kiswatu: Neno hili lina maana ya mwanamke mzuri, au msichana mzuri ambaye anavutia…
Ankara /Mapene: Ni pesa zote zina maana sawa “Ee bwana nasikia harufu ya Ankara” fedha.
Kuua Bendi: Kufanya kitu ambacho sio kizuri, kusababisha maafa, hii mara nyingi hutumika kama kuharibu.
Kumchomolea: Ni hali ya kukataa kitu Fulani, inawezekana msemo huu ukatumika zaidi katika kuruka jambo Fulani hata kama limetendeka au lina ukweli ndani yake, kukataa.
Kupewa Manyoya: Kumpa mtu ahadi ya uongo isiyokuwa na muendelezo, Ahadi ya Uongo.
Kuchomeshwa Mahindi: kumsubiri mtu kisha asiweze kufika kwa muda muafaka au asifike kabisa katika miadi ambayo mnakuwa mmepeana. Zinazokaribiana.
Pesa Mnakwezi – ni pesa kama sarafu inategemea kama ni shilingi mia mbili, mia moja, shilingi ishirini, kumi almradi ni pesa ya sarafu. Paund – ni sarafu ya shilingi kumi, Fiu – shilingi hamsini Bati /jiti – shilingi mia moja, Karume – shilingi mia mbili, bati tatu – mia tatu Jerome/ jero- mia tano, Samba / wekundu – elfu kumi
Fundi Redio: Mtu apendaye kuongea maneno yasiyo na msingi au mtu mmbea aongeleaye mambo ya watu yasiyomhusu
(NAWE TUTUMIE MANENO YAKO YA MTAANI: info@globalpublisherstz.com, uwazi@hotmail.com)[/color]
Kwa wenzetu mlio mbali na misemo ya mtaani, hii ni fursa nyingine ya kuwa na kamusi yako ya maneno ya mtaani ambayo tutayakusanya hapa ili yakuwezeshe kuelewa kinachoendelea unapokutana na vijana wa kibongo wakiongea.
KUJIACHIA: kuwa mtulivu, furahia.
MZUKA/MZUKS: Ari ya kutaka kufanya kitu safi
JIWE: Askari wanaopanda daladala ambao kwa kawaida huwa hawalipi nauli
KUMPA SHAVU:Kumshirikisha mtui kwenye kitu cha mafanikio