Na Saleh Ally ILIKUWA ni kama kilichopangwa maalum kwa ajili ya filamu, baada ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo kuamua kutoka ofisini kwake haraka haraka, dakika chache baada ya kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ kuingia ndani ya ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambamo pia zimo ofisi za Mbrazil huyo...
Na Saleh Ally MSHAMBULIAJI Boniface Ngaira Ambani amesema anatua jijini Dar es Salaam keshokutwa huku akisisitiza anafuata haki zake na si kuichezea Yanga na mwisho ameweka bayana sababu zilizomfanya agome kurejea...
Ingawa alikuwa ni mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa, Josia anaondolewa gerezani muda mfupi kabla kitanzi hakijakomesha uhai wake! Serikali imeamua kumpa operesheni maalum ya kukomboa mateka waliotekwa na majambazi kwenye ukumbi wa Golden Jubilee ambako watu wengi walikuwa wamekusanyika kulishuhudia kombe la dunia, mgeni rasmi akiwa Waziri wa Vijana Mheshimiwa Theofilo Maganiko Maganiko ambaye pia ni mtoto wa Waziri Mkuu.
Jeshi la polisi pamoja na wananchi walishindwa kabisa kuifanya kazi hiyo kwa sababu ya uwezo wa kulenga shabaha waliokuwa nao majambazi, wanajeshi wengi wakafa! Josia akaungana na Vivian katika operesheni hiyo ngumu ambako Vivian alipigwa risasi alipotokeza tu juu ya paa kabla hawajaanza kufanya lolote!
Josia akamshusha Vivian chini na kumkabidhi kwa maaskari wampeleke hospitali yeye akarejea tena juu ya paa kupambana na jambazi mmoja mwenye shabaha za ajabu aliyesalia, aliposimama tu wima risasi zilimpenya hata hivyo tayari alishafyatua risasi nyingi na kumpiga jambazi huyo akaanguka juu ya paa, Josia akakimbizwa hospitali akiwa na hali mbaya.
Baadaye alipozinduka aliulizia mahali alipokuwa Vivian, hapakuwa na mtu wa kumpa jibu, akapoteza fahamu ambazo zilimrejea baadaye akiwa ndani ya ndege, kando yake akiwepo Vivian! Walikuwa wakisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu, huko walitibiwa na kupona kisha kurejea nyumbani ambako walipelekwa moja kwa moja Ikulu kupokea tuzo ya Rais ya Ujasiri, hakuna mtu aliyekumbuka tena kwa Josia alikuwa muuaji aliyehukumiwa kunyongwa, kazi aliyoifanya ilimbadili jina na kuwa shujaa.
Sherehe ikiendelea ndani ya viwanja ya Ikulu, risasi zilisika zikilia kwenye lango kuu la kuingilia! Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
PARIS Lionel Messi has been selected among four Barcelona players on a shortlist of 10 for the Golden Ball award.
The Argentina forward was included Sunday along with teammates Zlatan Ibrahimovic, Xavi Hernandez and Andres Iniesta on the list by France Football magazine.
Messi is the favorite to succeed Real Madrid winger Cristiano Ronaldo, who is also on the list, as the best player in Europe. The winner will be announced on Tuesday.
Restricted to players in Europe, the annual Golden Ball winner is decided by a poll of football journalists compiled by the magazine.
The other players on the list are Didier Drogba (Chelsea), Samuel Eto'o (Inter Milan), Steven Gerrard (Liverpool), Kaka (Real Madrid) and Wayne Rooney (Manchester United).
Some 800,000 people were killed in Rwanda's genocide in 1994
*The Commonwealth has admitted Rwanda as its 54th member. The African country was admitted at the Commonwealth Heads of Government Meeting in Trinidad and Tobago, a statement from the group said...
Baada ya kupoteza pambano lake kiutatanishi Oktoba 10 dhidi ya Juan Lopez na kukataliwa pambano la marejeano licha ya kuonesha uwezekano mkubwa wa "kumuumbua" Lopez, bondia Mtanzania aishiye Philadelphia Rogers "The Tiger" Mtagwa atapanda ulingoni Jan 23, 2010 kupambana na bondia anayefanya vema saana na nyota ing'aayo toka Cuba, Yuriorkis Gamboa.
Pambano hilo litakalopiganiwa New York na kuonekana kupitia HBO, litakuwa ni la kuwania mkanda wa Gamboa wa uzito wa Unyoya (featherweight) unaotambuliwa na Chama cha Ndondi Ulimwenguni (WBA). Usiku huohuo na katika ukumbi huohuo, Juan Manuel Lopez ambaye alipata ushindi dhidi ya Mtagwa atapambana na Steven Luevano kuwania mkanda wa Shirikisho la Ndondi Ulimwenguni (WBO) unaoshikiliwa na Luevano.
Iwapo Mtagwa atavuka kigingi hiki kigumu (kulingana na ubora na upiganaji wa Bwana mdogo Gamboa) atakuwa amejiweka katika mazingira mazuri ya kurejea ulingoni na Lopez kama wataweza kuafkiana katika kuunganisha mikanda kwani yote ni ya uzito mmoja. Hapa chini ni Video ya pambano la Mtagwa la mwezi uliopita
Ajali ya gari ya mcheza Golf maarufu duniani, Tiger Woods, imezua mjadala mkubwa, wengine wanasema ni ajali kweli wengine wanadai alipigwa na mkewe...sikia jamaa anavyoongea kuhusu ishu hii..!
Mwanamuziki kutoka Nigeria, D’banj, jana alifanya onyesho la kufa mtu katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe jijini Dar es Salaam. Onyesho hilo lilikuwa maalum kwa wanafunzi wa vyuo katika tamasha lililojulikana kama 'STR8MUZIK FESTIVAL'.
Katika onyesho hilo lililokusanya watu wengi ambapo kiingilio kilikuwa shilingi 3,500, likiwa linakaribia kwisha, vijana wa kihuni walisababisha vurugu kubwa baada ya kutoridhishwa na nyimbo ambazo alikuwa akiimba mwanzo na ambazo walikuwa hawazifahamu. Vurugu hiyo ilikuwa ni pamoja na kelele na urushwaji wa vitu mbalimbali kama chupa za maji na makopo ya bia.
Mwanamuziki D’ banj (kushoto) akiimba pamoja na mwanamuziki mwenzake Ice Chuku katika onyesho hilo.
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Albert Mangwea, akitoa burudani katika onyesho hilo.
Jua Cali, msanii kutoka Kenya, akitoa burudani kabla ya D’ banj kupanda jukwaani.
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Keisha (Hadija Shaban), wa Tanzania, akimpiga picha D’ banj.
Akina dada ambao hawakutaka kutaja majina yao, wakiwa wamekaa chini wakimshangilia D’ banj.
Mabaunsa wakiwatuliza mashabiki wakorofi ambao walikuwa wakitaka kuvuka uzio ili waende jukwaani kucheza sambamba na D’banj.
Kijana mlemavu ambaye jina lake halikujulikana, akiwa ameutwanga usingizi wakati onesho hilo likiendelea
D’banj akipata kinywaji kabla ya kupanda jukwaani kuanza makamuzi yake.
Shabiki aliyepagawa akiwa amembeba D’banj alipokuwa akiimba kibao chake mahiri cha ‘Fall in Love’
MOSCOW MAAFISA nchini Urusi wamethibitisha kwamba mlipuko wa bomu ndio uliosababisha ajali ya treni iliyoua kiasi cha watu 26 na kuwajeruhi wengine wapatao 100...
WINDHOEK, NAMIBIA MATOKEO ya awali ya uchaguzi nchini Namibia yanatarajiwa kuanza kutolewa leo jioni. Chama tawala cha SWAPO nchini Namibia kinatazamiwa kubakia madarakani na Rais Hifikepunye Pohamba kupata ushindi mwepesi kwa muhula wake wa pili...
PORT OF SPAIN VIONGOZI wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola wanaowawakilisha watu bilioni mbili ulimwenguni, wamesema wataunga mkono maafikiano yatakayopatikana kuhusu kupunguza gesi zinazochafua mazingira katika mkutano wa kimataifa kuhusu hali ya hewa utakaofanyika wiki ijayo mjini Copenhagen...
KINSHASA SHIRIKA la kimataifa la Msalaba Mwekundu, limesema watu 73 wamefariki baada ya boti yao kuzama katika eneo la magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kituo cha Radio Okapi kimeripoti kuwa boti hiyo ambayo ilikuwa imewabeba abiria kinyume cha sheria, ilizama kutokana na hali mbaya ya hewa.
Idadi ya watu ambao hawajulikani walipo, haifahamiki, kwa sababu boti hiyo haikuwa na orodha rasmi ya abiria waliokuwa ndani wakati ajali hiyo ilipotokea.