arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 03.02.2010

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Ni mwaka wa Simba
» JAMANI TUKAE MKAO WA KU ...
» Maximo amkimbia Boban T ...
» HIVYO NDIVYO NAVYOISHI
» INATISHA
» SIRI WIZI NMB
» Akudo waimega FM Academ ...

 

TEST YOUR EYEZ III

photos  
TEST YOUR EYEZ III
Tumerudi tena, picha hii ya leo ina tofauti tatu tu ambazo unahitaji kuwa na macho makali kuzigundua. Hivyo changamsha macho yako na ututajie tofauti hizo tatu. Look simple, eh?
    (3 February 2010)
Views: 477 | Maoni (11) |

 

BOMU LAZUA KIZAAZAA DAR!

Videos  

Wakazi wa Msasani Bonde la Mpunga eneo la Maandazi Road jijini Dar es Salaam, leo walikumbwa na hofu baada ya mtu asiyejulikana kutelekeza bomu kwenye kichochoro kimoja mtaani hapo. Afisa Mtendaji wa Mtaa huo Bi. Rose Temu, alisema kijana mmoja alionekana mtaani hapo akitafuta mtu wa kumuuzia bomu hilo kama chuma chakavu lakini wanunuzi walionesha wasiwasi kuwa huenda ni bomu ndipo kijana huyo aliamua kulitelekeza mtaani hapo. Kufuatia tukio hilo kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kikosi maalum cha kutegua mabomu, kilifika eneo la tukio na kuthibitisha kuwa ni bomu hatari na kulichukua na kuondoka nalo.

BOMU LAZUA KIZAAZAA DAR! VIDEO



BOMU LAZUA KIZAAZAA DAR!
>>> Bumu likiwa kichochoroni lilipoterekezwa

BOMU LAZUA KIZAAZAA DAR!
>>> Wananchi wakishuhudia

BOMU LAZUA KIZAAZAA DAR!
>>> Gari la Kijeshi linatinga mtaani

BOMU LAZUA KIZAAZAA DAR!
>>> Dah! Imekuwa bahati, lingewalipukia wanachi wa Msasani kama ilivyokuwa Mbagala!

BOMU LAZUA KIZAAZAA DAR!
>>> Wanajeshi haoo wanaondoka na bomu lao


Still Picture: Issa Mnally, Video:Richard Bukos /GPL
    (3 February 2010)
Views: 98 | Maoni (3) |

 

AJALI MBAYA YAUA TENA WATU 24 TANGA, MABASI YAGONGANA USO KWA USO

Habari mbalimbali  
AJALI MBAYA YAUA TENA WATU 24 TANGA, MABASI YAGONGANA USO KWA USO

Video pekee inayoonesha ajali hiyo ilivyokuwa muda mfupi baada ya kutokea


AJALI MBAYA YAUA TENA WATU 24 TANGA, MABASI YAGONGANA USO KWA USO

AJALI MBAYA YAUA TENA WATU 24 TANGA, MABASI YAGONGANA USO KWA USO

AJALI MBAYA YAUA TENA WATU 24 TANGA, MABASI YAGONGANA USO KWA USO

MIKOA ya Kanda ya Kaskazini bado inaandamwa na ajali mbaya za barabarani baada ya watu 24, akiwamo dereva wa basi, kufariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso katika barabara ya Segera - Chalinze....
    (3 February 2010)
Views: 606 | Maoni (5) | Soma Zaidi

 

THE COMMEDY ENTERTEINMENT

Videos  

Sit bak, rilakx! Ze Komedi in akshen laaiv!, injoi ze shoo
    (3 February 2010)
Views: 61 | Maoni (1) |

 

PROMOSHENI YA ‘SHINDA GARI’ YAPAMBA MOTO!

photos  

BAHATI nasibu kubwa ya ‘Shinda Gari’ aina ya Toyota Vitz inayoendeshwa na kampuni ya Global Publishers Ltd, wachapishaji wa magazeti pendwa ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani,Uwazi, Championi na Risasi,imeendelea kuwa na msisimko wa kipekee baada ya kulitikisa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake. Wananchi wamekuwa wakiwania kununua kuponi za kushiriki bahati nasibu hiyo kila wakati gari la promosheni hiyo linapokatiza mitaani. Zawadi zingine zinazotarajiwa kutolewa na Global Publishers katika promosheni hiyo ni Pikipiki, Dinner Set, Jezi na Mipira.

MAMBO YALIVYOKUWA MITAANI

PROMOSHENI  YA ‘SHINDA GARI’  YAPAMBA MOTO!
Wananchi wakiwania kununua magazeti ya Global Publishers yenye kuponi zinazowawezesha kushiriki katika bahati nasibu hiyo.

PROMOSHENI  YA ‘SHINDA GARI’  YAPAMBA MOTO!
Mmoja wa wanenguaji wa promosheni hiyo akifanya maajabu yake jana jioni mitaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

PROMOSHENI  YA ‘SHINDA GARI’  YAPAMBA MOTO!
Msanii huyo aliendelea kufanya kufuru kwa staili zake za ‘kufa mtu’ kiasi cha kuwafanya watu kupandisha mzuka.

PROMOSHENI  YA ‘SHINDA GARI’  YAPAMBA MOTO!
Jamaa aliyejikuta akipandwa na midadi na kuamua kuanza ‘kusebeneka’ wakati wa promosheni hiyo.

PICHA: MUSA MATEJA /GPL
    (3 February 2010)
Views: 37 | Maoni (0) |

 

BOMU LAZUA KIZAAZAA MTAANI!

photos  
BOMU LAZUA KIZAAZAA MTAANI!

BOMU LAZUA KIZAAZAA MTAANI!
Habari zilizotufikia sasa hivi, zinasema kuwa wakazi wa Mandazi Road, Msasani, Jijini Dar es salaam, wameona kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu lenye ukubwa sawa na chupa ya chai na hivyo kuzua kizaa miongoni mwao. kwa mujibu wa Mapaparazi wetu, Issa Mnali na Richard Bukos, waliyeko eneo la tukio hivi sasa, mara baada ya kuona kitu hicho, wakazi hao walitoa taarifa Polisi ambao walifika mara moja na wao kutoa taarifa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao wanasubiriwa kuja kukagua na kuchukua hatua stahiki iwapo litakuwa kweli ni bomu. Imeelezwa kuwa kitu hicho kilitelekezwa na mtu mmoja aliyekuwa amebeba vyuma chakavu baada ya kutilia mashaka. Picha na habari kamili zitawajia punde..STAY TUNED!
    (3 February 2010)
Views: 37 | Maoni (0) |

 

Jerry Muro Na Falsafa Ya Ukuta

photos  
Jerry Muro Na Falsafa Ya Ukuta
Maggid Mjengwa


Jerry Muro Na Falsafa Ya Ukuta

Jerry Muro

Ndio kwanza nimemaliza kusoma kitabu cha mwandishi Sandelin Wundrak; The History Of Economic Thinking. Kisha nimepitia mtandaoni taarifa mbali mbali. Ndio, kwa hapa nyumbani, Jerry Muro ni habari kubwa, ni mshtuko. Jerry Muro. Sijapata kukutana naye. Nimefuatilia kazi zake tu, kwa kazi zake anaonekana kuwa ni kijana mahiri. Katika lililomfika, nina-sympathy nae. Yuko katika kipindi kigumu sana. Kwa mwanadamu mwenzako, ni kumpa pole tu, hayo mengine ni ya baadae. Juu hapo mnaona picha ya ukuta. Ndio, bado natafakari ziara yangu ya siku moja pale kijijini Kalenga, ni kwenye ngome ya Chifu Mkwawa wa Wahehe. Nilikwenda huko Jumamosi ya juzi hapa. Mkwawa ni yule shujaa aliyewatoa jasho Wajerumani. Katika kupitapita kwangu mitaa ya kijiji hicho nilikutana na.....
    (3 February 2010)
Views: 620 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

SHINDA GARI MWAKA 2010!

Videos  

TANGAZO
    (3 February 2010)
Views: 27 | Maoni (0) |

 

UBOVU WA FERI WAZUA HOFU KIVUKO CHA LIKONI MOMBASA

Habari mbalimbali  
UBOVU WA FERI WAZUA HOFU KIVUKO CHA LIKONI MOMBASA
Abiria wakishuka kutoka kwa mojawapo ya feri zilizozeeka katika kivuko cha Likoni jijini Mombasa. Hali ya wasiwasi imekuwa ikiwakumba wakaazi kutokana na kukwama kwa feri hizi zilizochoka kabisa.Juzi mlango wa mbele wa feri moja ulikatika katikatia ya maji na iliwalazimu maafisa wa shirika hilo kuharakisha kabla ya maji kuanza kujaa mbele ya feri hiyo.

Na KAZUNGU SAMUEL, MOMBASA
Huku wakazi wanaotumia kivuko cha Likoni wakiendelea kutaabika na kukodolea kifo macho kutokana na kukwamba mara kwa mara kwa feri zinazowavukisha hapa,mwenyekiti wa shirika la huduma za feri(Kenya Ferry Services) Bw Joseph Kingi amedai feri hizo zilifanya kazi kubwa msimu wa krismas na zinahitaji kupumzika kwani zilichoka. Akihutubia waandishi wa habari,
    (3 February 2010)
Views: 49 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

SAKATA LA ‘ALWAYS’ FEKI LAANIKWA

risasi mchanganyiko  
SAKATA la pedi za kike hususan zile za aina ya ‘Always’ ambazo ni feki, linaitikisa Tanzania kwa sasa na tayari serikali, kwa kutumia wataalamu wake, imetangaza athari kubwa ambazo wanawake wanaweza kuzipata kutokana na matumizi ya bidhaa hiyo feki.

Miongoni mwa madhara makubwa yanayoweza kusababishwa na pedi hizo feki ni pamoja na ugumba kwa wanawake, fangasi sehemu za siri pamoja na kansa. Hata hivyo serikali na wadau wake bado wanaendelea na msako mkali ambao unaonekana kuwa na mafanikio baada ya kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha pedi hizo hatari.

Mtandao huu makini uliweza kuzama kiundani katika sakata hilo kwa kuwasaka wahusika wa masuala ya pedi za ‘Always’, ambao ni kampuni ya Mek One General Traders Ltd iliyopo mtaa wa Bandari, Kurasini , Temeke, Jijini Dar es Salaam ambao ni wakala wa usambazaji wa ‘Always’ halisi nchini ambapo Mkurugenzi wake, Mohamed Eidha Awadhi, alielezea kusikitishwa na kuzagaa kwa bidhaa hiyo feki sokoni. Kikubwa zaidi ambacho Mkurugenzi huyo alipenda wadau wajue ni juu ya kuzibaini ‘Always’ feki na halisi.

“Kama ilivyobainishwa hapo awali na wataalamu wa afya, hizi pedi feki ni hatari mno kwa wanawake. Napenda kutoa tahadhari kwamba, wanaponunua pedi, cha kwanza ni lazima waangalie haya yafuatayo ili kujua hiyo ni feki.

“Kwanza waichunguze kama pedi hiyo imetengezwa China. Iwapo imeandikwa ‘Always Impact’ na pakiti yake ni kubwa. Wanapofungua ndani wakakuta haiko ndani ya kibahasha kipana na pamba yake unapoishika inapukutika kama unga, wajue hiyo ni feki na wasithubutu kuitumia,” alieleza Awadhi.

Aliongeza kwamba ‘Always’ feki pia kitambaa chake kinaweza kupitisha uchafu kirahisi na ina uwezo mkubwa wa kuingiza magonjwa kwani msichana anapoivaa inapwaya na uchafu unaweza kumchuruzika, na kwamba pedi halisi imeandikwa ‘Always Maxi’ na inatengezwa nchini Misri kwa pamba halisi inayovutika ambayo ni ndogo, ina pafyumu halisi, ina muundo wa kupitisha hewa ili kuhifadhi ubaridi na ina kibahasha kinachofunika pedi yote ikiwa na gundi ya kutosha.

Mtandao huu pia uliliweza kuwasiliana moja kwa moja na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya kusambaza pedi za ‘Always’ katika nchi za Afrika Mashariki aliyejitambulisaha kwa jina moja la Andrew anayeishi jijini Nairobi nchini Kenya ambaye alikiri kuwa hivi sasa pedi hizo feki ni tishio kubwa kwa warembo.

“Jamaa wanajaribu kuiga kila kitu. Ni vigumu sana kueleza tofauti ya pedi halisi na feki kwa sasa na ukaeleweka. Hii ni hatari lakini tunajitahidi kudhibiti hili kwa kushirikiana na wakala wetu wa Dar es Salam, kampuni ya Mek One General Traders Ltd, Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) kuhakikisha kuwa tunapambana na balaa hili la pedi hizi feki,” alieleza Andrew.
[b]

TOFAUTI YA ‘ALWAYS’ FEKI NA HALISI

SAKATA LA ‘ALWAYS’ FEKI LAANIKWA
Ni vigumu kutambua ‘Always’ feki na halisi kama picha inavyoonyesha.

SAKATA LA ‘ALWAYS’ FEKI LAANIKWA
Awali ‘Always’ ilikuwa ikitengenezwa katika umbo kubwa ikiitwa ‘Impact’ lakini baadaye ikabadilishwa ikapunguzwa ukubwa na kupewa jina la ‘Always Maxi’.

SAKATA LA ‘ALWAYS’ FEKI LAANIKWA
Pakiti ya ‘Always’ feki, inatengenezwa nchini China, na haina bahasha pana, haina harufu ya manukato, haina gundi ya kutosha na imetengenezwa kwa pamba bandia zinazopukutika, ni hatari kwa afya.

SAKATA LA ‘ALWAYS’ FEKI LAANIKWA
Pakiti ya ‘Always’ halisi, inaitwa Maxi, inatengenezwa nchini Misri, ni ndogo, ina harufu nzuri, iko kwenye bahasha pana, ina gundi ya kutosha, ina sehemu ya kupitisha hewa ili kuhifadhi ubaridi na inatengezwa kwa kutumia pamba halisi inayovutika ni salama na mtumiaji huweza kukaa nayo kwa masaa 8, bila kubadilisha au kukagua.
SAKATA LA ‘ALWAYS’ FEKI LAANIKWA
Hii ni Pakiti nyingine feki ya Always.

PICHA:CHRISTOPHER LISSA/ GLP
    (3 February 2010)
Views: 116 | Maoni (4) |

 

Fataki orijino atikisa jiji

risasi mchanganyiko  
Fataki orijino atikisa jiji
Na Mwandishi Wetu
Sakata la yule Fataki Orijino, Goodluck Kimaro kuwatenda ufurauni mabinti wadogo, limezua jambo na kwamba Jiji lote la Dar es Salaam limetikisika kwa habari zake...
    (3 February 2010)
Views: 1865 | Maoni (11) | Soma Zaidi

 

Gonjwa hatari

risasi mchanganyiko  
Na Mwandishi Wetu
Nyuma ya pazia la maisha ya wanandoa wengi Bongo, kuna gonjwa hatari linalochangia kupunguza nguvu za kiume, Risasi Mchanganyiko limebaini...
    (3 February 2010)
Views: 317 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

BAKWATA kutembeza bakora kwa mastaa

risasi mchanganyiko  
BAKWATA kutembeza  bakora kwa mastaa

Na Musa Mateja
Tabia ya kutembea matiti nje inayozidi kushika kasi kama moto wa kifuu miongoni mwa mastaa ‘the big name’ Bongo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni ‘fasheni’, sasa kuwatokea puani, Risasi Mchanganyiko limeinyaka...
    (3 February 2010)
Views: 806 | Maoni (16) | Soma Zaidi

 

Askari wa doria wamtia pingu Lord Eyez

risasi mchanganyiko  
Askari wa doria wamtia pingu Lord Eyez

Na Kyalaa Seheye
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ anayepiga mzigo kwenye Kundi la Nako2nako, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akitiwa pingu na askari wa doria baada ya kumshuku kuwa ana bangi ndani ya gari lake...
    (3 February 2010)
Views: 422 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Just hang me -28

hadithi za Shigongo  
Austine na Justine ni watoto mapacha waliozaliwa porini sehemu mbili tofauti na mama yao kufa mbele ya safari bila watu kujua alizaa watoto porini. Wakaokotwa na familia mbili tofauti, Justine akaokotwa na wakulima wa Kimarekani ambao baadae waliondoka Tanzania kurejea nyumbani kwao North Carolina ambako walimlea mtoto huyo kama wa kwao na kumfanya awe nyota wa mpira wa kikapu aliyeheshimika sana nchini Marekani.

Austine aliokotwa na mama wa Kimasai ambaye baadaye alifariki na kumuacha mikononi mwa Padri aliyepewa jina lake, mtoto huyu naye akaishia kuwa Padri mwenye ndoto ya kuwa Papa wa kwanza mweusi! Akahamia Vatcan kwa ajili ya masomo lakini akiwa huko, Padri Austine mkubwa akafariki dunia jambo lililomuumiza sana na kumfanya apoteze ndoto yake ya kuwa Papa mweusi wa kwanza na kutoroka Vatcan kurejea Tanzania lakini akiwa kwenye Uwanja wa ndege wa Schphol, Amsterdam Uholanzi anakamatwa kwa mauaji ya watu watatu ambayo anadai hakuyafanya na anasafirishwa kurejeshwa Tanzania kujibu mashtaka ya mauaji.

Hayo yakitokea Justine anaonekana kuwa katika mapokezi mazito ya msichana Nancy, kutoka Tanzania anayesoma kwenye Chuo kikuu cha North Carolina ambacho pia Justine alisomea. Amemkaribisha msichana huyo Los Angeles kwenda kushuhudia mechi yake ya kwanza akichezea timu ya LA Lakers! Amechukuliwa kwa ndege ya Justine hadi nyumbani kwake ambako anashangaa kila kitu anachokiona. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (3 February 2010)
Views: 610 | Maoni (2) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com