arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 25.11.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» MSIBA FAMILIA YA MAGESA ...
» Mtoto wa Babu Seya bado ...
» Manji, Julio mezani
» Tunataka viongozi wa ke ...
» MPENZI WA NAMNA HII HAK ...
» Ushuhuda kabla ya kifo ...
» Phiri anasa wanne Chipo ...

 

Niliukubali mkoba wa kichawi ili niwe tajiri! -3

Mikasa ya kusisimua  
Mpenzi msomaji, kijana Kafumu aliyefundishwa uchawi na bibi yake, anaendelea kusimulia mambo aliyokumbana nayo baada ya kwenda kuhudhuria kikao cha kwanza cha wachawi na bibi yake aliyemdanganya kwamba akikubali kupokea mkoba aliotaka kumkabidhi ambao awali aliukataa, angekuwa tajiri mkubwa kwa sababu ndani ya mkoba huo kulikuwa na pesa nyingi.

Wiki iliyopita uliona alipopelekwa makaburi kuhudhuria kikao cha wachawi ambacho kiliarishwa baada ya kiongozi wa wachawi kubaini maiti waliofufuliwa waliohitajika katika kikao hicho hawakufaa. Je, nini kitafuata? Ungana na KULWA MWAIBALE katika mkasa huu wa kichawi…
    (25 November 2009)
Views: 507 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Knocked Down? You can stand up! -20

Amani  
Kelvin na rafiki yake Mabula, watoto waishio mtaani mjini Mwanza wameamua kuzamia ndege iliyokuja mjini Mwanza kuchukua minofu ya samaki kwenda Ulaya, wamejificha ndani ya mizigo ya samaki bila kuelewa kuwa kabla ndege kuondoka, friji kali za kuhifadhia samaki hao zingewashwa na kusababisha baridi kali chini ya nyuzi ishirini ambayo hakuna mwanadamu angeweza kuihimili.

Waliposikia muugurumo wa ndege nusu saa tangu wazame ndani, hali ya hewa ndani ya chumba hicho ilibadilika, baridi kali ikaanza na kuwafanya waanze kukakamaa miili! Hali ya Mabula ikawa mbaya zaidi, Kelvin akaanza kumwita lakini hakuitika, yeye mwenyewe taya zake zilikakamaa kabisa kiasi cha kushindwa kutamka maneno vizuri.

Je, nini kitatokea? Watafika Uingereza au watakufa ndani ya jokofu hilo? SONGA NAYO…
    (25 November 2009)
Views: 467 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Hofu inavyoathiri maisha ya mwanadamu

Saikolojia na maisha  
HOFU ni jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linazuia mtu kuendelea au kupiga hatua katika maisha. Bila shaka hata wewe ulishawahi kuhisi au kugundua kuwa kwa namna moja au nyingine unashindwa kufikia malengo yako kwa sababu ya hofu iliyotawala maisha yako...
    (25 November 2009)
Views: 162 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Kama kweli mnapendana kwa dhati, usiri wa nini?

Mahaba  
HAYA karibuni tena kwenye ‘mambo yetu yale’ ya malavudave, si unajua bila mapenzi hakuna maisha! Huo ndiyo ukweli wenyewe, huwezi kuishi kama jiwe au mti...
    (25 November 2009)
Views: 127 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

AKINA MAMA DOT COM!

Habari mbalimbali  
Hichi ni kisa cha kweli kabisa, houseboy alikuwa amepewa majukumu ya kumuhudumia mtoto wa bosi wake kwa kumpeleka shule pamoja na kuwa naye nyumbani wakati wazazi wake wakiwa kazini. Pamoja na kazi nyingine kijana huyu alkuwa anamuogesha huyu mtoto. Sasa katika kumuogesha uko akaanza kumfanyia UNYAMA huu wa kutisha sana kwa kumlawiti uku akimtisha huyu mtoto mdogo kwa vitisho vingi.

Na kwakuwa muda mrefu huyu houseboy ndie alikuwa anakaa na mtoto huyu mara nyingine wazazi walimkuta mtoto keshalala na wakiulizia maendeleo ya mtoto walikuwa wakiambiwa na houseboy huyu kuwa mtoto yuko okey hana problem. Na ikumbukwe kuwa wazazi wa mtoto huyu walikuwa na imani kubwa sana kwa houseboy huyu kwa kuwa alikuwa ndie anampleka shule na kwenda kumchukua kwenye basi mchana.

Kwahiyo huyu kijana akawa ndie anafanya kazi zote za ndani na
    (25 November 2009)
Views: 959 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

MH. PINDA AZINDUA MAADHIMISHO YA UKATILI WA JINSIA

photos  
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda leo alizindua maadhimisho ya siku 16 za kupambana na ukatili wa kijinsia. Uzinduzi huo ulifanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo Mh. Pinda alikemea vitendo vya ukatiri vinavyoendelea kwa jinsia zote na kuitaka jamii kushiriki kikamilifu katika mapambano hayo.
MH. PINDA AZINDUA MAADHIMISHO YA UKATILI WA JINSIA
Mh. Pinda akihutubia hadhara katika viwanja vya Mnazi Mmoja mapema leo kabla ya kuzindua rasmi maadhimisho hayo.

MH. PINDA AZINDUA MAADHIMISHO YA UKATILI WA JINSIA
Mh.Pinda akibonyeza king’ora maalum kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho hayo.

MH. PINDA AZINDUA MAADHIMISHO YA UKATILI WA JINSIA
Mapaparazi kibao walihudhuria hafla hiyo ambapo kila mmoja alikuwa bize kunasa picha ya ukweli.

MH. PINDA AZINDUA MAADHIMISHO YA UKATILI WA JINSIA
Hapa akikionesha kijitabu hicho.

MH. PINDA AZINDUA MAADHIMISHO YA UKATILI WA JINSIA
Mhe.Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadau

MH. PINDA AZINDUA MAADHIMISHO YA UKATILI WA JINSIA
Hafla hiyo ilipambwa na kundi la matarumbeta linaloongozwa na mzee maarufu kwa kazi hiyo aitwaye mzee Hozza aliyesimama mbele.

MH. PINDA AZINDUA MAADHIMISHO YA UKATILI WA JINSIA
Miamba ya muziki wa dansi nchini kutoka bendi ya Msondo Music, Said Mabela (kushoto) na Maalim Muhidin Gurumo ambao waliongoza bendi hiyo kutumbuiza kwenye hafla hiyo wakiteta jambo viwanjani hapo.

MH. PINDA AZINDUA MAADHIMISHO YA UKATILI WA JINSIA
Sehemu ya mabanda yaliyokuwa viwanjani hapo.
PICHA: RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA/GPL
    (25 November 2009)
Views: 59 | Maoni (0) |

 

DAVE SHORE ABORESHA MTANDAO WAKE!

photos  
DAVE SHORE ABORESHA MTANDAO WAKE!

DAVE SHORE ABORESHA MTANDAO WAKE!
Yule mhamasishaji maarufu kutoka Uingereza, Bw. Dave Shore, ameboresha mtandao wake kwa kuweka version ya Kiswahili inayoelezea jinsi mtu anavyoweza kuondokana na umasikini kwa kutimiza ndoto zake za kuwa na maisha bora. Bw. Dave, ambaye kwa sasa yuko jijini Dar akitoa mihadhara sehemu mbalimbali, ikiwemo Chuo Kikuu cha Mlimani Dar es salaam, ni Motivational Speaker ambaye ameweza kuwa Milionea kwa kuwekeza dola 14 tu za Kimarekani na leo kuwa na dola milioni 14, zaidi ya Bilioni 14 za Kibongo ndani ya miaka minne! Ili kujua siri hiyo na mengine mengi nenda hapa:www.breakthrough4u.com na pia sasa kuna email address ambayo unaweza kumtumia email.

Pia Bw. Dave amekuwa akisaidia jamii, hasa ya Kitanzania kwa muda mrefu, kikiwemo kituo hiki cha yatima cha Bethany kilichopo Magu, mkoani Mwanza ambacho amekuwa akisaidiana na wasamaria wema wengine kukisaidia michango mbalimbali ya hali na mali. Tembela wavuti yao hapa:www.bethanyfamily.net/

Pichani Bw. Dave akiwa na mwenyeji wake Abdallah Mrisho katika ofisi za Global Publishers wakati alipokuwa akimuonesha marekebisho aliyoyafanya kwenye mtandao wake, maalum kwa wadau wake wanaozungumza lugha ya Kiswahili.


(PICHA: CHRISTOPHER LISA/GPL)
    (25 November 2009)
Views: 67 | Maoni (1) |

 

MWANAFUNZI ANAPOKUWA JEURI!

photos  
VURUGU kubwa ilitokea leo ndani ya ‘daladala’ karibu na kituo cha polisi cha Chang’ombe jijini Dar es Salaam baada ya mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa kugoma kulipa nauli ya shilingi 100 katika basi linalofanya safari zake kati ya Tandika na Mwenge. Katika ‘varangati’ hilo abiria mmoja alijikuta akimwaga damu baada ya kupigwa jiwe na mwanafunzi huyo ambaye baadaye alitaka kutimua mbio.

MWANAFUNZI ANAPOKUWA JEURI!
Mwanafunzi huyo akidhibitiwa na kondakta wa daladala hilo baada ya “kumpachika” abiria jiwe. Abiria huyo alipatwa na mkasa huo baada ya kuunga mkono kwamba alipe nauli.

MWANAFUNZI ANAPOKUWA JEURI!
Kondakta na dereva wake wakisaidiana kumrudisha mwanafunzi huyo mahali alipofanya “jeuri” yake ili ajibu tuhuma za kumjeruhi na kumsababishia maumivu abiria asiyekuwa na hatia.

MWANAFUNZI ANAPOKUWA JEURI!
Hapa akiingia kwenye daladala alikofanyia uhalifu wake.

MWANAFUNZI ANAPOKUWA JEURI!
Kushoto ni abiria aliyepigwa jiwe na mwanafunzi huyo akiingia kwenye daladala hilo tayari kuelekea kituo cha Polisi.

MWANAFUNZI ANAPOKUWA JEURI!
Daladala lililohusika katika masahibu hayo likielekea kwa “Pilato” kupata ufumbuzi.
PICHA: ISMAIL MANG’OLA /GPL
    (25 November 2009)
Views: 106 | Maoni (3) |

 

Muuaji aliyetoroka kifungo akamatwa

photos  

Muuaji aliyetoroka kifungo akamatwa
Jane Andrews, mfungwa aliyetoroka katika gereza la East Sutton Park Jumapili iliyopita.

Muuaji aliyetoroka kifungo akamatwa
Mmoja wa polisi waliokuwa wakimsaka mtoro huyo katika vichaka.

* Alimuua mwanamme kwa kukataa kumwoa
JANE ANDREWS (24) mfanyakazi katika familia ya kifalme nchini Uingereza, aliyefungwa kifungo cha maisha mnamo mwaka 2001 kwa kumuua mwanamme mmoja kwa kumpiga kwa rungu na kisha kumchoma kisu amekamatwa baada ya kutoroka kutoka gerezani usiku Jumapili iliyopita...
    (25 November 2009)
Views: 300 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

MAAJABU: VYOO VYAZIBA KWENYE NDEGE

Habari mbalimbali  
MAAJABU: VYOO VYAZIBA KWENYE NDEGE
Moja ya ndege ambazo zilitua Mumbai kwa ajili ya tatizo la vyoo kuharibika.

SHIRIKA la ndege la Cathay Pacific limesema kwamba ndege zake aina ya Airbus zimekumbwa na tatizo la kuziba vyoo...
    (25 November 2009)
Views: 256 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

D’banj kupagawisha Bongo ndani ya STR8MUZIK FESTIVAL J’mosi hii

photos  
D’banj kupagawisha Bongo ndani ya STR8MUZIK FESTIVAL J’mosi hii
D'banj kutoka Nigeria.

D’banj kupagawisha Bongo ndani ya STR8MUZIK FESTIVAL J’mosi hii
Juacali kutoka nchini, Kenya.

D’banj kupagawisha Bongo ndani ya STR8MUZIK FESTIVAL J’mosi hii
TID mmoja wa wasanii kutoka Tz watakaopanda jukwaani siku hiyo.

Mwanamuziki mahiri kutoka Nigeria, anayetamba na singo zake kali kama Fall In Love, Olorun Maje, Gbono Fele, Entertainer , Suddenly, na Igwe, Dapo Daniel Oyebanjo maarufu kwa jina la D’banj, anataraji kukandamiza shoo moja matata siku ya Jumamosi ya Novemba 28, 2009 katika viwanja vya Tanganyika Parkers (Kawe).

Wasanii wengine watakaoporomosha burudani sambamba na mkali huyo ni Juacali, Nonini na Nameless wote kutoka Kenya.

Tanzania itawakilishwa na wakali TID, Mangwea, Belle 9, Cpwaa, kundi la THT, Marlaw, Joh Makini na Quick Racker.
Burudani hiyo itaporomoshwa chini ya udhamini wa Str8Musics mahsusi kwa ajili ya Wanachuo wote.

Shoo inataraji kuanza mishale ya saa 11 jioni na kumalizika saa 8 usiku.
    (25 November 2009)
Views: 48 | Maoni (0) |

 

Waziri mkuu atembelewa na mwakilishi wa UNHCR

photos  
Waziri mkuu atembelewa na mwakilishi wa UNHCR
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mwakilishi wa UNHCR nchini, Yacoub El HIllo ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 25 , 2009 kwa ajili ya kuaga.

Waziri mkuu atembelewa na mwakilishi wa UNHCR
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago Mwakilishi huyo kabla ya kuondoka.
Picha: Ofisi ya Waziri Mkuu
    (25 November 2009)
Views: 71 | Maoni (0) |

 

DOGO KING’ANG’NIZI WEWE NGOJA NIKUPE NAMBA YANGU

photos  
DOGO KING’ANG’NIZI WEWE NGOJA NIKUPE NAMBA YANGU
Msanii kiraka kutoka kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Family, Chegge a.k.a Chegge Chibindu mtoto wa mama Saidi mvunja nazi kwa ugoko( kushoto) akimpa namba yake ya simu dogo mmoja king’ang’anizi ambaye alidai ni mwanamuziki ili waweze kuwasiliana.Picha hii imenaswa pande za Coco Beach jijini Dar es Salaam wakati alipokwenda kubarizi.

KUJENGA SHAVU MUHIMU
DOGO KING’ANG’NIZI WEWE NGOJA NIKUPE NAMBA YANGU
Mwanadada huyu alliyefahamika kwa jina moja la Nice alibambwa jana jioni akijipendelea mapochopocho katika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam.

FULL KUJIACHIA NA FEGI MKONONI
DOGO KING’ANG’NIZI WEWE NGOJA NIKUPE NAMBA YANGU
Demu huyu ‘waluwalu’ alinaswa ndani ya Ukumbi wa Mango hivi karibuni akijiachia baada ya kukoshwa na midundo ya muziki wa taarab iliyokuwa ikifurumushwa na kundi la New Zanzibar Stars Modern Taarab huku akiwa na fegi mkononi.

MNENGUAJI ANAYETIKISA AKUDO

DOGO KING’ANG’NIZI WEWE NGOJA NIKUPE NAMBA YANGU
Mnenguaji nyota nchini anayepiga mzigo katika bendi ya muziki wa dansi ya Akudo Impact ‘Chuo cha masauti,’ Said Abdallah ‘Chipsi kuku’ akiwa katika picha ya pozi.Msanii huyo aliuambia mtandao huu kuwa pamoja na umuhimu wa wanenguaji katika bendi lakini hawathaminiki kabisa.

MAN DOJO NIKO GADO
DOGO KING’ANG’NIZI WEWE NGOJA NIKUPE NAMBA YANGU
Msanii kiraka wa muziki wa kizazi kipya, Son Man Dojo ambaye anakamua pamoja na mchizi wake Domokaya, akiwa katika picha ya pozi.Msela huyo alidai kuwa licha ya kutokusikika sana hivi sasa lakini bado yuko gado kwenye ‘game’.

HII KALI
DOGO KING’ANG’NIZI WEWE NGOJA NIKUPE NAMBA YANGU
Mtaalamu wa kitengo cha Kompyuta na mtandao huu, Clarance Mulisa (kushoto) akifuatiwa na Rapa staa Bongo, Adolf Ramji 'Rado'(wapili kushoto) pamoja na Malkia wa muziki wa Zouk nchini, Stara Thomas (wapili kulia) wakiwa na washkaji zao wakifurahi wakati wa shamrashamra za Tamasha kubwa la Fiesta ‘One Love’ lililojiri Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita..
PICHA: CHRISTOPHER LISSA/GPL
    (25 November 2009)
Views: 98 | Maoni (2) |

 

Jiji lanusa mchezo mchafu stendi ya Ubungo

Habari mbalimbali  
Jiji lanusa mchezo mchafu stendi ya Ubungo
Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru ambaye familia yake ilikuwa inamiliki kampuni ya Smart Holdings

MAPATO katika Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo (UBT), yameongezeka kutoka sh milioni moja kwa siku hadi sh milioni nne...
    (25 November 2009)
Views: 544 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

POLISI WAZIDI KUUA RAIA KWA RISASI

photos  
Hivi karibuni, raia mmoja mkazi wa Ubungo Msewe, jijini Dar es Salaam, Bwana George Jackson De’Mzee Nyanda aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi CP Chediel George wa kituo cha Polisi cha Stakishari, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi na taratibu za kumpandisha kizimbani tayari zimeanza kufanywa.
Chini ni picha za shughuli ya mazishi ya marehemu Nyanda yaliyofanyika katika makaburi ya Rombo Jijini Dar es Salaam.
POLISI WAZIDI KUUA RAIA KWA RISASI
Marehemu enzi za uhai wake

POLISI WAZIDI KUUA RAIA KWA RISASI
Mwili wa marehemu George Nyanda ukiagwa katika kanisa la Mt Paulo, Ubungo Msewe.

Video hii inaonesha sehemu ya ibada ya kumuaga marehemu George


POLISI WAZIDI KUUA RAIA KWA RISASI
Vijana wa eneo hilo walizuia mwili huo kubebwa na gari na wakaahidi kulibeba jeneza hilo kwa mikono hadi makaburini kama wanavyoonekana pichani.

Haya ni maandamano ya watu wakielekea makaburini


POLISI WAZIDI KUUA RAIA KWA RISASI
Hatimaye jeneza likiingizwa kaburini.

POLISI WAZIDI KUUA RAIA KWA RISASI
Kukamilika kwa shughuli ya kumlaza marehemu George katika mapumziko ya amani.

PICHA PAMOJA NA VIDEO: AZIZ HASHIM NA HARUNI SANCHAWA /GPL)
    (25 November 2009)
Views: 110 | Maoni (3) |
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com