*Watu arobaini na nane wamefariki katika mji wa bandari wa Saudi Arabia wa Jeddah kufuatia kunyesha kwa mvua kubwa sana kuwahi kushudiwa nchini humo katika miaka mingi.
Mahujaji wa Kiislamu wakiwa katika Mlima Arafat nchini Saudi Arabia leo kukamilisha ibada ya hija.
Baadhi ya watu wamekufa maji, wengine wamekufa kutokana na kuanguka kwa madaraja na kutokana na ajali za magari.Ibada ya hija inayofanyika katika mji mtakatifu wa Mecca nchini Saudi Arabia imetibuliwa na mvua hiyo kubwa...
Taarifa kutoka Washington, zinasema kwamba, Rais Barack Obama, ameamua sasa kuhudhuria binafsi ule mkutano wa kilele wa kuzuia uchafuzi wa hali ya hewa utakaofanyika mwezi ujao mjini Copenhagen,Denmark.Marekani inapanga kutangaza mpango wake wa kwanza kabisa wa kupambana na moshi unaochafua mazingira...
Andrew alikuwa na umri wa miaka 11 aliponyanyaswa kingono.
KWA mujibu wa Ripoti itakayotolewa na Ryan (Ryan Report), msimamo ambao Kanisa Katoliki la Dublin linavyoshughulikia vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto, utakuwa ni wa kutisha...
Staa wa muziki wa injili nchini Jennifer Mgendi, Novemba 29 mwaka huu anatarajia kuzindua albamu yake iitwayo Kiu ya nafsi.Katika uzinduzi huo atasindikizwa na wasanii kibao wa muziki huo ambao ni Bahati Bukuku a.k.a Mama maadili, Cosmas Chidumule, Charles Jangalason, Neema Mwaipopo, Christina Mwang’onda, Ann Annie, Whispers Band, Trinity Band na Wema Sanga.
Shughuli hiyo itafanyika ndani ya Ukumbi wa Land Mark Hotel uliopo maeneo ya ubungo jijini Dar es Salaam, na albamu hiyo imebeba vibao kumi ambavyo ni Jaribu langu, Nivute kwako, Ni yesu Mnazareti, Nifundishe kusifu, Nitasubiri, fadhili, Kutapambazuka, Neno lako, Yesu yupo na Kwake nitatumai.
Jennifer Mgendi akiwa katika picha ya pozi
Hapa akiwapa akapela ya baadhi ya nyimbo zake waandishi wa mtandao huu alipotembelea ofisi za Global Publishers, Bamaga jijini Dar es Salaam leo.
Hapa midadi ya kuimba ilizidi kumpanda.
PAMOJA NA AJALI NITAKOMAA NA GAME-JITTA MAN Staa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Lissu Ibrahimu a.k.a Jitta Man au Nzagamba Mamba au Teminator kama anavyojiita hivi sasa akiwa katika picha ya pozi ndani ya ofisi za tovuti hii leo.Mchizi alisisitiza kuwa pamoja na ajali aliyopata Mwanza hivi karibuni na kumuathiri vibaya lakini bado ataendelea kukamua katika game.Jamaa yuko mbioni kuachia ngoma itakayokwenda kwa jina la Nawasabahi akimshirikisha The Heavy Weight MC, Bongo, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ a.k.a Mti mkavu.
Jitta Man (Kushoto) akiwa na Mhariri wa gazeti la Championi Elius Kambili ambaye ni swahiba wake mkubwa.
KISHOKA Jamaa huyu alinaswa na kamera yetu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam akichokonoa umeme bila kutumia vifaa vyovyote vya kujikinga hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wake.
Mwanahabari mkongwe ndani na nje ya nchi ambaye kwa sasa anafanya shughuli zake Washington nchini Marekani, Mobhare Matinyi, leo alitembelea ofisi za Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Amani, Risasi, Champion na Ijumaa Wikienda na kuongea na waandishi kuhusu tasnia ya habari na kuwaambia changa moto mbalimbali ambazo amezipitia wakati akifanyakazi na kampuni ya Business Times, wachapishaji wa gazeti la Majira na hadi kufikia huko aliko sasa. Amesema kuwa siri ya mafanikio yake ni kufanyakazi kwa bidii na maarifa.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Global Pulishers, Richard Manyota, akizungumza na wafanyakazi wa Global Publishers kabla ya kumkaribisha Mobhare Matinyi, kuzungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Matinyi (kulia) akiwa kwenye pozi kabla ya kuanza kuzungumza na wafanyakazi wa Global Publishers. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.
Sehemu ya wafanyakazi wa Global wakimsikiliza Matinyi.
Matinyi akisistiza jambo wakati akiongea kwenye mkutano huo.
Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota, akiwa kwenye kiti chake wakati akimsikiliza Matinyi.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho (kushoto), akimpa mkono wa pongezi, Matinyi baada ya kumaliza mazungumzo na wafanyakazi.
Mhariri Kiongozi wa magazeti ya Championi, Saleh Ally, akitoa shukrani kwa Matinyi kwa yale aliyomfundisha miaka kadhaa iliyopita katika fani ya uandishi wa habari.
Mhariri wa gazeti la Amani, Sifael Paul, maarufu kama Kigogo Mzito, akiuliza swali juu ya uwezekano wa waandishi wa nchini kushirikiana na magazeti ya Kiswahili yaliyopo nchini Marekani na Uingereza.
Msanifu kurasa wa Global, Moses Makambi, akinyoosha mkono kumshukuru Matinyi kwa kumfundisha kusanifu kurasa katika siku za nyuma.
Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho, akimshukuru Matinyi baada ya mazungumzo yaliyowapa hamasa na mafunzo wafanyakazi wa kampuni yake.
Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota akimpa mkono wa pongezi, Matinyi, baada ya kufunga mkutano huo. Katikati ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.
Baada ya mazungumzo, Matinyi alifika mezani kwa Mhariri Mtendaji wa Global kuangalia uzalishaji wa magazeti ya kampuni hiyo.
Matinyi (kulia) akiangalia kazi za mmoja wa wasanifu kurasa wa Global Publishers.
Mgeni huyo (katikati) alimalizia mazungumzo yake ofisini kwa Meneja Mkuu Abdalah Mrsho (kushoto). Kulia ni Mhariri Mtendaji Richard Manyota.
• Wakumbuke miafaka mitatu “waliliwa chenga” na CCM • Tatizo kubwa ni uadilifu katika chaguzi Zanzibar
Na Walusanga Ndaki
KWA watu wasiokuwa na ushabiki wa vyama vya siasa – watu wenye kuweka maslahi ya taifa lao kwanza, ni dhahiri wataunga mkono hatua ya Chama cha Wananchi – CUF – kumtambua Amani Karume kama rais wa Zanzibar na serikali yake. Lakini pia, kwa watu watu wasiokuwa na ushabiki wa vyama vya siasa, na ambao wamekuwa wakiyafuatilia kwa masikitiko matukio mengi huko Zanzibar tangu mwaka 1995 ni dhahiri watakumbuka kwamba pamekuwepo na makubaliano (Miafaka) yaliyofikiwa mara tatu kati ya CUF na Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Safu ya wanenguaji wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) wakishambulia jukwaa wakati bendi hiyo ilipofanya onesho ndani ya ukumbi wa Cub Billicanas (Muc Mo) uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mwimbaji nyota wa ‘Twanga’, Saulo John (Ferguson) akipagawisha mashabiki.
Mnenguaji nyota wa Twanga, Lilian Tungaraza (Liliani Internet) akiwa amemdandia shabiki na kumkatia mauno kisawasawa wakati wa onesho hilo.
Lilian Internet akionesha kipaji chake baina ya jukwaa na mwili wake.
Mnenguaji mwenye mvuto mahsusi wa wana-Twanga, Aisha Mbegu Madinda akiwajibika jukwaani.
Chiriku wa kike wa Twanga, Luiza Nyoni Mbutu akitoa burudani jukwaani.
• Makamu wake asema ni tishio UWT SAKATA la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), limechukua sura mpya, baada ya Mwenyekiti wa umoja huo, Sophia Simba, kuelezwa kuwa ni tishio, ndiyo maana amekuwa akipigwa vita na baadhi ya wanasiasa tangu kushika nafasi hiyo...
Aitaka serikali iwe wazi,itoe taarifa za kweli WIKI moja baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kusema Ikulu imeliachia Bunge kuamua sakata la mkataba wa kifisadi kati ya Shirika la Umeme (Tanesco) na Kampuni ya Richmond Development (LLC); Spika wa Bunge, Samuel Sitta ameibuka na kusema kuwa serikali lazima iwe wazi na kutoa majibu kwakuwa suala hilo ni la kwao...
Na Mwandishi Wetu MVULANA anayedaiwa ni mwana wa damu wa Naibu Waziri wa wizara moja nyeti Bongo (jina tunalo), amefanya aibu kubwa jijini Dar kufuatia kupiga picha chafu za utupu akiwa na Miss maarufu aliyeshiriki Shindano la Balozi wa Kiswahili 2009, Rehma Fabian ‘Video Queen’, Amani linapambanua neno kwa neno...
Bongo Fleva imekula bonge la shavu kwa mtasha baada ya The Hip hop icon Bongo, Ilunga Khalifa ‘C-Pwaa’ hivi juzi kati kubambwa akiminya kimtindo na demu mwenye rangi ya Bara la Ulaya...