINO
Rais wa Ufilipino, Gloria Arroyo ametangaza hali ya hatari kufuatia mauaji ya watu wapatao 46 katika machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini humo hivi karibuni.

Sehemu zilizotangazwa hali ya hatari kwa madhumuni ya kuwaruhusu askari polisi kuwatafuta wauaji ni majimbo mawili ya kisiwa cha Mindanao.

Waathirika wa mauaji hayo waliuawa wakati wakienda kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Mei, 2010. Hili ni miongoni mwa matukio mabaya ya vurugu za kabla ya uchaguzi kuwahi kutokea nchini Ufilipino.

Kumekuwa na taarifa nyingi za kuchanganya kuhusu idadi ya watu walionusurika katika maafa hayo. Jumatatu ya wiki hii iliripotiwa kuwa miili ya watu 22 iliokotwa kwenye mashimo visiwani humo lakini mpaka sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 46 wamepoteza maisha kutokana na vurugu hizo.

Imeelezwa kwamba idadi ya watu waliopoteza maisha inaweza kuongezeka zaidi endapo hali haitadhibitiwa mapema.
    (24 November 2009)
Views: 60 | Maoni (0) |

 

KESI YA LIYUMBA NGOMA INOGILE

photos  
Kesi ya ufujaji wa mamilioni katika Benki Kuu ya Tanzania BoT inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi Utawala na Fedha wa benki hiyo, Amatus Liyumba, leo imeendelea tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kusikilizwa.

Kesi hiyo imetolewa ushahidi na Mjumbe wa bodi ya benki kuu aliyekula kiapo kwa kujitambulisha kwa jina la Tatu Mwamba ‘hayupo kwenye mtandao kwa sababu maalum’, shahidi huyo pia ni Mhadhiri katika Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sambamba na cheo kingine alichokitaja mahakamani hapo kuwa ni Mwenyekiti wa Baraza Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), alipokuwa akielezea jinsi gani walivyokuwa wakifanya kazi katika jengo hilo la utawala.

JIKAZE KIUME MZEE HILI NALO LITAPITA
KESI YA LIYUMBA NGOMA INOGILE
Mtuhumiwa Liyumba akitoka katika sero ya mahabusu akipelekwa kizimbani kusikiliza shauri linalomkabili ambapo leo ilikuwa siku ya shahidi Tatu Mwamba kutoa ushahidi wake.

JELA KITU GANI BWANA!!!
KESI YA LIYUMBA NGOMA INOGILE
Mshitakiwa Liyumba akitembea kibabe kuelekea kizimbani huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa ‘walezi wa watukutu’ yaani askari magereza.

PANDA NGAZI SHUKA MPAKA LINI?
KESI YA LIYUMBA NGOMA INOGILE
Mshitakiwa Liyumba akipandisha ngazi kuelekea kizimbani kusikiliza kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo mishale ya saa nne asubuhi.

PICHA: ISMAIL MANG’OLA /GPL
    (24 November 2009)
Views: 67 | Maoni (1) |

 

Mfungwa aliyeua, akata rufaa dhidi ya kubaka

Habari mbalimbali  
Mfungwa aliyeua, akata rufaa dhidi ya kubaka
Steven Barker (kulia) aliyefungwa na mpenzi wake wa kike, Tracey Connelly (kushoto)

MMOJA wa watu watatu waliohukumiwa kifungo kutokana na kifo cha mtoto aitwaye Peter, leo atakata rufaa dhidi ya hukumu nyingine ya kumbaka mtoto wa kike aliyekuwa na umri wa miaka miwili...
    (24 November 2009)
Views: 370 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

China yawanyonga waliouza maziwa yenye sumu

Habari mbalimbali  
China yawanyonga waliouza maziwa yenye sumu
Watoto wakinywa maziwa hayo yaliyokuwa na sumu ambayo ilisababisha maelfu yao nchini China kuugua na wengine kufa.

China imewanyonga watu wawili walioshiriki katika njama kuhusu maziwa ya watoto yaliyotiwa sumu na kusababisha vifo vya watoto sita...
    (24 November 2009)
Views: 316 | Maoni (1) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com