arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 09.02.2010

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» MSHANGAO!
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» VALENTINE YA UFUSKA!
» Aisha wa Mpakanjia aibu ...
» Its time for change!Its ...
» Friends of Simba waibua ...
» JAHAZI
» MBINU ZA KUMSHAWISHI MW ...
» Simba yaivuruga Yanga
» Mwambata JWTZ amganda m ...

 

My Black Chapter -31

hadithi za Shigongo  
Baada ya kuchoma gari la bwana na bibi harusi na kujificha kwenye Jumba la Watawa kwa muda mrefu, ikiaminika kuwa alishakufa, hatimaye Maryjose ambaye hivi sasa anaitwa Sista Theresa, amejitokeza na kueleza kila kitu alichokifanya mpaka kuchoma moto gari na Alice (bibi harusi) kufariki dunia huku mume wake (David) akipata upofu wa maisha. Ni habari ya kusikitisha sana.

Yote hayo ni sababu ya mapenzi, pale Maryjose alipowekeza utajiri wake wa urithi kwenye matibabu ya David aliyekuwa na Kansa ya Uboho wa Mifupa, lakini alipopata nafuu na kupona akamwacha Maryjose na kumchukua rafiki yake Alice. Jambo hili lilimuumiza sana Maryjose na kuamua kulipa kisasi kisha kujiunga na Utawa ili ajifiche na kweli akafanikiwa kulifanya jambo hilo.

Sasa amejitokeza na baada ya maelezo yake anakamatwa na kupelekwa mahabusu, siku iliyofuata vyombo vyote vya habari vilikuwa vimeandika habari yake na ilitangazwa kwenye televisheni na redio, ikamfikia David na kuthibitisha alichokuwa amekifikiria. Baadaye wazazi wa Alice, mama yake mzazi walikuja ofisini kwake kumfariji na kumtaka amsamehe Maryjose kwa sababu alishaomba msamaha.

Akawawekea sharti moja; kama wanataka amsamehe basi wampeleke mahabusu akaongee naye, baada ya hapo ndiyo angeweza kutoa msamaha! Wakakubali bila kuelewa kuwa, David ameficha bastola yake kiunoni, hukaa nayo ofisini kwake kwenye droo kwa ajili ya kujilinda. Je, nini kitatokea? SONGA NAYO...
    (9 February 2010)
Views: 417 | Maoni (14) | Soma Zaidi

 

KENYA NDANI YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Videos  

    (9 February 2010)
Views: 20 | Maoni (1) |

 

MATOKEO MABOVU KIDATO CHA NNE NANI WA KULAUMIWA?

Habari mbalimbali  
JE? KATI YA HAWA WAFUATAO NANI WA KULAUMIWA KUTOKANA NA MATOKEO MABAYA YA KIDATO CHA NNE:
WAZAZI, WANAFUNZI WENYEWE, WALIMU AU SERIKALI?

MATOKEO MABOVU KIDATO CHA NNE NANI WA KULAUMIWA?
    (9 February 2010)
Views: 139 | Maoni (10) |

 

BARAFU ILISABABISHA KUANGUKA KWA NDEGE UWANJANI HEATHROW

Habari mbalimbali  

BARAFU ILISABABISHA KUANGUKA KWA NDEGE UWANJANI HEATHROW
Ndege iliyopata ajali baada ya kuanza kushughulikiwa.

BARAFU ILISABABISHA KUANGUKA KWA NDEGE UWANJANI HEATHROW
Ndege ya BA ikiwa imeharibika baada ya kuanguka.

BARAFU iliyokuwa imeganda na kuziba njia za kupeleka mafuta kwenye injini ndiyo sababu ya kuanguka kwa ndege ya shirika la British Airways (BA) la Uingereza miaka miwili iliyopita, imesema Idara ya Upelelezi wa Ajali za Angani ya Uingereza (AAIB) katika ripoti yake ya mwisho kuhusiana na ajali hiyo iliyotokea tarehe 17 Januari, 2008...

    (9 February 2010)
Views: 198 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

KISURA WA AFRIKA!

photos  
KISURA WA AFRIKA!
Mambo ya M-NET FACE OF AFRICA - Enarnia
    (9 February 2010)
Views: 126 | Maoni (9) |

 

DUBAI: JENGO REFU ZAIDI DUNIANI LAFUNGWA

Habari mbalimbali  

DUBAI: JENGO REFU ZAIDI DUNIANI LAFUNGWA
Jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa.

JENGO refu zaidi duniani (ghorofa) ambalo lilifunguliwa kwa mbwembwe mwezi mmoja uliopita nchini Dubai, limefungwa ghafla, jambo ambalo limewafadhaisha watalii waliokuwa wanapenda kwenda kwenye sehemu yake ya juu zaidi na kuangalia mandhari iliyo chini. Vilevile kitendo hicho kimeleta mashaka iwapo wapangaji wa kudumu katika jengo hilo wanaweza kuwa wamehamia humo katika majuma kadhaa yajayo.

Matatizo ya umeme yanaweza kuwa baadhi ya sababu za kufungwa kwa sehemu hiyo ya juu ya jengo hilo linaloitwa Burj Khalifa ambalo urefu wake kwenda juu ni nusu maili, urefu ambao ni sawa na sehemu ya (0.8) ya kilomita. Kutokuweko kwa habari yoyote kutoka kwa mmiliki wa jengo hilo kumefanywa kufungwa kwake kuache mashaka mengi kuhusiana na jengo hilo ambalo sehemu kubwa haina wapangaji.
    (9 February 2010)
Views: 83 | Maoni (2) |

 

WABONGO WANATEGEMEA RADIO ZAIDI - UTAFITI

Habari mbalimbali  
WABONGO WANATEGEMEA RADIO ZAIDI - UTAFITI

Tanzania: Radio main source of news
A survey has revealed that 66 percent of Tanzanians rely on radio as their main source of news. The research which was in the form of SMS raffle was intended to establish the main source of news for members of the public and also popularize the Journalists of the Year Awards in Tanzania, which were held December 19, 2009. According to the government owned Daily News despite having over 650 registered publications, the survey showed that only 14 percent of respondents preferred newspapers as source of news. “The poll actually shocked us,
    (9 February 2010)
Views: 36 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

IMMACULATE MOSHA: THE GENIUS GIRL!

Videos  

Kutana na Immaculate Mosha, msichana mwenye kipaji aliyeoongoza nchi nzima katika matokea ya mitihani ya kidato cha Nne 2009. Video kwa hisani ya Varsity College Tanzania.
IMMACULATE MOSHA: THE GENIUS GIRL!
    (9 February 2010)
Views: 334 | Maoni (11) |

 

BIASHARA YA WATOTO YASHAMIRI HAITI!

Habari mbalimbali  

BIASHARA YA WATOTO YASHAMIRI HAITI!
Kichwa cha habari cha News Of The World, gazeti lillofichua kashfa hii

BIASHARA YA WATOTO YASHAMIRI HAITI!
Watoto watano wakiuzwa wote kwa dola 30,000.

BIASHARA YA WATOTO YASHAMIRI HAITI!

Guerson, mtumishi wa kituo cha kulelea watoto aliyefichuliwa na waandishi akiuza watoto.

YATIMA mdogo aitwaye, Roudy, aliyejikuta katika hali hiyo kutokana na kupoteza wazazi wake katika tetemeko la ardhi lililoikumba nchi ya Haiti, anaitazama kamera ya waandishi wa habari bila wasiwasi wakati akiuzwa kwa wageni kwa bei ya Paundi 65. Anauzwa na mtu mmoja mwenye tamaa ya fedha ambaye ni kiongozi wa chama kinachotakiwa kuwasaidia watoto wa Haiti waliokumbwa na tatizo hilo na kubakia yatima...
    (9 February 2010)
Views: 248 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

JIMMY CARTER AWASILI NCHINI SUDAN

Habari mbalimbali  

JIMMY CARTER AWASILI NCHINI SUDAN
Jimmy Carter.

Aliyekuwa rais wa Marekani Jimmy Carter amewasili nchini Sudan kwa mashauriano na rais wa nchi hiyo, Omar al-Bashir na maafisa wengine wakuu serikalini...

    (9 February 2010)
Views: 84 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

HUJUMA ZAIBUKA KIWANDA CHA PARETO MAFINGA

uwazi  
HUJUMA ZAIBUKA KIWANDA CHA PARETO MAFINGA
.chadaiwa kukwepa kodi mamilioni ya shilingi
.Vigogo wa serikali wahusishwa
(ONLINE VERSION)

HUJUMA ZAIBUKA KIWANDA CHA PARETO MAFINGA

HUJUMA ZAIBUKA KIWANDA CHA PARETO MAFINGA
Kiwanda cha Pareto Mafinga

Na Rashid Mkwinda, Mufindi
HUJUMA na ubadhirifu vimeibuka katika kiwanda cha kampuni ya Pareto (Pyrethrum Company of Tanzania (PCT) chenye makao yake makuu mjini Mafinga, Mufindi mkoani Iringa baada ya rasilimali za kiwanda hicho zenye thamani ya mamilioni ya fedha kuuzwa kiholela huku mwekezaji chini ya usimamizi wa Meneja Mkuu raia wa Uganda Bw. Martin Oweka, akidaiwa kuhusika. Taarifa zinaeleza kuwa, kiwanda hicho ambacho kiliwekwa jiwe la msingi na aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Sokoine Agosti 19, 1977, kilianza rasmi uzalishaji wake mwaka 1984 chini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano kikisimamiwa na Bodi ya Pareto Tanzania ambapo hatimaye kilibinafsishwa mwaka 1998 kwa mwekezaji wa kigeni kampuni ya International Chemical Producers (ICP) ya nchini Afrika Kusini.

Inazidi kuelezwa kuwa kampuni ya ICP nayo iliuza hisa zake kwa kampuni ya....


HUJUMA ZAIBUKA KIWANDA CHA PARETO MAFINGA
Fundi wa kiwanda cha Pareto kilichopo Mafinga wilayani Mufindi akifungua moja ya mashine ya kusindika sumu ya pareto kwa ajili ya kuuzwa kama vyuma chakavu.
    (9 February 2010)
Views: 273 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

DAWA ZA MALARIA AFRIKA NI DHAIFU

Habari mbalimbali  

DAWA ZA MALARIA AFRIKA NI DHAIFU

Utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka Marekani wamependekeza, Waafrika wanaougua malaria huenda wakawa wanapata matibabu ya kiwango cha chini.

Watafiti kutoka kundi la Pharmacopeia wamegundua kwamba baina ya asilimia 26 na 44 ya dawa za kupambana na malaria Uganda, Senegal na Madagasacr ni zenye uwezo mdogo.

Kundi hilo, ambalo linafanya utafiti kwa niaba ya shirika la afya duniani WHO, limesema dawa za viwango vya chini zinatumiwa na watabibu wa hospitali za umma pamoja na za binafsi.

WHO wameonyesha wasiwasi kwamba dawa hizo zenye udhaifu mkubwa zinaweza kusababisha mwili usiweze kupambana na vijidudu vya malaria.
    (9 February 2010)
Views: 33 | Maoni (0) |

 

RICHMOND YAPANGWA SIKU YA MWISHO BUNGENI

Habari mbalimbali  

RICHMOND YAPANGWA SIKU YA MWISHO BUNGENI
Spika wa Bunge la Tanzania, Samuel Sitta.

ULE mjadala moto wa sakata zito la utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development LLC, utakuwa wa siku moja tu; siku ya mwisho ya Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri....
    (9 February 2010)
Views: 79 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

JK AHOFIA ROBO TATU YA WANAFUNZI KUPATA MIMBA

Habari mbalimbali  

JK AHOFIA ROBO TATU YA WANAFUNZI KUPATA MIMBA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ameuagiza uongozi wa mkoa wa Morogoro na wa wilaya ya Kilosa kujenga makazi ya muda katika shule wanazosomea wanafunzi walioathirika na mafuriko yaliyoikumba wilaya hiyo ili waishi hapo na kuwaepusha wasichana kupata mimba...

    (9 February 2010)
Views: 43 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

UTAPELI MKUBWA WAZIMWA UWANJA WA NDEGE DAR

uwazi  
UTAPELI MKUBWA WAZIMWA  UWANJA WA NDEGE DAR
UTAPELI MKUBWA WAZIMWA UWANJA WA NDEGE DAR
Mtego wa Polisi wanasa mmoja

(ONLINE VERSION)

UTAPELI MKUBWA WAZIMWA  UWANJA WA NDEGE DAR
Mtuhumiwa wa utapeli, Ashrafu Kingu,(kati) akiwa amedhibitiwa na askari kanzu wa uwanja wa ndege. Kulia nyuma ni Bi. Hilda.

Christopher Lissa na Richard Bukos.
Walinzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, kwa kushirikiana na askari kanzu , Februari 3, mwaka huu walifanikiwa kuzima jaribio la utapeli mkubwa wa mamilioni ya fedha uliokuwa ufanyike uwanjani hapo. Katika sekeseke hilo, Polisi walifanikiwa kumnasa mtu mmoja aitwaye Ashrafu Kingu ambaye inadaiwa ni tapeli mzoefu kutoka katika genge moja lenye mtandao mkubwa wa shughuli hiyo uliosambaa nchini kote na hata nje ya nchi. Inadaiwa kuwa, matapeli hao walisuka .......
UTAPELI MKUBWA WAZIMWA  UWANJA WA NDEGE DAR
...imeshakuwa soo...nitaficha wapi uso wangu...Ashrafu Kingu.
UTAPELI MKUBWA WAZIMWA  UWANJA WA NDEGE DAR
...dili limebumburuka...Ashrafu Kingu
    (9 February 2010)
Views: 2000 | Maoni (10) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com