Maryjose anarejea nchini kutoka India akiitwa Sista Theresa na kukabidhiwa kituo cha watawa wa shirika la Mt. Francisca, watawa wasiotoka nje, kazi yao ikiwa ni kusali tu! Anajishughulisha sana na kazi ya kutoa misaada kwa jamii, hakuna anayemkumbuka lakini siku moja David na wafanyakazi wake walipokwenda kwenye ofisi yake kutoa msaada wa shilingi bilioni mbili zimsaidie, David aligundua kuwa sauti ya Sista Theresa ni ya Maryjose lakini sista alikana.
Baada ya kugundua kwamba alikuwa mbioni kugundulika kwa David, Sista Maryjose anaamua kujitokeza mwenyewe na kujisalimisha lakini kabla hajafanya hivyo anakwenda Ukumbi wa Mkutano Maelezo huko anaomba mkutano na waandishi wa habari ambao wanafika kumsubiri ili aje aseme wapate habari za kuandika kwenye magazeti yao.
Sista Maryjose anafika lakini cha kushangaza anaonekana kuwa chini ya ulinzi wa polisi anaketi kwenye kiti na kukohoa kidogo kisha kuanza kutoa historia ya maisha yake na kuwaomba watu wote msahama akiwemo David kwamba alijulikana kwa jina la Sista Theresa lakini ukweli yeye alikuwa sista Maryjose na ndiye aliyehusika na kuchomwa kwa gari ambako kulisababisha kifo cha Alice na David kuwa mpofu.
Akaendelea mbele huku akisoma karatasi iliyokuwepo mbele ya meza yake, huku baadhi ya watu wakibubujikwa na machozi. Jovina alishindwa kabisa kujizuia, macho yake yakaanza kulengwalengwa. Historia ya Sista Theresa ambaye sasa alikuwa Maryjose tena ilikuwa ya kusikitisha mno na iliwafanya watu wote kwenye ukumbi wa Mkutano Maelezo waingiwe na huruma, baadhi wakahisi alistahili kufanya alichokifanya.
Alipofika hapo akanyanyuka na kutamka maneno kwamba tayari alikuwa kuhukumiwa kwa makosa aliyoyatenda, polisi mmoja akazunguka kwa mbele kuchomoa pingu kiunoni mwake na kumfunga Maryjose na kumtembeza kwenda naye nje, ambako waandishi waliendelea kupiga picha za matukio akapandishwa kwenye gari kisha kuondoka kwa kasi ya ajabu.
Je, nini kitaendelea huko anakopelekwa? Sista Maryjose atanyongwa? Je, taarifa hizi zimemfikia David? SONGA NAYO…
Bonyeza PLAY uwashuhudie walevi hawa wawili waliokwenda 'Supermarket' kufanya manunuzi lakini kilevi kikawazidia na kuamua kuuchapa usingizi ndani ya 'Supermarket' hiyo!
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Alan Johnson.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Alan Johnson, amesema kuwa serikali itapunguza idadi ya hati za kuingilia nchini humo au visa kwa wanafunzi wa kigeni ikiwa ni hatua inayolenga kukomesha utumiaji vibaya wa mfumo huo...
BAADA ya kuona matokeo ya juma lililopita kati ya makipa, Juma Kaseja wa Simba na Obren Curkovic wa Yanga, leo katika safu hii ya nani zaidi, tunakuletea washambuliaji wawili wa klabu hizo. Washambuliaji hao ni Mussa Hassan Mgosi wa Simba na Mrisho Ngassa wa Yanga, kwa ufupi ni kwamba wachezaji hawa wote wanacheza katika timu ya taifa ya Tanzania, (Taifa Stars), inayonolewa na Kocha Marcio Maximo raia wa Brazil. Katika msimamo wa wafungaji wa Ligi Kuu ya Vodacom, wanapishana kwa mabao mawili, ambapo Mgosi anaongoza akiwa na mabao 11 huku Ngassa naye akiwa amezifumania nyavu mara mara 9. Anza kupiga kura yako sasa kwenye sehemu ya kura kulia mwa page hii au toa coments zako hapa
KATIKA kuwafahamisha wateja wetu shamra za wikiendi zilivyokuwa jijini Dar es Salaam, kamera yetu ilivinjari sehemu kadhaa ambako wakazi wake walikuwa wakimalizia wikiendi kwa burudani ya muziki. Ungana na kamera yetu:
Wanenguaji wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) wakiongozwa na mwimbaji Chalz Baba wakiserebuka katika onyesho la bendi hiyo lililofanyika jana usiku katika ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni.
Kijana anayedaiwa kujihusisha na ushoga ambaye anajulikana kama 'Shoga Mtoto' akiwa amelivamia jukwaa na kunengua katika onyesho la bendi ya African Stars (Twanga Pepeta).
Mtoto aliyejitambulisha kwa jina la Saidi Mhando akiwa anacheza nyimbo za Michael Jackson katika viwanja vya Leaders kuwaburudisha waliofika hapo.
Mwanamuziki wa bendi ya Diamond Musica, Allain Kashama Mulumba, akiimba wimbo wa ‘Alowela’ katika Viwanja vya Leaders ambako wasanii mbalimbali hukutana kila siku za Jumamosi.
Ndugu zangu Wahehe wana msemo; Isenga imbofu na isenga indenyoofu. Kwamba ng’ombe kipofu ni sawa tu na ng’ombe aliyevunjika mguu, wote watakufa njaa. Ng’ombe kipofu hawezi kuyaona majani, na yule aliyevunjika mguu hawezi kujikokota kwenda kutafuta nyasi za kula. Tafakuri yangu iliyopita nilimalizia kwa kuuliza swali: Je, unafikiaje uamuzi wa ama kuingia vitani, au la? Huu ni mwendelezo wa nilipoishia. Naam. Tunavyoendenda kama jamii wakati mwingine ni sawa na ng’ombe kipofu na yule aliyevunjika mguu. Unaweza kuliona hilo nyumbani kwako, katika ukoo wako na hata mahala pako pa kazi. Tumekuwa jamii ya ovyo ovyo. Tunafanya mambo ya ovyo ovyo. Ni kutoka ngazi ya familia na hata ngazi ya kitaifa.
Ona migongano ya wanasiasa wetu sasa. Ona wanavyogawanyika katika makundi yao. Hawatangulizi hata kidogo maslahi ya wengi. Wanajigawa kwenye