Mtaalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa kuhusu madeni ya nje na haki za binadamu , Cephas Lumina ametoa wito wa kufutwa mara moja madeni ya Haiti inayodaiwa na wadeni mbalimbali na kuipa nchi hiyo fedha za msaada zisizo na masharti yoyote, na sio mkopo mpya...
Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Ivory Coast umeshuhudia ghasia hivi karibuni kwenye miji ya Katiola na Divo, na umetoa wito wa kuwepo na hali ya utulivu wakati shughuli ya uandikishaji wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu ujao ikifanyika...
Mkereketwa wa kiswahili nchini Kenya, Bw.Ludovick Mbogholi, alipokuwa akiongea na mwandishi wa Global nyumbani kwake jijini Mombasa . Mwana Kiswahili huyu alizua sokomoko nchini Tanzania mwaka 1995 wakati alipochukuliwa na CCM kumfanyia kampeini Ben Mkapa kupitia tungo na mikutano ya hadhara mkoani Kilimanjaro. Kampeni zake zilisaidia CCM kuibuka na ushindi licha ya malalamiko ya upinzani. Hivi sasa amezua gumzo tena baada ya kuwakashifu viongozi wa Kenya kuwa wanabeza kiswahili.
Na KAZUNGU SAMUEL, MOMBASA Mkereketwa wa lugha ya Kiswahili mwenye uasili wa taifa la Tanzania amewakosoa vikali viongozi na washika dau nchini Kenya kwa kuwa kikwazo katika juhudi za taifa hili kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya taifa. Kwenye kikao na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake mtaani Bamburi kwenye viunga vya jiji la Mombasa , Bw Ludovick Mbogholi alisema kuwa viongozi wa Kenya ikiwemo wajumbe wameingiwa na kasumba ya kutukuza lugha ya kiingereza hivi kwamba wanapuuza kabisa Kiswahili. “Ikiwa hata viongozi wetu wanasimama mbele ya
Serikali ya Finland na shirika la chakula duniani FAO wamekubaliana kuzisaidia nchi mbalimbali kuanzisha mfumo endelevu na ulio rahisi wa umilikaji ardhi , ili kuimarisha udhibiti wa ardhi katika maeneo ya vijijini na mijini...
Shirika la kimataifa linalohusika na masuala ya uhamiaji IOM limezindua kampeni ya utoaji taarifa nchini Sudan kuhusu athari zitokanazo na uhamiaji holela, kama sehemu ya juhudi za kupambana na matatizo ya uhamiaji Afrika ya Mashariki na pembe ya Afrika...
UNICEF na Shirika la Afya Duniani WHO wameelezea wasiwasi juu ya kuongezeka kwa wahudumu wa afya wanaoendesha vitendo vya ukeketaji. Inakadiriwa kuwa wanawake milioni 120 hadi 140 wamekeketwa na wasichana milioni 3 bado wako kwenye hatari ya kukeketwa kila mwaka...
Usiku wa kuamkia leo, bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini, The African Stars ‘Twanga Pepeta’ pamoja na mwanamuziki wa kibongo anayeishi nchini Japan, Fresh Jumbe walizikonga vilivyo nyoyo za wanazi wa burudani nchini, katika onesho lao ‘babkubwa’ lililofanyika ndani ya ukumbi wa Hoteli ya Landmark, Ubungo , jijini Dar es Salaam. Onesho hilo lilienda sambamba na Promosheni ya Bahati nasibu ya Shinda Gari aina ya Toyota Vitz na zawadi nyingine kibao kutoka kampuni ya Global Publishers Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Risasi, Amani, Championi, Ijumaa Wikienda na mtandao huu. Ilibamba si kitoto mtu wangu, hebu cheki mapicha haya...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Dk. Jakaya Kikwete, leo aliwahutubia wananchi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 33 ya chama hicho tangu kuzaliwa kwake zilizofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa mambo aliyosistiza kwa viongozi wa chama hicho ni utendaji bora, hasa wabunge na madiwani, kwani yeyote atakayeonesha udhaifu na kukataliwa na wananchi wake katika kampeni, chama chake hakitatumia mbinu yeyote kubadili fikra za wananchi hao.
Kabla ya kuanza kuhutubia, Rais JK aliwaomba wananchi wasimame kwa sekunde kadhaa kumkumbuka Hayati Rashid Mfaume Kawawa, aliyeaga dunia hivi karibuni.
Baadaye JK alianza kuhutubia
Sehemu ya wananchi waliohudhuria sherehe hizo
Kampteni John Komba (katikati) akitoa burudani kwa nyimbo za kwaya viwanjani hapo
Gazeti la Championi, linaloandika habari za michezo nchini, limepongezwa kwa kuwa miongoni mwa magazeti makini yanayoandika habari za uhakika na ambazo zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo nchini.
Pongezi hizo zilitolewa jana usiku na Kampuni ya bia ya Serengeti Lager katika hafla fupi ya kuukaribisha mwaka 2010 na kuwapongeza waandishi mbalimbali wa habari hapa nchini kwa kazi nzuri wanazozifanya.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo fupi alikuwa Mhe. Muhammed Seif Khatib, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano). Katika sherehe hiyo iliyofanyika katika ndani ya ukumbi wa Msasani Beach Club, uliopo Mikocheni jinjini Dar es Salaam, kampuni hiyo ilitoa zawadi ya cheti kwa gazeti la Championi linalomilikiwa na Global Publishers Ltd kwa mchango wake mkubwa wa kuandika habari zilizomakini kwenye medani ya michezo.
Mhariri wa gazeti la Championi Jumatano, Denis Fusi (anaye anekana mgongo) akipeana mkono na Jaji Mstaafu Mark Bomani ambaye kwa sasa ni Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Serengeti mara baada ya kukabidhiwa cheti na Waziri Khatib.
Msanii wa kundi la Wanne Star akionesha ufundi wake wa kucheza na moto.
Waziri Khatib akisakata muzik na Afisa Uhusiano wa kampuni ya Serengeti Lager, Teddy Mapunda.
Upepo mkali, uliosindikiza mvua kubwa iliyonyesha jana kuanzia mida ya saa nane na nusu mchana na kukadiriwa kudumu kwa muda wa saa moja, umesababisha hasara kubwa kwa baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro pamoja na Shirika la kuangaza maisha yetu, (Tanesco). Mvua, hiyo ambayo iliannza kama mvua nyingine, ilibadilika ghafla na kutishia baadhi ya wakazi wa Morogoro Mjini kwa kuonesha dalili kama za Kilosa (Mafuriko) ambayo baadae iliisha kabisa na jua kuchomoza utafikiri kulikuwa hakuna mvua. Lakini mara baada ya kukatika kwa mvua hiyo, kilichoshuhudiwa na mwandishi wetu ni uharibifu mkubwa wa magari, nyumba na nyaya za simu na umeme ambazo zilikatika baada ya kuangukiwa na miti mikubwa iliyongo'lewa kwa upepo. Athari nyingine iliyoonekana ni kuharibika kwa magari ambayo yaliangukiwa na kupondeka kabisa na barabara nyingi kuwa hazipitiki baada kuangukiwa na miti....ilikuwa ni kizaazaa cha aina yake...
..watu wakishangaa uharibifu uliosababishwa na mvua hiyo ya upepo.
....mitaa mingi iliathirika kwa kuangukiwa na miti
...iling'olewa hadi miti mikubwa kama unavyoonekana huu
...miti mingi iling'olewa na kuangukia barabarani
..gari haitamaniki baada ya kuangukiwa na mti
..askari wa usalama barabarani wakiangalia uharibifu huo
Mh. Rais JK kishaagiza viongozi wa Manispaa za Dar kuangalia uwezekano wa kujenga barabara za juu kwa juu (Fly Overs) ili kupunguza msongamano wa magari. Siku moja jiji la Dar linaweza kuwa na sura kama hii?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jana aliendelea na ziara yake ya kutembelea Mkoa wa Dar es Salaam. Katika ziara hiyo, akiwa kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Viwanja vya Sabasaba Temeke, aliongea na watendaji mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya hiyo ambapo aliwasisitiza juu ya kujiletea maendeleo.
Rais Kikwete akisalimiana na wenyeji wake mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
Rais akiongea na watendaji mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) waliofurika katika ukumbi huo.
Baadhi ya watendaji wa CCM Wilaya ya Temeke, wakimpungia mikono Rais Kikwete mara baada ya kuingia ukumbini.
Watendaji wa Wilaya ya Temeke, wakimsikiliza kwa makini Rais Kikwete alipokuwa akiwahutubia.
Kundi la ngoma za asili la Chama Cha Mapinduzi wilayani Temeke, likitumbuiza baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwasili katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere ambapo aliongea na watendaji wa wilaya hiyo.
Na Mwandishi Wetu Goodluck Kimaro, yule kigogo mwenye skandali la ufataki, anasakwa na hivi sasa dawa yake ipo inachemka ndani ya Jeshi la Polisi, Risasi Jumamosi lina kitu kamili...