arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » hadithi za Shigongo

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» BILA UKIMWI INAWEZEKANA ...
» To teachers, Parents, R ...
» MVUA YAITESA DAR
» Maandamano
» Waislam wadai kulipua t ...
» CHANZO MUME WA MTU
» Maftah: Bao la Echesa n ...

 

Just hang me! -41

hadithi za Shigongo  
Majibu ya DNA yametoka na Justine kuthibitisha kabisa kuwa mwanamke aliyeokotwa barabarani na baadaye kuzikwa akiwa hana ndugu huko Bagamoyo ndiye mama yake mzazi, barua aliyoisoma ambayo mwanamke huyo aliandika akiwalalamikia ndugu zake kwa unyama waliomtendea wakati hakuwa na hatia, ndiyo imemfanya Justine afikirie kulipa kisasi kwa wazazi wa mchumba wake Nancy ambao ndiyo kaka za marehemu mama yake. Jambo hili Nancy halifahamu wala familia yake.
Je, nini kitatokea? Justine atalipa kisasi kweli? SONGA NAYO...
    (20 March 2010)
Views: 225 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

The Spring of Sadness! -29

hadithi za Shigongo  
Walipoingia tu katika jiji la Guanzhou, walisindikizwa na mfanyakazi ndani ya meli aitwaye Msafiri aliyemua kuwasaidia baada ya kuokolewa baharini. Wakiwa nje ya lango kuu la kuingia bandarini, kijana huyo aliagana nao na kurejea melini bila kuelewa Zabron na Rhobi walikuwa wakisuburiwa na vijana wauaji wa kundi la WBC (Wipe Black Chinese) ambao kazi yao ni kuwaua watoto waliozaliwa na wazazi wa Kiafrika na Kichina.

Bila kutarajia Rhobi na Zabron wakaingia mikononi mwa vijana hao na kutekwa hadi porini ambako walifungwa ndani ya magunia na kutupwa ili wafe kwa njaa, siku tatu baadaye mmoja wa wauaji hao (Xin) alirejea na kumchukua Rhobi mpaka kwenye jumba aliloishi na kumgeuza mtumwa wa ngono!

Alimwingilia mara moja tu akiwa amemfunga minyororo, mara ya pili Rhobi aligoma, ukatokea ugomvi uliomkera Xin na kumfungia Rhobi chumbani yeye akaondoka bila kujua mshumaa uliokuwa ukiwaka ulianguka na kuliunguza pazia lilikokuwa likining’inia dirishani ambalo baadaye liliteketea kabisa na moto kushika godoro, mashuka na hatimaye chumba kizima.

Jirani aliwapigia simu wazima moto ambao walifika baadaye na kukuta nyumba imeshateketea, wakaingia ndani kukagua na kukuta mwili wa mtu mmoja ukiwa umeteketea vibaya kiasi cha kutotambulika.
Upande wa pili Msafiri alisikia watu wakiongelea vijana wawili waliotekwa kwenda kuuawa, akatoa taarifa kituo cha polisi na baadaye wakafanikiwa kumkamata kijana mmoja mwanachama wa kundi la WBC ambaye baada ya kupelelezwa alikubali kuwapeleka askari mpaka walikowatupa Rhobi na Zabron. Wakamuokoa Zabron peke yake, Rhobi hakuwepo.

Uamuzi uliochukuliwa ni kumpeleka Zabron kituo kikuu cha polisi cha Guanzhou ambako kijana waliyemkamata alikubali kuwapeleka nyumani kwa Xin, wakafika na kukuta nyumba ikiteketea kwa moto na kuingia ndani ambako walimwokoa Rhobi kabla hayateketea, wakaondoka kuelekea kituoni, njiani walipishana na magari ya zimamoto! Hivyo ndivyo Rhobi alivyookolewa kutoka kwenye moto bila watu kugundua.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (19 March 2010)
Views: 281 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Our Doomsday -10

hadithi za Shigongo  
Ilikuwa ni siku ya Jumapili iliyoanza vizuri lakini ghafla ikabadilika! Rais wa nchi akatangaza hali ya hatari na kuwataka wananchi wabaki ndani ya nyumba zao baada ya wadudu wa ajabu kuvamia taifa na kuwaua watu wote waliokutwa nje, Akitangaza hivyo watoto wa Walter na Theodora ndio kwanza walikuwa wameondoka kwenda kanisani, wasiwasi mkubwa ukawaingia.

Baadaye waliongea na dereva kwa simu ambaye aliwaambia walishafika kanisani lakini mchungaji akagoma kuwafungulia, Walter akamtaka dereva ajitahidi kurejea hadi nyumbani. Mpaka siku tatu baadaye walikuwa bado hawajafika, ingawa kutoka nyumbani hadi kanisani kulikuwa na umbali wa kama kilometa tatu hivi!

Hii ilimaanisha tayari walishakufa au walikuwa wamekwama mahali fulani, jambo hili ndilo lililowafanya Walter na mke wake watake kutoka ndani ya nyumba kwenda kuwatafuta watoto wao. Kabla hawajatoka walisikia muungurumo wa gari, wakarejea tena ghorofani na kuangalia. Lilikuwa ni gari lao, dereva alikuwa amewadia lakini likiwa limezungukwa na wadudu waliokuwa wakisubiri waliomo watoke ili waliwe. Wakajaribu kupiga siku bila mafanikio, wakabaki wamesimama dirishani kuchungulia.

Baadaye walichoka kusimama na kwenda kukaa kwenye viti wakisali, usingizi ukawapitia. Theodora alipozinduka usingizini baadaye alikwenda tena kuchungulia dirishani na kumuona dereva akishuka garini na kufunga haraka kisha kukimbilia getini, wadudu wakamzunguka na kumuua Theodora akishuhudia. Jambo hili lilimfanya Theodora aamue kutoka nje bila mume wake kufahamu.

Walter aliposhituka usingizini na kumkuta mke wake hayupo alianza kuzunguka huku na kule akimwita, alipohakikisha hayupo chumbani aliamua kwenda dirishani kuchungulia ndipo akamwona Theodora akiwa amebeba watoto wawili waliofunikwa na blanketi, hakwenda mbali sana, wadudu wakamzunguka na kumuangusha chini yeye na watoto.

Walter hakutaka kujiuliza mara mbili tena, yeye pia akatoka hadi nje alipolala mke wake na watoto. Wadudu wakamzunguka na kuanza kumuuma, akaanguka juu ya Theodora na watoto, sentensi pekee iliyomtoka mdomoni akiamini anakufa ni “Yes! This is our doomsday!” (Ndiyo! Hii ndiyo siku ya kuangamia kwetu!) Macho yake yakaingiwa na giza, hakuelewa tena kilichoendelea.
Je, nini kitaendelea? Walter, mke na watoto wake wamekufa? SONGA NAYO...
    (19 March 2010)
Views: 226 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Knocked Down? You Can Stand Up -36

hadithi za Shigongo  
Kijana wa Kitanzania (Kelvin) aliyewahi kuchezea Timu ya Liverpool ya Uingereza na kufanikiwa kuwa na jina kubwa katika ulimwengu wa soka anapata ajali mbaya ya gari na kupooza kuanzia shingoni mpaka miguuni, kichwa peke yake ndicho kinafanya kazi!

Hayo yakitokea mama yake pia anafariki kwa ugonjwa wa kansa ya damu. Matukio haya mawili yanasababisha Kelvin kufilisika kabisa na kuishi nyumbani kwa rafiki wa mama yake aitwaye Regina, aliyeishi kwenye kibanda kidogo cha nyasi.

Kwa walio wengi duniani, hii ingekuwa ndio mwisho wa safari yao na kusubiri kifo. Haikuwa hivyo kwa Kelvin, akiwa kitandani alisoma kitabu kiitwacho Knocked Down You Can Stand Up na kujikuta akipata nguvu upya na kuamua kutafuta mafanikio bila kulichukulia tatizo la kupooza kama kikwazo.

Taratibu akaanza shughuli ya kuhamasisha watu kujiondoa kwenye umasikini akibebwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kutumia machela, watu waliomsikiliza waliguswa mno na kulazimika kumchangia fedha za kumsaidia!
Hizo ndizo zilizomwezesha hatimaye kuingia Mwanza akitokea Bukoba ambako aliendelea kuzunguka hatimaye akamaliza Tanzania nzima akiwa tayari na kiasi kikubwa cha fedha kilichotokana na michango ya watu.

Bila kutegemea akajikuta amejulikana dunia nzima na kuanza kutembea sehemu mbalimbali duniani akihutubia mikutano mikubwa mpaka ya watu laki moja kwenye uwanja mmoja wakimsikiliza na na kumlipa kiasi kikubwa cha fedha! Maisha ya Kelvin yakabadilika kabisa na kujikuta anamiliki ndege yake binafsi, akathibitisha kwamba kupooza si kikwazo cha mtu kufanikiwa.

Akiwa London, Uingereza akakutana na mchumba wake wa zamani, waliyepata naye ajali (Martina) na kufunga ndoa, baadaye akatafuta daktari ambaye aliwawezesha hatimaye Martina kuwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kike kwa njia ya operesheni, ambaye walikubaliana kumpa jina la Koku kama kumbukumbu ya mama yake Kelvin, ambaye alitamani kumuona mjukuu wake kabla hajafa.

Ghafla wakiwa kwenye chumba alicholazwa Martina, mtoto akiwa kwenye chumba kingine, waliwaona madaktari na wauguzi wakikimbia kuingia kwenye chumba cha mtoto wakionyesha wasiwasi mkubwa, dalili kuwa mtoto wao Koku alikuwa katika hali mbaya.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (18 March 2010)
Views: 371 | Maoni (5) | Soma Zaidi

 

Just hang me -40

hadithi za Shigongo  
Justine anamchukua Nancy kwenda kumtambulisha kwa wazazi wake huko Jacksonville, North Carolina ambako Nancy alishangaa kukuta wazazi wa Justine ni wazungu! Alipouliza ndipo habari nyingine ambaye Justine hakuwahi kuifahamu ikaibuka. Kumbe Bwana na Bibi Lawrence Green walimwokota Justine kwenye msitu wa Zinga alipokuwa na umri wa siku moja, alizaliwa na kutupwa na mama asiyejulikana ndipo wao wakamlea mpaka kufika alipokuwa.

Jambo hili linamsikitisha Justine na anaamua kwenda Tanzania kufanya mambo mawili; kujitambulisha kwa wazazi wa Nancy kabla ya ndoa yao, la pili likiwa ni kuitafuta familia yake, moyoni mwake aliamini mama yake alikuwepo hai nchini humo na alitaka afaidi matunda ya kuzaa hata kama alimtupa.

Nchini Tanzania Justine alipokelewa vizuri na familia ya Nancy, bibi mzaa baba wa Nancy akamfananisha na binti yake aliyepotea (Tracy) na kulia sana. Baada ya mapokezi alikodisha chumba kwenye hoteli ya Sea Cliff na Nancy akawa analala nyumbani kwa wazazi wake jambo lililosababisha ugomvi mkubwa kati yao, Justine akidai hakuja Tanzania kulala peke yake akipigwa na baridi.

Ugomvi huu ulimfanya Justine aachane na Nancy na kuamua kufanya jambo la pili, ambalo ni kutafuta familia yake. Akakutana na mtu aliyemwokota mwanamke kando ya barabara karibu kabisa na shamba la bwana na bibi Lawrence Green tarehe hiyohiyo aliyozaliwa Justine na kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambako mwanamke huyo alifariki na kuzikwa na halmashauri ya mji bila ndugu yake kuwepo.

Ilithibitika hakugongwa na gari kama walivyofikiri, bali sehemu zake za siri zilionyesha alijifungua muda mfupi kabla ya kufariki. Justine akiamini mwanamke huyo ndiye mama yake baada ya kupewa maelezo, aliamua kwenda hospitali ya wilaya ambako alithibitishiwa yote na baadaye kukutana na mtu aliyemzika mwanamke huyo, wote wakaenda makaburini na kukuta juu ya kaburi lake kulikuwa na kaburi jingine! Justine akalia.

Waliporejea nyumbani alipewa barua iliyokutwa kwenye mfuko wa gauni la mwanamke huyo, ilikuwa barua ya kusikitisha mno ambayo Tracy aliwaandikia ndugu zake, waliomtenga sababu alipewa mimba na baba yake mzazi. Mpaka hapo, Justine akawa ameshakuwa na uhakika kuwa mwanamke huyo alikuwa ni mama yake na waliosababisha kifo chake ni familia Matetere, waliotarajiwa kuwa wakwe zake.
Je, nini kitafuata? SONGA NAYO...
    (17 March 2010)
Views: 473 | Maoni (5) | Soma Zaidi

 

Our Doomsday -9

hadithi za Shigongo  
Wadudu wa ajabu wanaofanana na nyuki wamelifunika kabisa anga la jiji la Dar es Salaam, jua halionekani, hali inaonekana kama ni usiku wa manane ingawa ni asubuhi ya siku ya Jumapili. Watu wote waliokutwa nje wameshambuliwa na wadudu hawa na kufa, Rais wa Jamhuri ametangaza hali ya hatari. Watu hawatakiwi kutoka nje ya nyumba zao wala kufungua milango mpaka watakapotangaziwa.

Tukio hili baya lilitokea muda mfupi tu baada ya Theodora na mume wake Walter ambaye ndiyo kwanza amerejea nchini kutoka Haiti alikokwenda kikazi, kuwaruhusu watoto wao wawili (Ipyana na Atu) kwenda kanisani wakiwa na dereva wa familia (John). Hofu kubwa imewapata baada ya kuliona tangazo hilo kwenye televisheni na kuamua kupiga simu ya John ili waulize mahali walikokuwa, simu ikawa haipokelewi.

Baadaye John aliwapigia na kuwaeleza tayari walishafika kanisani lakini mchungaji alikuwa amegoma kuwafungulia mlango ili waingie ndani kwa hofu kwamba yeye na familia yake pia wangekufa, kuna watu wengi sana kwenye uwanja wa kanisa ambao wamekufa kwa kuumwa na wadudu hao! Walter anamuomba dereva afanye kila kilichowezekana kuendesha gari kurejea nyumbani, baada ya hapo simu ilikatika na hawakuwapata tena. Hisia kwamba walikuwa wamekufa au wamekwama mahali fulani zikawatawala vichwani mwao.

Wakabaki ndani wakilia na kumwomba Mungu atende muujiza lakini haukutokea, mwisho wakafikia uamuzi wa kutoka nje kwenda kuwatafuta, kinyume na maagizo yaliyotolewa na Rais wa nchi! Hawako tayari watoto wao wafe, wakashuka ngazi taratibu mpaka kwenye mlango ambako Walter ameuzungusha ufunguo na kukikamata kitasa tayari kutoka nje, wote wawili wakiwa wamuomba Mungu si awalinde, bali azipokee roho zao kwani walikuwa na uhakika kabisa kilichokuwa mbele yao si kingine bali kifo. Je, ni kitaendelea? SONGA NAYO...
    (17 March 2010)
Views: 272 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Revenge of the dead (Kisasi cha Wafu - 37)

hadithi za Shigongo  
“Albert?” Mke wa Balozi Katunzi aliita akibubujikwa na machozi
“Naam mama!”
“Ni wewe?”
“Ni mimi mama!”
“Au tunaona kitu kingine?” Balozi Katunzi aliuliza
“Kama nini baba?”
“Mzimu! Maana wewe tulikuzika nyumbani Tanzania!”...
    (16 March 2010)
Views: 363 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Only Me (Mimi peke yangu - 5)

hadithi za Shigongo  
WAKATI penzi kati ya Peter, kijana aliyezaliwa kwa mama Mtanzania na baba Muingereza, binti maskini aitwaye Lilian limepamba moto, mama mzazi wa Peter anafariki dunia kwa ugonjwa wa saratani ya titi. Ni pigo kubwa kwa Peter kwani mama yake ndiye mtu pekee aliyekuwa naye, analia kupita kiasi, faraja kubwa anaipata kutoka kwa Lilian.

Baba mzazi wa Peter aliyekuja kutoa Uingereza kwa ajili ya mazishi ya mkewe anamwambia mwanaye kuwa ataondoka naye kwenda kuishi Uingereza, jambo ambalo Peter hakubaliani nalo kabisa, hataki kutenganishwa na Lilian.
Hali hii ya kutoelewana ilipotokea kati ya Peter na baba yake mzazi aliamua kuwasiliana na Ubalozi wake pamoja na Shirika la ndege la Uingereza na Wizara ya Afya ili aruhusiwe kumnywesha mwanaye dawa ya usingizi ili asafiri naye. SONGA NAYO...
    (16 March 2010)
Views: 406 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

The spring of Sadness! Kisima cha masikitiko -(30)

hadithi za Shigongo  
Hatimaye baada ya mateso makubwa njiani, Rhobi anafanikiwa kuingia katika nchi ya baba yake (Wang Fu), ni furaha kubwa kwake kufika China. Hajui kinachoendelea nchini humo, kuwa kuna kundi linalojiita WBC (Wipe Black Chinese) lililoanzishwa na vijana wa Kichina, likiungwa mkono kwa siri kubwa na Waziri Mkuu ambaye ni Wang Fu pamoja na rafiki yake mkubwa Lee Ming ambaye hivi sasa ni mkuu wa Usalama wa Taifa wa China.

Watu hawa wawili Wang Fu na Lee Ming ndio waliozaa watoto na wanawake wa Kiafrika nchini Tanzania wakiwa vijana wadogo, walipopelekwa nchini humo na Serikali ya China kujenga daraja na reli ya Tazara.

Ndoto yao ilikuwa ni uongozi wa juu wa Taifa hilo kubwa Duniani, hivyo ili kuepuka kashfa ya kuzaa wakiwa Afrika, Lee Ming aliongoza kundi la wauaji hadi kijiji cha Mwasamba, wilayani Magu ambako Rhobi na ndugu zake ambao wote walizaliwa na Wachina hao wawili, waliishi.

Ndugu zake wote wakauawa, yeye peke yake ndiye akanusurika sababu alikuwa chooni wakati wauaji wanafika. Akatoroka na kuingia Kenya ambako aliendelea hadi Uganda na baadaye Sudan, huko ndiko alikutana na vijana wengine, akiwemo Zabron ambao pia walizaliwa na baba wa Kichina na walikuwa safarini kuelekea kwenye nchi ya wazazi wao.

Rhobi akaungana nao na kusafiri hadi Misri ambako walizamia Meli lakini wakiwa katikati ya maji walitupwa na mabaharia ili wafe, Rhoni na Zabron peke yake ndio wakaokolewa na meli nyingine na kuendelea na safari hadi mji wa Guanzhou ambako walishuka na kuingia mitaani, wakakutana na kundi la vijana wauaji (WBC) bila kuwafahamu na kutekwa hadi porini ambako walifungwa kwenye magunia na kuachwa wafe kwa njaa.

Siku tatu baadaye mmoja wa vijana hao alirejea na kumchukua Rhobi hadi mahali alipoishi kwa lengo la kumgeuza kuwa mtumwa wa ngono, akamfunga minyororo na kumuingia wakati alikuwa bikira! Alipotaka kufanya mara ya pili Rhobi alikataa, ukatokea mzozo uliopelekea mshumaa kuanguka.

Kijana mtekaji (Xin) akaondoka na kumuacha Rhobi peke yake chumbani. Haukupita muda mrefu sana moto wa mshumaa uliokuwa ukiwaka ukashika kwenye pazia na baadaye godoro, juhudi za Rhobi kujiokoa zikashindikana ikabidi asubiri kifo. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (15 March 2010)
Views: 438 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Our Doomsday -8

hadithi za Shigongo  
Hali imebadilika ghafla, siku iliyoanza vizuri imegeuka balaa! Mabilioni ya wadudu wa ajabu ambao hawafahamiki walikotokea wameifunika anga ya jiji la Dar es Salaam, wameua watu wote waliokutwa nje kwa kuwauma.
Walter na mke wake Theodora waliwaruhusu watoto wao Ipyana na Atu kwenda kanisani wakiwa wamepanga kwamba wakireje ndio waende ufukweni kupumzika, lakini dakika chache tu baada ya watoto kuondoka ndipo hali hiyo mbaya ikatokea! Hawajui mahali watoto wao waliko na kama wako hai au wamekufa, kwani hivi sasa wakipiga simu ya dereva haipatikani, wamechanganyikiwa kabisa na sasa wameamua kutoka nje kwenda kusaka watoto wao, wako tayari kupoteza maisha yao .
Je, nini kitafuata? Je, watatoka? SONGA NAYO.
    (15 March 2010)
Views: 271 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

My black chapter -45

hadithi za Shigongo  
Umahiri na ujanja wa Wanasheria umemfanya Maryjose aachiwe huru ingawa ni kweli aliua. Mahakama imeshindwa kuthibitisha mauaji hayo, hivyo hivi sasa akiwa na hali mbaya sana ya afya kiasi cha watu kudhani kama asingeachiwa huru lazima angefia jela ndani ya mwezi mmoja, ametolewa Mahakamani na kupakiwa ndani ya gari tayari kwa safari ya kuondoka eneo hilo! Kamera za waandishi wa habari zinamfuata.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO.
    (15 March 2010)
Views: 347 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Just hang me! -39

hadithi za Shigongo  
Mambo yamebadilika baada ya mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu nchini Marekani Justine Lawrence Green na mchumba wake Nancy David Matetere kufika Tanzania, wawili hawa wameingia kwenye mgogoro mkubwa pale mila na desturi zilipomzuia Justine kulala na mchumba wake hotelini.

Kwa hasira Justine ameamua kuachana na Nancy ili afanye jambo la pili lililomfanya aje Tanzania ambalo ni kutafuta asili yake kwani alizaliwa Tanzania na kutupwa porini ambako familia ya Kimarekani ilimuokota na kuondoka naye.

Juhudi zake zimemfanya afike kijijini Kaole ambako anaishi mzee mmoja aliyeshiriki mazishi ya mwanamke anayedhaniwa kuwa ni mama yake Justine, kwa pamoja wanaondoka kwenda makaburini ili kijana huyo akaone kaburi la mama yake.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (13 March 2010)
Views: 504 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

The Spring of Sadness! -27

hadithi za Shigongo  
Baada ya familia yake kuuawa na Wachina, Rhobi anafanikiwa kutoroka hadi nchini Kenya ambako aliendelea na safari hadi Uganda na baadaye Sudan akiwa njiani kuelekea China, nchi ambayo baba yake Wang Fui alitokea na hivi sasa ni kiongozi wa juu wa serikali. Huyu ndiye aliyetuma Wachina wenzake kwenda kuwaua Rhobi na ndugu zake ili kuficha kashfa ya kwamba yeye na rafiki yake Lee Ming ambaye hivi sasa ni Mkuu wa Usalama wa Taifa nchini China, walizaa watoto barani Afrika jambo ambalo ni aibu kubwa kwao kama viongozi.

Akiwa Sudan, Rhobi anakutana na kundi la vijana wengine waliozaliwa na baba wa Kichina ambao pia wako safarini kuelekea China, kwa pamoja wanaungana katika safari yao hadi Misri ambako walizamia meli iliyokuwa ikielekea China. Njiani waligundulika na mabaharia kuwatupa majini wafe, Rhobi na kijana mwingine aitwaye Zabron ndio pekee walinusurika baada ya kuokolewa na meli nyingine iliyowapeleka mpaka mji wa Guanzhou ambako walishuka na kuingia mitaani wakisindikizwa na kijana aitwaye Msafiri, bila kuelekwa kuwa nje ya bandari kulikuwa na kundi la vijana waliokuwa wakiua watoto wote waliozaliwa na mzazi mmoja Mwafrika, mwingine Mchina.

Rhobi na Zabron wakaingia mikononi mwa kundi hilo, wakatekwa na kupelekwa hadi porini ambako walifungwa kwenye magunia na kuachwa hapo ili wafe kwa njaa. Siku tatu baadaye wakiwa taabani, gari lilifika porini, gunia la Rhobi likafunguliwa na yeye kutolewa ndani yake kisha kusafirishwa hadi mjini ambako aliwekwa kwenye chumba kimoja ndani ya jumba bovu, akafanywa mtumwa wa ngono.

Alikuwa bado bikira lakini kijana aliyemtoa porini (Xin) hakujali hilo, akaendelea kumuingilia mpaka Rhobi alipokataa na kusabisha purukushani ambayo iliuangusha mshumaa uliokuwa kando, kijana huyo akaondoka akimwacha Rhobi peke yake na kufunga mlango kwa nje! Hakujua kwamba mshumaa huo ulikuwa ukiendelea kuwaka, baadaye moto ukalishika shuka na godoro, chumba kikaanza kuwaka kwa moto na moshi ukaongezeka.
Je, nini kitaendelea? Rhobi atateketea ndani ya jumba hilo? SONGA NAYO...
    (12 March 2010)
Views: 489 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Our Doomsday -7

hadithi za Shigongo  
Hali ilikuwa mbaya. Wadudu wa ajabu waliofanana na nyuki walikuwa wamevamia jiji la Dar es Salaam kwa mabilioni na kufunika kabisa anga kiasi cha kufanya mchana uonekane kama saa sita za usiku! Watu wote waliokuwa nje walishambuliwa na nyuki hao na kufa, maiti nyingi zimetapakaa mitaani. Ni tukio la kusikitisha, pigo kwa nchi ya Tanzania ndio maana Rais ametangaza hali ya hatari kupitia luninga kwamba watu wasitoke nje na wasijaribu kufungua milango au madirisha.

Wakati jambo hili linatokea, Walter Lumisha alikuwa na masaa machache tu tangu arejee nchini kutoka Haiti alikokwenda kikazi akiwa mtumishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), yeye na mke wake wamewaacha watoto wao waondoke na dereva kwenda kanisani na wao kubaki nyumbani wakiwasubiri. Hali imewashangaza baada ya giza kuingia, hapo hapo wakaanza kupiga simu kufuatilia kama watoto wao walikuwa salama.

Ilikuwa kazi kidogo kumpata dereva (John) hata hivyo baadaye alipopatikana aliwaeleza kwamba alifanikiwa kufika kanisani ambako watu wengi walikuwa wamekufa, akampigia simu mchungaji ili awafungulie waingie lakini alikataa. Alichofanya Walter ni kumtaka dereva afanye kila kinachowezekana kurejea nyumbani na watoto jambo ambalo aliahidi kulifanya.

Theodora, mke wa Walter ana uchungu mwingi, roho inamuuma mno, hayuko tayari kuona watoto wake anaowapenda kupita kiasi wanakufa! Hivyo bila kujali kwamba nje kuna wadudu wa hatari ambao akifungua tu mlango atakufa, mwanamke huyu ameamua kwenda nje kuwafuata watoto wake, jambo ambalo Walter hakubaliani nalo na anamkamata akijaribu kumzuia lakini Theodora amemzidi nguvu Walter na kumsukuma, akaanguka chini, muda huo huo Theodora akaukimbilia mlango na kuanza kuufungua.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (12 March 2010)
Views: 333 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

My black chapter -44

hadithi za Shigongo  
Tayari mlinzi ambaye ni shahidi muhimu katika kesi ya mauaji inayomkabili Maryjose amekwishatekwa na kupelekwa porini huko Kimbiji, Kigamboni kwenda kuuawa. Kabla hajafyatua risasi, muuaji aliamua kumpigia simu Wakili Mafuru anayemtetea Maryjose ambaye pamoja na mzee Magesa na David, wapo kwenye kikao cha usiku wakipanga namna ya kupata ushindi na kumweka huru Maryjose. Lengo la muuaji kupiga simu hiyo ilikuwa ni kumtaarifu kilichokuwa kikiendelea, Mafuru akaomba aongee na wenzake juu ya hatua ambayo muuaji alikuwa amefikia.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (12 March 2010)
Views: 366 | Maoni (3) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2 3 ... 79 80 81  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com