arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » ijumaa wikienda » Miss TZ ni gundu Miss World

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» Nilikubali mkoba wa kic ...
» MISS DAR CITY CENTER!
» FROM CHINA WITH TRUE LO ...
» HOMA YA CCJ YATINGA NDA ...
» The Sex Slave -44
» KUTAFUTA MAISHA KUMENIF ...
» Mateso kwenye uhusiano, ...

Miss TZ ni gundu Miss World

ijumaa wikienda

Ripoti zinaonesha kuwa katika mashindano yote ya awali, hakuna hata moja ambalo Miriam alijitahidi, achilia mbali kulinusa kwa ukaribu, hivyo kuendeleza gundu la Miss Tanzania kwenye mashindano hayo.

Kutokana na hali hiyo, dalili zilionesha kuwa mrembo huyo wa Tanzania, ni mkumbo wa Miss Tanzania 2006-07, Wema Sepetu, Richa Adhia (2007-08) na Nasreen Karim (2008 -09) ambao ushiriki wao haukuwa na faida yoyote katika fainali za dunia.

Siku mbaya kwa Watanzania, ilijionesha asubuhi kwamba Miriam asingeweza angalau kufikia nusu ya pale, alipoweza Miss Tanzania 2005-06, Nancy Sumari ambaye alifika fainali (Top 6) na kutwaa taji la Miss World Africa, baada ya kuboronga mfululizo.

Katika mchakato wa kumpata Miss World mwaka huu, Miriam hakuonesha kufurukuta angalau kufika nusu fainali kwenye taji lolote, na hivyo kutoa taswira kuwa Miss Tanzania ni wazuri kwa kupeleka warembo wasio na sifa kwenye mashindano ya dunia.
Taji la kwanza kushindaniwa, lilikuwa ni la Michezo (Miss World Sports), lililofanyika Novemba 18, 2009 kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Bay, mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini ambapo mrembo wa Japan, Eruza Sasaki alishinda, wakati Mjamaika, Kerrie Baylis alishika nafasi ya pili.

Mrembo wa Hungary, Orsolya Serdiilt alikuwa wa tatu, wakati waliofika fainali Pooja Chopra wa India, Leva Lase (Lativia) na Maria Milagros Veliz wa Venezuela.

Nchi ambazo zilifika nusu fainali (Top 12) na warembo wao ni Sophia Lavers (Australia), Kaiane Aldorino (Gilbratar), Jennifer Colon (Puerto Rico), Mariatu Kargbo (Sierra Leone), Ashanna Arthur (Trinidad & Tobago) na Claudia Vanrell wa Uruguay.

Taji la mrembo mwenye kipaji (Miss World Talent), lililofanyika Novemba 22, 2009 kwenye Ukumbi wa Maonesho, Victoria Theatre, Johannesburg, Afrika Kusini ambapo mrembo wa Canada, Lena Ma na Mariatu Kargbo wa Sierra Leone walifungana nafasi ya kwanza.

Mtoto wa Korea, Kim Joo-ri alikamata nafasi ya pili, mrembo kutoka Norway, Sara Skjoldness alikamata namba tatu, huku namba nne ikienda kwa Sophia Lavers wa Australia.

Warembo 22 waliongia fainali na nchi zao ni Armina Mevlani ( Albania), Joanna Brown (Bahamas), Leah Marville (Barbados), Flavia Foianini (Bolivia), Andrea Sarac (Bosnia & Herzegovina), Antonia Petrova (Bulgaria), Tsira Suknidze (Georgia) na Kaiane Aldorino wa Gibraltar.

Wengine ni Imarah Radix (Guyana), Karenina Sunny Halim (Indonesia) Martine Andraos (Lebanon), Anais Veerapatren (Mauritius), Jelena Markov (Serbia), Carmen Laura Garcia (Hispania), Zoureena Rijger (Suriname), Pongchanok Kanklab (Thailand) na Vanessa Sibanda wa Zimbabwe.

Vazi la Ufukweni (Miss World Beach Beauty) ambalo lilichukua nafasi Novemba 25, 2009 kwenye Ukumbi wa Zimbali Resort, Kwazulu-Natal, Durban, Afrika Kusini, mrembo wa Gibraltar, Kaiane Aldorino alishinda huku Nadege Herrera wa Panama akishika nafasi ya pili.

Mshindi wa tatu alikuwa ni Katherine Brown wa Scotland, wakati namba nne ilikwenda kwa Chloe Mortand wa Ufaransa, huku namba tano ikienda Bolivia kwa mrembo, Flavia Foianini.

Warembo na nchi zao waliofanikiwa kuingia Fainali (Top 12) ni Leah Marville (Barbados), Karenina Sunny Halim (Indonesia), Perla Beltran (Mexico), Jennifer Colon (Puerto Rico), Tatum Keshwar (Afrika Kusini), Tran Thi Huong Giang (Vietnam) na Vanessa Sibanda (Zimbabwe).

Warembo walioingia nusu fainali (Top 20) ni Ivana Vasili (Croatia), Ana Contreras (Jamhuri ya Dominician), Lula Weldegebriel (Ethiopia), Kerrie Baylis (Jamaika), Kim Joo-ri (Korea), Happie Ntelamo (Namibia), Lisa-Marie Kohrs (Marekani) na Claudia Vanrell (Uruguay)

Miss Mwanamitindo (Miss World Top Model) ambalo lilifanyika Novemba 28, 2009, Turbine Hall, Johannesburg, Afrika Kusini, mrembo wa Mexico, Perla Beltran alibeba taji, wakati Tran Thi Huong Giang wa Vietnam alishika nafasi ya pili.

Mrembo kutoka Martinique, Ingrid Littre alikamata namba tatu, wakati warembo walioingia fainali (Top 12) ni Leah Marville (Barbados), Chloe Mortand (Ufaransa), Alice Taticchi (Italia), Kerrie Baylis (Jamaika), Thanuja Ananthan (Malaysia), Nadege Herrera (Panama), Katherine Brown (Scotland), Tatum Keshwar (Afrika Kusini) na Ebru Sam wa Uturuki.

Urembo na Nia (Beauty with a Purpose), walioingia fainali ni Leah Marville (Barbados), Alida Boer (Guantemala) na Pooja Chopra wa India.

Vazi la Ubunifu (Best World Dress Designer), ambalo lilifanyika Novemba 28, 2009 kwenye Ukumbi wa Turbine, Johannesburg, sambamba na lile la Top Model, mshindi ni Mariatu Kargbo wa Sierra Leone, wa pili ni Tatum Keshwar (Afrika Kusini) na aliyeshika namba tatu ni Kerrie Baylis wa Jamaika.

Walioingia fainali (Top 12) ni Leah Marville (Barbadov), Yun Sheng (China PR), Alice Taticchi (Italia), Kim Joo-ri (Korea), Maria Bragaru (Moldova), Nadege Herrera (Panama), Jennifer Colon (Puerto Rico) na Ebru Sam wa Uturuki.


 (Votes #: 3)
    (14 December 2009)
Soma Zaidi: 852 | Maoni Yako (4)

Udaku Mwingine

ijumaa wikienda
 
  • MISS WORLD 2009: TANZANIA KAMA KAWAIDA!
  • Mapenzi yamemponza Miriam Gerald
  • Kamati ya Lundenga lawamani
  • Miriam kuambulia chochote kesho?
  • Illuminata aangukia pua
  •    

    #1 Author: promise (14 December 2009 01:34)

    wapelekeni shule ma miss wenu, hawajiamini ndio kosa lao la kwanza.
     
    fast    

    #2 Author: Mkwaju (14 December 2009 03:18)

    Ilikuwa riski yake kupata hiyo Gari, hana Uzuri labda uzuri wa komo lake! then ukweli usio fichika Miss Tanzania lazima atowe rushwa ya ngono ndio apite......Ushahidi katika Film "MISS BONGO''
     
    fast    

    #3 Author: Rosemary (15 December 2009 01:53)

    halooooooooooooooooooooooooooooooo Tanzania kazi tunayo mh!
     
    fast    

    Add comments

    Name:
    E-mail:

    Code:
    Include security image CAPCHA.
    to renew the code
    Enter Code:

     

    Kura Yako / Poll

    Habari Katika Picha


    Gazeti la Uwazi


    Nani Yupo / Alikuwepo


    Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

     hit counter

    counters

    2008 © globalpublisherstz.com