Dili la mauaji ya Jeff linafanyika chini ya Kundi la Kimafia la Nyamangumu Camp, linaloongozwa na Master, lakini Roy aliyepewa kazi hiyo, anaamua kufanya dili ndani dili! Mchezo mzima unafanyika kwa kuagiza maiti iliyoharibiwa sura kutoka kwa Kijasho.
Maiti inavalishwa nguo za Jeff, inawekewa nyaraka mbalimbali za Jeff ili kuhalalisha kwamba ilikuwa maiti yake. Zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa. Baada ya hapo, Roy analiingiza gari kwenye mti na kusababisha ajali mbaya! Je, nini kitatokea? Endelea kufuatilia...
“Ndiyo jina lako au msafiri unakwenda mahali?” “Siendi popote.” “Khaa! Sasa hapa kwako?” “Hapana.” “Sasa kwanini umefungua mlango bila hodi na umepanda kitandani kulala bila ridhaa yangu?” “Nisamehe sana.” “Basi ondoka.” Kauli yangu hiyo haikupata jibu zaidi ya mlio wa kukoroma kusikika kama mwanzo. Nilimsogelea yule mtu pale kitandani kwa lengo la kumfunua shuka na kumwona vizuri. Niliishika shuka kwenye ncha moja, nikaifunua kwa nguvu…
Mpenzi msomaji, kijana Kafumu aliyefundishwa uchawi na bibi yake, anaendelea kusimulia mambo ya kichawi aliyokumbanayo katika maisha yake ambapo alirithishwa mkoba wa kichawi na uganga wa babu yake. Wiki iliyopita uliona alivyokwenda kuhudhuria katika kikao cha kichawi ambapo akiwa na watoto wenzake, walipelekwa makaburini ambako maiti sita walifufuliwa kisha kiongozi wa wachawi alikata kipande cha sanda aliyovikwa kila maiti kisha vipande hivyo akavifunga katika mkono wa Kafumu na wenzake. Baada ya kufanya hivyo, aliwaeleza kazi ya vitambaa hivyo vya sanda wataelezwa na wazee waliowaacha kwenye kikao. Waliporudi kwa wazee na wachawi wengine,kiongozi wao aliwafungua vitambaa hivyo na kuviweka ndani ya tunguri lake kisha aliharisha kikao lakini alitoa maagizo kwamba kila mzazi au mlezi wa watoto waliotakiwa kurithishwa mikoba ya kichawi, ampeleke mwanaye kwa kiongozi wa kichawi wa ukoo wake ili mtoto husika akaelezwe historia ya mtu anayetakiwa kuurithi mkoba wake ambapo yeye alipelekwa katika kijiji cha Kigwa kwa mjomba wake ambaye alimfahamisha uwezo aliokuwanao babu yake aliyeitwa Kafumu aliyetakiwa kuurithi mkoba wake.
Aliambiwa mambo mengi ambayo enzi za uhai wa babu yake aliyafanya, kama kuamuru mti upasuke kisha aliingia ndani yake, kugeuza nywele kuwa nyoka. Kufuatia muda wa wachawi kuwa nje ya nyumba zao kwisha, mjomba huyo aliharisha kikao na kumtaka bibi na Kafumu warudi tena kesho yake ili amalizie kumsimulia mambo ambayo babu yake aliyafanya.
Je, ni mambo gani hayo? Ungana na KULWA MWAIBALE katika mkasa huu wa kweli uliomkuta kijana Kafumu…
ILIPOISHIA Alikumbuka baada ya kuondoka na yule mrembo na kwenda naye mpaka kwake ambako kulikuwa na uzuri wa ajabu na kuweza kulala naye kitanda kimoja lakini hakukumbuka kama walifanya naye mapenzi. Na asubuhi alipoamka kujikuta chumbani kwake tena kitandani jambo lile lilizidi kumchanganya sana. SASA ENDELEA...
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA Usiku ulipofika licha ya kwamba yule muwindaji alinionesha chumba tofauti cha kulala lakini alinifuata na kunishawishi nifanye naye mapenzi. Ulikuwa ni mtihani mgumu! ...
Thabit kijana aliyekuwa akitoka kazini muda mbaya wa usiku na kujikuta akiwa peke yake katika kituo cha basi cha Mwenge. Bila kutegemea anatokewa na miujiza ambayo kwake ilikuwa kama yupo ndotoni, lakini kila kitu kilikuwa kweli na kumchanganya na kushindwa kuelewa kile ni kitu gani. Pia anakutana na mwanamke mrembo Nargis ambaye anazidi kumchanganya. Yule ni mwanamke wa aina gani ambaye bado hajamuelewa ni mwanadamu kweli. Je ile hali iliyojitokeza kituoni ni kweli na yule mwanamke ni nani? Ili kuyajua yote TUWE PAMOJA… ILIPOISHIA Alinyanyuka na kutoka nje akipitia ndoo yake yenye maji machache na mswaki mkononi alielekea bafuni kuoga. Baada ya kuoga alibadili nguo haraka kuwahi kazini kutokana na kuamka muda mbaya, baada ya kujiandaa aliongozana na rafiki yake. Njiani rafiki yake alimuuliza swali lililozidi kumchanganya. “Jana nilijua unalala kazini, vipi Wahindi wako wamekuleta na gari nini?” “Wala.”SASA ENDELEA…
Roy na Jeff wameshaweka mipango yote sawa, tayari Jeff ameshampatia Roy milioni sita kwa ajili ya kazi ile. Safari ipo njiani, Jeff yupo na mpenzi wake Davina wanazungumza. Kitu cha kushangaza sana, Davina anaonekana hana imani kabisa na ile safari ya mpenzi wake. Je, nini kitatokea? Endelea kufuatilia...
Nilikaa sehemu ambayo kulikuwa na nafasi ya mtu mmoja, yule mtu niliyekwenda naye sikumwona tena alikopotelea. “Bwaba umekuja huku, uko tayari kwa lolote?” Aliniuliza mzee wa kanisani ambaye sikuwa na mazoea naye. “Kwani hapa ni wapi?” Nilihoji. “Hapa ni kwa wachawi.” “Wachawi!” “Eee, umekuja kwa wachawi, kazini kwetu, karibu.” Alipomaliza kusema, alikaa chini, akasimama sasa yule mzee ambaye siku ile kanisani walipoingia wale watu wawili wa ajabu, yeye alikaa katikati yao. SASA ENDELEA…
Mpenzi msomaji, kijana Kafumu aliyefundishwa uchawi na bibi yake, anaendelea kusimulia mambo ya kichawi aliyokumbananayo katika maisha yake ambapo alirithishwa mkoba wa kichawi na uganga wa babu yake ambao awali aliukataa lakini bibi yake alimzidi ujanja na kumwambia akiukubali mkoba huo atakuwa tajiri mkubwa kama walivyokuwa baadhi ya matajiri wa mkoani Tabora miongoni mwao wakiwemo wenye asili ya Kiasia ambao alimtajia majina yao ndipo alikubali kuupokea. Wiki iliyopita uliona alivyokwenda kuhudhuria katika kikao cha kichawi ambako akiwa na watoto wenzake walipelekwa makaburini ambako maiti sita walifufuliwa kisha kiongozi wa wachawi alikata kipande cha sanda aliyovikwa kila maiti kisha vipande hivyo akavifunga katika mkono wa Kafumu na wenzake. Baada ya kufanya hivyo, aliwaeleza kazi ya vitambaa hivyo vya sanda wataelezwa na wazee waliowaacha katika kikao.
Waliporudi kwa wazee na wachawi wengine,kiongozi wao aliwafungua vitambaa hivyo na kuviweka ndani ya tunguri lake kisha aliharisha kikao lakini alitoa maagizo kwamba kila mzazi au mlezi wa watoto waliotakiwa kurithishwa mikoba ya kichawi, ampeleke mwanaye kwa kiongozi wa kichawi wa ukoo wake ili mtoto husika akafahamishwe historia ya mtu anayetakiwa kuurithi mkoba wake. Baada ya kusema hivyo, wachawi waliondoka kurudi makwao kwa kutumia usafiri tofauti, wapo waliotumia ndege za kichawi (ungo), kutoweka kama upepo, kutembea ambapo Kafumu na bibi yake walitumia usafiri wa Fisi.
Walipofika nyumbani, Kafumu alimuuliza bibi yake mambo mengi aliyoyaona kwenye kile kikao cha kichawi. Je bibi yake alimjibu nini? Ungana na KULWA MWAIBALE katika mkasa huu wa kweli uliomkuta kijana Kafumu…
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA Wale mamba walikuwa wengi, kwa jinsi ambavyo nilivyowaona, watu wa Kigoma huwaita Mamba wa Kutumwa, yaani wanatumiwa na wachawi kwa ajili ya kuratibu kazi zao za kila siku. Kwa haraka nikajua kuwa wale watakuwa ni watumwa wa wale wachawi ambao walinisababishia mimi nikawepo eneo hilo...
ILIPOISHIA Ghafla nyayo zile za moto zilipotea, wingu lilitoweka na umeme uliwaka, ajabu alijisikia mwili mwepesi na kujiuliza ile hali ilikuwa ni ndoto au kweli? ENDELEA ...
Roy ameamua kuokoa maisha ya Jeff, yupo kazini pale kwa ajili ya kumuua, lakini moyo wake umekataa kabisa kufanya jambo hilo. Sasa yupo katika mazungumzo ya siri na Jeff, tayari ameshamwambia ukweli. Jeff ameshtuka sana! Je, nini kitaendelea? Endelea kufuatilia...
Nilijipaka kidogo huku nikiwa nimeinama kuangalia chini. “Unaona nini?” “Sioni kitu.” “Haya, hiyo dawa ndiyo tunayotumia kufanyia kazi, tunapotoka usiku kwenda kazini kila mmoja anakuwa na dawa hiyo, ndiyo inayosaidia watu wasituone… “Fumba kiganja.” Nikafumba. “Fumbua.” Nilipofumbua, sikuona ile dawa, kiganja kilikuwa cheupe kama mwanzo. “Fumba tena kiganja.” Nikafumba…
Mpenzi msomaji, kijana Kafumu aliyefundishwa uchawi na bibi yake, anaendelea kusimulia mambo ya kichawi aliyokumbana nayo katika maisha yake ambapo alirithishwa mkoba wa kichawi na uganga wa babu yake ambao awali aliukataa, lakini bibi yake alimzidi ujanja na kumwambia akiukubali mkoba huo atakuwa tajiri mkubwa kama walivyokuwa baadhi ya matajiri wa mkoani Tabora, miongoni mwao wakiwemo wenye asili ya Kiasia ambao alimtajia majina yao ndipo alikubali kuupokea. Wiki iliyopita uliona alivyokwenda kuhudhuria katika kikao cha kichawi na bibi yake kwa kutumia usafi wa fisi.
Walipofika Kijiji cha Manoleo ambako ni eneo ambalo aliishi babu yake, ndipo wachawi wa Tabora hukutana kwa ajili ya kufanya mambo yao ya kilosi na kiganga, alishangaa kuona kundi kubwa la wachawi ambapo baadhi yao aliwafahamu. Kilichomshangaza zaidi ni kitendo cha wachawi kumfuata ambapo walimsalimia na kumpongeza kwa kukubali kwake kupokea mkoba wa kichawi wa babu yake. Katika kikao hicho kiongozi wa wachawi aliwafanyia dawa ya kumuondoa woga Kafumu na watoto wenzake waliotakiwa kurithishwa nguvu za kichawi. Je, nini kilijiri katika kikao hicho? Ungana na KULWA MWAIBALE katika mkasa huu wa kweli na kusisimua uliomkuta kijana Kafumu…