Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (kulia), pamoja na Mama Salma Kikwete(katikati), wakijiandikisha kama wapiga kura katika kijiji cha Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Machi 3, 2010.
Na Walusanga Ndaki UBORESHAJI wa Daftari la Wapiga Kura nchini kwa jiji la Dar es Salaam unaanza tarehe 22 Machi, mwaka huu Jumatatu kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)...
• Ni matokeo ya 'mabao' ya sh 3000 wanayopiga daladala, teksi RUSHWA ndogondogo za barabarani zimewanufaisha baadhi ya askari wa Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam (trafiki) ambao wanakusanya zaidi ya sh 10,000,000 kila siku kila mmoja, kutokana na mchezo wa kupokezana fedha (upatu) waliouanzisha hivi karibuni...
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe.
*Waziri atangaza 32,765 kwenda shule za serikali
Wanafunzi 32,765 waliomaliza kidato cha nne mwaka jana, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule 164 za serikali nchini. Kati ya wanafunzi hao, 897 wakiwamo wasichana 16 na wavulana 881, wamepangwa kujiunga na vyuo vinne vya ufundi ambavyo ni Chuo cha Mbeya (MIST), Dar es Salaam (DIT), Arusha (ATC) na Chuo cha Maji Dar es Salaam...
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Jamii (CCJ), Richard Kyabo (kulia), akiangua kilio baada ya yeye na Katibu Mkuu wake, Renatus Muhabhi, kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, katika kijiji cha Butiama mkoani Mara jana.
*Wabubujikwa machozi kaburini kwake *Wahutubia hadhara, kadi kama njugu Viongozi wa Chama Cha Jamii (CCJ) jana walifanya ziara nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na kufanya mazungumzo na wanafamilia hiyo...
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, amesema Azimio la Arusha halikufutwa bali lilizimwa na baadhi ya viongozi wasio wacha Mungu, waliokuwa chanzo kikuu cha kuuzwa kwa mashirika ya umma...
Ni miaka 3 iliyopita ambapo vijana 5 wa kimarekani walianza kuwasiliana na mtu waliyekutana nae kwenye mtandao wa facebook.com kwa kuwa rafiki huyo mpya alikuwa na nia ya kupata vijana wengi zaidi kwa ajili ya shuguli zao basi akajificha chini ya profile inayowapendeza vijana wale . Aliweka picha nzuri ya ......
Wanasiasa wa jiji la Roma wakionyesha nguo zao za ndani walipokuwa wakipinga sera ya Gianni Alemanno aliyegoma kupitisha bajeti ya mji huo.
Katika kile kinachoonyesha sasa wanasiasa wa nchini Italia wamecharuka kwa kutaka maendeleo, hivi karibuni maofisa wa Manispaa wa jiji la Rome, walikusanyika na kufanya maandamano kwa kuvua suruali zao wakilazimisha kupita kwa bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka 2010.
Moja kati ya bango walilokuwa wamebeba lilisomeka "Maeneo ya kupaki na bustani zimevunjwa", "Watu hawana makazi” Meya Sandro Medici wa Cinecitta alimtaja mwanasiasa Alemanno aliyekataa kupitishwa kwa bajeti hiyo kutokana na kudai kuwa na kodi ambazo sio za msingi.
RAIS Jakaya Kikwete amesaini Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya Mwaka 2010 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, katika moja ya matukio ya nadra kwa mkuu wa nchi kusaini sheria kwa mbwembwe tofauti na mazoea ya kusainiwa kimyakimya na kisha kuwekwa katika Gazeti la Serikali...
...Samuel Etoo akitupia bao la pekee katika mechi hiyo.
...Didier Drogba akitoka nje ya uwanja baada ya kuzawadiwa kadi nyekundu.
...Jose Murinho (aliyenyoosha mkono) akimpanikisha kocha wa Chelsea Carlo Ancelotti.
Mbio za Chelsea za kuwania taji ya klabu bingwa barani Ulaya zimeishia ukingoni baada ya kutandikwa bao 1-0 na Inter Milan wakiwa nyumbani Stamford Bridge...
Mchungaji wa Kanisa la African Inland Church (AIC), Jonathan Sabuni (60), Mkazi wa kijiji cha Kasamwa wilayani Geita, Mkoa wa Mwanza, ameua mwanaye Amos Jonathan (16), kwa kipigo kwa tuhuma za kumwibia Sh. 50,000...
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuzuru Zimbabwe hii leo ili kujaribu kutatua tofauti zilizopo kwenye serikali ya muungano kati ya chama cha ZANU PF cha Rais Robert Mugabe na MDC cha Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai...
Wafanyakazi watatu wa kampuni ya Barrick Gold wanahofiwa kufa baada ya kuporomoka kwa mwamba katika mgodi wake wa Bulyanhulu ulioko wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga...
MWANASHERIA Mkuu mstaafu wa Serikali Jaji Mark Bomani.
*ASEMA MFUMO WA UCHAGUZI NCHINI UNACHOCHEA UFISADI Na Ramadhan Semtawa MWANASHERIA Mkuu mstaafu wa Serikali Jaji Mark Bomani, ameandika waraka mzito kwenda CCM na serikali yake, ambao pamoja na mengine unaelezea mfumo wa sasa wa uchaguzi kuwa ni kichochea cha ufisadi katika kupata viongozi wa dola...
UPANDE wa mashitaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, umefunga ushahidi wake na kuiachia Mahakama kuamua kama mshitakiwa ana kesi ya kujibu au la...