arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for December 2009 Year

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» MSHANGAO!
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» VALENTINE YA UFUSKA!
» Apata ajali ya ajabu
» KUTAFUTA MAISHA KUMENIF ...
» Bezinski: NITAFANYA...
» THE LAST HOPE (tumaini ...
» SIMBA YAZIDI KUJIKITA K ...
» Kutafuta cheo kazini ku ...
» Ambani aendelea kutikis ...

 

RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA ULINGONI KESHO

photos  
Mabondia Rashid Matumla ‘Snake Boy’ na Joseph Marwa, kesho jioni wanatarajiwa kutwangana katika pambano lisilokuwa la ubingwa litakalofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa Idara ya habari jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa pambano hilo, Ramadhani Uhadi alisema maandalizi yote ya mpambano huo yameshakamilika.

RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA ULINGONI KESHO
Promota wa mpambano huo Ramadhani Uhadi akiwainua mikono mabondia hao Joseph Marwa (kushoto) na Rashid Matumla wakati akiwatambulisha.

RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA ULINGONI KESHO
Rashid Matumla akipima Uzito kwaajili ya mpambano huo.

RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA ULINGONI KESHO
Joseph Marwa naye akipima uzito.

RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA ULINGONI KESHO
Jeseph Marwa (kushoto) na Rashid Matumla wakichimbiana mkwara kabla ya mpambano huo.

RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA ULINGONI KESHO
Matumla akimwaga majigambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).

RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA ULINGONI KESHO
Marwa naye alipopata nafasi aliyaponda majigambo ya Matumla na kujitapa kuwa yeye ndiye kidume na kusema kesho ndio kesho.

PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL
    (31 December 2009)
Views: 82 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

MWILI WA MZEE KAWAWA WAHAMISHIWA LUGALO

Videos  

Marehemu Kawawa aliyefariki leo asubuhi saa 3:20 asubuhi, amehamishiwa hospitali ya jeshi la Wananchi ya Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa wakati mipango ya mazishi ikifanywa na kusimamiwa na Serikali. Zifuatazo ni picha za tukio zima jinsi lilivyokuwa:

MWILI WA MZEE KAWAWA WAHAMISHIWA LUGALO
Mke wa marehemu, (aliyejifunga kilemba cheupe katikati) Bi Asina, akiusindikiza mwili wa mumewe Mzee Rashid Mfaume Kawawa.

MWILI WA MZEE KAWAWA WAHAMISHIWA LUGALO
Mama Salma Kikwete (wa pili kushoto mwenye kilemba) alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliofika hospitalini hapo.

MWILI WA MZEE KAWAWA WAHAMISHIWA LUGALO
Huu ni msafara wa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kuelekea Hospitali ya Lugalo.

MWILI WA MZEE KAWAWA WAHAMISHIWA LUGALO
Kamishna mkuu wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova naye alikuwa miongoni mwa waombolezaji, ambapo alitumia nafasi hiyo kutangaza jinsi jeshi lake litakavyodhibiti usalama katika shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya 2010 usiku wa leo.

Picha: Musa mateja/GPL

Video mbili hapo chini, Mwili wa marehemu Mzee Kawawa ukitolewa Muhimbili tayari kupelekwa Hospitali ya Lugalo



    (31 December 2009)
Views: 160 | Maoni (2) |

 

KIFO CHA MZEE KAWAWA, TAIFA KUOMBOLEZA SIKU SABA

photos  

KIFO CHA MZEE KAWAWA, TAIFA KUOMBOLEZA SIKU SABA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ametangaza siku saba za maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mzee Rashid Mfaume Kawawa, aliyefariki duania leo saa 3:20 asubuhi baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu kwa muda huo bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti.

Rais alisema kuwa taratibu zote mazishi zitasimamiwa na serikali na atapewa heshima kwa muasisi wa kupigania uhuru wa Tanzania.

    (31 December 2009)
Views: 141 | Maoni (2) |

 

WASANII WASEMEANA MBOVU KWENYE 'YOU TUBE'

Videos  

Msanii wa Bongo Flava anayejiita Beezy anayeiishi nchini Ujerumani, akimpaka Producer Marco Chali kwa madai ya kumzika milioni 1 za kibongo...msikilize mwenyewe.




Msanii wa Bongo Flava, anayejiita Wakazi anayeishi Chicago, Marekani, akimtetea Marco Chali kwa kumponda Weezy kuwa hajui kuimba vile vile..msikilize mwenywe.... kila mmoja katengeneza clip yake na kuiweka You Tube kila mtu aone na kusikia, hili ni bifu la kufungia mwaka, kazi kwenu wadau
    (31 December 2009)
Views: 95 | Maoni (5) |

 

Nyumba nyingine BoT yagharimu Sh1.2 bilioni

Habari mbalimbali  

Nyumba nyingine BoT yagharimu Sh1.2 bilioni
Nyumba ya Gavana wa Benki kuu, Profesa Benno Ndulu

Nyumba nyingine BoT yagharimu Sh1.2 bilioni
Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu

WAKATI Wizara ya Fedha na Uchumi ikiwa katika uchunguzi wa gharama za ujenzi wa nyumba ya gavana wa BoT inayodaiwa kugharimu Sh1.4 bilioni, imebainika kuwa nyumba nyingine ya mmoja wa manaibu wake imegharimu Sh1.2 bilioni...
    (31 December 2009)
Views: 228 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

BREAKING NEWS: MZEE KAWAWA AFARIKI DUNIA LEO!

photos  
BREAKING NEWS: MZEE KAWAWA AFARIKI DUNIA LEO!
Marehemu Rashid Kawawa

BREAKING NEWS: MZEE KAWAWA AFARIKI DUNIA LEO!
Picha hii ilipigwa Februari 27 mwaka huu, wakati Rais J.K akimpongeza Mzee Kawawa baada ya kuzindua kitabu chake uliofanyika katika viwanja vya Ikulu. Kitabu hicho kinachoelezea maisha ya Mzee Kawawa, kimeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu chini ya usimamizi wa Profesa John Magoti, Mkuu wa Chuo cha Mwalimu Nyerere cha Kivukoni.

BREAKING NEWS: MZEE KAWAWA AFARIKI DUNIA LEO!
..hapa akitia saini kwenye moja ya vitabu vyake



Habari za kusikitisha za asubuhi ya leo zinasema kuwa Mzee Rashid Mfaume Kawawa, ambaye alizushiwa kifo jana, amefariki dunia leo asubuhi hii. Taarifa fupi ya Radio One Stereo iliyotolewa muda mfupi uliopita, imethibitisha kifo hicho. Mzee Rashid Kawawa, anafariki leo ikiwa ni siku ya mwisho kabisa ya kumaliza mwaka 2009 na anakufa akiwa na umri wa miaka 83. Mzee kawawa, ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la Simba wa Vita, ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Awamu ya Kwanza wa Serikali chini ya hayati Baba wa Taifa, JK. Nyerere. MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEPONI - AMIN!


    (31 December 2009)
Views: 196 | Maoni (1) |

 

Dk Slaa amtaka Rais Kikwete awaombe radhi Watanzania

Habari mbalimbali  

Dk Slaa amtaka Rais Kikwete awaombe radhi Watanzania
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk .Wilbroad Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk .Wilbroad Slaa, amesema kuna haja kwa Rais Jakaya Kikwete, kuwaomba radhi Watanzania, kufutia kitendo cha serikali yake, kushindwa kutimiza ahadi ya kuibua ajira 1,000,000, kama alivyokuwa ameahidi katika kampeni zake za mwaka 2005...
    (31 December 2009)
Views: 110 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Jeshi la Polisi, Tanesco waongoza kwa rushwa

Habari mbalimbali  

Jeshi la Polisi, Tanesco waongoza kwa rushwa
Mkurugenzi mkuu wa asasi inayojishughulisha na maendeleo katika nchi za Afrika( FORDIA) Bubelwa Kaiza akitoa maelezo kuhusu taarifa ya utafiti wa mtazamo wa rushwa jijini Dar es Salaaam jana.


WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), askari polisi na wafanyakazi wa Mahakama, ndio wanaoongoza kwa rushwa nchini, utafiti uliofanywa na Mtandao wa Concern for Development Initiative in Africa (Fordia) umeonyesha...
    (31 December 2009)
Views: 100 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

‘WAANDISHI’ MBARONI KWA RUSHWA MIL. 40

Amani  
‘WAANDISHI’ MBARONI KWA RUSHWA MIL. 40
Na Waandishi wetu
Njemba mbili zilizojifanya Waandishi wa habari wa Kampuni ya Global Publishers zilizotajwa kwa majina ya Mick John Nyenza ‘Franco’ na Edward Mabula, Jumatatu wiki hii walitiwa mbaroni baada ya kunaswa wakiwa katika harakati za kutaka kulamba rushwa ya shilingi milioni 40 kutoka kwa kigogo mmoja wa kampuni ya simu za mkononi nchini (Jina tunaliminya)
‘WAANDISHI’ MBARONI KWA RUSHWA MIL. 40
..waandishi feki (mwenye shati la njano na shati jeupe) wakiwa chini ya ulinzi mkali mara baada ya kunaswa
    (31 December 2009)
Views: 1124 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Mwisho wa Dunia

Amani  
Mwisho wa Dunia

Mwandishi Wetu na Mashirika ya Habari ya Kimataifa
Wakati wananchi wengi Bongo wakiwa wamezoea kuona vibaka wa kiume wanaoibia watu wakikumbana na raia wenye hasira na kuwahukumu kwa moto, hivi karibuni mwanamke mmoja alistaajabisha watu baada ya kudakwa kama kibaka, hali iliyoashiria kuwa mwisho wa dunia unakaribia, Amani limeinyaka...
    (31 December 2009)
Views: 2166 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Pata, potea

Amani  
Pata, potea

Na Mwandishi Wetu
Leo ndiyo kikomo cha siku 365 za mwaka 2009, wengi wakitumbulia macho kesho ambapo mwaka mpya, 2010 unaanza, wengine kwa matumaini, wengine kwa kukata tamaa, Amani linakujuza zaidi...
    (31 December 2009)
Views: 890 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Albamu ya Ushindi yawa tiba kwa watu wenye matatizo sugu

Amani  



Na George Kayala
Nivigumu kuamini lakini ni kweli juu ya mambo yanayojitokeza kwa watu wanaoisikiliza albamu ya Ushindi ya mpakwa mafuta wa Mungu Kabula J.George ambayo imegeuka kuwa tiba kwa watu wenye matatizo sugu ambayo yameshindikana kutibiwa kwa madaktari bingwa na waganga wa kienyeji...
    (31 December 2009)
Views: 179 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Nilikubali mkoba wa kichawi ili niwe tajiri-7

Mikasa ya kusisimua  
Mpenzi msomaji, kijana Kafumu aliyefundishwa uchawi na bibi yake, anaendelea kusimulia jinsi alivyosafiri na fisi akiwa na bibi yake hadi katika Bwawa la Kazima eneo ambalo wachawi wa Tabora hukutana na kufanya mambo yao lililopo karibu na kijiji cha Manoleo.

Anasema alipofika katika bwawa hilo alistaajabu kuwaona wachawi wa rika mbalimbali. Akiwa hapo bibi yake alimwambia ajichanganye kwenye kundi hilo la wachawi na kufuatilia kila kinachojiri. Akiwa amejichanganya babu mmoja alimfuata na kumbeba juu na kumwambia akiwa mkubwa atawasaidia watu wengi wenye matatizo kama alivyokuwa akifanya marehemu babu yake. Baadae babu huyo alimpeleka pembezoni mwa bwawa hilo alikowakuta akina bibi watatu, babu wawili,akina mama wawili na watoto wanne wa umri wake wakiwa wanachoma nyama na kula. Alipotakiwa kula nyama hiyo aligoma lakini baada ya kulazimishwa sana na kuambiwa kama angegoma kabisa angepoteza maisha alikubali. Nyama hiyo ni nyama gani na kwanini kama angekataa kula angekufa?
Ungana na KULWA MWAIBALE katika mkasa huu wa kweli…
    (31 December 2009)
Views: 314 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Aina za Saikolojia na faida zake! -2

Saikolojia na maisha  
Nawashukuru watu wote ambao wamekuwa wakifuatalia somo hili toka tulipoanza wiki mbili zilizopita, naomba tuendelee tena wiki hii kuangali mambo mengine muhimu kuhusiana na aina za saikolojia na faida zake katika maisha yetu ya kila siku...
    (31 December 2009)
Views: 108 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Asiyelithamini penzi lako la dhati, usimpe nafasi 2010!

Mikasa ya kusisimua  
Kwanza nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunijaalia kufikia siku ya leo nikiwa mzima bukheri wa afya. Nafanya hivyo nikiamini kwamba, wapo wengi waliotamani kuuona mwisho wa mwaka huu na mwanzo wa mwaka 2010 wakiwa wazima lakini kwa bahati mbaya leo hii wamelala kwenye nyumba za milele huku wengine wakiwa hoi mahospitalini wakisumbuliwa na maradhi mbalimbali...
    (31 December 2009)
Views: 216 | Maoni (0) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2 3 ... 39 40 41  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com