arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 08.02.2010

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» Aina 10 ya vyakula vinavyoo ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» Toto yaweka undugu pemb ...
» UJE KUTUTEMBELEA TENA!
» BLUE 3 KUMPA TAFU PROFE ...
» Kuacha, kuachwa na kuac ...
» Ushuhuda kabla ya kifo ...
» For my wife, i will di ...
» SHIBE KATIKA FARAGHA

 

BADO NINA MATUMAINI MAKUBWA NA NCHI YANGU TANZANIA

Pasua Jipu  
Miongoni mwa mambo ambayo namshukuru Mungu kwa kunipa ni nafasi ya kukutana na vijana wa nchi hii na kuongea nao bila kujali Itikadi zao za kisiasa, rangi za ngozi zao, dini nk.
Mambo haya kwangu mimi huwa hayana maana kubwa sana, cha muhimu kwangu ni Utanzania na Uzalendo wa kweli wa mtu aliyesimama mbele yangu hata kama tunatofautiana kwa vipengele nilivyovitaja hapo juu...
BADO NINA MATUMAINI MAKUBWA NA NCHI YANGU TANZANIA
    (8 February 2010)
Views: 18 | Maoni (0) |

 

REVENGE OF THE DEAD - 32

hadithi za Shigongo  
Waliangalia ndani na kukuta kila kitu kikiwa sehemu yake, kuanzia viatu mpaka nguo za Albert! Isingewezekana awe ametoroka akiwa ameacha kila kitu mpaka fedha zilizokuwa juu ya meza chumbani kwake. Hata hivyo, hawakupuuza fikra za kutoroka, wakaamua kutoa taarifa kituo cha Polisi ambako waliahidiwa kwamba angeendelea kutafutwa popote ambako alikuwa amekwenda.

Walishauriana kwa muda na wote wakakubaliana juu ya kupiga simu shirika la ndege la Zimbabwe na mfanyakazi wa shirika hilo akapokea na kukanusha kuwemo kwa jina la Albert katika orodha ya abiria waliosafiri, wazazi, ndugu na marafiki wakazidi kuchanganyikiwa kwa sababu waliamini akili za Albert hazikuwa sawa tangu arejee kutoka Kongo, mara kwa mara aliongea juu ya kukatisha uhai wake.

Wakapiga simu kujaribu kwenye kampuni zote za mabasi yasafiriyo kutoka nchini Zimbabwe kuelekea Tanzania, kote hawakukuta jina lake, mwisho wakaamini huenda Albert alipanda mabasi ya kutoka Afrika Kusini. Wakakubaliana wasubiri siku tatu baadaye ndipo wapige simu Tanzania kuona kama alikuwa amekwishawasili huko. Juhudi zao zilikuwa zimegonga mwamba wakaiacha kazi hiyo mikononi mwa Jeshi la Polisi.

Siku moja usiku wakiwa wameketi sebuleni wakitafakari juu ya nini cha kufanya simu inaita na Balozi Katunzi ananyanyuka na kuipokea, ilikuwa ni simu kutoka Polisi wakitoa taarifra kwamba Albert alikuwa amepatikana nchini Msumbiji eneo la Beira akiwa hajitambui na walitaka wafike huko haraka baada ya taarifa hizo hakuna aliyepata usingizi, muda wote ulitumika kwa maombi kumwombea Albert na kulipokucha asubuhi wote walitoka nje na kuingia ndani ya gari na kuondoka kwa kasi, dereva wa Balozi Katunzi akiwa kwenye usukani, hawakumruhusu mzee aendeshe kwa hofu kwamba angesababisha ajali maana alikuwa amechanganyikiwa mno.

Hapakuwa na magari mengi sana barabarani siku hiyo, hivyo ndani ya muda wa nusu saa walishaegesha mbele ya Uwanja wa Ndege wa Harare, wakakata tiketi na kuingia ndani wakiwaacha ndugu na marafiki wakiwa na huzuni kubwa.
Ndege waliyopanda iliruka dakika thelathini baadaye na kubaki angani kwa muda wa saa moja na nusu ndipo ikaanza kushuka taratibu mpaka kutua kwenye uwanja wa ndege wa Maputo, wakatoka nje ya uwanja na kuchukua teksi iliyowapeleka moja kwa moja hadi hospitali. Wamefika hospitali aliyolazwa Albert na kumkuta akiwa hajitambui. Kwa muda wanaongea na daktari ambaye anawapa matumaini kwamba yuko kwenye mikono salama na alikuwa akishughulikiwa ipasavyo. Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO...
    (8 February 2010)
Views: 1096 | Maoni (17) | Soma Zaidi

 

MADHARA YA WAPENZI KUACHANA KWA PUPA!

Mahaba  
Katika safari ya maisha ya mapenzi kuna kuchoka ambako husababishwa na mambo mengi ukiwemo ugomvi. Siku hizi kumekuwa na wimbi kubwa sana la wapenzi wanaochoshwa na mapenzi yao kiasi cha kuamua kuachana. Ndoa na mapenzi ya leo si ya kudumu, wiki moja mwezi, mwaka au miaka miwili tayari utasikia walioona kwa mbwembwe wameachana...

    (8 February 2010)
Views: 152 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Habari mbalimbali  
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
ZAIN YAZINDUA BIASHARA COMMUNITY

Zain, kampuni ya simu za mkononi inayoheshimika zaidi nchini Tanzania imezindua Jumuiya ya wafanyabiashara ambayo inaitwa Zain Biashara Community. Jumuiya hii inalenga kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo na wakati nchini ili kuongeza mchango wao katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

Kuanzishwa kwa Biashara Community kutawasaidia wafanyabiashara wadogowadogo na wakati kupata faida kwa upana zaidi ili kutimiza malengo yao katika nyanja za kiuchumi .
    (8 February 2010)
Views: 101 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

MATOKEO KIDATO CHA NNE, KIWANGO CHA UFAULU CHASHUKA ASILIMIA 11

Habari mbalimbali  

MATOKEO KIDATO CHA NNE, KIWANGO CHA UFAULU CHASHUKA ASILIMIA 11
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako

*Watahiniwa 7,242 matokeo yasitishwa, kisa
*410 wafutiwa matokeo yote, wengine wakosa sifa
*Kupata matokeo hayo BONYEZA HAPA: MATOKE KIDATO CHA NNE 2009 au nenda hapa BARAZA LA MITIHANI TANZANIA

Kiwango cha ufaulu kwa watahiniwa wa kidato cha nne mwaka jana(2009), kimeshuka kwa asilimia 11.18 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu kutoka kwa watahiniwa...
    (8 February 2010)
Views: 267 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

AKINA MAMA WAMPONGEZA KINARA WA MASOMO TANZANIA

Habari mbalimbali  

AKINA MAMA WAMPONGEZA KINARA WA MASOMO TANZANIA
Mwanafunzi bora wa kidato cha nne kwa mwaka 2009, Imaculate Mosha kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Marian ya mjini Bagamoyo, akipongezwa na kaka yake Eng. Dominic Mosha baada ya kupokea taarifa za matokeo hayo jana akiwa mjini Bagamoyo alipokwenda kufanya usaili wa kidato cha tano katika shule ya Marian.

Na Hemed Kisanda
Wanawake jijini Dar es Salaam wamempongeza mwanafunzi Imaculate Mosha wa shule ya sekondari ya Marian Girls iliyoko wilayani Bagamoyo mkoni Pwani kwa matokeo mazuri aliyoyapata kwenye mtihani wa kidato cha nne yaliyotolewa wiki iliyopita...
    (8 February 2010)
Views: 651 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

305 WA KIDATO CHA SITA WAZUIWA KUFANYA MITIHANI

Habari mbalimbali  

305 WA KIDATO CHA SITA WAZUIWA KUFANYA MITIHANI
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako.

(ORODHA KAMILI YA WALIONDOLEWA KATIKA USAJILI NA MIKOA YAOBONYEZA HAPA)

Na Hemed Kisanda.
Wakati wanafunzi wa kidato cha sita nchini kote wanatarajiwa kuanza mtihani wao wa taifa leo, Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limewaengua watahiniwa 305 waliokuwa wamejisajili kufanya mtihani huo, hivyo hawataruhusiwa kuufanya...
    (8 February 2010)
Views: 175 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

UMEWAONA MBUZI WA KICHINA?

Habari mbalimbali  
Mbuzi unaowaona pichani hupatikana nchini MOROCCO, inasemekana ni kawaida kuwaona mbuzi wakiwa wamepanda juu ya vichaka na miti midogo ni kwa sababu wanafuata matunda yajulikanayo kama ARGO, kutokana na kuyapenda sana matunda hayo basi mbuzi hao hudandia juu ya matawi ya vichaka ili kupata matunda hayo.

UMEWAONA MBUZI WA KICHINA?

UMEWAONA MBUZI WA KICHINA?

    (8 February 2010)
Views: 46 | Maoni (1) |

 

WASHINGTON YAZIKWA NA BARAFU!

Habari mbalimbali  

WASHINGTON YAZIKWA NA BARAFU!

Kazi zote katika mji mkuu wa Marekani zimesitishwa kwa siku ya tatu mfululizo Jumatatu hii, kutokana na dhoruba kali ya theluji. Idara zote za serekali kuu hazitofunguliwa ikiwa ni pamoja na shule zote za majimbo ya Virginia, Maryland na DC...
    (8 February 2010)
Views: 89 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

POLISI DODOMA WACHARUKA WAWAFUNGIA MADEREVA 17, WASIENDESHE MAGARI KWA MUDA WA MIEZI SITA!

Habari mbalimbali  

POLISI DODOMA WACHARUKA WAWAFUNGIA MADEREVA 17, WASIENDESHE MAGARI KWA MUDA WA MIEZI SITA!

Na Hemed Kisanda
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limewafungia kwa miezi sita Madereva 17 wa Mabasi ya Makampuni kumi yanayofanya safari zake kati ya Dodoma na mikoa mbalimbali hapa nchini pamoja na nchi za jirani kutokana na kuvunja sheria na taratibu za usalama barabarani...
    (8 February 2010)
Views: 161 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

ZANZIBAR: KURA YA MAONI YA NINI SERIKALI YA MSETO?

Habari mbalimbali  

ZANZIBAR: KURA YA MAONI YA NINI SERIKALI YA MSETO?
Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume akipeana mkono na katibu mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad.

• Je, wengi wakiikataa, Wazanzibar warudie uhasama wao?
• Mangapi yamepitishwa nchi hii bila kura ya maoni?
• Kura hiyo ni chambo cha wasioitakia mema Z’bar

Na Walusanga Ndaki

JE, iwapo watu wengi katika kura ya maoni watakataa kuundwa kwa serikali ya mseto Zanzibar nini kitatokea baada ya hapo?
Jibu la swali hili ni kwamba uamuzi huo utazaa mambo mawili ya wazi.
Kwanza, kwa Wazanzibar na Watanzania kwa jumla, pamoja na walimwengu ambao siku zote wametaka wananchi wa sehemu hiyo ya dunia waishi kwa amani na uelewano, ni dhahiri watasikitika kiasi cha kutowaelewa tena wananchi wa Zanzibar, kwani watakuwa wamedhihirisha nia yao ya kuendelea na uhasama baina yao!...
    (8 February 2010)
Views: 66 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

BASI LAGONGA TRENI!

photos  
BASI LAGONGA TRENI!
BASI LAGONGA TRENI!

Na Mwandishi Wetu
Taarifa zilizotufikia sasa hivi zinaeleza kuwa, basi moja la abiria (daladala) ambalo namba zake hazikuweza kupatikana mara moja, limegonga treni na kwamba mtu mmoja (mwanaume) amefariki dunia.
Ajali hiyo imetokea eneo la Davis Corner, Tandika Yombo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kufafanua kuwa watu 26 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Temeke kwa matibabu!


Video inaonesha basi lililopata ajali eneo la tukio leo. Video kwa hisani ya Michuzi

    (8 February 2010)
Views: 57 | Maoni (1) |

 

VIBAKA WAUAWA!

photos  
VIBAKA WAUAWA!
Wimbi la mauaji dhidi ya vibaka limeendelea tena ambapo mapema leo, vijana wawili, ambao hawakufahamika mara moja, waliuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kutaka kuiba ndani ya nyumba moja ya mkazi wa Ilala Mchikichini, nyuma ya kiwanda cha bia cha Tanzania Breweries Ltd. Wakazi wa maeneo hayo wamedai kuwa, wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuchoshwa na vitendo vya wizi na imeelezwa kuwa vijana hao ni miongoni mwa vibaka sugu waliokuwa wakisumbua wakazi wa eneo hilo.

VIBAKA WAUAWA!
..maiti ya kijana kama ilivyokutwa eneo la tukio.

VIBAKA WAUAWA!
...ahadi ya kifo imetimia

VIBAKA WAUAWA!
..maiti za vijana hao zikiwa ndani ya gari la polisi wakipelekwa hospitali kuhifadhiwa.
    (8 February 2010)
Views: 117 | Maoni (6) |

 

TAMASHA LA WASANII WA FILAMU BONGO LAZIDI KUSHAINI

photos  
Lile tamasha la wasanii ambalo hufanyika kila siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, hatimaye sasa linazidi kupendeza kutokana na wingi wa watu wanaofurika pande hizo na wasanii wengi kuzidi kumwaga Burudani.

TAMASHA LA WASANII WA FILAMU BONGO LAZIDI KUSHAINI
Steven Jackob ‘JB’ akifuatilia kwa makini burudani zilizokuwa zikiendelea mahali hapo, kushoto kwake ni mrembo ambaye jina lake hatukufanikiwa kulinasa mara moja.

TAMASHA LA WASANII WA FILAMU BONGO LAZIDI KUSHAINI
Kikundi cha Kaole Sanaa Group kikitoa burudani kali ya muziki wa asili katika viwanja vya Leaders Club.

TAMASHA LA WASANII WA FILAMU BONGO LAZIDI KUSHAINI
Baadhi ya wanenguaji wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ wakiwa kwenye picha ya pamoja siku ya Jumamosi katika viwanja cha Leaders Club wakishuhudia bonanza hilo.

PICHA:MUSA MATEJA/GPL.
    (8 February 2010)
Views: 60 | Maoni (0) |

 

MTANZANIA NOVATUS RUGAMBWA ATEULIWA NA PAPA KUWA BALOZI SAO TOME

Habari mbalimbali  

MTANZANIA NOVATUS RUGAMBWA ATEULIWA NA PAPA KUWA BALOZI SAO TOME
Baba Mtakatifu Benedikto XVI.

Na Hemed Kisanda
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita amemteua Monsinyori Novatus Rugambwa, kuwa Balozi mpya wa Sao Tome na Prince na kumpandisha hadhi kuwa askofu mkuu. Kabla ya uteuzi wake, Monsinyori Rugambwa alikuwa ni katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la shughuli za kichungaji kwa wahamiaji na wakimbizi...
    (8 February 2010)
Views: 259 | Maoni (2) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2 3  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com