Test Your Eyez ya wiki iliyopita leo imefikia ukingoni. Wengi umejitahidi sana, lakini aliyejibu vizuri tena 'in short n clear', si mwingine bali ni MKWARE ambaye alijibu hivi: 1.Nywele kisogoni. 2.Kamba inayoning'inia shingoni-moja fupi moja ndefu. 3.Mistari myeupe ya kwenye soli za raba-minigine imekunja kwa chini mingine imenyooka. HONGERA SANA - JARIBU NA KWENYE BAHATI NASIBU YA VITZ..UNAWEZA SHINDA ..TEH TEH!!!
LEO NI LEO NDANI YA EMIRATES, AMBAPO WATANI WA JADI MANCHESTER UNITED (MASHETANI WEKUNDU) NA ARSENAL (WASHIKA BUNDUKI) WATAMENYANA KATIKA DIMBA LA EMIRATES HAPO BAADAE MIDA YA SAA 1 JIONI!
KITENDAWILI NI KWAMBA NANI ATAIBUKA KIDEDEA? TUPE UTABIRI WAKO!!!
Wakati wa kukaribishwa kuzungumzia tatizo la chakula duniani, Rais JK, ambaye anahudhuria mkutano wa Kimataifa (WORLD ECONOMIC FORUM) alikaribishwa kama waziri Mkuu wa Tanzania! Baadae Rais alimrekebisha mkaribishaji, ambaye anatokea India ambako wana Waziri Mkuu tu kama kiongozi wa juu wa nchi, na hivyo kuzua kicheko!
Habari zilizotua hivi punde zinasema kuwa mpiganaji na mpambanaji nambari one wa vita dhidi ya rushwa, Jerry Muro, ameingia matatani na vyombo vya dola baaada ya kunasa kwenye mtego wa kupokea rushwa ya shilingi za kitanzania milioni 10! Newz hizo zinasema kuwa, Jerry alinasa leo asubuhi katika mtego uliotegwa na PCCB katika Hoteli ya Sea Clif iliyoko Masaki jijini Dar es salaam. Aidha imeelezwa kuwa mlungula huo ulitolewa na Kampuni moja inayomiliki vituo kadhaa vya mfuta nchini. Baada ya kunaswa, Jerry aliripotiwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay na kisha kuhamishiwa Central ambako anashiliwa hadi sasa. Katika siku za hivi karibuni, Jerry Muro, amejipatia umaarufu akiwa Mtangazaji wa Televisheni ya Taifa (TBC1) akitokea ITV ambako ndiko alikofanyakazi kwa muda mrefu na kujulikana na watazamaji wake.
Tukio la hivi karibuni liliompandisha chati na kumuongezea umaarufu mtangazaji huyo ni la kufichua kashfa ya rushwa ya askari wa usalama barabarani wa Mkoani Iringa kwa kuwaonesha kwenye Camera ya TBC1 jinsi walivyokuwa wakipokea rushwa kutoka kwa madereva wa malori. Tukio hilo lilioneshwa kwa kina katika kipindi chao cha Usiku wa Habari. Taarifa zaidi zinasema kuwa, Kesho Kamanda Mkuu wa Kanda Maalum ya Dar, Alhaji Suleiman Kova, ataongea na media kuhusu sakata hili - STAY TUNED!
The 12 M-Net Face of Africa semi-finalists impressed the judges and designers at Swahili Fashion Week during castings and early shows - but in this week’s tension-filled episode (Saturday January 30 at 19:00 CAT on M-Net), they take to the catwalk for the Fashion Week Finale knowing they’re just one step away from the Face of Africa Finale in Lagos on February 6. They all know that two of them will be leaving soon – but who will it be?
Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika amekuwa mkuu wa Umoja wa Afrika, akimrithi kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi katika mkutano unaofanyika mjini Addis Ababa.
Malawi ilikuwa chaguo la nchi zilizo kusini mwa Afrika, japokuwa Libya ilitaka kuongeza muda wa uenyekiti unaodumu kwa mwaka mmoja.
Bw Gaddafi alikabidhi madaraka hayo akitoa wito wa kuwepo umoja wa kisiasa barani Afrika.
Awali katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliwasihi viongozi wa Afrika kushirikiana pamoja ili kuzuia upande wa kusini wa Sudan kujitenga na kaskazini.
Kunatarajiwa kufanyika kura ya maoni nchini Sudan mwakani kuainisha iwapo upande wa kusini wenye utajiri wa mafuta ujitawale.
Bondia Mada Maugo aliyekuwa akijitapa kwa muda mrefu kuwa atamchakaza mpinzani wake, Maneno Oswald, jana aligeuziwa kibao na kujikuta akichezea kichapo ‘hevi’ toka kwa mpinzani wake huyo. Mchezo huo wa kuvutia, ulichezwa katika ukumbi wa DDC Kariakoo, maarufu kama Old Trafford, uliopo jijini Dar es Salaam, ambapo mpaka mwisho wa mchezo huo, Maugo alizidiwa kwa pointi.
Mtambo wa Gongo (mwenye njano) akimpiga konde la kidevuni Maugo.
Muda f’lani ilikuwa ni kama miereka.
Maneno Oswald, akichekelea wakati akitangazwa kuwa mshindi kwa pointi, aliye kifua wazi kushoto ni mpinzani wake, Maugo.
Timu ya Yanga, jana iliendeleza ubabe iliyouanza katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa kuichapa Majimaji ya Songea jumla ya mabao 3-0, yote yakipachikwa wavuni na mshambuliaji Boniface Ambani.
Golikipa wa Majimaji, Said Mohamed akiwa amedaka shuti la mshambuliaji wa Yanga, Boniface Ambani.
Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete akimenyana na mshambuliaji wa Majimaji, Kulwa Mobby, katika moja ya sekeseke zilizotokea kwenye goli la majimaji.
Beki wa Yanga Amir Maftah akimenyana na mmoja wa washambuliaji wa majimaji.
KATIKA safu hii ya “Nani Zaidi” leo tunakuletea walinda milango wawili mahiri katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ambao ni Juma Kaseja wa Simba na Obren Curkovic wa Yanga.
Kwa taarifa fupi tu ni kwamba Juma Kaseja anachezea klabu ya Simba ambapo msimu uliopita alikuwa Yanga pamoja na Obren ambaye wakati huo alikuwa amewasili kutoka kwao katika nchi ya Serbia alikokuwa anacheza soka. Obren Curkovic, ameitumikia Yanga kwa msimu wa pili sasa. Wakati anatua kwa mara ya kwanza msimu wa mwaka jana walikuwa pamoja na Juma Kaseja katika timu hiyo ya Wanajangwani. Tunataka kujua maoni yenu kuwa kati ya nguli hawa wawili ambao timu zao zipo juu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara hivi sasa ni “Nani Zaidi”? Tafadhali dondosha kura yako hapo sehemu ya kupigia kura au toa comment zako hapa. KUMBUKA, LEO KURA ZINAFUNGWA, MSHINDI KUTANGAZWA KESHO JUMATATU, PIGA KURA YAKO YA MWISHO SASA
Mwanamuziki mashuhuri wa reggae nchini Uganda, Bebe Cool a.k.a Moses Sali, akiingizwa katika hospitali ya Nsambya jijini Kampala baada ya kupigwa risasi katika klabu moja jijini humo.
Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la The Monitor toleo la mchana huu, risasi hizo zimevunja miguu yote miwili, amesema Daktari Mratibu wa hospitali hiyo, Dk. Martin Nsubuga.
Habari zinasema risasi zilirindima katika klabu ya Effendys katika maeneo ya Centenary Park, na kwamba kuna utata wa sababu zilizopelekea purukushani hilo. Inasemekana watu wengine watatu ikiwa ni pamoja na mabaunsa wa Bebe Cool na askari wa kikosi maalum pia walijeruhiwa. Chanzo cha habari SATURDAY MONITOR - UGANDA JAN 30, 2010
Sherly Cwele, mke wa waziri wa masuala ya kijasusi wa Afrika Kusini.
Mke wa waziri wa masuala ya kijasusi wa Afrika Kusini, Sherly Cwele (50), amekamatwa na kupandishwa kizimbani, akikabiliwa na tuhuma za kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya....
Esther Fulano ndilo jina lake. Binti huyu mrembo anatoka katika kampuni ya mitindo (Model) ijulikanayo kama Dollywood ya jijini Dar es Salaam. Ana ndoto za kujiingiza kwenye masuala ya urembo na mitindo na ndiyo maana amekuja kwetu ili tumlete kwenu wadau na kumnadi kiaina, je analipa?
Bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Music Band, usiku wa kuamkia leo iliipaisha kwa mashabiki wake ile bahati nasibu ya Shinda Gari inayoendeshwa na kampuni ya Global Publishers Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda, Uwazi, Amani na Championi. Msondo waliipaisha bahati nasibu hiyo wakati wa uzinduzi wa ukumbi wa Bull Dance uliopo eneo la Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo mashabiki walichizika vilivyo.
Wanenguaji wa Msondo wakilishambulia jukwaa.
Mwanamuziki mkongwe wa Msondo, Said Mabela akitekenya nyuzi za gitaa la solo wakati wa onesho hilo.
Ni kijana mdogo na ni miongoni mwa wasanii chipukizi wa Bongo Flava walioibuka kwa kasi ya kipekee mwaka jana baada ya kutoa nyimbo zilizokubalika katika medani ya muziki wa kizazi kipya. Anajulikana kwa jina la Diamond na kwa sasa anatamba katika vituo vya televisheni na redio station za Afrika Mashariki na kibao chake murua cha KAMWAMBIE! Angalia video yake ujiliwaze....