Na Phillip Nkini, Bukoba BAADA ya kuwa timu ya kwanza ‘kuifungisha breki ya pointi tatu’, Simba Sports Club, Kagera Sugar imejigamba kuwa timu zinazokutana nayo wakiwamo mabingwa watetezi Dar Young African wakae chonjo...
Na Phillip Nkini, Bukoba KOCHA Mkuu wa Simba Patrick Phiri amesema, ingawa wachezaji wake walilewa sifa alijua kuwa siku moja rekodi lazima itavunjwa, lakini amesisitiza nafasi waliyonayo, lazima watwae mabingwa wa Tanzania Bara msimu huu...
Na Jozaka Bukuku MSHAMBULIAJI wa Prisons ya Mbeya, Gaudence Mwaikimba amesema atarejea tena Vietnam kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa licha ya kuishia Uwanja wa Ndege nchini humo hivi karibuni baada ya kuisha kwa muda wake wa kufanya hivyo...
Na John Joseph KOCHA Mkuu wa JKT Ruvu inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa, Charles Kilinda amesema licha ya kuwa bado Tanzania inahitaji changamoto ya kocha wa kigeni, anasubiri kutajwa kwa vigezo vya atakayeajiriwa kukikoa kikosi cha Taifa Stars ili aweze kujitosa katika nafasi hiyo ikiwa atakidhi vigezo...
Mtoto anazaliwa na jinsia mbili, anakua na kuwa msichana mrembo kupita kiasi lakini ana siri kubwa moyoni mwake. Huyu ni Maryjose ambaye baadaye anakuwa mpenzi wa David, mwanafunzi mwenzake. Hakukuwa na tendo la ndoa kati yao ingawa David alitaka litokee, hali hii ilimfanya awe na uhusiano wa siri na rafiki yake Maryjose aitwaye Alice.
Baadaye wazazi wa Maryjose wanapata ajali mbaya ya gari na kufariki, anaachiwa urithi wote ambao kwa mapenzi aliyonayo kwa David anautumia kumtibisha ugonjwa wa Saratani ya uboho wa mfupa aliotakiwa kutibiwa nchini Uingereza kwa kubadilisha Uboho na kuwekewa mwingine.
Waliporejea nchini kutoka Uingereza, Maryjose alikuwa ameishiwa kabisa, hivyo kujikuta akiishi nyumbani kwao na David maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam, haukupita muda mrefu sana akaugundua usaliti ambao David alikuwa anafanya na kukiri mwenyewe kuwa asingeweza kumuoa Maryjose sababu hakuwa msomi.
Kauli hii inamuumiza sana Maryjose, hasa alipofikiria ujinga alioufanya kwa sababu ya David! Anafikia uamuzi wa kumuua lakini akashindwa kutekeleza kitendo hicho na kutoroka nyumbani kwao, kwa muda mrefu akajificha katika Utawa na David na Alice wakaendeleza uhusiano wao wakiamini alishakufa!
Siku ya ndoa yao wanapanda ndani ya gari la bwana na bibi harusi na linalipuliwa kwa petroli, upelelezi ulipofanyika ulionyesha aliyelipua ni Maryjose na msako ukaanza kumtafuta bila mafanikio. Alice akafariki na David kupatwa na upofu, hata hivyo akaendelea na kazi za baba yake Alice kwenye kampuni yake ya Uwakili.
Maryjose anarejea nchini kutoka India akiitwa Sista Theresa na kukabidhiwa kituo cha watawa wa shirika la Mt. Francisca, watawa wasiotoka nje, kazi yao ikiwa ni kusali tu! Anajishughulisha sana na kazi ya kutoa misaada kwa jamii, hakuna anayemkumbuka lakini siku moja David na wafanyakazi wake walipokwenda kwenye ofisi yake kutoa msaada wa shilingi bilioni mbili zimsaidie, David aligundua kuwa sauti ya Sista Theresa ni ya Maryjose lakini sista alikana.
David bado anaendelea kufuatilia ukweli wa jambo hilo, tayari amekwishachukua mwandiko wa sista Theresa na kwenda kuulinganisha na barua za mtu aliyekuwa akimtumia kumwomba msamaha. Watu walioutazama mwandiko walimhakikishia kwamba ni wa mtu mmoja, akawa na uhakika kabisa sista Theresa ni Maryjose, neno pekee alilosema ni; NITAMPATA TU. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Mmoja wa mbwa waliomshambulia “bwana” wao wakati akiwa katika bustani yake.
DAKTARI mmoja ambaye alishinda mapambano ya kisheria ya miaka minne ya kuwaokoa mbwa wake watatu wasikamatwe na kwenda kufungiwa mahali ambapo wasingeweza kutembea ovyo na kuwadhuru watu, ameuawa na mbwa haohao...
• Awasilisha risiti za pingu alizokamatwa nazo SAKATA la mwandishi wa habari za uchunguzi, Jerry Muro, limeingia katika hatua mpya baada ya kubainika kuwa ana risiti za pingu ambazo polisi walimkamata nazo...
Nashukuru kwa michango ya wote kuhusu sakata la mwanahabari Jerry Muro na CCJ. Lakini kama sisi kama sehemu ya umma na kama sehemu ya wachangiaji wa masuala yanayohusu hatma ya nchi yetu na raia wake tunahitaji kwenda mbele zaidi na kufanya uchambuzi (kihabari tunaita News Analysis) ili kupata picha pana zaidi itakayotusaidia sisi na jamii nzima.
Katika uchambuzi kunaweza kuwepo maswali mengi. Mfuatiliaji wa masuala ya kitaifa
Mtoto wa miaka miwili aliyenusurika katika ajali iliyotokea juzi na kuuwa watu 24 papohapo huku wengine 35 wakijeruhiwa
KATIKA kile kinachothibitisha maajabu ya Mungu, mtoto wa miaka miwili ametoka salama katika ajali iliyotokea juzi mkoani Tanga wakati mama yake mzazi anadaiwa kufariki dunia katika ajali hiyo....
Marehemu Imran Mtui, mtanzania aliyeuawa nchini India mapema wiki hii, anatarjiwa kurejeshwa nyumbani leo mida ya alasiri kwa ndege ya Shirika la Emirates. Marehemu, ambaye alikuwa masomoni nchini humo, mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege, anatarajiwa kusafirishwa kwenda Marangu, Moshi kwa ajili ya maziko. Uchunguzi wa kifo chake bado unaendelea.
Marehemu Imran Mtui
Watanzania mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za india walifunga safari na kujumuika na watanzania wenzao katika kuomboleza msiba wa mtanzania mwenzao. PICHA KWA HISANI YA HAKI NGOWI
Kundi la wakuu wa vyombo vya habari limeonya kuwa Rais wa Nigeria anayeugua, Umaru Yar'Adua lazima akabidhi madaraka kwa makamu wake katika kipindi cha siku saba au ajiuzulu.
Wamiliki wa magazeti 17 na mashirika ya vyombo vya habari wamesema katika ujumbe wa pamoja kuwa Bw Yar'Adua lazima ashitakiwe kwa kutumia madaraka vibaya kama atashindwa kutekeleza matakwa yao.
Rais huyo anayeugua amekuwa katika hospitali moja ya Saudi Arabia tangu mwezi Novemba mwaka jana. Kumekuwa na kesi kadhaa za kisheria zikihoji uwezo wa Rais kuongoza nchi akiwa amelazwa.
Katika kesi ya mwisho, mahakama kuu ilisema hakukuwa na kipengele chochote cha kikatiba kwa kiongozi yeyote wa mpito kuteuliwa.